NYERERE ALIVYOMTETEA KARUME ACCRA KUHUSU ”UHURU ZUIYA’

Written by  //  12/05/2017  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 1

NYERERE ALIVYOMTETEA KARUME ACCRA KUHUSU ”UHURU ZUIYA”
Mohamed Said May 10, 2017 0

Katika gazeti la Raia Mwema leo (Mei 10 – 16, 2017) Barazani Kwa Rajab, Ahmed Rajab kaka yangu na na mwalimu wangu katika uandishi kuna makala, ‘’Nyerere alivyomtetea Karume Accra.’’ Toka mapema leo washabiki wa Ahmed Rajab nje na ndani ya Tanzania wananiletea taarifa kuw akuna kigongo barazani kisinikose, lakini hawaniambii kigongo gani kwani kwa uoni wao hawataki kunipunguzia utamu. Naam Makala hii ni kigongo khasa wala hapana shaka. Ahmed Rajab kagusa vitu vitatu muhimu katika historia ya Zanzibar kwanza kuanzishwa kwa Afro-Shirazi Party (ASP) katika misingi ya ukabila na ubaguzi mwaka wa 1957 kije kipambane na chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) chama cha kizalendo cha kupigani uhuru. Hii Mosi. Pili ASP kuanzishwa kwa mkono wa Nyerere na tatu sera ya Karume na ASP sera yake ikiwa kukataa uhuru kwani uhuru utawanufaisha Waarabu. Anaetaka zaidi atamsoma Ahmed Rajab mwenyewe ila mimi nataka niguse pale aliposema kuwa hii siasa ya kuanzisha vyama vya siasa kwa misingi ya kikabila ilikuwa mbinu ya Waingereza kuwagawa Waafrka ili waendelee kuwatawala mbinu ambayo Ahmed Rajab kaeleza kuwa Waingereza waliijaribu Tanganyika lakini haikufaulu. Hapa Ahmed Rajab kanitaja kuwa mimi nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdulwahid Sykes…

Namyambua kidogo kitabu cha Abdulwahid Sykes (1924 – 1968):

”Kueleweka kwa nini Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere inahitajika uchambuzi kuelewa siasa za mfumo wa kikoloni katika Tannganyika. Mwaka wa 1951 Abdulwahid na Mwapachu walipokuwa wakishughulika kuifufua TAA, walijiwa na Ivor Bayldon, Brig. Scupham na V.M. Nazerali kuombwa kuunga mkono kuundwa kwa chama cha kisiasa kitakachojumuisha Watanganyika wa rangi zote. Hawa walikuwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria. Bayldon alikuwa mlowezi tajiri kutoka Nyanda za Juu za Kusini na alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini. Wajumbe wa Kiafrika wa Baraza la Kutunga Sheria walioliunga mkono wazo hili walikuwa Chifu Kidaha Makwaia na Liwali Yustino Mponda wa Newala . Watu wengine mashuhuri walioshauriwa na kuombwa kuunga mkono chama hiki walikuwa: Dr Joseph Mutahangarwa, Chifu Abdeli Shangali wa Machame, Chifu Mkuu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Haruna Msabila Lugusha, Dr William Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Dossa Aziz .

Huu ulikuwa mchanganyiko wa Wazungu ambao tangu hapo walikuwa raia wa daraja la juu, baadhi yao kama Bayldon walikuwa walowezi; machifu kama vile Marealle, Waafrika wasomi kama Mwapachu; tabaka ya wafanyabiashara wa Kiasia kama Karimjee na watu wa mjini kama Dossa Aziz na Juma Mwindadi. Wote hawa walikuwa viongozi waliokuwa na wafuasi katika jumuiya zao. Katika barua Nazerali aliyomtumia Ally Sykes miaka miwili baada ya kudhihiri kuwa chama kile walichokusudia kisingeweza kuundwa, Kwenye sehemu moja alikuwa na haya ya kueleza: ëHaja kubwa ilikuwa kuandaa kikundi cha watu walio wakweli, waaminifu na wenye imani katika maendeleo ya watu katika nchi yetu, pamoja na fursa sawa kwa wote.

Abdulwahid wakati huo akiwa katibu pamoja na wanachama wa TAA wasingeweza kukubali wazo kama hilo. Ingawa kwa kiasi fulani malengo ya chama hicho kilichokusudiwa yalionekana yanafanana na malengo ya wananchi hivyo kudhihirisha barabara kile ambacho TAA ilikuwa ikikipigania, Waafrika wasingeweza kuachia azma ya wa Tanganyika kwa dhamira njema ya wasiokuwa Waafrika na ambao walikuwa wakishirikiana bega kwa bega na serikali ya kikoloni. Ilikuwa dhahiri kuwa Wazungu na Waasia nchini Tanganyika hawakutaka kukubali kuwa Tanganyika kwa hali yoyote ile ilikuwa nchi ya Waafrika. Kwa TAA kukubali kuundwa chama cha siasa kitakachojumuisha mataifa yote, kulikuwa sawa na kuyaweka maslahi ya Waafrika katika mikono ya watu wachache…”

Chini: Ali Muhsin Barwani, Mohamed Shamte, Hasnu Makame na Abeid Amani Karume

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni Moja katika "NYERERE ALIVYOMTETEA KARUME ACCRA KUHUSU ”UHURU ZUIYA’"

 1. zanzibarmyhome 12/05/2017 kwa 3:56 um ·

  Sikubaliani na hoja kuwa ni Waingereza waloweka vyama hivi vua mrengo wa rangi…ili apate kuendelea kutawala. Walijua kuwa nchi hizi zilikua ni dhamana ya UN kwao na Zanzibar ni protectarate. Hivyo lazima watakabidhi hixi nchi kwa wenyewe.
  In fact wainfereza waliweka msingi mzuri wa democrasia kwa stage kila baada ya muda. Ingawa tuliona kama ni upendeleo kwa wazungu wahindi na waarabu….ila wakati ulufanya iwe hivyo kuwatayarisha kutawala.
  Walitoa uhuru wa nchi hizi za EA kwa mpango maalum na mazungumzo ambayo yenye lengo la kuyafanya mataifa maoya kujiendesha vizuri bila ya magomvi…
  Waleweka utaratibu mzuri wa democrasia ambao laiti tunge uimarisha leo nchi zetu zingekuwa sawa na nchi zilizo endekea.
  Waafrika wenyewe ndio matatizo makubwa sana…
  Nyerere alianza yeye kufuta vyama vingi na kuwa mtawala pekee, akafata Kenyata then Obote.
  Zanzibar kulikua na dalili ya mfumo wa vyama kuendelea, Nyerere hakupenda kuwa na jirani mwenye mfumo wa democrasia na zipo sababu za chuki na udini ulomfanya kuchochea na kupanga mapinduzi.
  Nchi zote za EA zikawa katika matatizo ya tawala za mtu mmoja chama kimoja hatimaye mifumo yote ya kitaasisi walio tuachia waingereza ikavurugika….na nchi miaka 50+ zimebaki kwenye dimbwi la umasikini wa kutupwa
  Suala la msingi ambalo tujiulize jee hii miaka 50 ilipotea bure ingekua bado tupo chini ya Muingereza nchi hizi zingekua katika maendeo ya namna gani 😣

Toa maoni

You must be logged in to post a comment.