WATOTO WA KARUME WAPINGANA

Written by  //  02/07/2013  //  Habari  //  Maoni 20

Hassan Ali Ame (TANZANIA Daima) Zanzibar

MTOTO wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Amani Karume, Balozi Ali  Abeid Karume, amekinzana na kaka yake, Rais mstaafu, Amani Abeid Karume na  wanasiasa wengine wanaodai Zanzibar kuwa na mamlaka kamili (Dola) akisema hilo  litavunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akihutubia mkutano wa hadhara huko Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, Balozi  Karume alisema kwamba madai ya wanasiasa wanaotaka Zanzibar ipate kiti chake  Umoja wa Mataifa hayana msingi kwa kuwa mamlaka kamili ya Zanzibar  yalikwishapatikana tokea Januari 12 mwaka 1964 yalipofanyika mapinduzi na  kuondoa utawala Sultani.

“Wazanzibari msikubali kuchezewa akili na wanasiasa wanaotoa madai hayo,  Zanzibar kuna Mahakama, Serikali na Baraza la Wawakilishi, hayo ni mamlaka  kamili. Hakuna mamlaka kamili ya uendeshaji wa nchi yanayopindukia hayo,” alisema Balozi Karume.

Akizungumzia historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Balozi Karume  alisema ulifanyika kwa malengo makubwa ya kuimarisha udugu na umoja pamoja na  kufungua njia ya Afrika kuwa moja.

Hata hivyo, alisema vijana Zanzibar lazima wakumbuke kabla ya mapinduzi ya  mwaka 1964 Zanzibar haikuwa na raia bali wote walikuwa chini ya Sultani, ndiyo  maana hata Waingereza Desemba 10, 1963 walimkabidhi Mfalme Jamshed bin Abdullah  hati za uhuru kabla ya wananchi kuamua kujikomboa kwa njia ya mapinduzi.

Balozi huyo alisema tokea mwaka 1964 hadi sasa hakuna jambo linalofanyika  kuinyima haki Zanzibar katika mfumo wa Muungano licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi na pande mbili za Muungano.

Alisema wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili wakifanikiwa ipo siku  watadai kujitenga kwa visiwa vya Unguja na Pemba.

Akifafanua alisema kwamba iwapo mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya ya Jaji  Joseph Warioba yatapitishwa kama yalivyo na mabaraza ya Katiba na Bunge lake,  muungano utakuwa katika hatari ya kuvunjika.

Alisema kwamba mfumo wa muungano wa serikali tatu haufai kwa maendeleo ya  Muungano kutokana na kuwa mzigo mkubwa katika gharama za uendeshaji wake na  upande mmoja wa Muungano kuwa na nguvu ndogo za kiuchumi.

Hata hivyo, aliwataka wanachama wa CCM wakati ukifika washiriki kutoa maoni  katika mabaraza ya katiba, huku wakichukua tahadhari kubwa dhidi ya watu  wanaofanya kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika muungano wa Tanganyika na  Zanzibar.

Alisema kuwa wananchi waende kutoa maoni wakitetea msimamo wa kuendelea na  muundo wa serikali mbili kwa sababu wanaotetea muungano wa mkataba wameshindwa  kuzingatia maslahi ya wananchi wa pande mbili na Muungano wenyewe.

Alisema sera ya mambo ya nje ya Tanzania imekubalika kimataifa ndiyo maana  mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani ikiwemo Marekani na China wamekuwa  wakitembelea Tanzania na kuunga mkono harakati za kiuchumi.

Sera ya kutaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili katika mfumo wa Muungano  imekuwa ikitetewa na Kamati ya Maridhiano, Rais mstaafu Aman Karume na kuungwa mkono na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.

Lakini Rais wa Zanzibar,  Dk. Ali Mohamed Shein amesema haitambui kamati hiyo ya maridhiano ambayo ipo  chini ya Mwenyekiti Waziri wa zamani wa Muungano, Hassan Nassor Moyo.

Wakati huo huo, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi  (CUF), amesema kuwa ataendelea kutetea msimamo wake wa kutaka Zanzibar kuwa na  mamlaka kamili katika mfumo wa Muungano licha ya jambo hilo kutozingatiwa katika  rasimu mpya ya mabadiliko ya katiba.

Msimamo huo ameutangaza juzi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa  hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema kuwa nchi yoyote duniani ili ikamilishe sifa ya kuwa nchi, lazima iwe  na mambo manne ikiwemo kutambuliwa kimataifa, ardhi, watu, serikali pamoja na  uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyengine.

Alisema kuwa mabadiliko ya katiba yazingatie umuhimu wa Zanzibar kuwa na  Benki Kuu yake, uhamiaji, uraia, sarafu, na mambo ya nje ili iweze kujitegemea  katika mipango yake ya kiuchumi na kudhibiti mzunguko wa fedha.

Alisema kwamba iwapo Zanzibar itarejeshewa mamlaka yake kutoka katika mfumo  wa Muungano itaweza kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU)  pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ya Kislamu (OIC).

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 20 katika "WATOTO WA KARUME WAPINGANA"

 1. fey 02/07/2013 kwa 11:20 um ·

  WewemAli Karume usituzingue, mama ako alikuwa akikusanya karafuu zetu halafu anakupa wewe na ndio maana leo ukatetea Muungano maana unafaida nao.

  Mwizi mkubwa usiyetosheka, wataka kutuuzia nchi kwa kuwa wewe unapopakwenda, una nyumba Hollywood haja yako sisi na vizazi vyetu tunyasasike kwa waTanganyika labda ushahadaliwa na wewe kuwa raisi wa future. Maana imekuwa nchi ya waasisi wa Afroshirazi tuu mwengine hana chance.

  • jazz 04/07/2013 kwa 9:08 mu ·

   mama ake Ali Karume Fatma Karume ni mtu wa bumbwini zanzibar, bumbwini kama kuna mikarafuu ni kidogo sana hii hoja mama ake Ali Akrume kuokota karafuu imetokea wapi,kwanini hatujifunzi kutoa hoja bila ya kutukana

 2. jazba ni udhaifu 03/07/2013 kwa 12:46 mu ·

  hawa ndio vibaraka wanaotegemewa lakini anamwambia nani wazanzibari wako macho taim hii,kama yeye keshatumwa na kuahidia vyeo sio znz aende tanganyika wamtume huko.

  anakuwa hayawani! watu wamepoteza maisha kugombania haki ya waznz huyu yeye ana macho wala haoni na maskio hasikii limekaa kama zombi hata fikra binafsi hana.

  zanzibar safari hii kitaeleweka kwa sababu tushajua tukikosea hapa basi ni miaka 100 ijayo,lazim kieleweke

 3. Alhabib 03/07/2013 kwa 12:54 mu ·

  Zanzibar ikipata mamlaka kamili atshitakiwa huyo killer kauwa huyo na watu hawajasau na serikali yamtetea ndio maana aogopa mamlaka kamili khabbithi wahed

 4. mohamed 03/07/2013 kwa 3:14 mu ·

  Babayako alokuzaa alisema”muungano ni kama Koti likikubana tu unalivua”sasa wewe mtoto mdogo unajuaje masuala ya muungano?watu tunakula sembe la njano wewe unakula vinono,huwezi kujua hata siku moja uchungu wa nchi kazi kukimbilia madaraka tu basso mwizi mkubwa.

  Tupo google tushakuona jitayarishe na kidomodomo chako ,huweZi kuujua uchungu wa nchi hata maramoja.tunashukuru Allah sana Kia mnajitokeza,tutakapo pats nchi inakua wepesi kukuwekeni kapuni.

 5. Ashakh (Kiongozi) 03/07/2013 kwa 6:04 mu ·

  Nimefurahia ile kauli ya Maalim Seif

 6. NGURUMO 03/07/2013 kwa 6:36 mu ·

  Keshalewa huyoooo muacheni !!! hana moja asilolijuwa ila anachokisema ni kuwafanya wajinga wale anaowahutubia mie nina hamu aje huku kwetu ahutubie tutakwenda wengi ila tukisikia anafanya usenge wake basi sote tunakimbia tunamuacha na hao watakaokubali kudanganywa kwa pipi kama watoto wadogo!! huyu asiwaumize kichwa jambo muhimu ni kumtambua mtu nia yake ila hao alokuwa anawahutubia na wakaendelea kumsikiliza basi wao ni sawa na kasuku wanaonga lakini hawajuwi wanaloliongea Uppuzi mtupu anajipendekeza kwa watanganyika apewe uraisi wakati hafai hata huo ubalozi wa nyumba kumi .
  zile point wanazotowa wale washenzi kule bara ndio anazo zinukuu yeye sasa mtu kama huyu kumpa nchi ni bora umpe sabri kwaa au abedi sisimizi

 7. Bablly 007 03/07/2013 kwa 7:07 mu ·

  mimi nadhani madaraka ulonayo bado hujatosheka au labda unatamaa kuna siku na wewe utawekwa na watanganyika ujekua rais wa zanzibar, katika viongozi wenye tamaa na walokua sio wazalendo mmoja ni wewe…..emu jiulize toka ulipopewa madaraka umeifanyia nn zanzibar mwizi mkubwa ww….

  Zanzibar yenye mamlaka kamili haina pingamizi….kwanza tuko bzy kukomboa nchi af tutadeal na viongozi wenye tamaa kama wewe

 8. wachok 03/07/2013 kwa 7:23 mu ·

  ama kweli ali karume kaishiwa

 9. Mrfroasty (Ufundi) 03/07/2013 kwa 6:36 um ·

  ““Wazanzibari msikubali kuchezewa akili na wanasiasa wanaotoa madai hayo, Zanzibar kuna Mahakama, Serikali na Baraza la Wawakilishi, hayo ni mamlaka kamili. Hakuna mamlaka kamili ya uendeshaji wa nchi yanayopindukia hayo,” alisema Balozi Karume.”

  Quote of the day, naona kama maada ingekuwa pumba za ali karume 😀

 10. Ghalib 03/07/2013 kwa 7:44 um ·

  Hawa ndo wale WANAOKATAA MABADILIKO, WAPINGA MABADILIKO, anajidai kukutetea muungano ili pewe urais wa zanzibar na tanganyika yagujuu.

 11. Bosco 03/07/2013 kwa 8:19 um ·

  RUBISH

 12. nuramo 03/07/2013 kwa 9:55 um ·

  Hivi huyu kama kweli anawapenda wazanzibari naomba kumuliza swali ?
  Alipokuwa pale balozi wa Italy aliwakuwa na msaidizi gani kutoka zanzibar?
  Dereva mfilipino
  Mfagiaji mfilipino
  SecretarY Mfilipino

  waliobaki ni watanganyika unataka kuongea na balozi wako unaambiwa hana nafasi Ubalozi wa Tanzania nchini italy Unashuhulikia nchi kumi sio Ugiriki tu peke yake

  Saasa saivi ndio kawa anaupenda huo Muungano au ndo anaona CUF wanachukua nchi na Muungano ndio haupo basi ndo ashamalizika tena?

 13. Kamshuu 03/07/2013 kwa 10:26 um ·

  weeee………….. MSHEENZI, UNAYAJUWA MAMBO ULIOKUWA UKIYAFANYA HATA

  IKABIDI UONDOSHWE HAPA ZENJI NDIO MWANZO YA KUIJUWA MALIZENI

  HUKO ULAYA. UMEWAFANYIA DADA ZETU MAMBO CHUNGU MZIMA NYAMA WE.

 14. MAWENI 04/07/2013 kwa 11:12 mu ·

  Hyu alikuwa katika vipenzi vya Nyerere. Alifadhiliwa sana nae. Nikatika wale samaki. Wanaghofu
  mabadiliko.
  Mr. Balozi nchi zilo huru zeynye mamlaka kamili ndio memba wa UN.

  ZANZIBAR KWANZA!

 15. mzaliwa 04/07/2013 kwa 6:36 um ·

  huyu mgonjwa wa akili kwa nini musimpeleke kidongo chekundu,
  We umesikia wapi kua na mahakama ndio uhuru wa nchi?
  Alisema Tanzania inajulikana na nchi kubwa kama marekani na china, hasa ujuwe Zanzibar haijulikani na hizo nchi na ndio inapigania kujulikana.
  Sijui ata kama umesoma mie naona umepewa cheo kwa jina la karume tu,
  Kaaukijuwa wazanzibari wamesoma na wamefumbuka macho na akili hawatokubali kuburuzwa, kunguru wee.
  Zanzibar huru.

 16. mzaliwa 04/07/2013 kwa 7:01 um ·

  jambo moja linalo nishangaza sheni anasema haijui kamati inayo tetea mamlaka ya mzanzibari na wakati alisema alikutana nayo alipowekwa madarakani ilikuja kumpongeza,
  Sasa shenu ujuwe iyo ipo kabla ya wewe kuja hapo sasa wacha kuchwa chaza.
  Zanzibar huru

 17. raschabi 05/07/2013 kwa 2:42 um ·

  Nyerere alitegemea baada ya miaka 50 waznz wote watakuwa na akili kama za kina “Ali karume” na “CCMznz”…..

 18. Abdul 05/07/2013 kwa 7:07 um ·

  engelikwenda kasikazini unguja au pemmba ndio akaseme ujinga huu

Comments are now closed for this article.