CUF MNAELEKEA WAPI JAMANI?

Written by  //  22/04/2017  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 4

TAFAKURI YA BABU.
CUF MNAELEKEA WAPI JAMANI?

Said Miraaj Abdulla

Huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuhusu mgogoro unaoendelea katika chama cha CUF na nikatanabahisha juu ya tabia ya kutukanana na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe na athari zinazoweza kutokea.

Bila ya kujali nani kafanya nini, baada ya tukio lililotokea leo la kushambuliwa waandishi wa habari, kupigwa watu kadhaa na wengine kujeruhiwa ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mali; KWA MTAZAMO WANGU sasa wakati umefika wa kufanyika yafuatayo:-

Viongozi wa CUF na wanachama wake watafakari kwa kina madhara ya mbegu wanayoipanda kwa chama chao, katika jamii, katika tasnia ya siasa na hata kwa wao wenyewe binafsi kama mtu mmoja mmoja na familia zao.
Viongozi wa juu wa CFU wanaoongoza pande zinazo kinzana wakemee kwa dhati tena hadharani tabia hizi ovu na kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu wakati wakitafuta haki ya kila upande huko mahakamani, tena bila kushutumiana.

Mahakama iharakishe kusikiliza mashauri ya CUF na kutolea maamuzi ya haki tena kwa uadilifu mkubwa ili mwenye haki ya ushindi afanye shughuli zake za kisiasa kwa salama na atakaeona kuwa upande ulioshinda hawezi kufanya nao kazi atafute pahala pengine pa kufanyia siasa, na huo ni uugwana tosha.

Wazee wa CUF wasio na upande katika mgogoro huu wakishirikiana na viongozi wa dini wanaoheshimika na kukubaliwa na pande zote mbili kuingilia kati mgogoro huu kwa maslahi ya taasisi hio na umma kwa ujumla.
Viongozi wa CUF wapunguze jazba na kiburi wakubali mapatano ya kusimamisha mapigano na kuongezeka kwa hasama miongoni mwao, kwa kuvumiliana huku wakiendelea na shauri lao mahakamani.

Kwa kua makundi yote mawili yameamua kila uchao kutumia vyombo vya habari kama ni ngao au silaha dhidi ya propaganda zao za kisiasa, nawaomba Ndugu zangu Waandishi wa habari waache kuandika habari zozote za choko choko, kashfa au dharau kutoka upande mmoja dhidi ya mwengine miongoni mwa wanachama wa chama hiki, na badala yake wajikite katika kuandika habari za maendeleo ya chama hiki kama zipo, ikiwa ni pamoja na kusaidia kupunguza mgogoro huu kwa kuonyesha njia ya kuufanya umalizike kwa amani.

Ili kurejesha imani ya viongozi wa vyama vya siasa na heshima ya ofisi ya Msajili wa vyama Vya siasa kama chombo muhimu kwa mahusiano ya kisiasa, mapatano, maridhiano, ujenzi wa demokrasia na kuvumiliana katika nchi yetu na kwakua Msajili binafsi amekua sehemu ya mgogoro huu na ana tuhuma dhidi ya uaminifu na uadilifu wa utendaji wake katika mahakama na anapaswa kujitetea kwa jambo hilo, ni wazi kwamba analazimika kuwa na maslahi binafsi katika kesi hii na kulazimika kushirikiana na upande anao tuhumiwa nao kwa pamoja jambo ambalo kwa kwawaida tuu haliwezi kumfanya tena kutoa maamuzi yoyote na kuaminiwa kuwa ni ya haki kuhusiana na chama hiki kikongwe na chenye nguvu za kisiasa katika bunge kwa mtazamo wa haki, hivyo ni vyema kwa Jaji Mutungi kuacha kutoa maamuzi yoyote kuhusiana na chama hiki kwa sasa na pia kujitazama upya katika nafasi yake aliyokabidhiwa na Rais.

Kadhalika ni wakati sasa wa Waziri Mkuu ambae ofisi ya Msajili iko chini ya dhamana yake kwa hekima na busara kubwa kutoa muongozo kwa ofisi hio na pia jeshi la Polisi nchini kuwa waangalifu na waadilifu katika kushughulikia jambo hili la CUF kabla na baada ya maamuzi ya Mahakama ili kuzuia uvunjifu wa amani na umwagaji wadamu unaoendelea na usiojuilikana mwisho wake katika chama cha CUF.
TUTAFAKARI PAMOJA.

FB

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 4 katika "CUF MNAELEKEA WAPI JAMANI?"

 1. stonetown 22/04/2017 kwa 6:45 um ·

  Huyu Said Miraji hana mpya ni kibaraka kama kibaraka mwengine tu

 2. Mrfroasty (Ufundi) 22/04/2017 kwa 8:31 um ·

  Mie nilidhani itakuwa ni somo hata kwa wale mazombi, wananchi lazima waoneshe ukakamavu wa kujihami wanapovamiwa na vikundi vya watu wachache wakivaa soksi/ninja.

  Niseme ukweli naunga mkono mawazo ya kujihami, isiwe ni rahisi rahisi tuu kwa kikundi fulani kuamua kuvamia wengine halafu watu wakaendelea kuwa watulivu.

 3. rasmi 23/04/2017 kwa 4:51 um ·

  Kujitoa fahamu. Suala lilikua liwe CCM wanatupeleka wapi? Tuseme mwandishi hajui ni nani mtengenezaji wa huu unaoitwa ‘mgogoro!’
  Ukipanda tegemea kuvuna ulichopanda…

 4. zamko 26/04/2017 kwa 10:56 mu ·

  Wazalendo

  ahsanteni kwa Mchango weni

  Mimi suali langu ninalomuuliza huyu MIRAJI

  Hivo Ndio bado hajuwi kama Mgogoro wa CUF hautoki ndani ya CUF bali ni kutoka CCM?

  Nakumtafuta Gaidi Mmoja wa Kitanganyika LIPUMBa wakampandikiza humo ndani ili awababaishe watu Wajinga kama huyu Saidi Miraji kwamba mgogoro huu ni wa Ndani ya Chama cha CUF.

  Hata hivo mimi naweza kukubaliana na maneno ya Sefu Ali Iddi Balozi wa Tanganyika Nchini Zanzibar. Pale aliposema Maalim ni Bwege ndio anaibiwa, usemi wake unafanana sana na huu ukimya na uzembe wa CUF kutokuwa na mikakati kabambe sasa yakupambana sawa sawa na Maaduwi zao.

  Ikiwa ni mahakama tayari CUf wameshapeleka kesi zao Mahakamani mara ngapi?

  nini kilichoamuliwa na mahakama? Hakuna kitu kwasababiu Mahakama zimetawaliwa na CCM, Utanganyika na Ukristo.

  Hata hivo nathubutu kusema kwamba Wakolini zetu kumbe wengi wao wako imara kwa kufanya Ujambazi tuu lakini sio kujihami au kumshuhulikia Jambazi kama huyu.Kama sio Mabwege huu tuite nini?

  Matokeo yapatayo 20 ya Uharamia yameshafanywa na Lipumba akisaidiwa na CCM, Media za Tanganyika na Zanzibar zinayajua hayo lakini wanaogopa kusema ukweli au wana pendelea upande mmoja wa shilingi. Yote haya yanatokea na CUF bado na wao wakishindwa kufanya mipango ya kujihami kwanza na baadae ndio mahakamani.

  Strategy yao yakutumia Mahakama za CCM tuu au kufunga mikono ku- Condemed mavamizi na ushenzi huo unaofanywa na watu wa Lipumba haitaipeleka CUF kunyakuwa Serikali au Viti vya ushindi ifikapo 2020?

  Kwasababu hawakujipanga au kusoma katika matokeo yaliotokea kwenye Mkutano wa Buguruni?

  Na uzembe huu unafanywa na hata viongozi wa CUF wa Zanzibar, na ndio maana LIPUMBA na MUTUNGI anaendelea ku-Dunda kama anavodunda MDUDU JECHA SALUMU JECHA?

  Hii yote ni kutoa ushahidi wa kutosha kama CUF sio Imara na wala haina Mipango yoyote ya Kimaendeleo au kuwaletea Wananchi wake Matumaini badala ya Uzembe.Hata hivo Mipango hii yote mimi nasema imefanywa na KANISA Linaloongozwa na SEriklai ya CCM Tanganyika.

  Ili Wawahujumu Wananchi Wasio Hatia hasa Wazanzibari na madai yao ya ushindi wa uchaguzi wa 2015. Kwasababu kama Ni Kufukuzwa Uwanachama Kiongozi wa Vyama vya Upinzani imeshawahi kutokea mara nyingi katika vyama vyengine. Kwanini iwe Kioja kufukuzwa Lipumba CUF?
  Mbona Dr Slaa amefukuzwa CHADEMA, lakini hatujasikia hata siku Moja CCM kumtumilia Slaa Mkatoloki Mwenzao Kuwahujumu Wakatoliki au Wakristo?
  kwasababu Mfumo wa Siasa na Muhimili wa Dola ni Wao.

  Hivo Wanatumiliwa Waislamu ( Alhaji) Lipumba na Vibaraka wengine Kuwahujumu Wazanzibari na Haki Yao. Na hili lisingefanywa ila linafanywa kwa Kukamilisha Ajenda ya KANISA..
  Kwamba Zanzibar ifikapo 2025-2035 Iwe ishakuwa Tarafa la Tanganyika.

  Jamani Viongozi wa CUF jifunzeni kutoka KENYA, Wapinzani tayari Wameshapata TUME ya Uchaguzi Mpya. Na Kama Lipumba, Jecha, Mutungi, Ndoo, au hili jambazi lilokamatwa hapo nakufanyiwa duwara . kama lingekuwa limekamatwa Zanzibar hasa Pemba.

  Basi lisingeondoka na Miguu miwili, lingekatwa miguu likakoma kuja kuvamia watu wasio hatia na kuwahujumu kwa interest zao za kushiba matumbo yao.

Comments are now closed for this article.