GOYA LA MZALENDO: ‘TUZIACHE SERIKALI NA KANISA ZITUHUJUMU’

Written by  //  30/12/2012  //  Makala/Tahariri  //  2 Comments

Wazungu wana msemo wao usemao, ‘ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya’.Cha kushangaza basi, katika uzoefu wa maisha ya mwanadamu si mara nyingi falsafa na ukweli uliomo katika methali kutumika kama faslafa ya nchi au taifa fulani. Lakini kwa sababu moja au nyengine, kuna misemo miwili mitatu hivi inaonekana kutoishia kuwa misemo tu bali imekuwa kama fasalafa inayoongoza maisha na malengo ya watu hapa duniani.

Kwa mfano, msemo mkongwe wa Wazungu utafsirikao kama ‘wagawe, uwatawale’ umetumika ipasavyo katika kuzitawala nchi na jumuiya mbali mbali duniani. Waingereza waliweza kuitawala dunia kwa msemo huu. Na wamarekani wameweza kufanya watakalo duniani kwa falsafa hii. Pia watanganyika wameweza kuitawala Zanzibar kimabavu kwa fasalafa hii pia. Wametugawa na kututawala.

Wakati hubadilisha mambo. Kwa muda wa mosi zipatazo sita (six decades), tangu uhuru, falsafa hii imekuwa ikifichwa kutumiwa kwake. Inafichwa sio kama haipo, ipo lakini dunia ya sasa ya utandawazi na haki za binaadamu, falsafa hii haipati nguvu ya kutembea utupu hadaharani tena kama ilivyokuwa mwanzo. Na kwa vile silaha hii imekwisha nguvu, tumeletewa silaha nyengine isemayo, ‘Ukitaka kumuuwa mbwa, mpe jina baya!’
Zanzibar, katika ramani ya siasa za dunia imekuwa ikifanyiwa kila bidii na njama ili iwe sawa na Palestina na mataifa mengine ya kiislamu yaliyoharibiwa na mayahudi na masara kupitia mataifa yao makubwa.Yaani Zanzibar inatakiwa isiwe na utaifa wala utambulisho wowote. Na hilo lilikuwa karibu mno kufanikiwa. Lakini kabla ya kufikia hatua hio, wazanzibari wameamka.

Wakaanza kudai haki zao. Na kwa vile wanzanzibari hawalengwi wala kuthibitikiwa na kuwa na haki ya kudai chao, pao, lao, wala ya kwao, hili limekuwa kosa. Sasa tunaitwa kila jina baya ili kuhalalisha kuangamizwa kwetu.Tunaitwa magaidi na waislamu wenye msimamo mkali. Tunaitwa hivi katika kipindi ambacho dunia imejengwa iamini kila Muislamu ni adui asie na haki ya kuishi katika mgongo wa dunia hii.

Kwa kusherehesha mjadala huu, katika siku za hivi makaribuni, Zanzibar imekuwa ikiharibiwa sifa na jina lake kwa maksudi na vyombo vitatu. Kwanza, kanisa ambalo limekuja Zanzibar sio kwa kufanya Ibada, bali kuifitinisha Zanzibar mbele ya jamii za Kimataifa. Kanisa lilikuwapo Zanzibar tangu na kabla ya kuja kwa Edward Steere hapa Zanzibar.

Kulikuwa kimya ilhali waislmu walikuwepo tena na wasomi wakubwa wa Enzi hizo wakiwa hai hapa Zanzibar. Ilikuwa kimya na wala hakukuwa na Mzanzibari aliewahi kuingilia uhuru wa kuabudu kwa wana kanisa. Na hivi ndivyo ilivyo mpaka leo. Zanzibar ni nchi pekee duniani iliyo na ustahamilivu mkubwa wa kidini (Religious tolerance) kuliko nchi yoyote.

Kwa vile wanaonekana Wazanzibari hawapendi ugomvi na wenzao wa kikristo, la kufanya ni kuwapachika kila aina ya sifa mbovu ili kuwachafua, hata kama hawamchokozi mtu. Kanisa, Zanzibar hufanya kila liwezalo, kuhakisha wanawakorofisha waislamu ili wajibu mapigo, wawaharabie sifa na malengo yao yatimie.
Hili lilishindikana na sasa kuna njama za maksudi za kufanya matukio yao weneyewe kama vile kutia moto baa, makanisa yao, na hata kujeruhiana na kisha wakasingizia waislamu wa Zanzibar ambao wengi wao, hawana habari na wakristo waliopo. Wazanzibari wa sasa wametiwa dhiki za maisha kiasi kwamba hata hizo sala tano ni shida kuzisimamisha, seuze kugombana na kanisa.

Chombo cha pili ni Serikali, ambayo ili kulinda maslahi ya Muungano, imeifanya Zanzibar kuwa ni eneo la hatari kidini na kisiasa. Na bila kujua athari ya maneno wanayosema mbele ya jamii za kimataifa, serikali imethubutu kuitangazia dunia kuwa Zanzibar kuna magaidi na wanaharakati wa kiislamu wenye msimamo mkali.
Huu ni ubaya ulio dhahiri wa Serikali dhidi ya wananchi wake wenyewe. Serikali haitambui kuwa kufanya hivi sio kuharibu taswira ya Zanzibar na waislamu tu, bali hata nchi nzima, na shuhuli nyingi za kiuchumi, lakini nani anafikiri hayo. Tupo kisiasa zaidi.

Taasisi ya tatu, mayahudi na manasara ambao kazi yao ni kuleta fitina katika ardhi hasa hasa ardhi za kiislamu. Watu hawa ambao wengi ni wazungu, huja hapa kama watalii na baadae kuanza kupanga hujuma na mitandao ya fitina zisizomithilika dhidi ya waislamu. Baada ya hujuma zao hizo kutimia ndio utaona wanatumia vyombo vya habari kuitangazia dunia kuwa Zanzibar kuna ‘ugaidi’ Waislmu wanawaonea wakrsito. Hii ni fitna tu.

Zanzibar hakuna lolote kati ya hayo wanayoyataja na cha kushangaza hakuna kiongozi wetu hata mmoja anaekanusha upuuzi, na kasumba hizi. Leo hii wazungu ndio wanaoongoza kwa kutembea uchi hapa Zanzibar. Waislamu wako kimya. Wao wapo hapa pia kuishwishi nchi hii ikubali ndoa za mashoga. Mambo ambayo huko kwao yameshawashinda, wanatuletea sisi huku.

Wazungu ndio walioleta nakama ya mahoteli, kuigiza na kuingiza mikanda ya ngono, na ndio wanaojazana hapa mwezi wa Ramadhani kuja kula mchana barabarani ili kuwaudhi waislamu. Hakuna anaesema. Tunafanyiwa maudhi na karaha ndani ya nchi yetu, bila kuheshimu mila na desturi za nchi yetu. Ukisema Serikalini unajibiwa, ‘Serikali haina dini’.

Wanzanzibari tumekuwa watumwa, watwana katika nchi yetu kwa wageni wajao kwetu. Na bahati mbaya waislamu wakisimama kudai haya, Serikali husimama kidedea kuwalaani Waislamu na kuwahujumu kupita kiasi. Serikali haijali wala kutambua kuwa katika nchi kama Zanzibar ambapo waislamu ni wengi, mila na desturi za waislamu hao hazina budi kulindwa na kuheshimiwa na kila mtu, licha ya kuwa seraikali haina dini, lakini viongozi wanayo dini.

Goya langu wiki juu ya hili ni kwamba Wazanzibar tunyamaze kimya. Tuwaache wakrsito watufanye watakavyo. Tukae kimya tuiache Seriakli iwalee wakristo kama watoto wao vipenzi na sisi waislamu tubakie kama watoto wa kambo, watumwa wa bwana au punda wa dobi. Tuache Serikali iruhusu wazungu kutembea uchi, kula mchana Ramadhani, na hata kuingiliana nje hadahara nnasi, achilia mbali kulewa hadharani.

Wazanzibari tuwaache, wazungu walindwe na Serikali. Waingie miskitini kupiga picha, wajisaidie humo na walale itikafu na vichuupi vyao humo. Kama hawajafanya watafanya muda si mrefu. Wazanzibari tusidai haki zetu, tuwaache wa Muungano wafanye watakavyo kwani sisi kwao hatuna thamani.

Thamani yetu ni wakati wa Uchaguzi tu, ambapo hutugawa tukawa kivyama zaidi kuliko dini zetu. Wakati wa siasi hutuita CUF na CCM. Hapo tukawachaguwa. Tukishakuwachaguwa, sasa hutuita Wazanzibari, waislamu wenye msimamo mkali. Hapana cha U-CUF wala U-CCM tena hapo. Kianchoffata ni mateso na dhiki, na tunayapata sote, wa vyama vyote, Unguja na Pemba.

Wazanzibari tulinyekee kanisa na tuwapambe maaskofu kwa mauwa. Tukiwaona njiani tulale chini tugare gare sote, maana tukisimama wanazweza wakashambuliwa ikawa sisi ndio wahusika. Wazanzibari tushukuru Mungu, tukae kimya huku taifa letu na dini yetu ikiangamizwa kama ilivyoangamizwa Somalia, ikafitinishwa Sudan na kugawiwa, na hatimae bara Arabu pia.

Tusubiri tuwe wapalestina katika nchi yetu wenyewe. Kwa kufanya hivi tutawaridhisha mabwana zetu kanisa, wazungu, na Serikali yetu isyo dini. Tukumbuke tu Allah Subhana wataala amesema, ‘Hawatakubali mayahudi na manasara, hadi muwafate nyendo zao’. Basi natuwafate wao tumuache Mola wetu mtukufu
Nauka na goya langu!

About the Author

View all posts by

2 Comments on "GOYA LA MZALENDO: ‘TUZIACHE SERIKALI NA KANISA ZITUHUJUMU’"

  1. Abdul 30/12/2012 at 8:35 um ·

    goyaa nimelifahamu sasa wacha tuende ila viongozi wetu ni mdobwedooooo

  2. Vizuke 08/01/2013 at 10:44 mu ·

    Hongera kwa goya hili. Kama watalipata hao Serikali basi watakuna vichwa kidogo.

    Tanganyika ni nchi kubwa ambayo sasa inatutawala, utawala wao ni ule wa hadithi ya watu waliochanganya mbuzi 1 kwa mbuzi 99 ili ati wawepo mbuzi mia (100) wa ushirika! haingii akilini, ilikuwa ni janja ya mwenye mbuzi 99 kumnyang’anya mwenye mbuzi 1 ili asiwe na kitu. Ndicho kinachoendel;ea sasa kwenye muungano huu.

    Tupigane mpaka dakika ya mwisho ili tutoke na mbuzi wetu 1, huyu atazaa na tutakuwa nao wengi.

    Tumesha amka, Zanzibar kwanza.

Comments are now closed for this article.