Zanzibar sasa hali ni tete

Written by  //  01/01/2013  //  Habari  //  9 Comments

.Balozi Seif asema wahusika wasakwe
.Hamad Rashid awanyooshea kidole CUF

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Padri Cosmas Shayo wa Kanisa la Roman Katoriki Jimbo la Zanzibar wakati alipokwenda kutoa mkonao wa pole kwa uongozi kanisa hilo na familia kufuatia tukio la kupigwa risasi kwa Padiri Ambrose Mkenda.

Ni dhahiri kwamba hali ya amani visiwani Zanzibar ni tete, huku viongozi wakitajwa kuhusisha dini katika harakati za kufikia malengo yanayotajwa kuwa na nia ovu.

Viongozi wa dini, wanasiasa na wanazuoni, wanaelezea umuhimu kwa Taifa kudhibiti uhalifu na kuwachukulia hatua kali wahalifu wanaochochea vurugu, ili kulinda na kuendelea amani visiwani humo.

Zanzibar inakabiliwa na kukua kwa vurugu, hujuma na njama za kutekekeza mali na maisha ya raia wasiokuwa na hatia, dalili zikionyesha wazi kuwepo ‘mkono wa wanasiasa.’

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ANENA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema serikali itahakikisha inawasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliompiga risasi Padri Ambrose Mkenda, Desemba 25, mwaka huu.

Balozi Seif alisema kitendo hicho kimetoa sura mbaya kwa Taifa na serikali, hivyo kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani na umoja wa kitaifa.

“Ni jambo baya na la kusikitisha, tena limetoa sura mbaya kwa Taifa. Serikali haitosita kuachukulia hatua dhidi ya watu waliofanya uhalifu huo,”alisema Balozi Iddi na kuwataka wananchi kuheshimu na kulinda misingi ya amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.

Balozi Seif alitoa msimamo huo wa serikali alipokwenda kutoa pole kwa uongozi wa kanisa hilo na nyumbani kwa Padri Mkenda mjini hapa jana.

Alisema SMZ imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika mazingira ya hofu isiyokuwa ya lazima wakati Tanzania ni nchi ya amani.

PADRI WA KATOLIKI AWAONYA WANAOWAPOTOSHA WATOTO

Padri Cosmas Shayo wa Kanisa Katoliki, aliiomba serikali kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao, kutokana na matukio ya hujuma yanayojitokeza visiwani humo.

Padri Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa kidini, inawajengea msingi wa maisha mabovu watoto hao.

“Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine, tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na mwelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye,” alisema.

Padri Shayo alisema serikali inawajibika kufanya uchunguzi wa kina kufuatia kupigwa risasi kwa kiongozi huyo.

Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa wamepanda pikipiki majira ya saa 1:45 usiku wakati akitoka kumuangalia mgonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja akiwa ndani ya gari wakati akisubiri kufunguliwa geti na mlinzi na hakuna kitu kilichoibiwa baada ya kiongozi huyo kupigwa risasi.

Tukio la kupigwa risasi mbili za shingo kiongozi huyo wa kiroho limetanguliwa na mkasa wa kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga wakati akifanya mazoezi ya viungo Novemba 6, mwaka huu.

Hata hivyo hakuna watu waliyokamatwa kuhusiana na matukio hayo. Lakini Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuwatafuta watu waliyofanya mashambulio hayo tofauti visiwani hapo.

HAMAD RASHID AINYOOSHEA KIDOLE CUF

Mbunge wa Wawi (CUF) Hamad Rashid Mohammed, alisema Zanzibar itaingia katika machafuko makubwa endapo hakutafanyika jitihada za haraka kukomesha chuki za kidini zinapandikizwa miongoni mwa raia wake.

Alisema hali si shwari visiwani humo, akiifananisha na ‘yai jeteta’ ambalo kupasuka kwake, kunaathiri watu wote.

Hamad alisema kihistoria Zanzibar ni nchi iliyokuwa na watu wenye uvumilivu wa kidini kwa miaka mingi na hakuna aliyetarajia siku moja watu watatengana na kuhujumiana kwa sababu ya tofauti za kiimani.

Alisema matukio ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti Fadhili Soraga na tukio la hivi karibuni Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni baadhi ya matokeo ya chuki hizo zilizopandwa na wanasiasa.

“Hali ya Zanzibar inasikitisha sana, matukio yote mawili ya kujeruhiwa viongozi wa kidini ni jambo la kulaaniwa kwa nguvu zote na inathibitisha kuwepo kwa watu wanaochochea hali hiyo kwa manufaa yao,” alisema Hamad.

Alisema kumekuwepo na viongozi wa kisiasa wanashindwa kukemea hadharani jambo hilo kwa sababu wanahusika kuwashawishi na kuwachochea viongozi wa dini kushiriki vurugu hizo.

“Uongozi wa kisiasa umeshindwa kukemea kwa sababu kuna baadhi ya wanasiasa wanahusika, wakati mwingine wanakwenda kwa viongozi wa dini zote kuchochea, lakini ikumbukwe ikitokea vurugu hakuna atakayepona,” alisema.

Mbunge huyo asiyetambuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) alichokitumia kugombea na kushinda kiti hicho, alisema suluhu ya tatizo hilo ni kuanzishwa mjadala wa kitaifa kujadili kuhusu chanzo halisi na namna ya kufikia suluhu ya kudumu.

Pia Hamad alisema hakuna viongozi wenye maoni na nguvu ya kuzuia jambo hilo, kwa vile viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa wanatofautiana kiitikadi.

Katika suala hilo alionyesha kufadhaishwa na msimamo wa viongozi wa CUF kutokuwa na upande wa kusimamia kuhusu Muungano, moja ya madai yanayotajwa kutumika kama kigezo cha kuchochea vurugu visiwani humo.

“Ndani ya CUF kuna watu wanataka Muungano wa Mkataba na wengine wanataka Muungano wa serikali tatu, tofauti na CCM ambao wana msimamo mmoja wa serikali mbili,” alisema.

“Hili ni jambo baya sana kwa viongozi wa CUF kutokuwa na msimamo wa kimaadili, haiwezekani chama kuwa na makundi mawili yenye tofauti ya msimamo, kutokana na hili huwezi kusimamia serikali hata mara moja,” aliongeza kusema.

Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alielekeza lawama kwa jeshi la polisi na kusema linafanya kazi kisiasa na kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Profesa Lipumba alisema kama polisi wangefanya kazi kwa weledi na kuachana na kutumika kisiasa, matukio yanayotokea Zanzibar yasingekuwepo kwa sababu wahusika wote wangekamatwa.

Hata hivyo alipinga hoja ya Hamad kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika kuidhibiti hali hiyo.

CHUKI ZILIATHIRI UTENDAJI WA TUME YA KATIBA MPYA

Wakati huo huo, imefahamika kuwa kutokana na kuenea kwa chuki za kidini, wajumbe wa Tume ya kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wanafanya katika hali ya tahadhari, baada ya kukabiliana na matukio ya kibaguzi.

Vyanzo vya habari vimeieleza NIPASHE Jumamosi kuwa baadhi ya wajumbe wasiokuwa waumini wa dhehebu moja wanaofanya kazi kwenye tume hiyo visiwani humo, wanachukua tahadhari kubwa huku wakishindwa kwenda kwenye maeneo yanayoonekana kuwa na watu wenye msimamo mkali wa kidini.

“Mimi mwenyewe ni muathirika wa mambo hayo, lakini siwezi kuzungumzia sana jambo hilo, tunachokifanya ni kutokwenda sehemu tunayoona kuna dalili mbaya,” kilieleza chanzo chetu kutoka tume hiyo.

CHANZO: NIPASHE

About the Author

View all posts by

9 Comments on "Zanzibar sasa hali ni tete"

  1. Makame Ame 01/01/2013 at 1:25 um ·

    Huyu Mh Hamad ni mwanasiasa, anajuwa hicho wanachokifanya. Na ikiwa anaushahidi kwa nini hapeleki kunakohusika ushahidi huotukapumzika?

    Ukweli anaujuwa lakini hataki kusema. Ni serikali yenyewe ndiyo yenye kuyatilia maji na mbolea hizo chuki za kidini. Hivyo mwenye mamch haambiwi tazama. Kipigo walichopata ndugu zetu wa Kendwa si za kisiasa bali ni sababu za kidini. Hilo halioni?

    Miskiti kunajisiwa na vyombo vya dola mbali maonevu kwa waislamu na kupewa kipa umbele wakristo na serikali si dalili tisha ya kupandikiza chuki hizo?

    Mh Hamad tafuta jengine la kutuaidh. Hili ukiwemo wewe ambaye unajisifu kuwa umelelewa na Nyerere basi umo katika dhima hiyo ya kupandikiza chuki hizo pamoja na wanasiasa wenzako….hamtoki na mtajuwa la kujibu mbele ya MwenyeziMngu.

    Tunakutakia kila la kheir kuamka kwenye usingizi huo wa kisiasa urudi kwa Mngu wako kabla ya jua halijachwa.

  2. Mrfroasty (Ufundi) 01/01/2013 at 2:33 um ·

    Balozi Seif anaona padri tuu, tuna viongozi wetu wa dini ya kiislamu wako ndani wanateswa hadi leo nae amenyamaza kimya.Tushusheni jamani!!

  3. mwanafunzi 01/01/2013 at 4:02 um ·

    Hamad Rashid hana mpya, Balozi Sefu kaishiwa.

    Sisi sote tunataka wahusika wanaswe na ni lazima wawe wanamiliki silaha za moto kwa kuwa huyo padri alijeruhiwa kwa silaha (ya moto) na wanaomiliki silaha ni vikosi vyenu.

    Wazanzibari wanataka nchi yao hata mufanye nini sisi haturudi nyuma.

  4. elbattawy 01/01/2013 at 6:36 um ·

    Hamad Rashid yeye mwenyewe ndo yai jeteta sasa atailaumu vipi CUF na chanzo cha vurugu kinajulikana, mbona hakuongelea suala la kutekwa nyara kiongozi wa uamsho sheikh Faridi na usalama wa Taifa? halafu kuhusu maoni mbona amekuwa na fikra za ki CCM hamad rashid? yale yanaitwa maoni kila mtu ana mtazamo wake katika maoni utawalazimisha vipi watu wote waseme wanataka mkataba? kama ni hivyo kuna haja gani rais kikwete kuleta tume ya maoni, kwani hawo CCM hawako waliotaka serikali ya Mkataba akina Mansour na Wenzake? au wakati wa maoni hamad rashid ulikuwa marekani ukila kuku kwa mrija? sasa kwa taarifa yako Mkataba ni 66% tunataka zanzibar yetu

  5. Bosco 01/01/2013 at 7:53 um ·

    Balozi seif ali idi anataka apewe urais wa zanzibar na anajua kua kanisa na mfumo kristo ndio waamuzi wa hilo hivyo basi anajipendekeza kwa makafiri ili apewe urais. Sina shaka huyu balozi seif ali idi akiambiwa avae msalaba atavaa tu.

  6. makame silima 01/01/2013 at 7:59 um ·

    Viongozi wa Ccm/Smz likumbatieni tu Kanisa Katoliki na Muwangamize Mashekhe waislamu wa Zanzibar na kuwabambikizia kila jina baya tuone wapi watakuwa na nusura kwa Allah .

    Kanisa hivi sasa ndio chachu na chuki ya kutaka kuivuruga na kuiangamiza Zanzibar sifa yake ukarimu na upole hii ndio weakness wanayo itumia Maskofu wa Zanzibar ambao ni Wazaliwa wa Bara.

    Fitina hii ina fanywa na Mapadri ambao wengi wao sio Wazaliwa wa Zanzibar.

    Hivi sasa Jumuia ya Maimamu wa Uamsho wako Ndani Baada ya sindikizo la Kanisa na uchochezi wake,

    Jee lipi kubwa Uamsho walilolifanya mpaka Kanisa likaja juu na kuwatia midomoni jumuia ya Uamsho?

    Hakuna siku hata moja Uamsho walo sema kuwa waislamu wa Zanzibar wakavunje kanisa au kuwabagua wakristo wa Zanzibar.

    Ukweli wenyewe nikuwa Uamsho walipotangaza kuvunja Muungano na kudai haki za Zanzibar kwa ku wa brean wash Wazanzibar hili ndio lililowakera Watanganyika waishio Zanzibar wawe Wakristo wawe Buuda wawe Waislamu wote ukitangaza kuvunja Muungano huwa kitu kimoja na husahau dini zao huu ndio ukweli wenyewe.

    Hii Kanisa Kuwasakama Jumuia ya Maimamu wa Uamsho ni Babaisha bwege tu,
    Matatizo ya Zanzibar yapo Zaidi kisiasa kuliko kidini Musituchafuwe na kutugoroga Maskafu wa Bara.

    Ikiwa uamsho kauli zao zikilinga sana Basi ni Muungano na Serekali Zake lakini sio kidini, Hii mumeileta nyie Maskofu kwa kuwa na agenda ya siri Zanzibar chini ya kivuli cha Muungano.

    Zanzibar hakuna chuki za kidini maana hao Wakristowenyewe ni asilimia %0 na wakazi wa Zanzibar ni wauislamu sasa vipi Maskofu mupurupuke kutaka kutuletea Chuki za Udini Zanzibar?

    Matatizo ya zanzibar yapo kisiasa zaidi kuliko udini kwa sababu hio ndini ya wakazi wa zanzibar ni %99.

    Musituletee fitina za kutaka kuliharibu jina la zanzibar na watu wake, isiwe ukarimu wetu wa kuwakaribisha Maskovu Zanzibar kwa jina la kuwa Tanzania ni 1 na haina Dini nyiyi Mukaitumia vibaya kwa Zanzibar .

    Baado wananchi wa Zanzibar ni waislamu na hatukuwa na machafuko na wenzetu wasio waislamu tulikuwa tunaishi pamoja na kusaidiana kwa upendo, lakini Mumekuja nyiyi Mapadri munataka kumwaga chuki za udini.

    Lakuangalia kwanza jitazameni muko asilimia ngapi % hapa zanzibar hata mukataka kuja kwa moto wa juu?

    Walicho kidai na kufanya mihazara yao Jumuia ya uamsho zaidi ilijenga kudai haki za wananchi wa Zanzibar katika maonevu ya Muungano sio Kanisa, au ndio tuseme Muungano ndio mfumo Cristo?

    Hivi sasa munajaribu Maskofu kuiponza Zanzibar katika vita vya udini na Ugaidi, jee kweli nyiyi muna nia Njema na Zanzibar ?

    Hili halitowakumba wananchi wa zanzibar pekeyao, hata viongozi wetu wa smz wenye kujipendekeza na Kanisa basi kikiwaka kisawa sawa na wao na jamaa zao watakuwa katika chombo kimoja.

    Nazani hili Seif iddi halijuwi yeye yuko zaidi kisiasa na kufika hadi Israil kutafuta suport, hivi sasa Smz wanalitumia kanisa zidi ya Upinzani lakini wasisahau kuwa wakristo lao moja zidi ya uislamu na nchi zilizo na waislamu wengi.

    Washe viongozi wetu wa Smz wajipendekeze tu kulikingia kifua Kanisa Katoliki wasisahau kuwa Mayahudi na manasara hawato furaishwa na chochote wakifanya cho waislamu ipokuwa wafuate mfumo wao.

    Kwa hio tayari Smz inaegemea Kanisa na wacha Kanisa lijitanuwe, ulimwengu hivi sasa unapata tabu kwa fitna na chuki za Makafiri kuto kukubaliwa agenda zao ambazo ni kinyume na mafundicho ya Allah.

    Kwa hio tamaa ya viongozi wetu wa Smz itawatokea puni baada ya Kanisa likisha izibiti zanzibar kisawasawa, wamulize Kamandoo alipokuja kutowa mwanya wa kumiminwa makanisa Zanzibar kila chochoro na yeye vipi alivyo hivi sasa.

    Hali ya Kamandoo hivi sasa yeye mwenyewe hajitambui kuwa Yuko nduniani au Laa, yote alofanya na kukumbatia hivi sasa yamemtumbukia nyongo maana laza ya hayo haioni tena husifiwa tu.

    Tayari amesha pofua na M/mungu anamuonyesha hapa hapa, hakujuwa kuwa uongozi ni zamana ya muda na nikitu chakupita tu.

    Hivi sasa silolote sio chochote hata kutajwa hataju tena ispokuwa mabaya yake aloyacha nyuma hayo ndio yanayomuangamiza kidogo kidogo.

    Kwa hio na hao wengine Seif Iddi 40 zao ziko, nipale tutakapo sikia kuwa anaanza safari za kwenda Muhimbili au India.

    Hii ndio realty yenyewe , hao Maskofu wamekuja juu kwasababu kuvunjika kwa Muungano ndio kuondoka kwa Kanisa na mahubiri yake Zanzibar .

    Na kanisa likisema uovu wa Uamsho hukusudia maana yake Waislamu wa Zanzibar ki -Tecnic .

    Jee kweli Wakrito Zanzibar ni asalimia ngapi hata Serekali ya Smz na viongozi wake wakalikumbatia Kanisa Katoliki?

  7. HALIKUNIKI 01/01/2013 at 10:28 um ·

    Hata wafanye nini lakini haki itasimama tu, kama lengo lao ni waislamu
    ndio waliofanya hivyo basi wache wafanye uchunguzi wa hao makachero
    wao na ukweli utadhihiri.

  8. siri 02/01/2013 at 9:08 mu ·

    Bwana Mtume (SAW) alituambia waislam… msiwagope makafiri kwani hawataweza tena kuwadhuru BALI waogopeni sana (NA mchukue hadhari nao) WANAFIKI .. WANAFIK.. hawa ndio watako RARUWA….. UISLAMU. Ndio hawa tunaowaona ndugu zetu wenye majina ya Uislam kumbe makafiri wakubwa .. wengine wanachukia hata kusali .. wanadhani wataishi milele. Tumuombe Allah atupe subira na nguvu za kupambana nao “pepo kwa watakao kufa na ushindi watakao bakia kama vile masahaba,” amin.

  9. Makame Ame 02/01/2013 at 9:17 mu ·

    Tanbihi:
    Aya ya 118 mpaka 120 katika Surat – aal-Emraan zinatutanabahisha:

    يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِنْ دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ
    ye who believe! Take not into your intimacy those outside your ranks: They will not fail to corrupt you. They only desire your ruin: Rank hatred has already appeared from their mouths: What their hearts conceal is far worse. We have made plain to you the Signs, if ye have wisdom
    Enyi mlioamini, musiwafanye wasiri wenu wale wasiokuwa nyinyi (wasioamini). . Hawatoacha kukuFanyieni ubaya. Wanalolitaka ni kuangamia kwenu. Imeshafichuka chuki yao kutoka midomoni mwao, lakini yaliyojificha vifuani mwao ni mabaya (makubwa) zaidi. Tumeshawabainishia dalili (ishara) zilizodhahiri ikiwa ni wenye kutumia akili.

    هَا أَنْتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
    Ah! ye are those who love them, but they love you not,- though ye believe in the whole of the Book. When they meet you, they say, “We believe”: But when they are alone, they bite off the very tips of their fingers at you in their rage. Say: “Perish in your rage; Allah knoweth well all the secrets of the heart.”
    Hivyo basi nyinyi ndio munawapenda watu hao, lakini wao hawakupendeni. Nanyi munaviamini vitabu vyote (Injili, taurat, zaboor, na Quran). Na wanapokutana nayi husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao wanakuumieni vidole kwa chuki zao. Sema: Kufeni kwa chuki yenu! Hakika MwenyeziMngu anayajua yaliyomo vifuani.

    إِنْ تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِنْ تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا إِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
    If aught that is good befalls you, it grieves them; but if some misfortune overtakes you, they rejoice at it. But if ye are constant and do right, not the least harm will their cunning do to you; for Allah Compasseth round about all that they do.
    Ikikupateni kheri huwaudhi. na ikikupateni shari hufurahikia. Na nyinyi mkisubiri mukafanya mema (yanayopendeza kwa MwenyeziMngu) , hila zao hazitakudhuruni kitu. hakika MwenyeziMngu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo.

    Aya mbili za kwanza zinatueleza ukweli uliopo. Na ya ya 120 inatufahamisha nini la kufanya. kazi kwetu. MwenyeziMngu atujaalie wenye kusubiri (atuongezee na subira yenyewe) tuwe waja wema na atuongoze jia iliyonyoka. Tunakuwachilia Wewe Bwana wabaya wetu hawa.

Comments are now closed for this article.