KUSHAMBULIWA PADRI AMBROSE- SI DOGO, LAKINI ‘DAL-SEK-NED’!

Written by  //  28/12/2012  //  Makala/Tahariri  //  7 Comments

Enzi zile Zanzibar kuna Taarab, kikundi kimoja kiliwahi kuimba wimbo uitwao ‘Watende wao’. Katika wimbo huo mwimbaji anasema, ‘Watende wao kina mwafulani. Kitendo wenzao, kutwa midomoni’. Kisha mwimbaji anaendelea kwa kusema, ‘ajabu ya watu hao, ajabu yakini, ajabu yakini, ajabu ya hao, yao hawaoni’. Mwisho wa kunukuu.

Nalazimika kunukuu vipande hivi vya wimbo, baada ya tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya, padre Ambrose Mkenda jioni ya siku ya Krismasi, huko nyumbani kwake Tomondo.Nanukuu si kwa maana ya kuhalalisha kitendo alichofanyiwa padre kwani, si kitendo cha kiungwana wala cha kibinadamu. Na kwa hili naungana na watu wote kulaani kitendo hicho cha kinyama dhidi ya padri Mkenda.

Kama kuna msomaji anafuatilia makala zetu nyingi hapa katika mzalendo, ataona kuwa mara nyingi tunapigania usawa na haki ya Mzanzibari katika Muungano.Ya kwamba, Muungano uwepo au usiwepo, kwa nguvu moja tunasema haumtendei haki Mzanzibar, na hasa akiwa muislamu. Kwamba kosa lolote lenye udogo mithili ya mdudu chungu, ilhali amelifanya Mzanzibar-muislamu, hilo huwa ‘mwao’. Huwa m’boga, ukatambaa, usifike mwisho. Dogo hukuzwa, na kusemwa na wakubwa na wanene wa nchi.Likawa jambo likatuojea.

Ni kweli kabisa, kitendo cha kujeruhiwa vibaya kwa padre Mkenda, si cha kiungwana. Na bila shaka kinastahiki uchunguzi haraka wa Polisi. Na kwa sasa polisi ya Zanzibar, imeshafunguwa upelelezi kabambe juu ya tukio hilo. Naamini kwa jinsi tukio lilivyotokea, polisi Zanzibar inatosha kufuatilia na kuweza kutambua ukweli na undani wa tukio hilo. Hii ni kwa sababu tunaliamini jeshi la polisi juu ya upelelezi, na ufanisi wa kesi kama hizi.

Tumeona jinsi sayansi na teknolijia ilivyotumika kuwatia nguvuni wahusika wa vurugu za bubu zilizopelekea kuuwawa kwa askari polisi. Pilisi, ilifanya upelelzi wake, na tuliyaona waliyoyagundua. Na kwa hili pia hatuna shaka wanaliweza.
Cha ajabu, licha ya kuwa tukio lenyewe ni kubwa sana, sioni haja ya kuletwa tena makachero ‘waliobobea’ kutoka bora, kwa kile kinachoitwa ‘kuongeza nguvu’ juu ya tukio hili. Suali la kuletwa makachero wa bara, wakati hapa kwetu tuna kitengo maalum, chenye ujuzi na uzoefu wa upelelezi, kunanipa shaka nyingi sana kuliko imani ya utendaji wenyewe unaolengwa kuongeza ‘nguvu’ na ufanisi unaodaiwa.

Hofu yangu ya kwanza ni kwamba kwanini kitengo cha polisi cha upelelezi cha Zanzibar kiongezewe nguvu kutoka bara? Kwani kiliomba kusaidiwa, baada ya kuzidiwa na hali? Na upande wa pili ni pale ukijadili dhana ya kuongeza nguvu inapohitajika. Kiuozoefu tunaongezea nguvu pahala palipoonesha kuzidiwa na hali iliyopo. Jee hili lishajitokeza kuwa Jeshi la polisi limeshazidiwa na ufuatiliaji wa upelelezi wa kesi hii? Nahisi bado mapema kuomba msaada wa aina hii bado.

Upande mwengine, unaposema unaliongezea nguvu jeshi, tena kwa kuleta makachero ‘waliobobea’ kutoka bara, unamaanisha kuwa makachero waliopo hapa Zanzibar ni ‘vibwengo, vichamba umande, au vimasantula’ tu, visivyo na uzoefu. Na kama hivi ndivyo, nalazimika kuleta tena shaka nyengine ya kwanini nguvu hii iongezwe kwa kujeruhiwa padre Mkenda tu?
Alikamatwa Sheikh Farid, lakini kwa bahati mbaya si jeshi la polisi Zanzibar wala bara lilianza upelelezi wowote. Suali la Farid liliachwa kama alietekwa ni paka au mbuzi tu, na hata baada ya kuonekana aliishia kutiwa hatiani na kufungiwa rumande badala ya kuwatafuta waliomteka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kisa, ni Mzanzibari na muislamu.

Karibuni hivi alimwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soraga. Kwa sadfa ya tukio hili utaona Sheikh Soraga ni ‘mwenzao’. Kwa ufupi na lilipotokea la Soraga, kila kiongozi alipania kumuona kumjulia hali Sheikh. Kwa upande wa jeshi la polisi Zanzibar, waliapa kuanzisha upelelezi mkali dhidi ya kadhia hii. Kwa bahati mbaya tena, hatukuwasikia makachero wowote kutoka bara walioletwa kuja kupelelza kadhia ya soraga, na mpaka hii leo hatujui kesi hii ilipokomea.Au hili halikuhitaji kuongezewa nguvu?

Sambamba na haya, kuna matokeo chekea ya uhalifu nchini hapa ambayo yalipuuzwa kufuatiliwa na wala hayakuchukuliwa hatua zozote za kufaa. Cha ajabu, akijeruhiwa mtu wa kanisa hata kama alikuwa na ugomvi na watu wengine, kwa bahati mbaya au kwa maswali yao ya mipango binafsi basi hilo hufanywa kubwa. Na kuanzia hapo tunaanza kulipa ukubwa na kulizidisha mada na shadda, tukianzia na ni sisi Wazanzibari wenyewe.

Kwa mfano, mara tu baada ya tukio, taarifa ya awali ya polisi ilihusisha tukio hilo la ujambazi na uwezekano wa padre huyo kuwa na pesa alizozipata katika michango ya waumini siku hio ya krismasi. Kauli hii aliekimbilia kuitoa, inaonekana haikuwaridhisha wakubwa, na wakoloni wetu kwani haikutegemewa isukwe hivyo. Taarifa kama hii ilikuwa isukwe, kwa kuhusishwa waislamu na jumuiya ya uamsho. Hapo wenzetu na viongozi wetu wangeridhika, japo kuwa sio kweli.
Pia Balozi Seif Idd, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zanzibar kulikozesha tukio hili. Na ni kwa sababu ya kauli yake yeye ndie makachero ‘waliobobea’ wakaletwa. Na kwa wale wajuzi wa lugha wajue kuwa hii ‘kubobea’ hapa ni kuwa na ujuzi uliopindukia wa kuchonga, kuumba-umba na kuzua mambo yaliyokuwa ndiyo na yasiyokuayo. Ya kweli na ya uongo. Huo ndio ubobevu wenyewe.

Hofu yangu, kwanini iwe hivi, tena kwa matukio yawahusuyo watu Fulani tu kuwa yaonekane ndio wenye haki zaidi mbele ya sheria na akina Fulani wawe si chochote si lolote? Nakumbusha tena kuwa silioni dogo tukio la Padri Mkenda, lakini kwanini iwe kwa akina hawa tu? Nionavyo, kuna kijambo kinatafutwa hapa. Sio bure maana kama ni la upelelezi tu, hakukuwa na haja ya kulikozesha na kulitia madda na shadda kiasi hiki. Tutende haki, tukiamini watu wote wana haki sawa mbele ya sheria.
Natoa hoja

About the Author

Ni mwalimu kitaaluma ktk shule moja hapa mjini Unguja.

View all posts by

7 Comments on "KUSHAMBULIWA PADRI AMBROSE- SI DOGO, LAKINI ‘DAL-SEK-NED’!"

  1. Abdul 28/12/2012 at 10:51 um ·

    mfumo kristo na muungano kinacho tafutwa hapa ni agenda ya benard membe kusema kuwa juu ya jumuiya za kimataifa wazanzibar wanauwa wakrito ili kuzima nguvu na joto la wazanzibar juu ya mataifa ya njee

    sefu idi mungu anamuona na inshaalah atampa la kutokana na uwovu wake kwa waisilamu na uisilm

  2. pambanua 29/12/2012 at 7:02 mu ·

    MTU SI JIBWA

  3. salali 29/12/2012 at 8:19 mu ·

    Hawo ni Majini Subiani mpaka wawatowe watotowawo tena vipenzi ili waendelee kuupata ufalme wa duniani,wanalia sana kwa uchungu wa kuondokewa na mwana (lakini) hiyo yote danganya toto mchana usiku wanashereheka.Hapo inaonesha ni namna gani wa Tanganyika wanavyojaribu kuuhadaa ulimwengu wa kimataifa ili wapate sababu za kutuburuza zaidi kama mateka waliokutwa wamechoka katika vita, huwo ni mchezo umechezwa na usalama wa taifa kwa kushirikiana na vikosi vya hujuma vya ccm,mbwa mwitu,ubayaubaya, kisonge,kachororank ili wapate sababu ya kuendeleya kutuganda(Muungano) na kutuburuza wakati Dunia imesha elewa wa Zanzibari 66%wanataka mkataba.Eti kapigwa na bastola “ngogo” sindiozile bastola wanazowapa waendesha gari za ng”ombe ili kuhujumu Demokrasia Zanzibar” ” “……….

  4. Wamtambwe 29/12/2012 at 11:30 mu ·

    @shamhuna
    Tatizo kubwa tlilonalo ni wangu wanafiki kama nyinyi shamhuna. Yalipotokea kwa mashekhe kama wa uamsho wewe ndie uloandika mada Farid acha utoto. Kwanini hukusubiri ukafanywa horosho. Leo unakuja kutuambia eti waislamu wanaonewa. Wacha unafiki wako huo.

  5. Wamtambwe 29/12/2012 at 11:43 mu ·

    @shamhuna
    Tatizo kubwa tlilonalo ni wangu wanafiki kama nyinyi shamhuna. Yalipotokea kwa mashekhe kama wa uamsho wewe ndie uloandika mada Farid acha utoto. Kwanini hukusubiri ukafanywa upelelezi? Leo unakuja kutuambia eti waislamu wanaonewa. Wacha unafiki wako huo.
    Au ndio nyinyi mchana munaingia msikitini usiku kanisani? Mimi sikuelewi wewe kama ndie yule Shamhuna tunayemjua sisi, lakini komments zako zinatupa wasiwasi wengi humu mtandaoni

  6. mchongoma 29/12/2012 at 12:32 um ·

    Kunamsemo unasema:- USIJIGAMBE/USITAMBE UKAJIONA ETI LEO UNAKULA PILAU/BIRIYANI KWA KIJIKOO!! ANG’AZA LA KESHO NA KESHOKUTWA, UKIPOROMOKA? UTAKULA *BIYE NA CHOCHONI KWA MWIKOO!!!!!!!

    Nimesoma hadith sharif sahih inayoelezea hivi ifuatavyo:-HIBBUL AKHIYK KAMAA TUHIBBU LINAFSIKA.
    Tafsri yake:-MPENDE NDUGU YAKO KAMA UNAVOJIPENDA NAFSIYAKO.

    Neno *NDUGU* lililotajwa hapo juu; halikusudiwi kuwa ni yule ndugu yako wa tumbo moja au ayla/ukoo mmoja, bali kusudio lake kubwa limelenga kuwa waislamu woooote ni NDUGU MOJA.

    Kwa hivo ikiwa nyinyi baadhi ya Viongozi wetu wa ‘SMZ’ lengo lenu kubwa ni kuidamirisha na kuiteketeza/kuigharikisha/kuimaliza Zanzibar, waZanzibari, waIslamu na Uislamu kwa ujumla; kwa kutumia njama mbaya sana na visingizio vilivo ajabu ajabu kwa matumainio ya kuwafurahisha mabwana wenu kule Tanganyika/Ukokaland, kuzidi kuboresha utawala wa MKOLONI MWEUSI hapa Zanzibar na upembejeyaji/unyenyekevu wa kinyonge ili ubakishiwe “TONGE” yako na ulindiwe “KITUMBUWA” chako kisijekikakuponyoka ilal abad, ni mfano wa ndoto ya mchana!!. Mimi sidhani kuwa AZIMIO/”KHUTTAH” hii mulioiweka mbele yenu; yaani mulioipachika nyusoni mwenu itaweza kuzaa matunda au kuleta manufaa na sura nzuri hapa Zanzibar!! Khususan kwa KARNE hii tulionayo hivi sasa!! Kwani ukiangalia waZanzibari wa leo sio wale wajana na juzi, takriban sooote tumeshaamka na nijambo mustahil kwetu kuweza kutughilibu bisuhula au kutuchezea kama machezo wa TENNIS.

    Enyi Wazalendo wenzangu, waZanzibari wenzangu hadi tufahamu kuwa kutoka JUZI, JANA na hata HII LEO nikuwa Nchi yetu ya Zanzibar imeshageuzwa JAA/RUBBISH-HEAP/MUKHALLAFAT lakutupiwa kila aina ya “MAOVU”/”EVIL” tumesikia kwa masikio yetu na tumeshayaona kwa macho yetu, si-jambo lakuhadithiwa tukadhani kuwa kuna mtu anataka kuchocheya au kupachika/kutia FITNA BAINA YETU!! Dini dhidda ya Dini nyengine! kwani tunavojuwa tangu hizo enzi za UJAHILI hapa Zanzibar zipo Dini za kila ayna ambazo zinaabudiwa ni wahusika! na haijaweza kutokea khitlafu yeyote au uchokozi wowote baina ya Dini hizo tunazozifahamu sisi hapa petu!!. Sasa imefika wakati wakujiuliza baina yetu; kwanini UCHOKOZI, KHITLAFU na SUITAFAHAM ichomoze wakati huu mgumu tulionao wakudai kuikomboa Nchi yetu **Zanzibar**??

    Mimi nahisi kuwa hivi vitendo vinavotokea/vinavojitokeza haliyyan; yaani siku hizi!! leo kabla ya kesho? si-bure! lazima pananjama za siri zilizoazimiwa kufanywa ili kuudhofisha UMOJA WA waZANZIBARI uliopo hivi sasa hapa Zanzibar, kwa lile lile lengo la ujanja ujanja:- WAGAWANYE TUWATAWALE, kwa hivo nilazima na niwajibu wetu kuwa macho na tusikubali kudang’anywa!!

    Mwisho nawausia baadhi ya Viongozi wetu na nikijiusia nafsi yangu; kuwa MTOTO MCHANGA akilia au tuseme akililiya kitu? ni wajibu wa mzee wake kumchombeza au kumuangalia ni kipi kinachomliza! pengine ni mgonjwa, anajaa au aliliya kitu fulani akipendacho! allij matatizo ya mtoto kwanza; sio ukurupuke kwa ghadhab kwa sababu hupati usingizi, ukanza kumpiga/kumtandika makofi au bakora!!, mwisho wake utamfanya mtoto awe SUGU na hatimaye lawama na majuto yatakuangukia wewe mwenyewe!!!!

    NATONGOWA
    MCHONGOMA

  7. serelly 05/01/2013 at 7:00 mu ·

    @Watambwe.

    You are on the truth with the truth. Keep going

Comments are now closed for this article.