Zanzibar huru si kwa leo wala kesho!
Written by Bablee // 18/12/2012 // Habari // 39 Comments
A.aleykum,
Wazanzibar wameshachoka kutawaliwa na Tanganyika, kila mmoja kwa sauti yake analia akitamani aachiwe apumuwe! Lakini ukweli ni kwamba tutaendelea kulia na kutamani, kuna uwezekano mkubwa sana “generation” yetu ikapita bila kuipata Zanzibar huru! Lakini kama tutaamuwa kuchukuwa hatua za makusudi, basi Inshaallah pindi wajukuu au watoto wetu huenda wakaipata Zanzibar yao, iliyo uhuru na yenye mamlaka kamili! Lakini si leo wala kesho…!
Acha nilipasue jipu, maana nshachoka kuli bembeleza kwa kulichorea duara kwa peni…husikia raha, lakini nkiliacha tu lapwita kwa maumivu, huhisi kama latuta!
Kwa asieijuwa siasa ya Zanzibar ni rahisi kusema Zanzibar ni CUF na CCM tu, laiti ingekuwa hivyo, (CUF na CCM tu), basi hamad! Nchi tungeshaipata zamani sana! Lakini si leo wala kesho….!
Zanzibar ni zaidi ya CUF na CCM… ndani ya CUF kuna makundi matatu (3) yenye mitazamo tofauti, na ndani ya CCM kuna makundi manne yenye mitazamo tofauti! Ubaya ni kwamba katika makundi hayo, kila moja kutoka chama kimoja lina ugomvi na uhasama na pea wake kutoka chama chengine. Kundi la 4 lililopo CCM tu, hili hunufaika uwepo wa makundi hayo hasimu! Lenyewe ni kama kunguru, panzi wakipigana ndio furaha yake! Makundi yaliyopo ni haya, kama hujayajuwa:
1. Mapinduzi daima CCM vs wapinga mapinduzi CUF, niweke wazi si kweli kwamba CCM wote ni mapinduzi daima kama vile ilivyokuwa sikweli kwamba CUF wote ni wapinga mapinduzi! Kuna CCM tena vindaki ndaki wasioyashabikia mapinduzi, vile vile kuna CUF waanzilishi hasa wasioyapinga mapinduzi! Ubaya upo kwa haya makundi mawili la wanaotaka kuenzi mapinduzi, na kuamini kwamba mpaka hii leo mapinduzi bado yapo katika maisha yetu ya kila siku, wanaamini kwa dhati kwamba aliepinduliwa ni sultani, na mpemba ni kibaraka wa huyo sultani! Vile vile uwepo wapinga mapinduzi, wanaoamini kwamba mapinduzi yalikuwa haramu, yalimwaga damu za wazanzibar na kupinduwa utawala halali wa mzanzibar ambae ni mpemba! Uhasama wa makundi haya ndio unaofikia hatua kuigawa Zanzibar kati ya Unguja na Pemba! Ni hatari! Na kwa hali hii si kwa leo wala kesho….
2. Lipo kundi ndani ya CUF wanaomini kwamba ili uwe mzanzibar halisi lazima uwe na rangi nyeupe japo kidogo, huwezi kuwa mweusi tii, halafu ukawa mzanzibar! Utatafutiwa asili yako bara, utaambiwa huyu wa mrima tu, na hutoitwa kwa cheo chako wala ukazi wako,utaitwa kwa rangi yako, si tumesikia Seif Mweuisi n.k! Na kwa ushahidi wangu mwenyewe, kwa macho yangu na masikio. Kulifanyika mkutano wa CUF pale Starlight (DSM), 2001, mkutano ule alihutubia maalim Seif! Pale nje mlangoni paliwekwa walinzi, ambao walitakiwa wahakikishe ni waZanzibar tu wanaoingia kwenye mkutano ule…cha ajabu akienda mtu mweupe mwenye rangi rangi ya kirabu/kimanga, haulizwi jambo, afunguliwe mlamngo apita, hata kama ni mwarabu wa Tabora, Kigoma au Mwanza. Lakini akienda mtu mweusi, hata kama ni mpemba wa fyoko wa mtambwe Nyali, ataulizwa maswali ya kipuuzi..sijui sema “haluwa kwa chai” , mara twambie maana mbili za tutu! Ilimradi ni kukupa ujumbe kwamba wewe ni mweusi huwezi kuwa mzanzibar!
Na yuko mwakilishi mmoja Pemba kwa tiketi ya CUF, yeye ni mweusi tii, alituelezea jinsi alivyokuwa akinyanyaswa wakati wa kuchaguana huko kwenye matawi na mashina, kila wakimtafuta asili yake wanaishia mtambwe uwondwe… “lakuwa haliwanwa” Allah akamjaalia akapita, kwa nguvu ya Maalim Seif, mpaka sasa ni mwakilishi! Hawa wapo CUF, lakini na CCM kuna pea yake!
Huko CCM kuna wanaoamini Mzanzibar halisi ni mweusi, hawa weupe ni vibaraka wa sultani tu, sio wenye nchi, wala hawafai kupewa nchi! CCM hawa wamefika mpaka kusema kwenye mikutano hasa, walimuuliza Dr. Shein kwanini umempa mwarabu cheo kwenye usalama wa taifa na kwanini ukampeleka kusoma na watu weusi wapo tele CCM? Hawa walifika hatua kumpinga Dr. Salim wazi wazi wakimwita hizbu alipotaka kukombea urais zanzibar! Makundi haya yenye mtazamo wa kirangi ni hatari kama kundi hilo hapo juu! Na hakika si kwa leo wala kesho….!
3. CCM sera vs CUF sera, hili ni kundi lenye wafuasi wachache na wengi ni wasomi na waelewa! Kundi hili halina tabu na ZANZIBAR huru, ni kundi lisilowafurahisha watawala (Tanganyika)! Kundi hili hutofautina kisera tu, na ni upo uwezekano wa kundi moja kuunga mkono hoja au sera ya kundi pinzani kama ataona sera hiyo au hoja hiyo ina manufaa kwa Zanzibar! Mfano ni akina Mansour na wenzake wachache CCM zanzibar, na kwa CUF ni kama alivyo maalim Seif, Marehemu Mloo, Babu Duni na wenzake wachache (Jussa hayumo kundi hili)
4. Hawa ni waTanganyika waliopo CCM zanzibar, ni kundi la nne na lipo CCM tu, kundi hili hufurahia uwepo wa mtafuruku na uhasama baina ya wazanzibar, wao ndio huwa mtaji wao. Kundi hili huongeza petroli na kuchochea chuki baina ya makundi hayo hasimu. Hawapendi wala kutamani kuona wazanzibar wanakuwa pamoja! Lakini uzuri ni kwamba halina nguvu.. kama tu waZANZIBAR TUKIAMUWA!
SULUHISHO
Ili vizazi vyetu siku moja vije viipate Zanziabr huru na mamlaka yake kamili, ni lazima sisi tuekeze katika hilo! Tuwekeze katika kuwalea na kuwasomesha juu ya Zanzibar moja, hakuna Zanzibar bila Unguja na hakuna Zanzibar bila Pemba, Pemba na Unguja hazikuungana, ni ndugu kwa asili! Lazima pia tuwalee na kuwasomesha mpaka wafahamu bila shaka kwamba Uzanzibar si rangi ya mtu, Uzanzibar ni uzalendo kwa Zanzibar na watu wake, hili walijuwe na kuamini kwa toka moyoni kabisa! Tuwafundishe historia ya mapinduzi ya Zanzibar kama historia tu, sio kuwajenga chuki au visasi kutokana na historia hiyo.
Mapiduzi ni historia tu, ifundishwa kama vile tunavyowafundishwa vita vya maji maji, vitakuu ya 1 au 2 ya dunia! Mapinduzi hayapo tena katika maisha yetu ya sasa, waliopinduliwa washakufa na waliopinduwa hawapo tena! Hichi ni kizazi kipya (new generation)! Tuyasimulie mapinduzi kama tukio la ki histori tu, ikiwa alipinduliwa mpemba sawa ndo alishapinduliwa sasa tunampemba Rais na Makamo wa kwanza, tena wanalindwa na ving’ora hasaa! Lau kama alipinduliwa muarabu pia sawa, lakini hatuhusu, alikimbilia UK, na pengine kashakufa, hivi sasa tunaongoza wenyewe waZanzibar!
Tusiwafundishe watoto wetu historia ya mapinduzi kisha tukaweka misimamo yetu, No! Tuwafundishe kama historia ya yaliyopita tu! Kama tunavyofundishwa Theories Of Evolution, waalimu hawatupi misimamo yao kwamba wanaikubali ipi, na sisi wanafunzi hatuweki misimamo yetu, hubeba kama theories za waliopita kabla yetu! Na ndivyo tufanye kwenye kuifundisha historia ya mapinduzi kwa watoto wetu!
Tuiwache “past” na yaliyokuemo yapite, kuendelea kuyavundika ndio yanayotupelekea kutugawa, na tunagawiwa kama mafungu ya masheli sheli! Tutaendelea kuvutana sie kwa sie kishabiki, wakati kiukweli sote (CUF na CCM Zanzibar) twaitaka Zanzibar yetu huru, lakini kwa uhasama wetu hatwendi pamoja, na kwa misingi hiyo ZANZIBAR HURU, SI KWA LEO WALA KESHO..!



39 Comments on "Zanzibar huru si kwa leo wala kesho!"
Nakutolea heko mwandishi,lakini kama tutakuwa na umoja tutaweza kupata
unafuu fulani japo sio kuwa huru kabisa.
Kama ulivyosema kubaguana ndio udhaifu wetu mkubwa tulionao na hata hao
watawala wetu ndio silaha yao kuu wanayoitumia.
Cha msingi nini tufanye ni kuwa wamoja na tuache tafauti zetu za kivyama ili
tuigomboe nchi yetu .
Mada yako haiendi sambamba na meudhui yaliyomo ndani, kinachoonekana zaidi unazungumzia hisia za mtu mmoja mmoja kuliko sera za vyama ulivyovitaja hapo juu.
Binaadamu kimaumbile ALLAH kasema : “Hakika ya nafsi ni yenye kuamrisha mabaya na maovu”. Kutokana na maumbile hayo tumetakiwa tupigane jihadi kubwa ya kuishinda nafsi badala ya kutuamrisha mabaya sisi tuamrishane mema na hapo tutakuwa tumefanikiwa katika jihadi kubwa.
Tukija katika mada kwa ulivyoelezea ni kama kwamba unajua mengi katika cuf na ccm sijui ni kweli au unabahatisha tu. Tunavyofahamu wengi Sera ya cuf ni kuiona Zanzibar iko huru ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania na hili linasemwa wazi na hata viongozi wa juu katika chama hicho na wananchi walio wengi wanataka hivyo na wafuasi wa cuf hawafichi wanatamka wazi na kukuelezea mafaniko yanayotarajiwa kupatikana iwapo tutafanikiwa kuipata Zanzibar iliyo huru. Kwa upande wa ccm Zanzibar sera yake ni Serikali mbili (nasema hivyo kwa sababu viongozi wa ccm bara wanapozungumza na wafuasi wao hawazungumzii sana sera ya serikali mbili kama wanavyozungumza Zanzibar huwa wanazungumza mengine) na hili linasemwa wazi bila kificho na kila mtu analielewa.
Pamoja na kuwa wanakubali kunahitajika mabadiliko makubwa ya Muungano na hayo mengine hayawezi kufikiwa katika mfumo wa Serikali mbili (Raisi wa zanzibar kuwa na mamlak sawa na rais wa muungano) lakini hawawezi kusema zaidi ya serikali mbili kwani utakaposema hivyo utaondolewa katika uongozi wa ccm na wengi hawajakuwa tayari kwa hilo (mifano iko wazi kwa mansuri).
Hapa tunaona hata ccm kumbe wako wanaotaka zanzibar iwe huru lakini baadhi yao wakiwa viongozi hawawezi kusema hadharani kwa kuhofia kupoteza nyadhifa zao lakini wasio viongozi tunashuhudia wengi tu wakisema zanzibar ni lazima iwe huru.
Tukichukua hitimisho la yaliyoelezwa hapo juu tunaona kwamba wazanzibari walio wengi wanataka zanzibar iwe huru lakini tusisahau kuna mkono wa dola, kama dola haikukubali tutaendelea kuona tunabaki katika hali hii hii kwani hata kama itapigwa kura ya maoni watabadilisha matokeo kama wanavyobadilisha katika chaguzi zilizopita.
Kwa hayo machache nadhani mtoa mada utakuwa umepata japo maneno mawili yatakayokufaa na kuhimiza umoja wa kuipata zanzibar huru badala ya kuendelea kutuletea hadithi za rangi nyeupe na nyeusi kwani hata wachaga na wahindi ni weupe sio waarabu tu.
Tujitahidi kuitetea zanzibar iliyo huru kwa faida ya vizazi vyetu.
Mwnanfunzi ume comment nje ya context….! Umeanzisha mada yako mpya ndani ya mada yangu!
Hebu isome tena hiyo mada yangu, kisha njoo unipinge kwamba hili halipo nazua! Mimi ni Mzanzibar, naishi kwenye jamii ya wazanzibar hivyo nliyoyaandika hapo nayajuwa kwa uzoefu sio hadithi za kuhadithiwa tu, ndo maana nayajuwa ya CUF na CCM zanzibar!
Na mwisho nipinge, kwamba Zanzibar huru itapatikana kwa hali hii hii… tena kupitia katiba mpya ya Warioba!
Mwanafunzi unasema nanukuu “Mada yako haiendi sambamba na meudhui yaliyomo ndani…” What do you mean? Nini mada? Nini maudhui? Naomba nifahamishe namie maana ya maneno hayo ili mara nyengine nikijaaliwa kutoa mawazo yangu ” mada” na “maudhui” viendane!
Mimi naamini kwamba tatizo kubwa linaloikabili Zanzibar na kukwamisha ukombozi wa Zanzibar si makundi wala mgawanyiko wa kisiasa au itikadi, tatizo ni viongozi wa Zanzibar ambao hawako tayari kuona mabadiliko yanayoelekea kuwapa Wazanzibari uhuru wao kamkli bila kutawaliwa na Watanganyika.
Mgawanyiko uliopo Zanzibar ni wa kawaida popote pale duniani huwezi kukuta watu wote katika nchi wana itikadi na imani moja 100%, labda Corea ya kaskazini. Lakini mgawanyiko ulioko Zanzibar ni wa kawaida na upo miaka nenda miaka rudi lakini pindi ukiwapa Wazanzibari nafasi ya kuchagua wanachokitaka kwa maslahi ya nchi yao watatoa maamuzi ya pamoja na kueleweka nini wengi wanakitaka. Na hicho ndicho kitu muhimu.
Angalia kura ya maoni juu ya serikali ya umoja wa kitaifa 66% waliikubali na 33% waliikataa. Agalia vile vile maoni juu ya katiba mpya, 66% wamesema wanataka muungano wa mkataba na 31% wanataka serikali mbili kama zilivyo. Ingawa hatujajua wale wa barua wanasema nini lakini tunaweza kujaalia trend iko hivyo hivyo kwa sababu sampling ni hile hile hakuna sababu kuwe na tafauti kubwa sana.
Sasa ninahakika kama viongozi wa Zanzibar wangetaka suala hili liamuliwe kwa kura ya maoni basi matokeo yangekua takriban ni hayo hayo ya 66%/33% lakini viongozi hawako tayari kwa mabadiliko, bado wanaona bora kulinda maslahi yao kuliko ya nchi.
BABLEE hicho ulichokiandika hapa naona kama ni hisia zako tu … Zanzibar tunayoitaka ambayo itakwenda na wakati itapatikana tu na sio mbali, kisha kumbuka kwamba harakati za ukombozi (kihalali) hazikuwanza zamani nadhani ni kwenye miaka ya 90 ndio vyama vingi vilianza kuruhusiwa na umeona maendeleo na muelekeo wa wazanzibar na Zanzibar pale fursa inapojitokeza kama vile, uchaguzi, kura ya maoni kuhusu serikali umoja, maoni kuhusu uundwaji wa katiba, haya mambo ni ya kupigiwa mfano na inaonesha wazi wazi wapi muelekeo wetu….kisha unaposema kwenye cuf unapokuwa na rangi ndio ndio unaaminiwa kuwa wewe ni cuf na unapokuwa mweusi inakuwa wee sie, hehehe, hebu nambie nani mwenye rangi kuanzia kwa marehem Shaabani Mloo, kina Lipumba, Seif Sharif,Duni,Abubakar na wenginewe nani hasa mwenye rangi labda Jussa,,Bablee Zanzibar tunayoitaka itapatikana tu na sio mbali,,,,,
@Msemaji mkuu, hivi unadhani ni kwanini hao viongozi hawataki mabadiliko yanayowapa uhuru wa zanzibar hali yakuwa na wao ni wazanzibar? Kwanini waona bora kutawaliwa na waTanganyika kuliko kujitawala? Naomba majibu tafadhali.
Nikweli ulimwenguni kote watu hawawi na itikadi moja, lakini sehemu yoyote ile duniani ambako makundi yanatofautiana kwa misingi ya urangi, chuki kama hizo za mapinduzi, basi kamwe watu wa aina hiyo hawapati maendeleo au mafanikio ya pamoja! Lazima utofautishe kutofautiana itakadi au sera za vyama, hilo halina tabu, na ndo maana nikasema hilo kundi la 3 hapo juu si baya, ndio democracy yenyewe.
Wengi wenu huwa hamusomi mada husika, au husoma mukiwa na majibu yenu kabla hamjaelewa! Jitahidi kusoma mada mukiwa na mawazo huru….UCCM na U-CUF utawapeleka pabaya!
Sale…na wewe ndo wale wale, hivi huwa mwasoma hizi mada kweli? Au hamuzielewi, au mwajifanya tu hamuelewi!
Nimekwambia ndani ya CUF kuna kundi linalaoona Mzanzibar safi (sio CUF safi) lazima awe mwenye rangi nyeupe japo kidogo…hawaamini kwamba mweusi tii aweza kuwa mzanzibar! Someni muelewe jamani kabla hamjaandika comments! Halafu CUF hata kama hao Mloo na Duni wapo CUF kama wa Zanzibar, ndio sababu si CUF wote wanaoamini katika dhana hiyo. Wapo wengi tu akiwemo maalim Seif mwenyewe ambae anaamini Mzanzibar anaweza kuwa mweupe, mweusi, kijani, buluu n.k. Ndo maana hata huyo mwakilishi wa pemba alipita kwa ambri yake yeye maalim Seif.
We ukisema hizi ni hisia zangu, sawa tu! Ila huo ndo ukweli na wewe waujuwa! Au tuseme hata ile video iliyowekwa hapa ya ule mkutano wa CCM pale magomeni hukuona? Hukuona kiongozi wa vijana (tena mpemba) akilaumu kwanini mwarabu kapewa cheo, na kapelekwa kusoma kuwa usalama wa taifa? Nani asiejuwa kwamba Dr. Salim Ahmed Salim aliambiwa yeye ni murabau hizbu na CCM alipotaka kugombea urais wa Zanzibar (au ulikuwa hujazaliwa?). Jee hata hili la baadhi ya ma CUF kumwita Seif Ali Idd, Seif Mweusi pia nihisia zangu? Wengine wanasema wazi wazi kwamba yule ni wamrima? Basi hata hayo yanayowekwa hapa huyaoni? Sikwambii hayo ya mitaani ambayo wewe wasema ni hisia!
Vipi balahau, waishi kwa drip za Jussa, Zanzibar huru utaiota hivo hivo, yaguju! Kama hamjataka kuukubali ukweli na mkajisahihisha, basi hadithi itabaki ni hiyo hiyo…labda usubiri kaburi na pepo huru, Allah akujaalie uwe miongoni mwetu (amin), lakini si Zanzibar huru!
Samahani bablee, sina nia ya kulumbana kwenye ukumbi huu kwani naelewa si lengo, lakini imekuwa vizuri umetutajia jina lako la mzalendo. Kama hayo unayoyasema kuhusiana na ccm na cuf ni kweli jee wewe una wadhifa gani ndani ya hivi vyama? nilitangulia kusema kuna mawazo ya watu binafsi na mawazo ya vyama ndani ya vyama.
Suluhisho ulilopendekeza tayari limeanza kufanyiwa kazi miaka ishirini iliyopita, kazi ya kuwafahamisha wazanzibari nini maana ya Mzanzibari na mzanzibari anastahiki haki gani ndani ya Muungano wetu na duniani kwa ujumla na hadi sasa kazi hiyo bado inaendelea kupitia makundi na taasisi mbali mbali (UAMSHO, KAMATI YA MARIDHIANO, UMOJA WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU, nakadhalika) na matokeo yake tunayaona leo hii.
Tunapotofautiana na mawazo yako usihamaki na kusema hatukusoma uliyoandika, uelewe kwamba si lazima kila mtu akubaliane na mawazo yako na hili ni la msingi kabisa na ndio maana hata hao hao viongozi wa ngazi mbali mbali tunawaeleza hayo wasikilize wananchi wanasema nini sio watulazimishe wanayotaka wao.
Kwa hayo machache kama utanipatia majibu ya msuala niliyouliza utakuwa umefanya jambo la busara la ikiwa huwezi basi nyamaza tu na wala usilete malumbano, huu ni wakati wa kuipigania Zanzibar huru tuwe kitu kimoja, tuelimishane, na hatimae tuifikie hiyo Zanzibar huru tunayoitaka.
@Bablee
Naona nilikupa sababu kwa nini viongozi wa Zanzibar hawataki Zanzibar ikomboke kutoka utawala wa Tanganyika. Lakini kama hukuelewa nitakueleza zaidi. Sababu ni kwamba wao katika hali ilivyo hivi sasa ni manufaa zaidi kwao kwa sababu muungano huu ndio unaowaweka madarakani. Chaguzi kuu zote tangu 1995 CCM wanashindwa lakini viongozi wa juu wanakuja kutoka Tanganyika na kulazimisha nani atangazwe mshindi. Na wao kubaki madarakani ni manufaa kwa matumbo yao. Leo hii Zanzibar ikiwa huru, CCM haiko tena madarakani kwa sababu Watanganyika hawatakua tena na uwezo wa kulazimisha atangazwe mtu asieshinda uchaguzi.
Kiini cha mada yako kilikuwa ni juu ya ZANZIBAR KUWA HURU. Ukasema kutafautiana ndiko kunako kwaza lengo hilo. Mimi sikubaliani kwamba hilo sio tatizo, tofauti ni tofauti tu ziwe za kidini, kisiasa, kirangi kiitikadi au zozote hizo zote ni tofauiti lakini kwa Zanzibar hivi sasa kinachotakiwa ni MAJORITY wawe na uwamuzi mmoja na hilo lipo. Nimekupa mifano mitatu ambapo Wazanzibar pamoja na tofauti walizonazo wameonesha kukubaliana kwa 66%. Hiyo inatosha kabisa kuwafanya washinde kura yoyote ile kama itakua ya haki na huru. Kwa hiyo pamoja na kuwepo hizo tofauti lakini hazizuii Zanzibar kuwa huru, kinachozuia ni hao viongozi walioko madarakani kwamba wanahofia madaraka yao. Sio lazima watu wawe100% kitu kimoja, hilo halipatikani popote pale ulimwenguni.
Mimi nachallenge kama leo itapigwa kura ya maoni juu ya kuutaka au kutoutaka muungano basi Wazanzibari 66% wataukataa muungano, na huo ni ushindi wa kutosha kwa Wazanzibari. Watakao kuwa na tofati zao za kidini, kisiasa, kiitikadi au kirangi sawa wacha wabaki nazo lakini hazitoathiri ushindi kwa Wazanzibari waliowengi.
mada ninaiunga mkono sehemu moja tu kuwa kuna ccm tanganyika zanzibar hawa ndio sababu ya yote haya kina shawana seif khatib hwa ndio sababu ya yote hayaa
ila zilizobaki ni pumba juu ya zanzibar mumngu akipenda zanzibar huru itakuja
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/370593-makinda-atabiria-kifo-ccm.html#post5254549
Makinda atabiria kifo CCM
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda
• Mangula atoboa siri ya uteuzi wake
na Mwandishi wetu
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kujiondoa chenyewe madarakani kutokana na tabia ya baadhi ya viongozi kutanguliza maslahi binafsi badala ya chama na wananchi kwanza.
Makinda alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwasalimu wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Njombe, waliokutana mjini hapa.
Alisema utapeli ndani ya CCM unatisha na watu hawataki kujenga utamaduni wa ujamaa na kujitegemea na kusisitiza iwapo wanachama watashindwa kujitegemea, chama kitakufa.
Alisema hata rushwa kwenye uchaguzi wa CCM inachangiwa na baadhi ya viongozi wasiopenda kufanya kazi na kutegemea kuchuma pesa za rushwa kutoka kwa wagombea.
“Rushwa ndani ya chama inatokana na tabia hii ya watu kushindwa kufanya kazi halali za kujitafutia kipato na kuishia kuwarubuni wagombea na kuwaomba fedha kwa ahadi ya kuchaguliwa. Iwapo wana CCM wataendelea kuomba fedha katika uchaguzi ni mwanzo wa kuua chama na hata vyama vya upinzani haviwezi kuiua CCM ila CCM itajimaliza yenyewe kwa tabia yake,” alisema.
Alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wapiga kura wa jimbo lake ambao wamekuwa wakimchangamkia na kumsalimia na mwisho wa salamu, huishia kuomba pesa.
Makinda amewataka viongozi wa CCM kurejea misingi ya kiapo cha mwachama na kukifanyia kazi kiapo hicho ambacho kinatamka wazi kuwa sitatumia cheo changu kwa maslahi yangu na iwapo kiapo hicho kitaendelea kukiukwa kwa baadhi ya viongozi wanaochaguliwa kugeuza nafasi zao ni mitaji ya kuombaomba fedha kwa wabunge, chama hicho hakitadumu.
“Mimi mwenzenu jana baada ya kumaliza mkutano wa mapokezi ya Mangula nilianza kucheza ngoma na muziki na wananchi waliofika katika mapokezi hayo, cha ajabu wengine walikuwa kukisalimia na kuniomba pesa ….sasa hii ni hatari sana kama watu wamekuja wenyewe katika mapokezi baada ya kumaliza mkutano, wanamvamia mbunge na kumwomba pesa,” alisema Makinda.
Kutokana na hali hiyo, Spika Makinda aliwataka wanachama wa CCM kufanya kazi na kuwa na shughuli nyingine za kuwaingizia kipato badala ya kuendelea kuwavizia wabunge na kuwaomba pesa na wasipopewa wamekuwa wakiwachukia na kukichukia chama.
Makinda aliwataka pia wajumbe wa mkutano huo kuwa na miradi ya kiuchumi au kujiunga katika kilimo badala ya kuendelea kuomba fedha kwa wabunge.
Alisema hivi sasa watu wamechoka kuombwa fedha na hata waliokuwa wakikisaidia chama, pia wamechoka hivyo lazima CCM ijitegemee kwa kuwa na miradi ya kiuchumi.
Wakati huohuo wajumbe wa mkutano huo wamemchagua kwa kura za kishindo mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa toka wilaya ya Njombe baada ya kupata kura 37 kati ya kura 45 zilizopigwa kati ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Njombe.
Akitangaza matokeo hayo katibu wa CCM mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike, alisema katika wilaya ya Ludewa kulikuwa na wagombea watatu katika nafasi hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa, Matei Kongo, aliyepata kura 25 na Damiani Mwapinga aliyepata kura 24 na washindi ni wajumbe Filikunjombe na Kongo.
Walioshinda katika ya wilaya ya Wanging’ombe na kura zao kwenye mabano ni Anaupendo Gombela (36) na Happiness Bomba (31).
Washindi kutoka wilaya ya Makete ni Elizabeth Haule (28) na Francis Chaula aliyepata kura 23.
Wakati huohuo, mbunge wa Ludewa, Filikunjombe, amewalipua watendaji wabovu serikalini, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, bara, Philip Mangula.
Filikunjombe ambaye alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe, alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kusababisha wananchi kukichafua na kukichoka chama tawala.
Hivyo alisema kuwa imani ya wana CCM kwa safu mpya ya uongozi chini ya Katibu Mkuu Abdalaman Kinana na Makamu Mwenyekiti Mangula na Makamu wake Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein, na viongozi wengine ndani ya CCM ni matumaini mapya kwa wana CCM na tishio kwa vyama vya upinzani.
“Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe, chama chetu CCM ni chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete, Mangula na Kinana ni safu ya uhakika na itakiwezesha kuendelea kuaminiwa zaidi na Watanzania …ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao,” alisema.
Kwa upande wake Mangula mbali ya kusifu mapokezi aliyopata, alitoboa siri ya uteuzi wake kwamba alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi huo na kwamba alishangaa sana kupokea simu ya Rais Kikwete na kumueleza kuhusu kusudio la uteuzi huo.
“Kweli mimi nilikwenda Dodoma katika Mkutano Mkuu wa CCM kama mualikwa ila nikiwa hotelini nilipokea simu ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete, akiomba kuniteua kuwa Makamu Mwenyekiti na baada ya kwenda ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio…kweli namshukuru sana Mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha,” alisema Mangula.
Alisema hatafanyakazi kwa kulipa kisasi kwa wana CCM waliokuwa hawaelewani naye.
Chanza Tanzania Daima
“Lipo kundi ndani ya CUF wanaomini kwamba ili uwe mzanzibar halisi lazima uwe na rangi nyeupe japo kidogo”
“Huko CCM kuna wanaoamini Mzanzibar halisi ni mweusi, hawa weupe ni vibaraka wa sultani tu”
kamanda muandishi asante kwa mada yako hii,hayo hapo juu mimi nayaita “Jini litulalo limo nguoni mwetu” . Bila ya wazanizbar kuyondoa hayo katika utamaduni wao basi zanzibar itaendelea kutawaliwa mapaka mwisho wa Dunia
“Divide and rule” wakoloni weni wanatumia kuwagombanisha wanaowatawala ili wapate nguvu zaidi ya kutawala,
Thank god I am not mpemba,lakini nawaheshimu wapemba kama ndugu zangu,nawambia ndugu zangu wakipemba bila kuacha ubinafsi zanzibar itaendelea kuwa kama ilvyo.
Nnane rafiki yangu kutoka pemba ambae ni mweusi hana hachanganya na uarabu,amewahi kuneeleza vipi alinyanyaswa na ameshawahi kuambiwa kuwa CUF in kwa wapemba wenye rangi,Jamaa aliamua kujiunga na CCM
@BABLEE
Wewe ni Mgeni na mzalendo net?Kama ni mgeni ngoja nikuibie kidogo!Hapa ukitaka support lazima uitukane CCM na uikandie vya kutosha,halafu isifie CUF na Alhabiiib wetu.Hapa hata kama uliyosema ni ya kweli lakini kama hayawafurahishi Uongozi wa mzalendo net i, e Ashakh(Kiongozi) na wenzake mada yako itafutwa na maoni yanayopingana na wao watayafuta.
Ulichoandika hapa ni ukweli mtupu,na tunayo mifano hai!Na asilimia kubwa ya wachangiaji na waandishi wa makala humu mzalendo net wapo kwenye kundi la Pili na la tatu.Wengi humu ni CUF na wanaamini kabisa wao ndo wazanzibar halisi na wao ndo wenye uchungu na Zanzibar.
Wapo humu wanaoamini kuwa maoni yao ndo sahihi na ya wengine hapana!Humu watu wanauwezo wa kujua rangi yako kwa kusoma maoni yako tu.
Kundi la CUF sera NA ccm SERA sera wapo wachache sana kwa bahati mbaya,lakini hili ndio kundi linalohitajika kwa ukombozi wa Zanzibar.Na bahati mabaya zaidi kundi hili hata kwenye Mzalendo net halipo.
Mwisho hongera mwandishi kwa kuuusema ukweli.Humu watu husoma vichwa vya habari tu kisha hutoa maoni,hawasomi mada yote kwa hiyo usikate tamaa kwa maoni ya fikra mgando.
Hili kundi la pili ndo hatari zaidi kuliko makundi yote!Ona CUF anaweza kuja mamluki na akashika mpaka ngazi ya juu ya uongozi kwa sababu ni mweupe tu,na vile vile watu weusi wanaweza kuogopa kujiunga CUF kwa sababu hizohizo za kubaguliwa tu.CUF ina uwezo mkubwa wa kushinda Zanzibar lakini kosa kubwa ni hilo la kujinabisisha na uarabu.Kwa CUF mzanzibar halisi ni yule mwenye rangi nyeupe au aliye na asili ya ajemi.
Kwa CCM hivyohivyo ukiwa mweusi tu hata kama si MANZIBAR HALISI watakukumbatia na watakupa madaraka mpaka ya ngazi za juu,Refer BI kastiko saga!Wabara wengi sasa hivi wanapata kazi Zanzibar bila usumbufu wowote kwa sababu ya rangi tu.Wazanzibar halisi wanakosa kazi kwa sababu ni weupe.
Na ili uwe kiongozi wa ngazi ya juu AU MGOMBEA URAISI KWA CUF Zanzibar amini lazima uwe mweupe kama maalim ukiwa kama Machano au Duni utaishia umakamo.Upuuzi huu na kwa CCM vilevile lazima uwwe mweusi na umeusikana na bara kidogo ndo utapata madaraka makubwa refer Maraisi wote wa Zanzibar!
@SHAMUHUNA
“Kwa CCM hivyohivyo ukiwa mweusi tu hata kama si MANZIBAR HALISI”
“Kwa CUF mzanzibar halisi ni yule mwenye rangi nyeupe au aliye na asili ya ajemi.”
Sadakta SHAMUHUNA kama haya mambo wazanzibari hawakuyatoa katika itikadi zao basi zanzibar itabaki vile vile…
Nakumbuka nilikutana na jamaa mmoja katika ndugu zangu wa kipemba alinimbia kuwa Unguja haina mwenye,mimi nikamuliza Pemba je? akasema Pemba ina wenyewe,nikamuuliza sasa hawa mabibi zetu walioishi hapa kabla hata hao warabu hawajafika hapa vipi? akanyamaza kimya
kama kasumba hizi hazikuondolewa basi zanzibar itabaki kama ilivyo
@Mwanafunzi nakuomba tena isome mada yangu kwa utulivu, huenda ukaelewa…naona kwa mara nyengine tena maoni yako hayaendani na mada yangu! Hivi ni kweli suluhisho lililopendekeza ndilo wanalo lifanya UAMSHO, KAMATI YA MARIDHIANO, UMOJA WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU? Maana mie sijatoa suluhisho la kuwafundisha wa zanzibar haki na wajibu wao, wala kuwafundisha faida zakuwa huru, wala athari za muungano. Hilo nna hakika mpaka sasa wanalijuwa! Soma tena suluhisho nililopendekeza kwa utulivu, kisha nambia limefanywa na kundi gani? Kwanza suluhisho hilo halifanywi bali ni jamii nzima ya wazanzibar, ni mabadiliko kutoka kwa kila mtu na kizazi chake! Nisome tena balahau!
@Msemaji mkuu, Mfano wako wa kura ya maoni zizilizo pigwa Zanzibar kuhusu SUK ambapo 66 % walisema ndio na 33 % walisema hapana, haujaonesha kwamba uwepo wa makundi hayo nliyo yataja yanayohasimiana ni faida kwa maendeleo ya Zanzibar, lakini ndo yameonesha kwamba ni hatari kwa maendeleo ya Zanzibar!
Hivi wewe kwa akili zako ulitegemea watokeze watu 33 % wakatae amani, yaani watu 33 katika kila watu 100 wanakataa kuishi kwa amani na ushiriakiano! Hivi na hili pia waliona ni lakawaida?!
Basi kwa wapembuzi wa mambo huu si ushindi wa kufuarahia, wala si kielelezo chema, kumbuka hii haikuwa kura ya kuchaguwa CHAMA ilikuwa ni kura ya kukubali amani na upendo na kusahau yaliyopita au kutokubali kheri na tuendeleze shari! Sasa 33 % wanachaguwa shari! We bado waona ndo mfano! Tena hapo ni baada ya viongozi woote wa CCM na CUF, kupiga kampeni nchi nzima kuwaomba watu wapiga kura ya ndio! Na bado kuna 33 % wakasema hapana! Usiangalie figure (namba) tu lazima ujaribu ku interpret hizo namba, kisha jiulize hivi kweli Mzanzibar, tena muislam akataa kheri? Kuna nini? Ndo mwisho utaelewa nilichoandika hapo juu! Hilo sio la kawaida!
Jee CCM wangehamisashina kwa nguvu moja na wakatumia hila zao kama wafanyavyo kwenye uchaguzi wa rais hizo 66 % zingepatika? Wala usiniambie oooh, mbona kwenye kutoa maoni ya katiba 66 % wametaka mkataba! Kuchukuwa idadi ya watoa maoni katika katiba ukataka u relate na kura, ni kujitia uchizi usiokuwa nao! Mana wajuwa fika kwamba ili upige kura lazima uandikishwe kwenye daftari la kupiga kura, halafu hiyo siku ya kupiga kura jina lako likaonekane kwenye mbao za matangazo! Wajuwa fika kwamba daftari lilompa Dr Shein ushindi ndilo hilo hilo litakalotumika kupiga kura katika katiba mpya….jee hao wa mkataba walotoa maoni wakafika 66 % watapiga kura wapi? Halafu lazima ujuwe kwamba katika kutoa maoni CCM hakutumia nguvu kubwa sana, sababu wengi wanajuwa kwamba huo mkataba ni porojo tu, wao washapendekeza serkali 2 kule DODOMA, na ndio itakayokuepo kwenye rasimu, mtapambana kwenye kura ya ndio au hapana! Na mwisho tume ya itakayosimamia kura ndio kuhusu rasimu ya katiba ndio iliyosimamia kura za rais wa Zanzibar 2010, what do you expect?
@Abdul jipe moyo kama mgonjwa wa UKIMWI na ARV! Lakini kwa chuki na visasi Zanzibar huru sahau!
@Jazz Ahsante sana kwa kunielewa ndugu yangu, kweli darasa moja mwalimu mmoja lakini wengine hupata 0 % na wengine 100 %! Wewe umekuwa mkweli wanafsi yako na umenielewa vizuri, tuendelee kuwaelemisha na hawa wengine (japo wanaujuwa ukweli), ila ni asili yao kukataa kila wasilopenda kusikia!
@Shamhuna Ahsante maalim wangu, kuna watu wanapenda uwongo ilimradi uwe unawafurahisha na kuwasifia, lakini wanachukia ukweli unaowakosoa hata kama unawajenga! Ila amini kwamba ukiwaambia ukweli hata kama watakupinga kwa maandishi hapa Mzalendo, lakini nafsini mwao wanakiri na kuumia! Endelea kuwapa dozi maalim usichoke!
@Shamhuna
Kwa CUF mzanzibar halisi ni yule mwenye rangi nyeupe au aliye na asili ya ajemi.
Kwa CCM hivyohivyo ukiwa mweusi tu hata kama si MANZIBAR HALISI watakukumbatia na watakupa madaraka mpaka ya ngazi za juu,Refer BI kastiko saga!Wabara wengi sasa hivi wanapata kazi Zanzibar bila usumbufu wowote kwa sababu ya rangi tu.Wazanzibar halisi wanakosa kazi kwa sababu ni weupe.
Na ili uwe kiongozi wa ngazi ya juu AU MGOMBEA URAISI KWA CUF Zanzibar amini lazima uwe mweupe kama maalim ukiwa kama Machano au Duni utaishia umakamo.
Kama ni kweli hayo maneno ya Basi CUF ndio chama cha Wazanzibari.
Lalkini mimi nafikiria Zanzibar tatizo sio Rangi tatizo ni Uunguja na Upemba. Kuna watu wanaamini ya kwamba Wanamapinduzi nu Watu wa Unguja na waliopinduliwa ni Wapemba, kwao wao ni mwiko kwa mpemba kuchukua uraisi wa Zanzibar.
Kuhusu Rangi wazanzibari sio weusi tititi, isipokuwa ni shida zinazowafanya hivyo . Umesema Juma Duni akipewa uraisi kesho atakuwa mweupe kama Salimini. Kwani huyo Salmini hivi sasa ni mweupe tena kama alivyokuwa raisi?
Wewe ni mmoja wao!Soma vizuri maoni yangu utanielewa,nimesema kwa sasa Zanzibar unaweza ukawa Mzanzibar halisi na ukakosa kazi sababu ya weupe tu hata kama ni mzanzibar halisi.Sijasema kuwa Mzanzibar halisi ni mweupe!
Eti kuhusu rangi wa Zanzibar sio wusi tititi,unaamanisha nini?Msome vizuri mwandishi amegusa mwote humo.Na wewe kwa kusoma tu maoni yako nimeeshakujua wa kundi gani.Kwa ubaguzi huu Zanzibar huru ni ndoto!!!!!!!Hata miaka Elfu mbili mingine,Shamba kwetu donge tuna msemo kwa jambo lisilowezekana “MIHUDI”Nami niseme kupata uhuru Zanzibar mihudi.
Eti Shida ndo zinawafanya watu wawe weusi,acha matusi hayo,mbona Maalim hakuwa MWEUSI pamoja na shida zote za kukaa gerezani?Kama wapigania Zanzibar wenyewe ndo aina hii ya kwako wewe tusahau huo mnaouita UHURU wa Zanzibar!
@SHAMUHUNA hahahaha wawaona hao akina wa mtambwe basi ndo sampuli ile….wamejaa tele japa Mzalendo! Hivi we wa mtambwe unafikiri ukisham’baguwa na kumkashifu mtu kwa rangi yake au asili ya kisiwa chake, wategemea itatokea siku atakuunga mkono hata kama hilo jambo unalolisimamia ni jambo jema? Yaguju!
Lazima kwanza muondokane na huu upuuzi wenu, la sivyo itakula kwetu (wazanzibar ) siku zote!
Namnukuu SHAMUHUNA “..kupata uhuru Zanzibar mihudi”
@ Nimesema rangi kwa Maksudi, kwa sababu najua ya kwamba Zanzibar hapana Mtu mweupe kuna baadhi yetu ni weusi sana na wengine kidigo wanangara lakini sio weupe. Kama kuelewi mtu mweupw ni nani uliza utafahamishwa, Ikiwa waarabu kutoka Dubai, Wahindi, Red Indians, Waasia wote hao hawachukuliwi kama ni watu weupe duniani, Zanziba kuna waswahili hata kama wanaasili ya Oman, India, Persia wote hawa ni waswahili. Ni sawa na Marekani hivi sasa Wamarekani weusi waliozaliwa Kule huwezi kabisa kabisa kuwalinganisha na Waafrika waliozaliwa Afrika.
Sisi tunachokita na Zanzibar huru ya Wazanzibari, kama wanaasili ya Bongo (mrima) India, China, Oman, kuwweit, Iran Iraq wote hawa ni wazanzibari sasa
Kazi kweli kweli
@Bablee
“Lazima kwanza muondokane na huu upuuzi wenu, la sivyo itakula kwetu (wazanzibar ) siku zote!”
wewe ulikuwepo wapi siku zote hizi,wambie ndugu zetu wakipemba hali halisi ilivyo,hawatambui kuwa bila ya waunguja kuridhika na harakati zinazoendela hamna kitakachofanyika!!! itakula kwetu wazanzibari (wanguja na wapemba)
@Stone town(Kiongozi)
Sema chochote yakhe,dada yangu Ashakh(Kiongozi) vipi mbona kimya kwenye ukweli huwa mnakaa mbali kabisa lakini ngoja ziwekwe pumba hapa muone mnavyotokwa na povu la mdomo!
Ni watu na nadharia zao kila sehemu haziepukiki, hoja nyingi hazina mshiko kuzinasibisha na chama moja kwa moja ila ninavyofahamu kipo chama kimoja kinawatetea wazanzibari bila kujali rangi zao, asili zao wala makabila yao, lakini pia kipo chama chengine hakipo kuwatetea wazanzibari na ndio mana kimepoteza mvuto kisiasa na kinazidi kuanguka kila leo.
Kuwepo kwa watu wachache (kundi fulani) lenye nadharia fulani kwa watu fulani kwa lengo fulani haimaanishi chama fulani kina sifa fulani ila itabaki ni sifa ya kundi lenye nadharia fulani katika chama fulani.
Kuwepo kwa watu wachache kwenye familia wenye tabia ya kulewa haitomaanisha kwamba familia hiyo ni ya walevi.
zipo baadhi ya hoja zina ukweli fulani ila zaid zipo kishabiki hazikigusi chama husika na nadharia hizo inabaki ni mawazo ya kundi fulani tu.
kazi ipo.
msilete chokchoko za kuleta fikra mbaya na kurudisha nyuma nguvu ya wazanzibar ya kujitafutia uhuru wao!wala msitukatishe tamaa!hayo mambo ya rangi kama yapo basi ni kwa wajinga wachache wasijua historia ya znz.kwa anaejua vizuri basi rangi haina nafasi.
sijui watu hua wanatumwa ili kutafuta mbinu ya kuwagawa wazanzibari?
jamani waznz sote mweusi, buluu ,kijani mwekundu, mweupe or any colour au chama chochote anaeitakia kheri nchi hii na wananchi wake tujifinge kibwebwe msimamo ni uleule ZANZIBAR KWANZA na inshaallah tutashinda.
Mhh…. Sibure, hapa pana kizabizana inaoonekana inaweza ikaingia maanani ikiwa labda asilimia fulani ina waiwasi na mabadiliko yakija haraka zaidi kuliko walivyotegemea.
Ila kwa zanzibar nikuwa huru kwanza naikiwa nia ipo kwenye Uzanzibari basi itawezekana
na inawezekana kwani kama maoni ndio hayo ila ikiwa ni ubinafsi basi sawa,lakini mimi naona
kwa sasa uchama, urangi uunguja na upemba sio ishu kwa wengi,zanzibar huru ndio ishu hapa
ikiwa sio leo au kesho kutwa hilo ni jengine, ila naweza kufahamu kiasi fulani mtoa maada wapi umelenga ila wapo wana wazalendo wenzako mtabadilishana mawazo.
Kwa kumalizia Zanzibar ni ya Wazanzibar na itarudi kwa wazanzibar.
BABLEE.. nilikuwa kazini sasa nimerudi lakini kabla sijaendelea ningependa kukuuliza unavyofahamu wewe ZANZIBAR HURU ni vipi? Hata ukaushirikisha u cuf na u ccm, urangi? Ukasahau wazanzibar wasioshabikia vyama vya siasa?
binafsi hushangazwa sana na watu wanaoamini kua matatizo yetu hayahusiani na rangi wakati hilo hasa ndio tatizo lenyewe na huo uunguja na upemba, mfano ni hapo juu mchangiaji anaposema kua znz hakuna mtu mweusi titii maana yake nini mzanzibari hawezi kua mweusi? au kua mweusi ni shida ya maisha, juzi kati nilikua na banchi mmoja hivi akawa anasoma kitabu flani cha kitalii (free edition) kulikua na picha ya vp2 jamaa akaisogeza ile picha juani akasema “afadhali hapa anaonekana kidogo” nikamuangalia jamaa yaani yeye na huyo vp2 kiufupi hawachekani.nyani asieona kundule. bila ya kuaddress the real issues tutabaki kunyoosheana vidole, kuna zingatio muhimu alilotoa mtoa mada kuhusiana na kura ya maoni,kuna wana ccm wengi ambao hawakupiga kura ile ambao kama wangepiga wengi wao wangepiga kuikataa gnu hivi kuna faraja gani kuona asilimia 33 ya wazanzibar hawataki zanzibar huru? ni kwa nini watu wengi hivi hawataki kuondokana na mfumo huu ambao hauna tija na znz?wakati kimsingi wanakubaliana kua kero zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi. @ stonetown njoo ujionee legacy uliotuachia ya kutukana wabara mji mkongwe ubaguzi ni ubaguzi tuu ili uupe uhalali unauvalisha koti lolote tuu. najiuliza kama wangekua waarabu wa tabora ungewakashifu kama vile. i cant stand bigots
Mimi hii mada sikubaliani nayo, kwa sababu imejaa chuki za kibaguzi na sio kweli kabisa, ispokuwa nakubaliana na kundi ambalo linarejesha nyuma mabadai yetu wazanzibari, ambalo kundi hili limo ndani ya ccm, hawa wote sio kwa sababu ya ubaguzi tu, bali ni kwa maslahi yao binafsi, njaa zimewakaa moto, hawa watu hawakusoma na ndio maana wana njaa za madaraka, wanachokiamini kwao zanzibari huru ikipatikana basi wamekufa njaa na madaraka kwao ndio imetoka.
Msomi wa kweli always huwa anajiamini katika kupambana na maisha, msomi huwezi kulaghai kwa upande wa kanga, hata hao wasiokuwa wasomi basi yule mwenye akili timamu ambaye mwenye uzalendo huwezi ukamghai kwa upande wa anga ikisha akaseme mbele ya binadamu wenziwe na kusifu mapinduzi ya mauwaji ya waislamu au binadamu yoyote na muungano.
@Bablee
Baba yangu ni mwanasiasa ,miaka 20 sasa toka kuanzishwe vyama vingi,napata akili zangu timamu naona harakati za mzee wangu katika siasa, mimi ni mmoja ambaye nikimsaidia baba yangu kutengeza bendera za cuf, na katika chama hiki cha cuf yeye alikuwa mwenyekiti wa wilaya ya mjini maghribi mpaka akaamua kuwacha wazifa huo yeye mwenyewe, na mara nyingi kunapotokea uchaguzi wa kuchagua viongozi wa chama basi anapita, rangi yake ni mweusi hana asili ya rangi nyeupe ,nyumba yetu ndio ilikuwa ngome kuu ya cuf ukiwacha ile ya kule Amani makao makuu.
Kati ya wahaini wa 1996 mzee wangu yumo, sikutafunii maneno kama unataka ushahidi niwachie email nikutumie, au kama unataka kuuliza kwa huyo maalim seif mwenyewe atakuwambia, hakuna chama kisichokuwa na rushwa hilo kwa ufahamu katika uteuzi, hilo mimi nishalishuhudia mwenyewe, na mara nyingi katika uteuzi inatokea kuwa na wapinzani wengi, lazima upite mchakato wa uchakachuawaji,hilo ufahamu, sasa hao wanao kuwambia kuwa eti anaangaliwa rangi sio sio kweli, kinachoangaliwa sana uzalendo, uwajibikaji katika chama, pia zaidi ujikubalishe kwa viongozi wengine, ili uweze kuchakuguliwa katika chama, iwe mwenyekiti, au kugombania ubunge au uwakilishi vyovyote vile uchakachuwaji ni lazima, hapo ni bahati yako, na mara nyingi hupitishwa watu kwa kura, huyo maalim seif huwa hana uwezo wowote, member wenyewe ndio wanao kupigia kura sasa niambie huyo muakilishi wako alipita vipi ? Au maalim seif alimwambia tu kuwa tunakupa ugombee wewe uwakilishi kwa juhudi zake ?
Mbona juma duni mweusi,abubakar na wengine ? Hivi ni chuki za kibaguzi ambazo zinawala sana watu kama nyinyi, unajua watu ambao hawana elimu iwe ya dunia walakhera basi tunatakiwa tukae nao mbali sana, kwa sababu za kipuuzi kama hizi za kibaguzi, ubinafsi, kama hawa kina borafia tunao waona, ukiangalia cv zao hawana lolote vichwani mwao.
Ubaguzi baina yetu upo kila pembe ya dunia,weupe kwa weupe wanabaguana, weusi kwa weusi pia wanabaguana, mweupe kwa mweusi vile vile, pia utaifa kwa utaiufa,hilo lipo,lakini tusichukulie big deal, wenzetu walichoweza kuwa nchi zao zina misingi ya sheria, huwezi kumbagua mtu kwa ulemavu, rangi, nationality,sexuality,na mengine, ikitokea hilo vyombo vya sheria vinakuhukumu.
Tuache siasa zilizo pitwa na wakati, tufungue ukurasa mpya, zanzibar kwanza, hichi ndio cha msingi, tuwaombee dua hawa waovu wetu waongoke,hicho ndio cha msingi, siku zinavyokwenda mbele watu wanazinduka,tatizo hapo awali kulikuwa na ukosefu mkubwa wa elimu ndio maana wale ambao wachache walisoma walitumia mwanya huo kututawala na kuwagawa watu kimakundi.
Alhamdu llah leo hii tuna toa wasomi wengi ambao vijana nguvu kazi, angalia tuna vyuo kibao hapa zanzibar kila mwaka wanafunzi zaidi 800 wana graduate, hebu piga hesabu miaka ya 2000 kuja chini wanafunzi wangapi wana graduate zanzibar ? 10 tu ambao hupelekwa Mlimani !
Kizazi cha leo huwezi kumwambia maneno ya kama hayo uliyo yaandika sasa hivi, dunia imekuwa tandawazi, kama hukusoma skool utasoma kwenye tv, angalia sasa hivi kila mtu nytumbani kwake kuna kebo.
Hapo awali watu wanaangalia tv au kusikiliza redia kwa mjumbe wa nyumba kumi, ikimaliza tarifa ya habari kazima redio yake utammalizia charge zake za betry.
Ndugu yangu zinduka uko dunia gani wewe ?
Zanzibar kwanza. Uwamsho – wacha tupumue, CUF- Haki sawa kwa wote.
@Ghalib
Nimejaribu kukusoma mara mbili lakini sijapata hasa unachokusudia kusema…kwanza unaonesha mada hujaielewa au umeamuwa kuilewa sivyo! Kwenye mada nimeweka wazi kwamba wenye mtazamo wa u- rangi kwenye CUF na CCM ni kundi moja katika makundi! Sio CCM wote wala si CUF wote! Hivyo pamoja na uwepo wao bado hawawezi kuathiri maamuzi ya ndani ya vikao vyao CUF kwa sababu kwa CUF kundi hili ni kundi moja katika matatu (1/3 ) na kwa CCM kundi moja katika manee (1/4)! Na ukisema Maalim Seif hana hawezi kuamuwa lolote kwa wagombea wa uwakilishi au ubunge…balahau wajidanganya AU hujui yanayotokea ndani ya CUF wakti wa kuchaguwana! Hivi huna habari kwamba hata Hamad Rashid alipata kugombea tena baada ya kubebwa na Maalim Seif, lakini huko shinani, tawini mpaka wilayani walishamkataa, na wengine wengi tu, walipata nafasi kwa recommendation ya Maalim, lakini vikao vilishawakataa! Muulize huyo Babeyo atakwambia!
Ghalib, unaniita mie mbaguzi, nanukuu “Hivi ni chuki za kibaguzi ambazo zinawala sana watu kama nyinyi…” Sijui kwa kutumia hoja ipi unaniita mie mbaguzi wa rangi, nlitegemea uniite mpinga ubaguzi, maana kwenye mada yangu ni address na kukemea wabaguzi wa wrangi kutoka pande zote! Lakini nshakufahamu, ulipenda niwashutumu CCM tu, maana CUF kwenye CUF hakuna wenye makosa wala wabaguzi! Sasa hili lakukutajeni wabaguzi wa rangi kwenye CUF kwamba pia wamo basi limekukera na mada yangu yote ukaiona sio, namie nikawa mpuuzi! Hongera kake!
Halafu unajichanganya…maana unakataa hakuna ubaguzi wa rangi wala hauathiri harakati za upatakanaji wa Zanzibar huru lakini wakati huo huo unasema nanukuu ” Tuache siasa zilizo pitwa na wakati, tufungue ukurasa mpya, zanzibar kwanza, hichi ndio cha msingi…” Naona ume summarize suluhisho nililolitoa katika mada yangu. Kwa vile hujaona tatizo, wala hakuna ubaguzi wowote, nlitegemea useme hivi ” Tuendelee tu hivi hivi, hizi ndio siasa za kisasa zilizopo ulimwenguni kote na Zanzibar huru tutaipata kupitia katiba mpya ya Warioba”
Halafu nashangaza umeweka miguu yako yote kutetea kwamba hakuna wenye mtazamo wa u rangi kwenye CUF lakini unakubali kwamba CCM wapo…ebo! Wajifanya kipofu wakati unamacho. Na jee hata wapinga mapinduzi CUF hawapo? Njoo unijibu tena kwamba ndani ya CUF hakuna wanaoamini kwa dhati kwamba mapinduzi ni haramu na aliepinduliwa ni Mpemba! Njoo ujitie tena uziwi unambie baba yako ni ni muosha bendera za CUF na nyumbani kwenu ndimo anamolala Seif Sharif lakini hujawahi kuwasikia wanaopinga mapinduzi! Njoo unambie kwamba uhasama huo wa Mapinduzi daiama sababu aliepinduliwa ni Sultani wa kirabau na kibaraka wake mpemba vs Mapinduzi haramu aliepinduliwa ni Mpemba hayapelekei kuigawa Zanzibar mapande mawili ya Unguja na Pemba!
Njoo hapa unambie kwamba hao vijana wanaosoma hivi sasa kwa wingi ukiwemo wewe msomi sana, mnaofundishwa mapinduzi kwa mitazamo miwili tofauti kwamba hamjengi chuki baina yenu! Njoo unambie kwamba wewe binafsi huyaoni kwamba Mapinduzi ni haramu!
Kama hujui ubaguzi hauondolewi kwa kusoma, ni kuamuwa tu! Kama elimu ya ondoa ubaguzi, basi Afrika kusini wale makaburu walikuwa na elimu kuliko wa afrika lakini wao ndio waliokuwa wabaguzi wakubwa! Na vile vile chuki za mitazamo haziondoshwi kwa kusoma wala kuangalia TV…kama elimu Dr. Bilali ni msomi wa PhD na bado anaamini Mapinduzi yalimuondoa Sultani na kibaraka wake Mpemba, na Jussa ni msomi wa sheria na yeye anaamini mapinduzi yale ni haramu yalimuondoa madarakani Mzanzibar mwenye asili ya Pemba wala hakuwa kirabaraka!
Hata musome mpaka kila raia awe na PhD, na mufunge kebo mpaka kwenye mabanda ya kuku na mavani, bila yakuondokana na hayo makundi mawili hasimu niliyoyataja hapo juu, kamwe WaZanzibar hatutakuwa pamoja katika kudai Zanzibar huru na hilo litatuchelewesha sanaa kuipta Zanzibar huru!
@Bable
Bado unaturudisha kule kule tunakotoka,zanzibar hakuna siasa ya ubaguzi wa rangia ambao unaotufanya tusidai zanzibar huru, ni ujinga tu wa kisiasa ambao unaotutawala kwa kutumia vyama,lakini ukweli uko pale pale,tunaowana baina yetu mweusi mweupe, au hujui hilo ! Umeondoka zanzibar baada ya mapinduzi wewe !
Hii mada nimeosoma yote ,nimeifahamu 99 %
Naona sio mimi ambaye nilikuwa sijakufahamu,hata walio nitangulia huwaoni ! Hivi hata maoni ya katiba hufatilii, kama utafatilia hilo utagundua kuna makundi gani !
Unasema mapinduzi kapinduliwa mpemba kivipi ? Hebu nieleze nikuelewe, hivi hujui kwamba mapinduzi tumepinduliwa wazanzibari ! Unasema mpemba ! Inamana sisi waunguja jee hatukupinduliwa !
Kwa kweli hata wewe nashindwa kukuele umekusudia nini mada yako,umetuchanganyia mtama na kunde,kama unaongea ubaguzi wa rangi basi ungejaribu kutochanganya na siasa kwa sababu utakuwa unatuvuruga sisi na vizazi vyetu,naona kama hii mada ina uchochezi baina yetu
Narejea tena” UHURU”wanaoutaka si ccm au cuf tu namaanisha vyama na wanasiasa wao,ni Wazanzibari tena waliowengi wanataka zanzibar yao msituletee usiasa wenu, uko uko kuna watu zaidi ya hao kumi na nne na elfu sita zanzibar na ukizingatia population ni milioni na kitu hawajenda kutoa maoni yao kwa sababbu kama hizo mnazozizungumza,wanasubiri kura kwani kura kila mtu ni siri yake na hao ni wazalendo raiya wa kawaida hawafungamani na vyama
ndio maana hata kwenda kusimama juwani kuchezeshwa ukuti hawataki kuna wazanzibari kwa maana ya Uzanzibari wako nje ya zanzibar wakaazi nje tu ila ni wazanzibari wenye upeo wa kuyafahamu maisha yalivyo kwa watu na kwao na umuhimu wa nchi yao na vilivyomo ndani yake.
Hawa ni wengi na wanaitaka Zanzibar huru, hayo myasemayo yapo kila pahala hata kwenye kilabu ya mpira, sikubaliani nayo ati ndio yatachelewesha Uhuru kwa sababu tu ya fikira zao, ikwa ni hivyo ni ubinasi wao wenyewe,ikiwa wanahisi ni faida na waendelee, ila sisi Tunakwenda mbele na kama mashekh pia ni Upemba, Uunguja, Urangi, basi sasa na Wakwezi na wafuvi watasimama hadharani Muda si mrefu.
na nyinyi endeleni kucheza michezo yenu,Manaake sisi tukisema Kwenda nyinyi mnajitia kula, tukisema hema nyini mnasema kulala, Hamueleweki hamfahamiki, sisi hatutaki mtuambie mambo yenu ya ndani ya vyama hayo yenu nyinyi sisi Zanzibar Huru baadae tutajadili nani anataka rangi gani
na nani ana taka wapi shauri zao, hizo rangi na siasa watazifanjia wapi bila ya nchi na hizo rangi watajigambia wapi ikiwa hunapakuzionyesha
@Bable.Kila mtu ana mtizamo wake na maoni na nashimu mawazo yake ila ina onekana Mada inaanza kuelekea kwenye malumbano na vijineno vya udoho udoho vya kuzarauliana vimeanza kujitokeza nigependa busara zitumiike ikiwa wote tunalego na nia moja na kuipenda Znzibar yetu
na nyini mwenye kuyajua mengi mtupe kwa njia itakayotupa faraja, unajua saa njengine ukweli unauma hayo matatizo yapo na tunaishi nayo ila bado tumeishi mpaka sasa bila ya kugawana Ukaskazini na Ukusini, hiyo heri,hayo hanatengenezeka donda ndugu ni HUU MUUNGANO USIOFAHAMIKA. tukipata kuweka sawa hili natumai urahisi wa matatizo yetu ya ndani itakuwa
ni wepesi na nadhani viongozi hilo wameliona na ndio naona hayo mabadiliko yanoyoendele sasa.
M/mungu atatupa wepesi.
Zanzibar Kwanza.
Ah huyu BABLEE hisia zake mi zishanishinda ama sijui hajiamini na rangi yake au hajiamin na asili yake hata mi sijui,,BABLEE ukikulia (msingi) kwa elimu ya uongo na kuiamini basi matokeo yake hata uongozi wake ni mbovu kama huyo BILALI uliesema ana PHD (anaamini kuwa mapinduzi ya 64 kapinduliwa mpemba) anayofanya Bilali ama anayosema ni tofauti na anasema Jusa (anaeamini mapinduzi ya 64 ni zidi ya serikali halali ya zanzibar) BABLEE,, ubaguzi utakuwepo na utaendelea kuwepo hapo nyumbani na dunia nzima ama nipatie nusu nchi huru moja tu isiokuwa na urangi, ukuja, uasili ama uchama,, kumbuka kwamba mweusi ataitwa mweusi tu, na mweupe ataitwa mweupe, mpemba ataitwa mpemba, muunguja ataitwa muunguja, na kama unasubiri mweusi aitwe mweupe, mweupe aitwe mweusi, na mpemba aitwe muunguja ndio Zanzibar huru itapatikana, basi ni kweli Zanzibar huru si leo wala kesho,
@Gahlib and Sale.
Let us make this way… You are either too genius to understand my dumb topic or you are too imbecile to get my topic clear! Sorry, no effense meant! Thus, I can not help you by any means to grasp this piece of information! Therefore, I am out!
BABLEE …Tusen takk og jeg ønsker deg like til videre.
@BABLee n BRUCLee
Subra ndio iliowafanya Waislamu wakashinda baada ya madhila ya makafiri na mimi nakwambiya Wazanzibari watashinda bi idhni Llahi baada ya madhila tunayofanyiwa kwa wakati huu huu maadam harakati zipo ujue na mambo yapo .
Sale@Bablee;Translation,
Thank you so much I wish you the best forwards.
Got gjort Sale.
Sale@ Tack så mycket och lycka till!