KITENDAWILI CHA KUJERUHIWA KWA PADRI ZANZIBAR

Written by  //  29/12/2012  //  Makala/Tahariri  //  3 Comments

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefika njia panda kutokana na matukio mabaya na ya ghafla yanayotokea hapa Zanzibar, hasa yanayobeba sura ya ‘hit and run attacks’ ambayo pia yanaingia katika sura ya visasi (revenge) — kuanzia lile la Soraga hadi la huyu Padri.

Kuna nadharia nyingi hapa zinazohusu uhalifu (theories on criminology) — au hata conspiracy theory.

Nadharia 1: hujuma inafanyika lakini hakuna clue/au hata alama ya namna uhalifu ulivyofanyika — hapa inakluwa taabu kwa wapelelezi kugundua namna ya ualifu huo ulivyofanyika, au vipi umefanyika, na hata kuanzia pa kufanya upelelezi.

Nadharia ya 2: Uhalifu umefanyika, aliyefanyiwa uhalifu yuko hai, na kauli thabit anaweza kusema. Hapa inakuwa rahisi sana sana kwa makachero kujua na kuanza upelekezi wa kina. Kesi zote mbili zilizotokea Zanzibar (Soraga na Padri zinaingia hapa).

Wote wazima na wote wana kauli thabit. Padri ameweza kuzungumza na kuweza kuidhalilisha POLISI kama taasisi pale alipotoa kauli yake kumpinga RPC Aziz.

Kauli ya Padri dhidi ya jeshi la polisi inaonyesha dhahir kuwa kanisa linataka watendewe vile wanavyotaka wao; na sio hali halisi ilivyo. Ingawa hakusema wazi wazi, lakini indirectly, ana maana ya kusema kuwa ‘polisi ni muongo, au waongo’. Hii ni idhalali kubwa kwa jeshi la polisi.

Kw auhakika ni kuwa padri huyu alikuwa anashika pesa, whether awe mhasibu by professional or not. Kwa uhakika 100% padri huyu ndiye signatory wao.

Bila yeye haitoki pesa. Je, na hili atalipinga. Naomba hao makachero wa kutajika kutoka Dar, waanzie hapa kama ndio ‘lead’ yao. Tumelewwana? Muanzie hapa. Je, haiwi kuwa ‘internal job’.

Angalia sequence za kihalifu zilizofanyika TZ karibuni:
i. Afisa wa kuzuia rushwa apigwa na kuuliwa na mwenzake Dar
ii. RPC Mwanza apigwa risasi na kuuliwa Mwanza.
iii. Pesa nyingi zimeibiwa duka la Dar (150m) — kitendawili mpaka leo???? Au kwa sababu hili limetokea Zanzibar. Achane kuwa bias!
iv. Kuna mauwaji mengi yametokea Dar during chrismas time, mzungu mmoja amenyongwa hotelini, na wengine kuuwawa kikatili …kimya! kimya!

Nadharia 3: Nadhani kanisa, CCM TZ na serikali zote zitafurahi sana kama report ya makachero hayo zitasema kuwa UAMSHO ndio waliofanya kosa hilo. Mimi naomba kuwasaidia kitu.

Mpaka sasa, ukweli ni kuwa, waislamu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hawajafikia level hiyo ya kutumia silaha au kuhujumu. Hili linajulikana na liko wazi. Kisocholojia, bora hata siasa Zanzibar zinaweza kuwa ni ‘problem’ kuliko hata dini.

Mimi naomba serikali ya JK, Shein na IGP Said Mwema muwe waangalifu sana na trend hii inayojitokeza. Mjaribu sana kuwa fair na wakweli – otherwise, mnaimaliza nchi hivi mnajiona. Your careless minds — JK, Shein, Mwema and others — inaweza kuleta bad feelings kwa waislamu ambayo wanaamini kuwa Zanzibar ni nchi yao na nchi ya kiislamu. Hivi JK kuoni fakhari kuwa hivyo, yaani Zanzibar ndio kama kigezo kwa dunia v.s Tanzania.

Kumbuka kuwa mnapewa pesa za bure na nchi za kiislamu kupeleka hajj waislamu (ni kupitia mgongo wa Uislamu wa Zanzibar, na sio Tabora au Singida n.k); then mnachagua wakereketwa kwenda huko Hajj na kuacha waumin wa kweli.

Chokochoko hizi za dini, na hasa ukiristo — hautoijenga TZ, ila itaivunja vunja viapande vipande – angalia secratian war — Northern Ireland, former Yugoslavia [Kosovo, Serbia n.] Iraq n.k.

Shein na JK mnakaa na kubabaishwa na washauri wenu; na hamtaki kutumia akili zenu mlizojaaliwa hata 0.01%. Hebu tafuteni ukweli wa mambo. Huu ndi ushauri w abure kutoka kwangu.

* Na balozi Seif Ali Iddi acha kuwa bias. Mbona hujaenda kumuona Fadhil Soraga mpaka leo? umeamua kwenda wewe na Mohammed Aboud kumuona Padri na aila yake na wafuasi wake.

* Naomba tena hao makachero waliokuja Zanzibar waanzie pale benki anapokwenda kuchukua ‘hela’ padri huyu ambaye pia ndiye signatory mkuu, benki xxxx! nendeni hapo mkaone transaction alizokuwa anazifanya padri huyo, na kama kuna bank reconciliation zinazokubalika — au shaghla baghala tu.

* Na kama je, hali ya makusanyo na matumizi ya kanisa hili yanaridhia financial regulations za Tanzania, Zanzibar na bank of Tanzania. Check …kama kuna a kind of money laundry hapo?

Kwa ufupi matukio haya bado yamebaki kuwa kitendawili (unresolved mystery).

About the Author

View all posts by

3 Comments on "KITENDAWILI CHA KUJERUHIWA KWA PADRI ZANZIBAR"

  1. abdisalum 29/12/2012 at 7:11 um ·

    Naomba tuelewe kuwa matukio kama haya sio mageni kabisa. Na hili halina shaka sana na matukio mengine ya robbery.

    1. Kuna jamaa alikuwa na duka pale Darajani makontena, akiitwa BAHAMAD, huyu alipigwa risasi na watu kama hao, walikuw ana vespa au pikipiki anaingia kwake Kijichi, in front of the gate — walimfyatuliwa risasi na kumuuwa hapo hapo, walichukua cash na kila kitu.

    2.Juzi tu, kuna mfanyabiashara mmoja ameuliwa kikatili hapa Zanzibar, nadhani maeneo ya Magaomeni/Mwanakwereke.

    3. Kuna wale miaka ya nyuma kidogo waliokuja (mmoja Mnyarwanda) na kuiba na kuuwa duka la kubadilishia pesa la Said Makka, Darajani — mchana kweupe! Na Mahita, ex-IGP siku hiyo alikuwepo pale Muzammil Store, Darajani —ah . what a coincidence???

    4. Kuna matukio mabaya zaidi ya hili, mahoteli yamevamiwa juzi tu huko Nungwi, Uroa, Kiwengwa na pale maeneo ya Bububu – inaitwa HAKUNA MATATA beach lodge.

    5. Kwa hesabu, 4Q ya mwisho ya mwaka huu 2012, matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na kuuwa ni mengi sana, yanazidi 100. Jumuiya ya ZATI wanaweka kumbukumbu ya uhalifu unaofanyiwa wawekezaji wa utalii hapa Zanzibar. Wanazo data na polisi wanazijua.

    6.Naomba polisi msilichukulie tukio kama special case. NO.NO. hili ni kama hayo mengine tu.
    Au kama nia ni kufitinisha Wazanzibari waombane hasa uislamu v.s christian — hilo jengine, lakini kama alivyosema mtoa mada, JK na Shein nchi iko mikononi mwenu, mtoe uamuzi wa maana na wa kweli – make no mistake kwa hili. Vyenginevyo wakiristo wameshasema eti kuwa na wao watalipiza kisasi, kisasi kipi, na kwa nani?

    Leo Padri anathubutu kumkana polisi, ana maana gani. Tukumbuke kuwa katika maelezo yake juzi na waandishi wa habari amekiri na kusema kuwa ‘aliiona pikipiki inamfuata kwa nyuma, sasa je, hakuweza kuisoma number yake’.

    Ameweza kuwa na kauli ya kulitusi jeshi la polisi, lakini ameshindwa kuwa na kauli na kujua na kusema ni pikipiki aina gani, na vipi? Naomba polisi pia waanzie hapa, aseme ukweli hii ni pikipiki gani, na kwa nini ilikuwa inamfuata? Itakavyokuwa padri huyu anajua nini alichokifanya na kinachoendelea, ila sasa anataka kupanda sumu, fitna na kusababisha mauwaji kwa waislamu wasiokuwa na hatia. Na Shein na JK watapiga vigelegele. Nyie amkeni akina JK na Shein??

    Athari nyengine hapa ni jeshi la polisi kwa miaka yote limekuwa bias, washabik, unprofessional, sasa haya ndio matokeo yake wanatakiwa waseme kile wasichokijua na kisichostahili – kwa sababu huko nyuma wamekuwa wanaabuni kesi dhidi ya wapinzani, na wlaifurahia hilo; sasa wanashindwa kutenda haki na kuonyesha ukweli. Muyaone….!

  2. mchongoma 29/12/2012 at 8:43 um ·

    A/Alaikum..Ahli Zinjibari.

    Kunamsemo unasema:-
    USITAMBE UKAJIONA ETI LEO UNAKULA PILAU/BIRIYANI KWA KIJIKOO!! ANG’AZA LA KESHO NA KESHOKUTWA, UKIPOROMOKA? UTAKULA *BIYE NA CHOCHONI KWA MWIKOO!!!!!!!

    Nimesoma hadith sharif sahih inayoelezea hivi ifuatavyo:-HIBBUL AKHIYK KAMAA TUHIBBU LINAFSIKA.
    Tafsri yake:-MPENDE NDUGU YAKO KAMA UNAVOJIPENDA NAFSIYAKO.

    Neno *NDUGU* lililotajwa hapo juu; halikusudiwi kuwa ni yule ndugu yako wa tumbo moja au ayla/ukoo mmoja, bali kusudio lake kubwa limelenga kuwa waislamu woooote ni NDUGU MOJA.

    Kwa hivo ikiwa nyinyi baadhi ya Viongozi wetu wa ‘SMZ’ lengo lenu kubwa ni kuidamirisha na kuiteketeza/kuigharikisha/kuimaliza Nchi/Dola ya Zanzibar, waZanzibari, waIslamu na Uislamu kwa ujumla; kwa kutumia njama mbaya sana na visingizio va ajabu ajabu kwa matumainio ya kuwafurahisha mabwana wenu kule Tanganyika/Ukokaland, kuzidi kuboresha utawala wa MKOLONI MWEUSI hapa Zanzibar na upembejeyaji/unyenyekevu wa kinyonge ili ubakishiwe “TONGE” yako na ulindiwe “KITUMBUWA” chako kisijekikakuponyoka ilal abad. Huu ni mfano wa ndoto ya mchana ambayo haiaguliki wala haithaminiki isipokuwa ni shamra shamra za IBLIS kujaribu kukurambisha ASALI iliyochanganyishwa na SUMU!!. Mimi sidhani kuwa AZIMIO/”KHUTTAH” hii mulioiweka akilini mwenu; yaani mulioipachika nyusoni mwenu itaweza kuzaa matunda au kuleta manufaa na sura nzuri hapa kwetu Zanzibar!! Khususan kwa KARNE hii tulionayo hivi sasa!! Kwani ukiangalia waZanzibari wa leo sio wale wajana na juzi, takriban sooote tumeshaamka na nijambo mustahil kwetu kuweza kutughilibu bisuhula au kutuchezea kama machezo wa TENNIS.

    Enyi Wazalendo wenzangu, waZanzibari wenzangu hadi tufahamu kuwa kutoka JUZI, JANA na hata HII LEO Nchi yetu ya Zanzibar imeshageuzwa JAA/RUBBISH-HEAP/MUKHALLAFAT lakutupiwa kila aina ya “MAOVU”/”EVIL” tumesikia kwa masikio yetu na tumeshayaona kwa macho yetu, si-jambo lakuhadithiwa tukadhani kuwa kuna mtu anataka kuchocheya au kupachika/kutia FITNA BAINA YETU!! Dini dhidda ya Dini nyengine! kwani tunavojuwa tangu hizo enzi za UJAHILI hapa Zanzibar zilikuwepo Dini za kila ayna ambazo zinaabudiwa ni wahusika! na nathubutu kusema kuwa haijaweza kutokea khitlafu yeyote au uchokozi wowote baina ya Dini hizo tunazozifahamu sisi hapa petu!!. Sasa iweje vitendo vya ukatili na ujambazi vishamiri hapa Visiwani kwa kila sa’a au dakika? Kwa kweli imefika wakati wakujiuliza baina yetu; kwanini UCHOKOZI, KHITLAFU na SUITAFAHAM ichomoze wakati huu mgumu tulionao wakudai kuikomboa Nchi yetu **Zanzibar**??

    Mimi nahisi kuwa hivi vitendo vinavotokea/vinavojitokeza haliyyan; yaani siku hizi!! leo kabla ya kesho? si-bure! lazima kuna vidudu mtu wamejichomeka wakiwa na njama za siri zilizoashiriwa/zilizoazimiwa kufanywa ili kuudhofisha UMOJA WA waZANZIBARI, AMANI NA UTULIVU uliopo hivi sasa hapa Zanzibar, kwa lile lile lengo la ujanja ujanja wao:- WAGAWANYE TUWATAWALE, kwa hivo nilazima na niwajibu wetu kuwa macho na tusikubali kudang’anywa na kutiwa vitanzi vya roho bila ya kutaka!!

    Mwisho nawausia baadhi ya Viongozi wetu na nikijiusia nafsi yangu; kuwa MTOTO MCHANGA akilia au tuseme akililiya kitu? ni wajibu wa mzee wake kumchombeza au kumuangalia ni kipi kinachomliza! pengine ni mgonjwa, anajaa au aliliya kitu fulani akipendacho! jaribu kutafuta ufumbuzi/solution, baadae allij matatizo ya mtoto kwanza; sio ukurupuke kwa ghadhab kwa sababu eti hupati usingizi!!, ukanza kumpiga/kumtandika makofi au bakora!!, mwisho wake utamfanya mtoto awe SUGU na kumtowa imani, hatimaye lawama na majuto yatakuangukia wewe mwenyewe!!!!

    Namalizia kwa hapa:- AN ANCHOR OF A SHIP IS ALWAYS AT SEA BUT NEVER LEARNS TO SWIM
    .
    NAWASILISHA
    MCHONGOMA

  3. makame silima 30/12/2012 at 9:15 um ·

    Mtowa Madaa

    Maada yako mzuri lakini tu ,tujuwe kuwa swala hili naungana mkono na wezangu wenye kusema kuwa halina tafauti na hayo ya ujambazi na matokeo ya kisiasa huko yuma.

    Lakini Hivi sasa Kanisa lenye ambalo lina Wachungaji wake takribani wote kutoka upande wa pili wa Muungano wana jaribu kuipaka Mavi zanzibar na watu wake kwa kuipakazia kidini ulimwenguni.

    Hii ndio kazi kubwa ya Kanisa Zanzibar kwa sasa wanayo ieneza Maskoffu Maskofu kuichafua Zanzibar kwa teknic ya udini,

    Hii imekuja baada ya mtikisiko mkubwa wa wananchi wa Zanzibar kudai kuwa Muungano uvunjike , Kwa upande wa Kanisa una vita vyake vya chini kwa chini zidi ya kueneza jina la Baba.

    ikiwa Muungano utavunjika Basi hofu ya Kanisa ambalo Wachungaji wake wakubwa ni wa upande wapili wa muungano watachindwa kulieneza jina la Baba ndani ya Zanzibar ambako wakaazi wake %99 ni wadini ya kislamu.

    Hii ndio hofu ya kanisa kwa sasa, na kitendo chochote kinacho ligusa Kanisa /Wachunga kiwe cha ujambazi ,kisiasa au wahuni basi wahanga huwa ni waislamu Zanzibar na hichi ndio kichiko wanachokwenda nacho ili waichafue Zanzibar na watu wake ulimwenguni.

    Na hali hii bado kwa viongozi wa Smz wanaipalilia kisiasa bila kujuwa mvua ikinyecha Wazanzibar na nchi yao wote watanyeshwea , tusome kutokana na nchi za kislamu zilizovamia kwa jina la uislamu na ugaidi vipi hali zake?.

    Kwa hio kanisa Zanzibar limeona halina sauti zidi ya wananchi wa Zanzibar na kuona viongozi wa kidini ya Uislamu Zanzibar wana sauti kubwa Zanzibar kuliko Serekali yenyewe.

    sasa kwa hali hio Kanisa sasa ina tumia mwanya wa udini ili kuiharibu Zanzibar na watu wake.

    Ndio waZanzibar sasa husema Kanisa ndio Muungano na Muungano ndio kanisa kutokana na kanisa kuchukuwa kila claim na kuitupia jamii ya kislamu na wao kujifanya victim wa udini wao.

    Wazanzibar tuwe na tahazari na chokochoko za Kanisa katoliki.

Comments are now closed for this article.