Wazalendo: Hivo TCU Inafanya Kazi na Ofisi Ya Utumishi Zbar?

Written by  //  17/12/2016  //  Habari  //  Maoni 8

Assalamu alaikhum Warahmatullah Wabarakatuhu Ndugu zangu Wazanzibari Wa ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu. Na Habari Zenu Nduguzetu Wengine munaosoma Mtandao huu. Ndugu Wazanzibari makala hii inahusika na dhulma kubwa za wazi wazi tunazofanyiwa na Serikali ya Tanganyika. Ndio nimeona hakuna budi ila kuifikisha kadhia hii katika mitandao ya Jamii ili Tuweze kusaidiana Mawazo nini chakufanya kama Wananchi Wa Zanzibar tuliokuwa hatuna Mtetezi.

-TCU Watoa amri, Waajiriwa wote Zanzibar Wapeleke Vyeti Vyao Tanganyika.

-Usajili wa Vyeti ni kwa Wazanzibari Tuu, Watoto Wa Malaika Weusi na Miungu Isiojuwa hata kunawa mavi na kuoga Janaba wao huwa hawasajiliwi?

– Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni Vyombo vya Muungano, Huyu Afisa Wa Utumishi Yeye ana Elimu gani hapo Utumishi?

1.TCU Watoa amri, Waajiriwa wote Zanzibar Wapeleke Vyeti Vyao Tanganyika
Nduguzangu Wazanzibari mimi leo nimepigwa na Mshangao mkubwa baada yakuona Mwanangu niliomsomesha kwa pesa yangu ya Kuvuja Jasho- Maanayake sikupewa (Mkopo kwa Fitna) na hata hakiba ya Sanda Sina. Alipomaliza masomo mwezi uliopita ametakiwa na Wizara ya SMZ (ATI) mshahara wake hauto-ongezwa wala kuajiriwa mpaka Cheti chake Hicho ambacho amesoma Katika Chuo cha Eldorate Nairobi. Akipeleke TCU kitambuliwe kama Chuo hicho Kimefikia Viwango vya Elimu ya Juu.

Mtoto wangu alichanganyikiwa kuona kwamba Wizara za SMZ au Ofisi ya Utumishi inatumika Kuwakandamiza Ndugu zao Wazanzibari kwa kisingizio kwamba Elimu yao Imetolewa Nje ya Tanzania. Mwanangu huyu hakusita ila akasubiri tulipopata vijipesa akaenda BARA kuwaona hao TCU . Alipofika aliambiwa kwamba Vyeti vyake Avikabidhishe Ofisa mmoja na akapewa risiti. Na kuombwa arudi baada ya Wiki- Emagine kuveryfied Vyeti Inachukuwa Wiki hii kweli inaingia akilini. Mtoto wangu alifanya hivo na aliporudi TCU baada ya ile wiki waliomtaka alikuta Vyeti havionekani na aliambiwa na Maaofisa hawa kwamba Huyu mtu aliemtaja wala hajulikani na wala hakuna mfanyakazi mwenye jina hilo… Alipoanza kuzozana nao na kutoa ushahidi wa jina na cheo cha huyo karani ndipo alipotupiwa maneno ya kejeli ” Nyinyi Wazanzibali muna matatizo sana nyinyi… enda zako ..”
Kesi hio pia nimemsikia msichana mmoja ambae amesoma chuo cha TMBI- Tanzania Commission of Univercity. Na chuo kimesajiliwa na Bord ya Vyuo vikuu vya Tanzania. Lakini Watoto wengi hasa wenye asili ya Kizanzibari wakimaliza Vyuo hawapati ajira. Na wametakiwa Vyeti Vyao Ati Wavipeleke TCU vifanyiwe Usajili kwamba ni Vyeti Halali.

MaSuali langu Ndugu Wazalendo na naomba munisaidie Jibu.
. Hivo Utasajilije Chuo halafu Vyeti vya Wanafunzi Useme Huvitambui? Huo Sio Ujinga na Unyanganyi wa Serikali ya Magufuli na Kundi lake la Wezi?
. Hivo Vyuo vya Egarton, Eldorate, Kenyata, Makerere vitakuwa Chini Kielimu kuliko Vyuo vyetu vya Tanganyika ambavyo Vina Uvyama na Ubaguzi.?

2. Usajili wa Vyeti ni kwa Wazanzibari Tuu, Watoto Wa Malaika Weusi na Miungu Isiojuwa hata kunawa mavi na kuoga Janaba wao huwa hawasajiliwi?
Nataka kuuliza tena kwamba Usajili Huu wa Vyeti Umeanza lini? Na kwanini TCU kama Wana Mashaka na Watahaniniwa Hawawaulizi Wakuu wa Vyuo hivo au Academic Secretary? Kwanini Wawasumbuwe wananchi Wanyonge ambao wamehangaika kutafuta Elimu ilio Bora kwa ajili yakuisaidia Nchi yao Sasa wanasumbuliwa?.

Hivo hawa Watoto wa Wafalme Weusi wa Kimalaika, na Miungu MYeusi wao Watoto Wao ( tunawajuwa wanasoma UK. Malasyia, China, UsA) Jee wao hutakiwa pia Vyeti vyao viende TCU vikachakachuliwe. Au ni Watoto wa Kizanzibari tuu ndio wanao fanyiwa Hivo?

Inasikitisha kuona kwamba Ofisa wa Utumishi wa SMZ ndio Vikwazo vikubwa vya Ajira za Wazanzibari waliosoma. Na Kule Wizara ya Afya na Kilimo Ndio Kumekuwa Kuna Waomi Wasiokuwa na Vission.

Wizara ya Kilimo Imepoteza Millioni ya Fedha kuwasomesha Wafanya kazi wao ambao ni tegemeo lakuendeleza Sector hio. Leo Wamemaliza Masomo Wanawataka Wapeleke Vyeti Vyao TCU ili Vipate Kuibiwa na kuuziwa Watu wengine.. Hivo kweli Zanzibar tutafika hivi.?

3. Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni Vyombo vya Muungano, Huyu Afisa Wa Utumishi Yeye ana Elimu gani hapo Utumishi?

Naomba nipatiwe Jibu jengine kwasababu sasaivi nazidi kuchanganyikiwa, hivo Wizara ya Kilimo, Afya, Elimu ni vyombo vya Muungano?
Kwanini ajira katika wizara hizo hazitoki mpaka Watoto wetu Wapeleke vyeti vyao Bara? Hivo CC Wazanzibari hatuwezi kujitambua na Ku- Veryfy Vyeti vya Wananchi wetu Mpaka vipelekwe Tanganyika..

Tunataka kujuwa Amri hii yakuwataka Wazanzibari wanaorudi masomoni Nje ya Tanganyika wapeleke Vyeti Vyao TCU imetoka kwa Malaika Gani ?

WASIA:

Ningewaomba nduguzetu wa Kizanzibari kwamba wasifanye mchezo wakuchukuwa Vyeti Vyao nakuvipeleka TCU. Kwani Wizara hio kwanza ina upendeleo. Pili ni Wizi wa Kuuza Vyeti. Tatu ni Wizara ya Tanganyika na haihusiani hata kidogo na SMZ au Wizara ya Utumishi ya Zanzibar.

Hivo nakuombeni shikamamneni na muache mara moja kuchukuwa Vyeti vyenu kwenda Kuwagaia Walanguzi ambao Asili yao nikunyanganya Haki za Watu hasa Wazanzibari.

Huo Mtindo wakusikia Vyeti Tuvipeleke TCU tayari umeshawabana watu Wengi na kupoteza Shahada zao za Juu za masomo.. Kama kweli TCU kinafanya kazi kwa Kisheria hakina haja yakutaka Ku Veryfied Vyeti kwakutumia Watu kupeleka vyeti hivo. Kwasababu kwanza hawana uhakika huyu mpelekaji wa Cheti hicho cheti ni Chake.

Kwa Utaalamu wa Uchekiji Vyeti na So call Veryfication kuna Mitandao ya Vyuo Vikuu na TCU wanakuwa na Access yakuwasiliana na Vyuo hivo vya Kenya, Uganda, South Africa, Zimbabwe, Botwasana n.k. Kama kweli Wana nia yakutaka kuhakiki Vyeti kama ni halali ni lazima Wao TCU wawasiliane na Academics Secretary wa Vyuo hivo na Wapeleke Jina series number ya Mtu ambae cheti chake kinataka kuhakikiwa na wao Watapata Reselt. za Mtu huyu kama Cheti chake ni halali au laa.

Njia nyengine yoyote ile hii haikubaliki na nilazima Wazanzibari Tusimame Imara Kuupinga Utawala huu Wa Kidhalimu Unaotaka Kutuibia hata Shahada zetu za Masomo.

Wabilahi Tofiq

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Wazalendo: Hivo TCU Inafanya Kazi na Ofisi Ya Utumishi Zbar?"

 1. zamko 17/12/2016 kwa 2:39 um ·

  @ Wazalendo
  Ninachokiona ni Mtihani mkubwa tulioshushiwa na Allah lakini Umetengenezwa na Watu ambao Wamejiweka Madarakani bila ya Ridhaa ya Wananchi.

  Watu hao wanachokifanya ni Kuendeleza Dhulma kwa faida zao na Famila zao na Hakuna Standard ya Uendeshaji wa Serikali hata mmoja.

  Nchi haitawaliwi na WAJINGA tukapata Neema na hii ni dalili moja ya Kiama kwamba Nchi zitaanza kutawaliwa na Watu Wasio Elimu ya Dunia Wala Dini. Zanzibar hivi sasa tuko katika kipindi kigumu Kuliko kile kinachoitwa cha BAMKWE baada ya Mapinduzi.

  Hii nikutokana na kwamba Wazanzibari hawana hata haki yakujiajiri kwa Mfumo Mbovu wa Ubaguzi wa Tanganyika. Na Wawakilishi Waliokaa Katika Baraza Kwasababu Uhali Wao Kikatiba Sio Wananyamaza Kimya Kuicha Tanganyika Kuwanyanganya Wazanzibari hata Ardhi zao za Urithi na Kuwapa Vibaraka wa Vertican So Coll Hoteli Investors.

  Nini chakufanya ikiwa Watu Wakesha Kusoma Hupeka Vyeti Vyao Kwa Wezi Wakavi Doublecate na kuvitumia kwa Further Education?..

  Kuna Siku Yule Mzanzibari alieibiwa Cheti atakuja kuambiwa Yeye Ndio Mwizi na mwizi Ndio Mwenye Cheti. Hawa wenzetu hawafanyi kwakubahatisha haya Wanayafanya kwa Mipango yao ya Baadae.
  Na kila siku Zinaposonga mbele Visiwa Vinapokonywa mamalaka yake ya utendaji wa ndani. Hii Ndio SMZ ya Sefu Ali Iddi na Sheni Waliomuomba Kikwete Awaletee Jeshi Lakuwatisha Wazanzibari Na haki Zao.

  Na Hii Ndio Zanzibar ya CUF Walio Wazuia Wananchi Kudai haki Yao Siku ya tarehe 28.10.2015… Kwa kutegemea Maalim Sefu Ataapishwa Tuuu, Ataaapishwa Tuu, Ataapishwa Tuu..

  Labda akaapishwe Akhera.

 2. shawnjr24 17/12/2016 kwa 4:59 um ·

  Ukweli ni kwamba Tanganyika wanataka kuwaondoa wasomi wote wenye msimamo na zanzibar na kuweka watu wao. Bila ya kusahau miaka mitano (5) hii wanataka kuimaliza zanzibar yote na kukata mzizi wa fitna. Kwani vikwazo vya kimataifa vimewakera wao na wameamua kuonesha hasira zao, kuna mikakati inapakwa kuwaondoa wazalendo wote wanaoitetea zanzibar kama wanavyo wamaliza kule bara.

 3. moyo 17/12/2016 kwa 6:12 um ·

  Muungano una faida nyingi kwa wazanzibari moja ya faida hizo ni hii ya kupokwa vyeti na majambazi na malaghai wa kitanganyika.

 4. MAWENI 17/12/2016 kwa 9:30 um ·

  Malalamiko na madai ya waislamu wa Tanganyika kuhusu haki zao za kimsingi hasa elimu ; tokeya kupata uhuru 1961 mpaka hii leo yana baki pale pale mpaka leo. Dhulma inaendelea. Zanzibaar kwa kuwa wanchi wake na viongozi ni waislamu ilikuwa ni kikwazo kwa mikakati yao. Wakaanza kuwa kumtumia karume 1970 kuzuiya mitinani ya Cambridge kufanywa na watoto wanao maliza secondary Scool. Karume ( baba) Akaanzisha Zanzibar National exam. Nyerere akagutuka akamuambia bora iwe ” Tanzania” nzima na inatayarishwa huko Tanganyika. Contoll imeanza hapo. Dasturi wao hawana haraka. Dr.Salimini alipo taka kuanzisha Chuo kikuu Zanzibar ilimpata kazi. Lakini kwa uchachamavu wake kaweza. Mwaka jana mume sikiya vipi walivyo futa pre univesity programe huko Suza. Kwa kuwa watoto wa wana ccm; vichwa mchwa hawapasi.
  Wazanzibari wengine walikimbiya nchi kutafuta elimu. ” Ittlub al ilmu walau bi siin” . Tafuta elimu japo China.Hilo ni agizo kwa waislamu. Wazee wengine kwa jasho lao wame amuwa kuwasomsha watato wao nje ya nchi.
  Mfumo kristo wameona itafika siku za mbele , Zanzibar hawatoweza tena kuiburuza kwa kuwatumia mabwege . Ndio hiyo mikakati mipya kwa Wazanzibari . Wazanzibar waliosha amka ambao wame toka nje na kuona ulimwengu ulivyo. Waislamu wa Tanganyika ndio wamedhi bitiwa. MFUMO KRISTO. Alla yarham Sheikh Ilunga.Amee…n!
  Mie naona wazanzibari wasi ogope kusoma nje na wazee wasisite kuwapeleka watoto wao kusoma nje. Kwani hao Wakoloni wetu ndivyo wanavyo taka tuvunjike moyo.
  2- Wale watao maliza masomo yao nje wakipata shada zao wafnye copy wazipigishe muhuri wizara ya elimu ya juu ya hiyo nchi walio soma au taasisi yoyote inayo shughulikia Shada za wanfunzi wa kigeni walio maliza viywo vikuu va nci hiyo. Halu wapige Muhuri ubalozi wa Tanzania wa nchi hiyo wanayo soma.
  3- wakirejea Tanzaniya watowe copy za hizo walo pigisha mihuri. Orignal wazioneshe tu. Ili walinganishe .Wasiwape hao wakandamizaji wa Wazanzibari. Orignal wazingaganiye siku zote.Hata hizo cerified copy ulo fanya nje zi nganganiye. Ikiwa ni kweli wao ni kitengo cha kuhaki Shahada kwa copi zenye serial No, na jina la mwafunzi wanaweza kusaliana na hicho Chuo alicho soma mwanafuzi kwa haraka bila tabu wala kuchelewa . Kwa ulimwegu huu wa leo.
  4-Huyo alie zuiliwa shada yake au iliyo “potezwa” Shada yake ya chuoni basi basi amfungulie kesi huyo alie mkabidhi ikiwa anayo karatasi ya istikbadhi ya huyo alo mpa.
  5- Aikiarifu chuo alicho soma kuwa shada yake imepoteya .Watamleteya nyengine.
  6- Wale watao rudi nyumbani , na hata wa walio maliza masomo yao hapo nchini. Wafikirie kupata njiya za kufanya kazi binafasi zinazo lingana au kukaribyana na masomo yao.
  Tuna safari ndefu kwanye ukombozi . Elimu na uchumi muhimu sana.
  Wakloni hawa ishiwii na mbinu. Tukiwa smart tunaweza kuwa predict na kundaa mikakati.
  TUTA FIKA INSHA ALLAH.

 5. Abdul Zakinthos 17/12/2016 kwa 9:59 um ·

  Elimu ya juu ni ya Tanganyika sio ya ZANZIBAR na ndio maana masomo ya DINI yakafutwa katika kupasi mtihani wa Form six au mlisahahu?

  Chengine Tungeanza na Kina Lukuvi walopewa cheti na Mtu na Mkewe waloanzisha website wakasema wanatoa degree za bure ,virtual online Degree

  halafu nashangaa hivi elimu inakuwa watu wa chini tu ,si wangeanza na mawaziri kufuatilia elimu yao?

 6. Kamshuu 17/12/2016 kwa 10:29 um ·

  Matatizo munayajuwa yako wapi, haovwote wanatumwa wawafanyie hivo wazanzibar hao sio wenzetu, wala hawana uchungu na wazanzibar ndio maana maamuzi yao ni kuwatesa tu kwa kila upande ili yao yafanikiwe tu kwa Mungu hakuna kubwa

 7. Tengoni 18/12/2016 kwa 5:47 mu ·

  Pole sana kama mmoja wetu alivyokushauri hapo juu, na mie namuunga mkono, ni kurudi chuoni haraka kufanya utaratibu wa kupata shahada nyingine, vinginevyo utajisumbua bure, hiyo shahada tayari iko sokoni. Nataka muelewe Tanzania na Zanzibar, wanaongoza kwa ghushi ya vyeti, tasisi itatowa tangazo la kazi na kutoa sharti la photo kopi za vyeti, kuambatanishwa na barua ya maombi. Wanaangalia vyeti vizuri, na kutafuta ndugu zao, kuwambia wabadilishe majina kupewa jina la mleta maombi mwenye cheti kizuri, ndugu huajiriwa kwa jina jipya. Mwenye cheti yuko nyumbani anasubiri majibu, ambayo hayatokuja kamwe. Unaweza hata kuitwa kwenye interview, mbele ya bodi, na bodi ikapendezwa na wewe, Secretary, akaagizwa akuandikie kuja kuajiriwa, basi Secretary atamwita mwingine,ambae atabatizwa jina la yule aliepitishwa na bodi, hiyo ndio Zanzibar na Tanzania, kuweni macho.

 8. Jino kwa Jino 18/12/2016 kwa 8:19 mu ·

  Nilisema zamani tuko ktk vita lkn hamukunifahamu sio vita ya cuf na ccm ni ya ya Wazanzibari na Watanganyika ni vita baina ya Uislamu na Ukristo kwa njia ya kukumoona bila ya kuuwana kwanza mm naona huo ni wazima upeleke cheti chako Original ukampe mtwana wa bara wakati yy mwenyewe hana hicho cheti unategemea nini Jamani tumieni akili zenu Riski anatoa Allah ww hata ukaona Wanaanza hayo basi ujue tumbili akisha mwitu huja mwilini Wazanzibari si sifa zetu za kufoji ikiwa mtu kasoma basi kweli kasoma na kama hakusoma ndio hakusoma .Musipeleke vyeti vyenu Original akitaka mpe copy hataki mwambie kwendaaa.

Comments are now closed for this article.