Mzanzibari Zinduka: Usaliti wa Lipumba na Khammnyaharuna Sio wakuachiwa.

Written by  //  16/03/2017  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 5

By Zamko & Ashakh

Asalamu aleikhum ndugu zangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu adhimu, ama kwa upande wetu tunamshukuru Allah SW kwakutupa pumzi, uzima na wasaa wakuandika makala hii muhimu. Makala hii itakuwa na Phase 1, 2 na 3. Hii ya leo tutaanza naphase 1 tu.
Kabla yakuanza hio phase 1, nataka Wazanzibari nyote muelewe kwamba migogoro katika Vyama ni jambo la kawaida. Na migogoro hii huja na kupita, lakini mgogoro ulioko CUF kwavile ni wakuandaliwa na CCM na malengo yake ni kuwazuia Wazanzibari kupata HAKI yao ya Ushindi wa Uchaguzi halali wa 25.oct.2015. Ndio pesa nyingi ilioibiwa chamani inatumika kuendeleza mgogoro huu ambao. Lipumba alishauriwa na Sefu Ali Iddi kuwatumia baadhi ya Viongozi wa Pemba ili awaingize katika TIMU yake ya Hujuma ili wawatoe Wananchi na CUF katika msimamo wake.
Pia nataka ieleweke wazi kama sisi hatuikingii kifua CUF, laa hasha. Tunajuwa katika CUF kuna matatizo kama ilivyo vyama vyengine vyote. Lakini matatizo ya CUF hayata ondoka kwa akina KHAMNYHARUNA kujiunga na Lipumba. Matatizo ya CUF yataondoka wakati Wazanzibari watakapo pata Haki yao ya Ushindi na Wananchi na Viongozi kuifumua CUF na kuijenga upya.
Makala ya 1:
Kwanza nini maana ya neno KHAMNYHARUNA? Khamnyharuna maana yake ni: –
Kha= Khalifa. 2. Mny= Mnyaa. 3. Ha= Haroub. 4. Ru= Rukia. 5. Na= Nasor.
Kisheria hasa LIPUMBA ni nani? Lipumba ni:-

Rai tu wa kawaida kama mimi na wewe na sio Mwanachama wa CUF labda tuseme ni Kibaraka wa CCM kwasababu alijiuzulu mwenyewe na Kikao cha CUF chenye wajumbe waliotimia walikubali kujiuzulu kwake. Na kwisha kumfukuza Uwanachama. Hivo Lipumba kwa sisi Wazanzibari sio Mwanachama, wala Katibu wa Chama na kundi lake ni dogo sana. Hivo Lipumba asijaribu kuja kutuchafulia Visiwa vyetu akahisi kwasababu ana Ungwa mkono na Akina Khamnyharuna. Atabakia Salama. Ku Sucrify Msaliti mmoja katika hao kwa ajili ya Kuinusuru Nchi yetu na chama chetu ili kirudi kwenye malengo yetu ni Halali kwa kila Mzanzibari. Tukumbuke Tulikotoka na tunakotaka kupelekwa na kundi hili.

Kwakuanzia na makala yetu nataka kwanza Wazanzibari muelewe ni nini hasa Malengo ya CUF kwenu nyinyi Wazanzibari? Malengo ya CUF ni: –
1. Kutambuwa Uwepo wa Zanzibar kama Nchi (Visiwa) Huru.
2. Kuwatambua Wazanzibari na Kuilinda Identity Yao Popote pale Walipo.
3. Kuitetea ” HAKI” za Zanzibar na Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu.
4. Kuleta Usawa kwa Wazanzibari wote wa Ndani na Nje ya Visiwa vyetu.
5. Kuwaunganisha Wazanzibari wote wa Ndani na Nje kuwa kitu kimoja kama Wazanzibari.
6. Kuheshimu na Kuzilinda Haki zao, Utu wao, Mali zao, Mipaka yao, na Rasilimali zao
7. Kuleta Maendeleo ya kijamii kwa Wazanzibari bila kubaguwa rangi, kabila, jinsia au sehemu anayotoka mtu.
8. Kuleta Mamlaka kamili na maendeleo ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali zao za nchi.
9. Kuwaunganisha Wazanzibari na Majirani zao wa Africa na Nje ya Africa.
10. Kuisimamia Zanzibar na Kujenga Uhusiano mwema Kitaifa na Kimataifa utakao leta mafanikio kwa jamii na Dunia kwa ujumla.

Ndugu zangu Wazanzibari, hayo hapo juu ndio Malengo makubwa ya CUF, hivo tunatakiwa tuzinduke na tujiulize masuali. Ni nani Mtetezi wa hayo?

Wazanzibari tusidanganywe na tusikubali kugombanishwa na watu wa BARA, kwani wao Wana Nchi yao ya Tanganyika iliokuwa na Mapori ambayo hata kuguswa hayaja guswa. Sisi tuna Vijisiwa vyetu vidogo sana ambavyo kama itatokea Umwagaji wa Damu au jenginelo – basi hakuna Mtetezi. Huyo Lipumba na hao Nduguzetu wa damu (Tanganyika) likitokea “Tatizo” hapa Zanzibar wengi wao Hulifurahia tatizo hilo.
Ni nani alietetea Maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari hadi ukaja Uandikwaji wa Katiba mpya kama sio Allah kuwapa Imani Wazanzibari Wazlendo na CUF?

Ni nani aliepigania Suali la Mafuta na Rasilimali za Zanzibar ikiwemo uzuiwaji wakuiba rasilimali ya Mafuta ilioko katika kisiwa cha Fungu Mbaraka kama Sio Allah kuwapa Imani Wazanzibari wazalendo na CUF?
Ni nani aliepinga suali ya Kura ya Maoni ya Rasimu ya CHENGE na CCM kama Sio Allah kuwapa Imani Wazalendo Wazanzibari na CUF?
Ni nani aliepinga Uchaguzi haramu ulioletwa na Wahafidhuna wa CCM wakisaidia na maadui zetu (CCM -Tanganyika) kama sio Allah kuwapa imani Wazanzibari wazalendo na CUF?

Jee mumeona jinsi gani wazanzibari walivoitikia wito na kuiacha CCM Zanzibar kuadhirika katika Uchaguzi Ule wa 20. march 2016?
Hapa nataka munielewe wazi kwamba tusichukulie kuwaona CCM wanaongoza Nchi. Viongozi wote wa Nchi2 hizi Tanaganyika na Zanzibar hawana Amani ndani ya nafsi zao kwa dhulma waliowafanyia Wazanzibari. Wanaongoza Nchi kwa khofu na izara yakushindwa na wako kama Gamba la Koa tuu. Hawana lolote lile na hawaiwezi Nguvu ya Umma unao dai haki kama utasimama pamoja. Isipokuwa kutumia Vyombo vya Dola. Ikiwa sio Jeshi na Polisi CCM isingekuwapo tena. Hasa kwa Upande wa Zanzibar. Hilo CCM wanalijuwa na ndio maana Wamefanya mikakati yote ya Kumtumilia LIPUMBA na baadhi ya Vibaraka hao niliowataja hapo juu.

Ni nani aliepiga Kelele kuhusu kisiwa cha Fungu Mbaraka, kama sio Allah kuwapa uwezo Imani Wazanzibari wazalendo na CUF?
Nataka tuelewe ukweli kwamba hakuna wakuleta mabadiliko hayo kama Sio CUF. Tayari tumeweza kuona Jinsi Zanzibar Ilikotoka- kuanzia kwenye UDICTOTOR. Baadae ukaja Ukoloni Mambo leo Wa Chama kimoja (CCM) na kuambiwa kwamba Chama ndio kilichokuwa kimeshika hatamu. Katika vipindi hivo kuna watu hawavikumbuki kwasababu hatukuwa tumezaliwa, lakini tulisikia hadithi zake. Bila ya kuelezea hapa. Lakini tunaweza kutofautisha baina ya Tawala za SMZ zilizokuwa zikiongozwa na Chama kimoja – na ule utawala ulioongozwa na Mfumo wa GNU.
Makala itaendelea Phase 2 Ambayo tutawachambuwa hawa Khamnyharuna na nini Wamewafanyia Wazanzibari katika kipindi chote cha Ubunge na nyazifa zao za uongozi ndani ya CUF.

Tunawaomba Samahani ikiwa tumewakosea.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 5 katika "Mzanzibari Zinduka: Usaliti wa Lipumba na Khammnyaharuna Sio wakuachiwa."

 1. Ashakh (Kiongozi) 16/03/2017 kwa 9:23 mu ·

  Hakuna samahami, imeeleza kiilivyo nawe kama Mzanzibar kuipigania platform yetu. Hii ndio sauti yetu

 2. zamko 16/03/2017 kwa 12:44 um ·

  @ Ashakh ( kiongozi)

  Ahsante sana kwa maoni yako ni lazima wazanzibari walioko CUF na Wasiokuwa na Vyama kama, mimi, lakini nia Imani kubwa juu ya CUF na kwamba ni Chama ambacho kwa Muda wa Miaka 20 sasa tokea Iasisiwe imekuwa Ikipiga kelele kuhusu Zanzibar na Uwepo Wake.

  Najuwa kwamba Viongozi wa CUF sio malaika wana matatizo yao kama Binaadamu wengine wote. Lakini Munafikiria CCM na Lipumba, Nassor Seif, Khalifa, Haroub, Mnyaa na Musa Kombo wao they are so Innocent? Kuna wengine humu ndani ya kundi hili la wasaliti wa CUF walioteuliwa na Lipumba Ati wanasema ndani ya Cuf kuna matatizo. Na wao kama ni waanzilishi ( The FOUNDER) wa Chama hichi cha CUF ati walijitia Nongwa za Kike Wakaigomea CUF ati kwasababu za kijinga.
  Kwanini hawakukaa kutatua matatizo hayo.

  Hivo kujiunga na LIPUMBA Mtanganyika Asiekuwa na Fadhila kutafanya Matatizo ya CUF yawe Solved?

  Au Kutaeneza mafuta ya Chuki ndani ya Nyoyo za Wazanzibari hasa Wakiona kwamba Wanacho Kitetea ni Haki yao ya Ushindi wa 25. oct. 2015 na Ni haki yao ya Kiraia. Hakuna mtu anaesimama kwakudai jambo haramu hapa. Tunadai maslahi ya Kura zetu tulizopiga na kumchaguwa Maalim Sefu. Kwanini Hawa Nguruwe Mwitu wanataka kuja kusababisha matatizo?

  Katika majina ya Viongozi hao ambao kwa ufupi wake tumewaita KHAMYNHARUNA.

  Tunatakiwa Wazanzibari tujiulize masuali mengi sana wakati walipokuwa viongozi wa CUF. Wamewafanyia Fadhila Gani Wananchi wa Zanzibar katika Uongozi Wao , Vibaraka hawa wa Lipumba na CCM?

 3. salali 16/03/2017 kwa 2:54 um ·

  Hata dini yetu inasema ukisha lima shamba na kuvuma mazao pumba magugu ni takataka za kupigwa moto, sasa kama kutuchanganyia mchele na pumba (magugu)tumawajuwa uchafu wao tutawatoa mmojammoja na kuwatia moto, hiyo minguruwe pori inawanza m’gono tu pesa zote walizokua wakilipwa na chama chetu walikuwa wanazifanyia n’gono katika mahotelini tunawajuwa mmoja baada ya mwengine huyo musa haji kombo si hasha kama hajauvaa upupu.

 4. mzeekondo 16/03/2017 kwa 5:05 um ·

  @ Zamko

  Nikushukuru kwa makala, maoni na jitihada zako za kila siku za kuvitetea visiwa hivi,kuna watakao dhani unapoteza muda wako bure, na wengine tunao hapa barazani, siku zote wanakuja na majina tofauti lakini ni wazanzibari wenzetu kindakindaki na ni wale wale, ambao tutakuwa nao siku zote mpaka siku ya kupatikana visiwa hivi, au siku ya kiama, basi bado wao tutakuwa nao, na watakuwa na misimamo yao ile ile, ya lazima sisi tumtumikie mkoloni mpka dakika ya mwisho,na hii ndio demokrasia, sio watu wote tunaopenda kujitawala,wengine ni lazima watumwe,wateswe,wanyanyaswe,wakaripiwe,wabaguliwe,wabaguwe,watukanwe,wanyonywe,wapigwe au ikibidi hata wauliwe ndio waone raha.

  Usichoke ndugu yangu wala usivinjike moyo,kwani kama kuna mtu alidhania nchi hupatikana baada ya chukuzi za dhulma, sita au saba peke yake ana hiari yake,wengine tunajua, hii kazi ni ya kizazi kizima au viwili, yaani miaka mpaka mia mbili ikibidi,sisi inawezekana tusije kuiona Zanzibar iliyo huru,ya haki na ya watu wanopendana, lakini hilo au hiyo haina maana ndio tuanze kuvuta sigara, na kuacha kuitafuta Zanzibar na kuirudisha katika ramani na nafasi yake ilipokuwepo duniani.

  Mgogogro unaoendelea katika chama cha wananchi cuf,utaleta matatizo mengi kwa walio utengeneza mzozo huu,sio siku zote unapopandikiza mgogoro kuwa kuna uhakika wa kupata matokeop uliyoyakusudia,wasi wasi wangu kwa chama changu cha mapinduzi kwa wale walio husika kuupa baraka msuguano huu baina ya Maalim na Lipumba,ni vema nikawafahamisha kuwa huenda machafuko yatakayotokana na balaa hili yakawa nje ya uwezo wetu,Zanzibar kwa sasa panafukuta moshi,moto upo wa uhakika sasa ujanja wa Balozi na wenziwe unaweza kutuletea balaa la Rwanda,jee kuna mtu yeyote amekaa kitako akafikiri hilo au bado tunadhani sisi hatuwezi kufika huko kwa kuwa ccm wana DOLA.

  Shauri zetu, tunachezea moto na viwembe, tukitegemea woga utatusaidia kuepuka majaga,nimeusia sana huko nyuma, tukitaka tusitake Zanzibar iko salama kisiasa, kwa sababu Maalim bado utu alio nao unatusaidia,Odinga wa Kenya ilifika wakati aliamua,ndio maana waliuwana kiasi cha watu elfu mbili,baada ya maafa hayo ndipo walipoweza kukaa kitako wakaandika upya katiba ya nchi yao na kuanza kuheshimiana mpaka leo,kila jamii moja, inaiheshimu jamii nyingine,wamejua kuitafuta amani kwa matone.{sio maji}

  Sisi bado hatuheshimiani, kwa kuwa bado hatujatiana adabu,sasa kama ni lazima tufike huko, hayo ndio tunayosubiri, tusiseme WOGA ndio asili yetu,sisi USTAARABU ndio asili,sifa na utu wetu, ZANZIBAR haikusifika duniani bure,kulikuwa na wana nzuoni na watu wenye ilmu za kila aina,sasa tumejizamisha kwenye vyama vya siasa, mpaka tumesahau sisi ni watu gani,na tuna imani gani,sote tunapigania nchi ijitawale, na itawaliwe,sasa kama tuna woga,basi ni woga wa kuogopa kujitawala na ule wa kuogopa kumkosa mkoloni, hayo ndio makundi yetu,siku ikifika hatutoogopa kumuondoa TANGANYIKA katika ardhi hii kwa gharama yoyote ile, hili tulijue, historia ndivyo inavyotufundisha na kujirudia sasa kazi kwetu.

  Hatokatazwa mtu kumpenda mkoloni lakini tusilazimishane,wengi wape,mkataa wengi mchawi,umoja ni nguvu,usipowapa wenye nguvu, watachukua kwa nguvu zao,tuna misemo yetu mingi ya hekima ya kiswahili, sote tumesomeshwa na tunaijua, tutumie vichwa vyetu kujikumbusha, tutagundua jawabu ni rahisi na iko usoni mwetu inatusuta.

  Mapambano ndio kwanza yanaanza, ‘Aluta’ ndio inachanua na itakontinua.

  Nakushuru na kuwashukuru.

 5. shawnjr24 17/03/2017 kwa 12:19 mu ·

  Kuna haja ya Wazanzibari wanaoishi nje kurekodi audio au ujumbe wa maandishi za kuwapa darasa Wazanzibari juu ya kuipenda na kuilinda nchi yao. Na kuzisambaza kwenye whatsapp, Facebook na Instagram, njia hii itasaidia kufikisha ujumbe kwa Wazanzibari wengi. Sio kila mzanzibari anasoma mzalendo, mfano njia waliotumia Uamsho kuwaamsha watu kwa kufanya mikutano. Ujumbe wao ndio uliwafanya Wazanzibari wengi kuamka, ujumbe au audio utakaotumwa uwe wenye kuigusa nyoyo za wasikilizaji na kujua samani yao na nchi yao ilipo na inapopelekwa. Pia baadhi ya ujumbe utumike kuwa shuhulikia wasaliti. Mfano mpiganaji boxing kocha wake anamwambia mpige hapa hatochukua muda utamshinda. Kama ccm wameamua kutia wali mchanga kwanini na sisi tuwaachie wale mchuzi kwa mikate?? Kuna nukuu nyingi hapa zinasema Wazanzibari waoga hio mimi nakataa hakuna binaadamu muoga kwenye kutetea haki yake. Binafsi nishapigana na hao wabara na west Africans wengi tu na huwapiga sema kwa makelele na vitisho ndio vyao lakini ukiingia mwilini wanaanza kutafuta suluhu au hukimbia. Huwezi kumuachia mwanao kila siku apigwe shuleni na kumwambia asichokozeke wakati anaharibika kisaikolojia. Wakati wewe akikukosea nyumbani unaanza kumpiga mikwaju, kwanini na wewe usichokozeke ukamuachia tu. Hawa wasaliti ukiwaachia ndio watazidi kwasababu wanajua hawatoguswa ndio maana wanazidi kila kukicha. Na maisha yalivyo magumu hata kwa chakula cha mwezi wako tayari kuviangamiza visiwa vyao. Mtoto akikosea anahitaji mikwaju ili asirudie tena kosa lile lile.

Comments are now closed for this article.