YALIYOJIRI KATIKA SEMINAR KUHUSU KATIBA YA TANZANIA (UK)

Written by  //  01/03/2015  //  Habari  //  Maoni 7

katuni-nipashe-bonge-la-katiba-100214

Hatimaye Taasisi ya kijamii ya Uingereza na Tanzania (British – Tanzania Society, UK) wamefanya semina kubwa siku ya Jumamosi wiki katika ukumbi wa chuo kikuu cha London, SOAS hapa nchini Uingereza. Semina hiyo ambayo imeleta msisimko mkubwa kwa wajumbe na watu wengine mbali mbali waliouhudhuria umejumuisha wasemaje wakuu wanne, ambao walijadili mambo tafauti yahusianayo na katiba.

Semina hiyo ambayo mwenyekiti alikuwa Bwana Andrew Coulson, ilimwaalika msemaji Fredrick Longino ambaye alizungumza kwa upana matarajio ya wananchi hasa kwa upande wa bara juu ya katiba mpya. Msemaji wa pili alikuwa Profesa Abdul Paliwala ambaye alizungumza suala la katiba kwa mtazamo wa kisheria nchini Tanzania .
Yussuf Hamad, mhadhiri chuo kikuu cha London, SOAS alizungumza kuhusu nafasi ya Zanzibar na matarajio yake katika katiba pendekezwa. Mwisho alizungumza mwanablogu maarufu ambaye alikuwa mwanamke pekee katika mjadala huu Mwanadada, Aikande Kwayu ambaye alizungumza kuhusu nafasi ya wanawake katika katiba inayopendekezwa.
Pamoja na kutolewa kwa hoja nzuri na wachangiaji wawili wa mwanzo, yaani, Bwana Abdul Paliwala na Dr. Longino, mjadala ambao uliamsha maswali mengi na mbishano mkubwa ni ule uliotokana na mchango na maoni yake aliyotoa kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Katiba pendekezwa ambapo baada ya kumaliza kuwasilisha tu, alijikuta akivurumishwa maswali kutoka kwa wachangiaji.
Mmoja kati ya wachangiaji waliomsakama na kupingana vikali na maoni yake ni mwandishi wa BBC Swahili Bibi Zuhura Younis, ambaye alianza kwa kumpongeza Bwana Hamad kwa kuweza kuwasilisha hoja za muungano na katiba kutoka Zanzibar bila kuonesha kuegemea itikadi ya chama chochote cha siasa. Mara baada ya hapo Bi Zuhura alianza kwa mjadala wenye msisimko uliotosha kuitwa mechi!
MATCH OF THE DAY: Yussuf Hamad Vs Zuhura Younis

Hoja: Alichokisema Hamad ni kuwa Zanzibar kiujumla ilihitaji Muungano wa mkataba. Akaongezea kwa kusema kwamba Wazanzibari walihitaji katiba ambayo itaondoa kero za muungano ambazo zimekuwa zikileta sintofahamu kwa muda wa miaka zaidi ya 40.
Akasema, kuwa Wazanzibari wanahitaji muungano wenye kufuata misingi ya usawa, sio usawa wa uwiano lakini usawa wa maridhiano ya kila maamuzi yanayofanywa katika Muungano. Alitoa mifano ya kero mbali mbali za Muungano kama vile mgao wa Zanzibar wa mapato katika muungano, mapato, bandari, petrol na mambo mengine ambayo kwa kuongezwa kwake yamekuwa sababu ya mgogoro kati ya washirika wa Muungano.

Bwana Hamad alihitimisha kwa kusema, Wazanzibari hawaukatai Muungano ila wanahitaji Muungani wenye misingi ya usawa na kuheshimiana. Na kwa maana hiyo katiba nzuri yenye maslahi kwa Zanzibar ni ile itakayotokana na misingi ya usawa (Fairness) baina ya washirika wa Muungano. Pia alisistiza kuwa, ili kuondoa kero nyingi na migogoro ya kikatiba isiyokwisha, ni vyema kwa Tanzania kuzingatia katiba yenye kuzingatia matakwa ya wananchi walio wengi na sio inayosimamia misingi ya kivyama, dini wala kikabila.
Idadi ya wachangiaji kutoka Zanzibar kwa bahati mbaya ilikuwa haizidi watu wanne katika ukumbi. Kwa maana hiyo, michango mingi ilitokana na watu kutoka Tanzania bara ambao walionekana kubaliana na mengi yaliyozungumzwa na wasemaje wote. Pia walitoa michango endelevu sana hata kuhusu hoja za nafasi ya Muungano na Katiba kwa upande wa Zannzibar.
Hata hivyo, Bi Zuhura Younis, ambaye ni mmoja kati ya Wazaznibari wachache waliohudhuria alipingana na karibu hoja zote. Kwanza alianza kwa kusema kuwa Wazanzibari, hasa wa upande wa pili, wamekuwa wakilalamikia muungano kila siku, kama kwamba Muungano huo hauna jema lolote kwa Zanzibar.

Pamoja na hilo akaongezea kuwa kero ziko lakini ni ndogo ndogo sana na akasisitiza kuwa mgao wa asilimia 4.5% wanaopatiwa Zanzibar ni sahihi kwa sababu Zanzibar ni nchi ndogo sana kiidadi ya watu ukilinganisha na idadi ya watu walioko bara. Kwa hiyo hakuna haja ya kulalamika lamika.
Bi Zuhura aliisuta kauli ya Bwana Hamad kuhusu mafuta akisema, Zanzibar hakuna mafuta kamwe na kwa maana hiyo hakuna haja ya kujenga mlima kwa kichuguu cha sisimizi kwa kitu ambacho hakipo kabisa. Akihitimisha maoni na michango yake, Bi Zuhura alidai kuwa katiba iliyopo inaifaa sana Zanzibar na inalekea kwamba malalamiko makubwa ya katiba yanatokana na kelele za wapinzani ambao ni sehemu tu ya wananchi wa Zanzibar ambao nusu ni CCM na nusu ni CUF kiujumla.

Alipopewa nafasi ya majumuisho na kufafanua hoja alizozisema na zile zilizochangiwa, Hamad, alianza kwa kusema kuwa kumekuwa na dhana iliyojengwa kwa makusudi ili kuwadunisha watu fulani kutoka upande fulani kwa kuwahukumu kisiasa isivyo haki na kukana hoja zao kwa misingi hiyo. Alitoa mfano kwa kusema, katika mijadala kama hii, wasemaje wengi wanaposikia anayezungumza ni Mzanzibari au Mpemba, basi huyo huitwa ‘Mpinzani’ wa muungano hata ikiwa mtu huyo hana mfungamano na chama chochote.
Alifafanua pia kwa kusema kwamba baadhi ya wanasemina walimfahamu vibaya alizpozungumza neno ‘Fair’ wakidhani alimaanisha ‘equality’. Kwa ufupi alichokusudia kusema ni kuwa kuwe na msingi ya haki na usawa katika kufanya maamuzi ya mambo ya muungano. Moja kati ya mambo hayo ni kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili kwa msingi ya ukweli na uwazi. Alihitimisha kwa kusema kwamba Katiba yenye kujali na kusikiliza maoni huru ya wananchi walio wengi, ndio suluhisho moja la migogoro inayoweza kuunusuru Muungano wa Tanzania.

Kuhusu Mtunzi

I am particularly interested in combining photography with graphic design to communicate the message of the peace to a specific audience.

View all posts by

Maoni 7 katika "YALIYOJIRI KATIKA SEMINAR KUHUSU KATIBA YA TANZANIA (UK)"

 1. MAWENI 01/03/2015 kwa 3:38 um ·

  TULITARAJIYA KWA WATU WALIO ISHI KWENYE NCHI AMBAYO NI SHINA LA DEMOKRASIA WATA SEMA KWANZA LAZIMA WATU WA ZANZIBAR NA TANGANYIKA WAULIZWE WANAUTAKA MUUNGANO AU LA. NA IKIWA WANAUTAKA UWE WA AINA GANI.
  HAO WALIO ANZISHA HUU UNAO ITWA MUUNGANO HAWA KUWA WATUME. NA HAYO MSKUBALIANO YA HUWO MUUNGANO SI AYA ZA QURA’A TAKTIFU AU AGANO LA BABLIYA TUSIZUNGUKE MBUYU. KWA NINI SEMINA KAMA HIZO ZI SIANDALIWE HUKO NJE KABLA KATIBA YA VIJISENTI HAIJA ANDIKWA NA WENYE NCHI CCM. HUYO BI ZUHRA YUNUS ATAFANYA KAMA WAZANZIBARI HATUU JUI HAKI YETU. HUU SI MUUNGANO NI UKOLONI. MGEREZA KAUONDOKA KAMUACHIYA KIBARAKA WAO NYERERE KUIKALIYA ZANZIBAR KWA JINA LA MUUNGANO. ASOJUWA SABABU HASA ZA MUUNGANO HUU ATAFUTE LECTURE ZA MAREHREMU SHEIKH ILLUNGA NA KITABU KII TWACHO : AMERICA FOREIGN POLICY AND THE CREATION OF TANZANIYA. BY AMRIT WILLSON.

 2. mohammed Rashid 01/03/2015 kwa 6:12 um ·

  tunapo msikia bi zuhra redioni unahisi kama ni mtu mwenye maana, lakini dah, maskini kumbe ndo walewale madalali, ivi huyu bibi kaichambua vizuri hii katiba au ndo kuropokwa tu ilimradi ipite?

  mi nataka kumuhakikishia bi zuhra labda huyajui yalio[po zanzibar, sasaivi wazanzibar wameamka tena tumeaka barabara na wala huwezi kutudanganya chochote katika katiba hii kwani watu wengi wameelimika yani siku hizi zenji kila mtu anaijua sheria hata kama hakusomea sheria na hii ni kwasababu tumeamua kufuatilia kwa kina huu upumbavu wa chenge, na alhamdulillah, kila siku zinapozidi makundi kwa makundi yanazidi kuelimika kupitia taasisi na mikutano ya wanayoitakia mema zanzibar. bi zuhra wazenji tushaamka wala hatukubali tena, mi nakusihi tusiandikie mate ila tumuombe allah atujaalie uhai na uzima ili tujionee wenyewe.

  zanzibaaaaaaaaaaaaaar kwanza mambo mengine badae, na pengine tuuvunjilie mbali kwani lazimaaaa?

 3. MAWENI 01/03/2015 kwa 7:10 um ·

  Huyo bibi ni katika wanachama wa tawi la ccm huko uk. Usi taajabu kuwa hata ni katika wale waitwao Uchafuzi Wa Taifa. Viji centi vina fanya kazi.

 4. Makengeza 02/03/2015 kwa 4:30 mu ·

  Na nyie waandaaji wa hiyo semina hamwishi hasa. Eh tokea lini mjadala wa katika ukenda ukafanywa UK. Unamsaidia nani? Mshaambiwa kuwa “katiba mpya hatuitaki na hatushiriki”. Sasa kilichowapata nnini kwenda kupoteza muda wenu kuandaa kitu kama hicho. Mlikuwa mnataka kuwapa hao CCM kina huyo dada hashuo Zuhura Yunnus namna ya tu ya kujinadi na uCCM wao. Vijana waliosomeshwa na CCM hao na kutafutiwa kazi na CCM sasa wanakitetea chama. Huyo dada hana mbele hana nyuma. Ni hiyo sauti yake ndio iliyompeleka BBC. Kama si BBC basi angekuwa mtiribu akiimba taarab. Anachosema hakina tofauti na wanachosema CCM wengine. Umbumbumbu ndio unaowahangaisha.
  Pia najivunia matunda ya muungano kwa kuwa kaolewa na Salim Kikeke ambae ni jamaa wa bongo. Sasa yeye fikra zake ni kuwa muungano utavunjika.

 5. Ghalib 02/03/2015 kwa 6:56 mu ·

  Hawakotoa taarifa kuhusu huo mdahalo kwa sababu waliandaa watu wao upande wa zanzibar kama makada wa ccm. Shame on them

 6. MAWENI 02/03/2015 kwa 9:37 mu ·

  Asitie wasi wasi Atabaki na mumewe. Hata Zanzibar yenye mamlaka kamili haito mfukuza.

 7. mpetehalisi 02/03/2015 kwa 12:40 um ·

  Haya ndio matatizo yetu zanzibar hasa kwenye huu mtandao, mtu akitoa mawazo yake tofauti na mtazamo wa huu mtandao basi inakuwa shiida kwelikweli, Zuhra Yunus katoa maoni yake kama mzanzibar na mtanzania jinsi alivyoiona katiba, leo tunamshambulia na huenda karibu tutamwambia si mzanzibari. Huu mtandao wachangiaji wake wanaongoza kwa ubaguzi na kwa hivyo vita ya ubaguzi haiwezi kwisha msitudanganye. Ubaguzi upo hasa kwa wachangiaji kwenye huu mtandao, bi Zuhra hata akiwa ni CCM kwani kosa, au mlitaka awe CUF. Na kasema kweli upande wa pili wa znz ndio mnopenda kulalamika na kutusababishia vurugu visiwani kwetu, na hii inatokana na kwamba hamjakinahi na mlichonancho, you have almost every thing, lakini bado tuu malalamiko kila siku.

  Tuakupendeni wenzetu lakini uvumilivu unamwisho wake, kuna siku itafika yatafanyika maamuzi magumu, potelea mbali. Tumechoooooka kuishi kwa wasiwasi unguja, zamani haikuwa hivyo.

Comments are now closed for this article.