SERIKALI IMEONGEA MUDA WA KUHESABIWA SENSA:Lazima Ipo Namna!

Written by  //  01/09/2012  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 3

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa TZ imetangaza kuanzia leo kuongeza wiki moja zaidi ya kuhesabiwa zoezi la sensa 2012, Kamishna wa Sensa TZ, Bi.Amina Mrisho (Hajat) ametangaza rasmi Dar Es Salaam mbele ya vyombo vya habari leo/jana.

Serikali inajaribu sana kulazimisha zoezi hili lifanikiwe ilhali wenye makosa ni wao.

Kwa mfano sehemu nyingi Zanzibar makarani wa sensa hawajapita, eg. maeneo ya Tomondo, Kinuni, n.k — huko kwao Bara usiseme, wananchi wanalalamika kuwa makarani wa sensa hawajafika huko, na makarani wanalalamika kuwa hawana hata karatasi na penseli/kalamu za kuandikia – licha ya kuwa hawajalipwa pesa zao.

Sasa kosa la nani? Serikali, Uamsho, wananchi au uongozi mbaya wa nchi na hiyo ofisi ya takwimu kwa ujumla. Ukibahatika kuulizwa maswali na hao makarani utacheka, na baadhi ya maswali hayamo hata hizo wanazoziita ‘dodoso’ zao.

Mimi wamekuja kuniuliza maswali: umesoma mpaka darasa la ngapi? Nikawajibu: std 2; then wameniuliza mbona unajua kusoma na kuandika? mimi nikawauliza ‘wale wanafunzi 500 TZ waliofaulu kuingia form 1 mwaka 2011/2012 ambao hawajui kusoma wala kuandika, wamefika vipi form 1, na wamefanya vipi mtihani, na wamefanya mtihani wa aina gani mpaka wameingia form 1 bila kujua kusoma na kuandika?

JK na serikali yake akishirikiana na koloni lake la Zanzibar (secretaries of the colony) wanalazimisha zoezi kwa nguvu, kwa mtutu wa bunduki — lazima, lazima, lazima: KUNA NINI? LAZIMA KUNA KITU HAPA KIMEJIFICHA, IPO AJENDA YA JK NA WENZAKE WANATAKA KUKIFANYA DHIDI YETU.

Kuna matukio mabaya sana yametokea hapa Zanzibar – Matemwe and elsewhere, watu wamevunjiwa nyumba zao, watoto wamepigwa – polisi wameingia kwa nguvu ndani ya nyumba za watu, wamevunja na kuiba – kuna habari pia kuna watoto wa kike wamefanyiwa
mambo mabaya kwa lazima. Jamani kweli haki hiyo?

Dr.Shein uko wapi, Maalim Seif uko wapi na Balozi Iddi — mtakwneda kujibu nini mbele ya allah? Misikiti mnainajis kwa amri zenu, waislamu mnawatesa dhahir shahir, mnanajisi watu kwa amri zenu — iko siku M/Mungu atakutieni mkononi. Kama mnaringia pumzi, mtakuja kuona Allah atapopiga bakora yake iwe kwenu au kwetu sote.

Je, hamtaki kusoma kwa nini? meli mbili zimezama na kuuwa watu chini ya kipindi cha mwaka mmoja. Hmataki kufahamu tu, na kutanabah.

Na nyie mahajat akina Amina Mrisho – kama mnaona kula mali ya watu (tayari wengi wenu mmeshachuma sana kupitia sensa, basi hizo mtakwneda kuzipila mbele ya haki, huo U-alhaji na uhajat bure tu. Ni unafik uliopindukia mipaka.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni yamefungwa.