Watu 17 Dar kizimbani kwa ugaidi

Written by  //  18/07/2014  //  Habari, Kitaifa  //  Maoni 9

Watu 17 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwamo za kujihusisha na matukio ya ugaidi nchini na katika nchi jirani ya Kenya.

Pia, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama za kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo ya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.

Washtakiwa hao ni pamoja na Jihad Swalehe, ambaye alisomewa mashtaka peke yake ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.

Washtakiwa wengine ambao pia walisomewa mashtaka ya kula njama za kuingiza watu nchini na kushiriki vitendo vya ugaidi ni Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed na Mohamed Yusuph.

Wengine ni Abdallah Hassan, Hussein Ally, Juma Juma, Said Ally, Hamis Salum, Said Salum, Abubakari Mngodo, Salum Salum, Salum Amour, Alawi Amir, Rashid Nyange na Amir Juma.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mchana chini ya ulinzi mkali wa polisi na kisha walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo na jopo la mawakili wa serikali lililoongozwa na wakili mwandamizi, Prosper Mwangamila. Mawaklili wengine ni George Barasa, Mwanaamina Kombakono na Brenda Nick.

Kati ya waliopandishwa kizimbani, washtakiwa 16 ni wakazi wa Zanzibar na wengine wakazi wa Dar es Salaam.

Wakili Barasa alidai kuwa kati ya Januari, 2013 na Juni, 2014 katika maeneo tofauti nchini washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa kinyume cha Sheria ya Ugaidi ya mwaka 2002, kwa kuwaingiza watu ili wafanye makosa ya ugaidi.

Katika shtaka la pili, Barasa alidai kuwa katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, kwa pamoja walikubaliana kuwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Hellen Liwa anayesikilIza kesi hiyo aliwaeleza kuwa hawapaswi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa litasikilizwa na Mahakama Kuu.

Wakili Mwangamila alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na akaomba kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Jumatano ijayo, akisema kuwa wanatarajia kuwa na maombi maalumu.

Hakimu Liwa alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Jumatano ijayo. Pia aliamuru washtakiwa kurudishwa rumande.

Baada ya washtakiwa hao kumaliza kusomewa mashtaka, alipandishwa kizimbani Swalehe na kusomewa mashtaka na wakili Brenda.

Wakili Brenda alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Machi 21, 2013 na Juni 2, 2014, eneo lisilofahamika mkoani Dar es Salaam, mshtakiwa alikula njama na watu wengine ambao hawajafikishwa mahakamani, kutenda kosa la kusaidia kutenda vitendo vya ugaidi.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho, mshtakiwa kwa kujua na kwa kutumia mawasiliano ya facebook aliwasiliana na Nero Saraiva na watu wengine kwa ajili ya kupata malighafi, fedha na ujuzi kwa nia ya kuweka mabomu sehemu tofauti nchini Kenya ili kusababisha majeraha na hofu kwa Wakenya.

Mshtakiwa huyo pia hakutakiwa kujibu chochote na upande wa mashtaka ulieleza kuwa upelelezi haujakamilika. Hivyo upande wa mashtaka uliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo..

Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, 2014 itakapotajwa.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mchana wakiwa ndani ya mabasi mawili yaliyokuwa yakisindikizwa na magari mawili ya Kikosi cha Kuzuia na Kutuliza Ghasia (FFU) na mengine watatu yaliyokuwa na askari wakiwa wamevalia kiraia.

Baada ya kusomewa mashtaka, washtakiwa waliondolewa mahakamani hapo kwa kutumia basi ndogo la magereza wakisindikizwa na magari manne ya FFU.

MWANANCHI Posted Ijumaa,Julai18 2014 saa 10:1 AM
Dar es Salaam.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 9 katika "Watu 17 Dar kizimbani kwa ugaidi"

 1. Invisible 18/07/2014 kwa 10:42 mu ·

  Polisi wanatekeleza maagizo ya william lukuvi.

 2. nuramo 18/07/2014 kwa 11:39 mu ·

  Hii inaonesha ni jinsi gani Serikali ya Sheni ni Dhaifu,Hivi Mabomu yatokee Arusha huko washtakiwa 16 watoke ZNZ?

  Vile vile waliona ZNZ mahakama zetu zina imani kwa vile watuhumiwa wa kumua padri na tindikali wapo mitaani?

  Hili sijawahi kuona Kosa litokee ZNZ mshtakiwa akasomewe shtaka mahakama isiyokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo Bara .

  sasa kama haina uwezo kusikiliza si wangelisikilizwa na mahakama za ZNZ tu pia hazina uwezo hadi watakapoamua kuipata mahakama yenye uwezo?

  Huu ni uvunjifu wa sheria na vile vile ubadhirifu wa mali za umma utamuombaje hakimu aakhirishe kesi asie na uwezo nao,au utamfikishaje mahakamani kupoteza fedha za uma wakati unajua haina uwezo? hivi walipofungua shtaka mahakama haikusema kama haina uwezo wa mashtaka hayo hadi wapelekwe?
  tunajua ndio ile nenda rudi miaka 10

 3. sabra 18/07/2014 kwa 12:04 um ·

  Km wanawadhulumu laana za Allah ziwe juu yao ramadhani yote hii maskini wanatesa waislam.mungu awape subra.tunaijua nchi tanganyika km wamepewa agizo hilo lkn mungu yupo na anaona na iko siku na wao watakwenda kuhukumiwa na mfalme wa wafalme hakimu wa mahakimu.

 4. sabra 18/07/2014 kwa 12:10 um ·

  Viongozi munajukumu kubwa sana kwa Allah dhulma kwenda mbele inaendelezwa.mtu kijio chake hajui akipatie wapi na family yake leo munaenda kuwaundia kesi haziwahusu kwa vile waislam tuu wanafuata maamrisho ya mola wao.wapi ugaidi na wazanzibar hata haya.hamuoni viongozi munatesa watu km hivyo masikin za mungu!! Sawa

 5. makame silima 18/07/2014 kwa 2:27 um ·

  Muelekezea china mwenzake ncha humchoma yeye, leo viongozi wa smz wanawatoa muhanga watoto wetu wakizanzibar kuwapeleka Tanganyika kuhukumiwa doooo.

  Lakini iko siku hatuko mbali Ishallah hao wenye kujiona leo wana nguvu na madaraka kesho tutakuja kuwaona wao na watoto na wao wakipelekwa huko huko kuhukumiwa .

  Huu Muungano sio na una mazonge mengi nikama laana hii tumeikaribisha katika nchi yetu ,ili kuzalilisha dini yetu na utamaduni wetu, leo unambiwa katika magaidi hao 17 ni moja tu mkazi wa Tanganyika?.

  Wazanzibar hapo hakuna gaidi kuna kuzalilishana tu na njia pekeyake yakuwazalilisha Wazanzibar ni kuwaita magaidi ili ulimwengu uwaunge mkono kwa hilo.

  Kama kweli wazanzibar tunataka nusura basi nikuvunja huu Muungano wenye chuku zidi ya uislamu na Waislamu Zanzibar.

 6. Kidekide 18/07/2014 kwa 2:28 um ·

  Wee Papax mwenyewe ni gaidi namba moja. Uko Bara huko umepewa idara ya kuisambaratisha Zanzibar, Unadhani hatukujuwi wewe na wenzio?

 7. sabra 18/07/2014 kwa 6:57 um ·

  PAPAX na serikali yako kumbe muamsho ndio magaidi? ndio maana mukawakamata watu wasio na hatia kwa ajili wanaunga mkono muamsho?na sheni maskin yupo tuu kama sanamu eti ndio rais hawezi hata kuitetea haki maskini kawekwa tuu.hapa km znz haijajitoa ktk muungano wallah watatutesa sana hawa.lkn kilio chetu mungu anakisikia in shaa allah ipo siku.maskini wengine eti siku waliotoka kina ustadh farid yy ndio katumia gari yake kuwapakia hilo tuu ndio mtu azuliwe balaa km hilo kwa hiyo tusiwasalime viongozi wa muamsho kosa.na wengine walichinja kwa furaha ya kutoka mashehe wetu.hii dhulma gani tunayofanyiwa na nyie kina PAPAX pumzii tuu hizo ubabe na uhodari una mwisho huo.FIRAUN YUKO WAPI MBABE KULIKO NYIE ALIKUWA. DHULMA KAFARA MUTAJUTA IKO SIKU NGUVU ZA ALLAH ZIKIKUTIENI MKONONI.ramadhani yote hii maskin dua zetu zitawapiga nyote munaofanya dhulma.mabomu munaripua wenyeo musingizie wenzenu.

Comments are now closed for this article.