Wasiopenda kusikia jina la Dr shein wakamatwa

Written by  //  26/12/2016  //  Habari  //  Maoni 5

WASIOPENDA kusikia jina la Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano ya uongozi wa msikiti wao, sasa wamekamatwa, anaandika Mwandishi Wetu.
Waliokamatwa na Serikali ya Dk. Shein wanatajwa kuwa wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao ni waumini wa Msikiti wa Kijiji cha Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye msikiti huo kuliibuka mgogoro baada ya mtoa mawaidha wakati wa Swala ya Ijumaa kutaja jina la Dk. Shein kinyume na makubaliano ya waumini wa msikiti huo waliopiga marufuku kutajwa jina hilo.
Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Salum Hamda Simba (37), Jamal Hamdi Khatibu (40), Khatib Jamal Jabu (62) na Ali Dogi (44).
Haji Khamis Haji, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, waumini wa msikiti huo walikubaliana kutotajwa jina la Dk. Shein kwenye msikiti huo kutokana na makovu ya kisiasa yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mzozo ulianza baada ya jina la Dk. Shein kutajwa ndani ya msikiti huo huku waumini wakionesha kukerwa kwa mtoa mawaida huyo, taratibu mzozo ukaanza kuibuka.
Hata hivyo, kabla ya vurugu kuwa kuwa, baadhi ya waumini kutokana na kukerwa na jina la Dk. Shein ndani ya msikiti huo, waliamua kutoka nje.
Ilipofika usiku wa saa tatu, Jeshi la Polisi lilivamia msikiti huo uliogomea kutajwa jina la Dk. Shein na kuanza kupiga mabomu.
Baada ya polisi kuvamia na kupiga mabomu, hali ya taharuki ilitanda na kusababisha watu wanaoishi jirani na msikiti huo kuanza kukimbia.
Said Ahmad Muhammad, Ofisa wa Ofisi ya Mufti wa Taasisi ya Kiislam anayeshughulikia Fatwa (maamuzi) alinukuliwa akisema, kuwa mgogoro kwenye msikiti huo anaujua.
Na kwamba, pande hizo zilieleza umuhimu wa kutuingiza masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada.
Hata hivyo, baada ya pande hizo mbili kuelezwa umuhimu wa kutenganisha siasa na ibada, walikubaliana kuwa Dk. Shein hatotajwa tena kwenye msikiti huo na kuwa, alishangaa jina hilo kutajwa kinyume na makubaliano.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 5 katika "Wasiopenda kusikia jina la Dr shein wakamatwa"

 1. moyo 27/12/2016 kwa 4:18 mu ·

  Sasa twamtaka Mohd Aboud atoe karipio la Siri kali la kukemea na kukataza kuchanganywa dini na siasa chafu za domokrasia kuingizwa katika nyumba takatifu za Allaah.

 2. Mkandaa 27/12/2016 kwa 5:58 mu ·

  ni busara kwa wanaojua historia wakatoa ufafanuzi wa kuanzishwa kwa utaratibu wa kutajwa jina la Rais wa Zanzibar na kuombewa Dua katika hotuba za Ijumaa.

 3. Zdaima 27/12/2016 kwa 7:52 mu ·

  Masahihisho.

  Waliokamatwa ni kama ifuatavyo.

  1. Salim Hamad Simba
  2. Jamal Juma Kombo
  3. Khatibu Jamal Jabu
  4. Ali Dobi

  • Ghalib 27/12/2016 kwa 11:16 mu ·

   Shukran hio habari kutoka Mwanahalisi

 4. Abdul Zakinthos 27/12/2016 kwa 12:49 um ·

  Akah!
  Huu mzozo mbona siku nyingi ulishamalizika Zanzibar,hivi mlishawahi kusikia komandoo akitajwa kwa Marhem Sh.Nassor Bachu?

  Walifika watu hadi kutoa aya Atiu Allah wa Atiu Rasul waulul amri minkum, lakini Bachu alijibu vile vile kwa evidence hao ulul amri ni wapi

  Huwezi kuwatii watu wasiotakia neema Nchi au Uislam

Comments are now closed for this article.