Abdulrahman Kinana

Written by  //  17/09/2015  //  Makala/Tahariri  //  Maoni 4

14

Na Abdulrahman Kinana
“ Mwaka 2013 wanawake wawili wakiwa ni waalimu wa kujitolea, Katie Gee na Kirstie Trup, wakati huo wote wakiwa ni matineja- walifikwa na shambulio la kutisha wakiwa Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano iliyopo Afrika Mashariki, pale ambapo watu wawili wakiwa wanaendesha piki piki walipowashambulia kwa kuwamwagia tindi kali ya sulphuric nyusoni mwao.

Wakakimbizwa kwao Uingereza, madaktari ikawalazimu kuondoa kutoka mwili wa Katie, ngozi kiasi cha asilimia 30 ya mwili wake. Mwaka mmoja baadae, bado analazimika kuendelea kuvaa kinga kwenye uso wake kuficha makovu katika eneo hilo.
Kwa kusaidiwa na wachunguzi kutoka Idara ya Polisi ya Uingereza ya upelelezi Scotland Yard na Shirika la Kimataifa la uchunguzi wa jinai Interpol, mamlaka za Tanzania hatimae ziliwakamata washukiwa wa vitendo hivyo ambao ni wanachama wa kundi la Uamsho, ambao ni kundi la Kiislamu la kigaidi lenye uhusiano unaojulikana kabisa na kundi jengine la kigaidi la Boko Haram.

Washukiwa hao hivi sasa wapo Mahakamani. Uamsho ina historia ya kuwalenga wageni kwa mashambulizi na hata viongozi wa kidini wa Kiislamu na Kikristo ambao hawaungi mkono dhamira zao za kuuchania mbali muungano wa Tanzania kupitia ugaidi na kuigeuza Zanzibar kuwa ni dola ya kigaidi.

Hata baada ya kuwashambulia Gee na Trup, ambao walikuwa Zanzibar kuwasaidia waliohitaji msaada na hawakuwa na madhara kwa mtu yoyote, tumeona katika wiki za mwanzo tu za Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kuwa Edward Lowasa, mgombea Urais wa upande wa Upinzani ameonyesha wazi wazi kuwa na imani na malengo ya watu hawa wenye siasa kali.

Kwa miaka sasa hadhi ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa ni suala muhimu kwa watu wa visiwa hivyo. Kikundi kidogo tu cha watu kinalingania kujitenga kutoka Tanzania Bara upande ambao uliungana nao katika mwaka ule ule ambao Zanzibar iliupindua utawala wa Kiarabu

Hakuna kosa kwa kuwa na kuendelea kuwa na mijadala halali ya kisiasa iwapo tu mijadala hiyo itaendeshwa kwa njia usalama na kidemokasia.
Ila suala linakuwa itachukua muda gani kwa mijadala hiyo kuendelea kuwepo katika hali ya salama iwapo pale Upinzani unapotaka kufanikiwa katika Uchaguzi Mkuu ujao? Lowasa, ambae baada ya miezi 18 tu akiwa katika nafasi ya Waziri Mkuu, alilazimishwa na Bunge kujiuzulu nafasi hiyo kutoka na kashfa ya rushwa, ameahidi kuwatoa watu hao waliofanya shambulizi hilo la tindi kali.

Kuruhusu kuachiwa kwa watu hao, na bila ya shaka yoyote, kurejelea matendo kama hayo ya kampeni za vitisho kutatishia usalama wa wananchi wa kawaida wa Zanzibar na Tanzania Bara – wengi wao wakiwa na fikra za kidini za wastani kama ni Waktristo au Waislamu – na wageni kutoka nje wanaokuja nchini, wengi wao wakitoka Uingereza.
Lowasa anapendekeza haya ikiwa ni sehemu ya juhudi yake ovu na jadidi ya kuutaka Urais. Baada ya kukataliwa na wapiga kura pale alipotaka kuteuliwa kupitia ngazi za Chama cha Mapinduzi kinachotawala, na pale pale kuhamia Upinzania ambako alichaguliwa kuwa mgombea wao.

Viongozi wenye mawazo ya wastani kama Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa chama chenye Wazanzibari wengi cha Civic United Front, wamejiuzulu wakipinga na kuamua kuuinga mkono Serikali. Inatubidi tudhanie kuwa uamuzi wa Lowasa kujenga ukuruba na makundi haya ya siasa kali na ugaidi ni katika kuziba pengo la kukataliwa na watu wengi wa Zanzibar, kwenye mizizi ya Upinzani kwa muda mrefu, wamekuwa hawawafiki juhudi zake za kuutaka Urais.
Na kwa hakika haishangazi. Hatua hii ya Lowasa kuhusu kuwaachia magaidi hawa imewakasirisha viongozi wa Kikristo ambao waliwahi kuitolea wito Serikali kufiksha tamati za kesi zao haraka kutokana na matendo yao ya kuchoma nyumba za ibada, yaani makanisa na mashambulizi ya tindi kali.

Ni wazi kuwa matakwa ya Lowaa hayapo kabisa katika kutaka kuwasaidia Watanzania, bali ni kujipatia madaraka, na mali na mapesa ambayo anaamini atayapata. Na kwa vyovyote, tabia na wasifu wa Lowasa unajuliana sio tu ndani bali hata nchi za Magharibi. Shirika la Wikileaks limefichua kutokana na simu nyingi za maandishi za aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Green kuwa “ Vitendo vya rushwa vya Lowasa vimekuwa ni siri ya wazi nchini Tanzania kwa miaka mingi.”

Si Tanzaniana wala si nchi za Magharibi ambazo zinataka Tanzanwe ni mpaka mpya wa ugaidi Barani Afrika jambo ambalo litatokea kwa vitendo vya Lowasa. Pamoja na kuwa makundi ya kigaidi ya ndani ya Tanzania yamekuwa yakifanya vitendo vya kutisha, lakini hadi sasa hayajaonesha na hayawezi kufananishwa na makundi kma ya Boko Haram au Al Shabab.
Ingawa suala la nani atashika uongozi wa Tanzania ni suala la raia wa nchi yangu ndio wenye walijibu, lakini ni haki kwa Uingereza na washirika wake katika mapambano dhidi ya ugaidi lazima liwahusu kwa undani iwapo itatokea kuwa Lowasa atashinda uchaguzi na kuchukua hatua aliyoisema kuhusu watu wenye siasa kali.

Wakati Al Shabab walipofanya mashambulizi West Gate, Nairobi mwaka 2013, Uingereza na Marekani zilitoa ushauri wa kutotembelewa kwa sehemu nyingi za nchi hiyo na raia wao. Hili lileta athari kubwa katika biashara ya utalii : na hapana shaka yoyote kurejelewa vitendovya kigaidi huko Zanzibar kutahasiri sekta ya utalii Tanzania, lakini hasa kwa Zanzibar, ambapo ndio tegemeo lake kuu la kiuchumi.
Kwa hivyo chaguo ambalo linawakabili Watanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao lina athari ya ndani na pia nje ya mipaka yetu. Iwpo Lowasa na waungaji wake mkono wa Upinzani watashinda, jambo ambalo lina uwezekano finyu kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kuwa nchi hii itakuwa ni uwanja wa mapambano ya kigaidi, katika wakati ambao ugaidi huo umekuwa ukishindwa katika nchi nyingi Barani Afrika.”

Kuhusu Mtunzi

I am particularly interested in combining photography with graphic design to communicate the message of the peace to a specific audience.

View all posts by

Maoni 4 katika "Abdulrahman Kinana"

 1. Mzambarauni Takao 18/09/2015 kwa 12:20 mu ·

  Hili Babu domo lake utadhani vutu la bata.

 2. Feisal Amour 18/09/2015 kwa 6:10 mu ·

  Mfa maji hushika maji. Hali nzito CCM kiasi watafute jini lisilosema. Mwaka huu watalala chale.

 3. zamko 18/09/2015 kwa 6:54 mu ·

  @ Ndugu Wachangiaji,

  Hii sio Makala yakufanyiwa upuuzi na Masihara hii ni Makala ambayo Imetayarishwa na Balozi Sefu Ali Iddi, Pinda, Lukuvi, Na Kinana Kapachikwa kati kwasababu Wazanzibari Walioko CCM Wanabebwa na Tanganyika Ndani ya Koti la Ukoloni Mambo Leo Unaoitwa MUUNGANO wa Tanzania.
  Mchezo huu unapikwa ndani ya Balozi za Mataifa na huwenda ukaja Ukatuathiri sisi Wazanzibari kama hatujachukua hatua yakuiondoa CCM kiDemocrasia..

  Nikisema Kuiondoa CCM Kidemocrasia Sitegemei Kura tu Bali Nategemea Baada ya Uchaguzi kama Matokeo ya Uchaguzi wa Raisi hayajatangazwa basi Watanzania Wote Wa Bara na Visiwani nilazima tufanye Maandamano ya Amani.. Maandamano haya Hayatakiwi Yawe na Hisia au Kulenga Upande wa Dini yoyote ile… Kwasababu Nimesikia Wazanzibari siku Watakayofanya Maandamano Watavaa Kanzu Wafanye Maandamano yakusimama na Jihadi..

  Nafikiri Kuja kufanya hivo ndio kutatukosesha Haki yetu ya Kidemocrasia ambayo Tayari Iataporwa siku ya Uchaguzi.. Maadamano yatakayofanywa Yawe ya kawaida na Mabango ya Kupinga matokeo ( kama ndsio Watakataa kuyatangaza)… Na Watu wanatakiwa Wavae Nguo za Kawaida bila yakutaja Dini au CC ni Nani.. Watanzania Wa Dini zote na Wazalendo ambao wanataka mageuzi ya Uongozi wa Serikali Ya CCM ndani ya Visiwa vya Zanzibar na Tanganyika. Nilazima tusitishwe kudai haki zetu..

  Hii Ndio Plan ya CCM ya Mwisho ikiwa Watashindwa Kufanya Fujo na Kuiba Kura za Uraisi Tanganyika na Zanzibar.. Kinachosuburiwa na CCM Top Leader Nikukataa Kuyatangaza Matokeo ya Uchaguzi Wa Raisi wa Zanzibar ili Wananchi Wachukue hatua ya Maandamano.. Na Kwasababu Wamewasikia Wananchi Wakipiga kelele juu ya Jihadi Hivo Wanategemea Ku SET FIRE ya Boko Haramu Ndani ya Macho ya Kimataifa ili CCM wapate Support yakuendelea kututawala.

  Mpango mwengine wa Viongozi wa CCM Kutoka Tanganyika Nikufuta CUF na Maalim Seif ktk SUK…….Tukumbuke Ndugu Wazanzibari CCM ikishika Madaraka Bara basi Zanzibar itakuwa haipo tena. Katika makala hii hivo Walivosema kwamba Watafanya Mjadala wa Amani juu ya Muungano . hakuna Mjadala ila kukamatwa kwa Viongozi wa juu wa Upinzani UKAWA na kuwekwa ndani… Wazanzibari tumekufa kwasababu hapa kwetu SUK haitofanyakazi kama tunavyoona hivi Sasa inavo Seka Seka. SUK ya 2015 baada ya Uchaguzi Itakuwa ya CCM na Hamad Rashid na Viongozi wa CUF watakuwa Eliminated. Huo Ndio Mpango Kabambe uliopangwa na CCM Wahafidhuna Wakisaidiwa na CCM Watawala..Akina LUKUVI, PETER PINDA na Kinana.

 4. ambassodor 18/09/2015 kwa 11:24 mu ·

  ANA SURA MBAYAA NA UPARA KAMA JIWE LA MOTONI KWAZAMBI ALLAH AMLAAN HUYU FIRAUNI ANA MDOMO SIO KAMA MVUTU WA BATA ILA ANA MDOMO KAMA MVUTU WA CHONJWE KWA HULA MALI HARAMU LANATU LLAH

Comments are now closed for this article.