ZANZIBAR YAFUNGULIWA MLANGO #CAF

Written by  //  16/03/2017  //  Habari, Michezo  //  Maoni 3

#ZANZIBAR YAFUNGULIWA MLANGO #CAF

Alhamdulillah leo #Zanzibar tumepiga hatua moja mbele. Nami napenda niungane na wenzangu kulifurahia hili na kuwapongeza wale wote waliosimamia na kupiga kampeni, rasmi Zanzibar ni mwanachama wa 55 #CAF (Shirikisho la mpira wa miguu Afrika). Pamoja na furaha yetu naomba kidogo tulizime hili dufu tujiulize maswali yafuatayo:-
1)Tanzania itawakishwa na nchi mbili, suala la kujiuliza hapa ni nchi zipi #Zanzibar na #Tanganyika? au Zanzibar na Tanzania?

Maana hata kwenye mtandao wa #CAF wameweka picha inayoonesha bendera na jina la Tanzania ambayo kisheria unaposema Tanzania maana yake Zanzibar imo humo ndani. Kisha kwa chini yake “kama picha inavyojionesha” imewekwa Zanzibar kwa jina lake na hiyo bendera yake (iliobuniwa hivi miaka ya karibuni)

2) Kwenye mashindano ya #CECAFA ambayo hayatambulikani na #FIFA Zanzibar inashiriki sambamba na Tanganyika pia lakini swali linakuja hapa, Tanganyika inaingia kwa jina la Tanzania Bara na bendera inatumia ya Tanzania sasa tuseme Tanzania Bara (kama wanavyojiita) hawana bendera?

3) Vipi kuhusu suala la ligi. Au Tutaendelea kuwa na ligi ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara?

4) hali itakuwaje kwenye mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu. Zanzibar itapewa fursa ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa barani Afrika au itaendelea kupewa ubamba wa kunde kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho?

5) na wimbo wa taifa nao ni alama muhimu mchezoni hasa katika mashindano ya ngazi Taifa, #Zanzibar tunao wimbo wa taifa je Tanganyika wanao na kama wanao wanautumia?

FB

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "ZANZIBAR YAFUNGULIWA MLANGO #CAF"

 1. rasmi 16/03/2017 kwa 5:41 um ·

  Watatema kimoja kimoja na tunawakumbusha ile ahadi ya kuzima umeme wasisahau inaweza ikawa dawa pia ya kuanza kujitafutia umeme mbadala…

  #Zanzibar 4 CAF imebamba, vijana wetu katuwakilisheni na kuitangaza nchi yetu sasa…

 2. Fuad Suleiman 16/03/2017 kwa 7:30 um ·

  Zanzibar imepata uwakilishi katika makombe ya africa lakini hii ni danganya toto kwani passport ya wapi zanzibar au tanganyika kwa hivyo watakuwa wachezaji huru mpaka tutakapokuwa na muhuri wetu

 3. moyo 17/03/2017 kwa 11:58 mu ·

  Ukiyatizama utayaona ni masuala ya mpira tu lakini yana nafasi kubwa katika mustakbal wa Zanzibar na siasa za Tanzania.

  Ahsante sana muandishi wa makala kwa makala yako nzuri na masuala yako machache tu ambayo hakuna hata kiongozi mmoja wa Tanganyika atakaeamua kuyajibu ila atapatwa na kigugumizi na kujitafuna midomo.

  Hapo sasa pataaaamuuuu.

  ALLAAH ATUPE ZANZIBAR ILIO HURU NA MAMLAKA KAMILI.

Comments are now closed for this article.