CUF ISIKUBALI TENA KUFANYWA ‘KUKU LALA LALA’ NA CCM

Written by  //  14/11/2015  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 7

bw-jecha-salim-jecha-mwenyekiti-wa-tume-ya-uchaguzi-zanzibar

Kwa kila mtu anayefuatilia sakata la uchaguzi wa Zanzibar la tarehe 25 mwaka huu, awe wa ndani au wa nje bila shaka anajua fika kuwa kuna usanii mkubwa na kuonana wapumbavu kuliko pitiliza viasi kunakofanywa na CCM na tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia mwenyekiti wake Jecha wa Jecha.

Katika uchaguzi huo ambao ulimalizika kwa CUF kuigaragaza CCM kifo cha mende, kiasi ambacho kila binadamu aliye juu ya mgongo wa dunia hii ameona na kukiri yaliyotokea inasikitisha sana kuona kuwa nchi yetu inayojitapa kwa kuwa na utawala wa kidemokrasia na utawala wa sheria ikianzisha machafuko yasiyo na haja tena kwa sababu tu za ubinafsi na uchoyo wa madaraka.

Machafuko hayo yalikuja baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar bila kuwa na mamlaka yeyote kisheria na kikatiba kwa kuchukua hatua ya kuuvunja na kuufuta uchaguzi huo wa Zanzibar na matokeo yote ilhali ameshatangaza matokeo ya majimbo 31 (70%) kati ya 54 ya Unguja na Pemba kwa kisingizio kuwa uchaguzi huo ulikuwa batili.

Mataifa na taasisi za nje na ndani zimeshuhudia aibu hii ya kukiukwa kwa sheria na demokrasia lakini kwa vile CCM wanaona wana hati miliki ya nchi hii, hawaoni haya wala aibu ya kufanya vyovyote wakijua hakuna UN/USA/UK wala EU wa kuwaingilia kati kwa hili.

Kwa hakika uamuzi wa Jecha haukuwa na mashiko ila ulitokana na shindikizo la CCM na hasa hasa kutoka kwa makamo wa pili wa Rais Balozi Sembulike Ndunde Ndamba (Balozi Seif Ali Idd anavyojiita) na wenzake kwa kuwa wana uhakika hakuna mtu wala kichungu cha watu wa kuwawajibisha kwa lolote lile wanalofanya. Na kwa kuwa wana imani hiyo tayari, ndio wakafanya watakalo.

Kwa asiyejua, CCM wanalotaka ni kurejewa kwa uchaguzi wakijua wazi kuwa watatumia nguvu watakazo na jeuri zao zilizopitiliza kuhakikisha CUF haishindi kwa gharama yeyote. Ifahamike kuwa, iwapo uchaguzi wa Zanzibar utaendeshwa kwa misingi ya haki, CCM haiwezi kushinda hata ingekuwa mawakala wao wote ni Juja wa Maajuja. Wangeshindwa kama walivyoshindwa zamu hii au zaidi. Na hilo wote wanalitambua.

Wakati CCM ikilazimisha kurudiwa uchaguzi kwa kile ikionacho kuwa hakuna mwenye haki zaidi ya kutawala nchi hii zaidi ya CCM, kuna kila dalili kwamba Wazanzibari wamechoka sana madhila ya CCM inayoendelea kuwachuuza na kuwakaandamiza kwa misingi ya Uunguja na Upemba ilhali wakiacha neema zote zikifunikia bara kwa mwavuli wa Muungano.

Ukweli ni kwamba, CCM haiwezi kushinda chochote Unguja na Pemba kwa haki. Na kwa kuwa uchaguzi wa zamu hii ulisimimamiwa kwa misingi ya haki na uwazi, walipoteza kiasi ambacho hawakuweza kuamini kabisa kile kichotokea. Hawakuamini, sio kwa kuwa wana tamaa ya ushindi, ila kwa kuwa njama na makununu yao ya wizi yalifikia ukingoni wakashindwa kuchakachua.

Na kwa magube na magumashi ndio njia yao pekee ya kujipatia kile wakiitacho; ‘Ushindi wa Kishindo’ na bahati mbaya mara hii wamekosa, wanafanya liwezekanalo – ima faima, kuvunja sharia na katiba na yote watayafanya na ikibidi, vifaru na bunduki zishaletwa za kuwauwa wazanzibari wote watakaosimama kudai haki yao, mradi tu wabakie madarakani hata ikiwa hatuwataki hata kuwaona.

Ninachoiomba CUF na washirika wao UKAWA, wasikubali tena kufanywa KUKU lala lala mara hii. Tumeona nini kimetokea 1995, 2000, 2005, na 2010. Ni wizi na dhulma na hatimaye wazanzibari wamepitia miaka yote ishirini isiyo na maendeleo yeyote zaidi ya porojo za kisiasa za mabavu. Nasema wazanzibari wamechoka. Wamechoka kwa maana ya kuchoka na majibu yao yanaonekana kwenye matokeo ya kura halali ya mara hii.

Kuna ushahidi usio chenga kuwa CCM hawana nia ya kuiachia nchi hii kwa gharama yeyote. Kwa hivyo, naiomba sana CUF, chonde chonde, isijekubali tena uchaguzi urudiwe. Itakuwa aibu na kashfa zaidi. Kama CUF inakimbia watu kufa hapa kwetu, ikikubali tena kwenda uchaguzini, watu watauliwa kama kawaida.

Na kwa kuwa Serikali ya Magufuli ishasimama, tena kwa kura zile zile haramu za Zanzibar ambazo Jecha na Bosi wake Sembulike wameona hazifai kumpa ushindi Maalim Seif. Kutimiza azma yao ya kutawala kwa mabavu, CCM italeta wamakonde na waluguru wote Zanzibar kuja kuvoti hapa. Na CUF wakihoji madudu yanayofanywa kwenye vituo vya kupigia kura, wataishia kupigwa risasi na hakuna litakalokuwa!

Iwapo uchaguzi huo haramu na batili kwa maana zote za kisheria na kikatiba utafanyika na CUF ikashiriki, itashindwa ushindi wa kimbunga. Tutaishia kuimbiwa ule wimbo wa CCM usemao ‘Wembe kuliko Ule’ na matusi ya Kisonge ya wamakonde na waluguru wanaoishi Unguja kwa kugaiwa ruzuku na CCM kwa kazi yao nzuri ya kufanya fitina na ufujifu wa amani visiwani.

Nasema kwa msisitizo kuwa CUF isikubali uchaguzi urudiwe, kwa kuwa CUF ina tabia ya kujiamini sana. Kwa mfano, uongezwaji wa majimbo Unguja ulifanywa makusudi kuipa CCM ushindi. Tukawaomba CUF waukatae lakini wakakubali wakisema kashata unavyoikata huzidi utamu. Mungu akajalia wakashinda majimbo 27. Lakini kila siku si ijumaa. Nasema Kwa hili wasije wakajaribu kucheza BINGO wakasema natuvoti tena. Kufanya hivyo ni kuhalalisha kilichobatili na haramu. Ni kosa la jinai.

Ifahamike kwamba CCM wanachokifanya sasa ni danganya toto na mchezo wa kuku lala lala tu. Hoja zao na maamuzi yao ni batili. Na batili na haiwezi kupata uhalali kwa kuiunga mkono au kuikubali kwa busara na hekima ya eti ‘liingialo mjini si haramu!’.

Kwa hili mara hii, nasema tena kwa upana wa kinywa changu; CUF na UKAWA wasikubali tena kabisa kurudiwa kwa Uchaguzi kwa gharama yeyote kwani kufanya hivyo ni kuunga mkono batili na haramu ya tume ya Uchaguzi na SMZ ambayo haina mamlaka yeyote ya kufanya maamuzi waliyoyafanya ya kufuta uchaguzi na matokeo yake. Batili ni batili tu.

Kwa maana hiyo, ni busara zaidi kuwaachia CCM wakaendeleza uhuni na ubabe wao wa kuitawala Zanzibar kimabavu kuliko CUF na UKAWA kuwaunga mkono kwa dhulma yao hii kwa kushiriki uchaguzi. Waliozoea kudhulumu watadhulumu milele. Na sifa ya madhalimu hawajui dhambi wala thawabu. Wanachojua ni kutimiza malengo yao tu. Itakuwa ni kosa la jinai iwapo CUF na UKAWA watafikia maamuzi yeyote yale yatayounga mkono kurudiwa kwa Uchaguzi huu ambao si halali kisheria na kikatiba.

Natoa wito na mbiu ya mgambo, CUF na UKAWA simameni kidedea kuidai haki ya wananchi waliowapa imani na kuwachagua. Mkishindwa kwa kuzidiwa nguvu na dola la madikteta, umma utawaelewa na kuwaheshimu kwa juhudi zenu za kupinga dhulma na batili ya CCM nchini na hamtahesabiwa kuwa sehemu ya madhalimu walioipiga mnada nchi yetu kwa kuikalia kidikteta siku zote.
Na historia itawakumbuka kwa hilo. Fungeni mkanda, na sisi tuko tayari kwa lolote lakini msituletee kabisa, msamiati wa kuku lala lala; ‘ETI uchaguzi urudiwe!’ Mtakuwa mmefanya ujuha wa Alinacha! Haramu itabakia kuwa haramu na batili itakuwa batili hata ikipambwa kwa johari na yakuti!
CUF/UKAWA Daima mbele! Peoples power first!

Kuhusu Mtunzi

I am particularly interested in combining photography with graphic design to communicate the message of the peace to a specific audience.

View all posts by

Maoni 7 katika "CUF ISIKUBALI TENA KUFANYWA ‘KUKU LALA LALA’ NA CCM"

 1. Mrfroasty (Ufundi) 14/11/2015 kwa 7:52 um ·

  Watu wajiandae kisaikolojia juu ya hatua watazo chukua siku Jecha na genge lake watapoamua kutanganza siku ya uchaguzi mpya.

  Ikiwa watu hawa wamethubutu kukaa madarakani wakati muda wao umeshapita kikatiba – ni sawa na majambazi tutarajie lolote!

 2. zamko 14/11/2015 kwa 8:10 um ·

  Mimi Nafikiri hapo Kuwe na Maandamano ya Kike na KIUME, Watoto na Vijana.. Hakuna Kurudi Nyuma.. Wala hatuna haja yakuomba Kibali.. Hii Ndio Solution .. Huko CCM Wanakotaka kutupeleka Kutakuwa ikiwa Wataitisha Uchaguzi..

  Wasifikiri Kwamba Humo Ndani ya Vikosi Watakuwa Wana Supporti kama waliokuwa nayo Mwanzo.. Siamini.. Hapo Ndipo Tutajuwa Wao au Wananchi Ndio Wenye Serikali.

 3. rasmi 14/11/2015 kwa 8:24 um ·

  Mia fil mia nakubaliana nawe mwandishi, na kwa upande wangu CUF siku watayofanya mchezo wa kuwachezea wananchi akili kukubali kurejewa uchaguzi basi mimi binafsi nitazuia familia yangu yote kushiriki upuuzi huo. Pia nitakua wa mwanzo kupiga kampeni watu waikatae CUF kuwa ni wasaliti wa Wazanzibari na viongozi wa CUF ndio wataokua adui yangu nambari 1 na si Sisiem ama Fisiem.

  Mwendo CUF ni kuendelea hapa hapa walipokwama mafisiem, wakikubali tu matakwa yao wameula wanavyosema ndio ‘goli la mkono’ limekubali.

  Tulio nje na ndani ya nchi tupo tayari kwa subira na maandamano ila si kurejea mchezo huu wa ‘foliti’ wa uchafuzi iwe mwisho. CUF wakishindwa kupata suluhu suala wawaachie wananchi kama walivyoahidi. CUF hawana haki ya kuwaamulia wananchi haki yao waliyoichagua kuikataa CCM wairejee tena…

 4. zanzibarmyhome 14/11/2015 kwa 8:38 um ·

  Kutoshiriki tu haitoshi. Maalim atangaze rasmi tutaandamana kuwa tutaandamana siku ya uchaguzi kuupinga. Neno lake litaheshimiwa na kutekelezwa na wazanzibar.
  Tumemuona kila mtu anavo hangaika kuleta amani na suluhu . Ila hili la kurejea asikubali na pia usifanyike period.

 5. salali 14/11/2015 kwa 9:29 um ·

  Huyu kasha fanywa vibaya na mwamunyange hafai tena yuko na virusi vya kila aina ukimwi,ukoma na sasa anataka kutuambukiza abakiye huko huko kwa basha wake aliko kwenda kuchukuwa ukoma.

 6. Nonini 15/11/2015 kwa 4:48 mu ·

  Sio kuandama ni mtaa kwa mtaa kujitoa mhanga Biidhni llah .

 7. Usingizi-Kiongozi 15/11/2015 kwa 7:46 mu ·

  ….maamuzi swahihi wakti swahihi….msingi imara….

Comments are now closed for this article.