Wananchi: Uzembe wa Uongozi wa CUF hauvumiliki tena

Written by  //  26/04/2017  //  Habari  //  Maoni 8

Asalamu aleikhum Warahmatullah Wabarakatuhu Nduguzangu Wazanzibari na Wale wa Tanganyika au kama wanavopenda kujiita (Watanzania Bara).

Ama kwa leo napenda kuchukua nafasi hii kueleza wasi wasi wangu juu ya Chama hichi cha CUF ambacho hapo miaka ya mwanzo tulifikiria kwamba CUF ndio tegemeo letu wananchi wanyonge wa Zanzibar na Tanganyika na ndio Muokozi wa kusimamisha HAKI na USAWA.

Lakini kila nikiiangalia miaka inavosogea nakuona Uzembe wa Chama hichi cha CUF unaofanywa na Viongozi wake wa ngazi mbali mbali- Napenda kuwazinduwa Wananchi wenzangu kwamba Chama cha CUF kimepoteza Muelekeo na viongozi wake ni Wazembe wa Hali ya Juu wasiokuwa na VISION wala MISSION au Mikakati yakupambana na Maaduwi zake.

Kwanini nimekuja na mada hio hapo juu?
Hii nikwasababu sisi Wannachi wa Tanganyika na Zanzibar, tayari tumeshuhudia hujuma nyingi zinazofanywa na CCM dhidi ya Wananchi wa kawaida na Chama cha CUF. Na hata kufika Watu kuuliwa, kuwekwa vilema vya maisha na wengine kusukumiziwa kesi mbali mbali zisizo na maana. Hata hivo tunasikitika sana sana kuona kwamba Chama cha CUF bado hakijaweza kujipanga sawa sawa kupambana na hujuma hizo badala ya DOMO KAYA la Viongozi Wake wa Juu na Chini.

Mfano:
Hili tokeo la Uvamizi wa Mkutano wa CUF uliotokea siku hizi za karibuni huko Kinondoni Tanganyika. Kwa Maoni yetu sisi Wananchi tunasema Uvamizi huu sio wa Mwanzo na wala hautokuwa wa Mwisho. Lakini kinachoshangaza Viongozi wa CUF kwavile ni Wazembe wa hali ya juu. Wameshindwa kuandaa mikakati Kabambe yakupambana na hujuma hizi kwa nguvu zao zote Once for All.

Itakuwaje Chama imara kiache Mazombi 4 wa Lipumbavu wapite mlangoni na waulize walinzi sehemu inayofanyika Mkutano bila yakugunduliwa kwamba hao sio Wanachama wa CUF?

Itakuwaje Chama Imara kiache Mazombi ya Lipumba yapite ndani ya jengo hilo bila yakuwasachi, kuwauliza masuali, au kuwapiga picha watu hao?

Hivo Hawa Walinzi wa CUF wa Tanganyika Ushujaa Wao ni Kuitawala Zanzibar kimabavu tuu?

Hivo Hawa Wananchi wa CUF hawakusoma ule Uvamizi wa Mkutano wa CUF uliofanyika BUGURUNI?

Kwanini Viongozi wa Chama cha CUF Tanganyika wamekuwa Wazembe na Wapole Kiasi hichi?.

Huyu Kijana aliepatikana na kuzingirwa na Wananchi, ilikuwa wananchi hao Wasimuache hapo akiwa Mzima. kwani Kufanya hivo nikuhatarisha maisha ya watu wengine.

Huyu kijana alikuwa apigwe kichapo chakumuweka Kilema maisha yake kama sio chakumuondoa Duniani. kwani Watu hawa tayari wameshakusudia shari.Nashangaa kakaa kati kati akiwabegi watu wamsamehe bila yakumkukutia Bakora. Hapo alitaka Waje Vijana wa CUF na Masoksi kama wao Walivovaa Masoksi na Kumpiga mijaledi sawa sawa na kumchana chana mwili wake. Wananchi hao wangefanya hivo Usalama huyu wa Taifa naamini asingejaribu kurudi tena na kuhujumu mikutano ya CUF.

Masuali yote hayo tunaweza kujipa majibu kwamba Chama cha CUF hakiko Imara wala sio NGANGARI kama Kinavosema, bali ni maneno tuu na hakina nguvu wala Mipango kabambe kupambana na Maaduwi zake wa Ndani na Nje na Ndio maana LIPUMBA na Jaji MUTUNGI bado Wako WanadundaTanganyika.

Viongozi wa CUF Tanganyika na Zanzibar ni lazima wachukue mifano ya Nchi za Jirani kama vile Kenya. Vyama vya Upinzani Kenya, ingekuwa Lipumba na Mutungi wako Kenya basi naamini Wangekuwa ni MAREHEMU na kama sio Marehemu basi wangekuwa Walemavu au wako ICU. Na Ushenzi Huu unaofanywa na CCM ungekomeshwa mara moja.

Tayari Vyama vya Upinzani vya Kenya kwa Kuungana kwao wameweza Kubadilisha KATIBa na TUME ya UCHAGUZI KENYA Imeshabadilishwa. Sisi Kule Zanzibar Maalim Sefu na Kundi lake Bado Wanapita Wakitutia DRIPU za Uongo ati Haki Itasimama. Huku JECHA na Akina ALI VUAI Sefu Ali Iddi Wanadunda Mitaani.

sio Hivo Tuu hata Wale Wamakonde na Watanganyika (MAZOMBI) Walioletwa Zanzibar Kupiga na kuuwa Watu Mitaani na katika Vituo vya Habari wasingekuwa Hai au wazima kama CUF iko Ngangari kweli au viongozi wake wana Vission na Mission ya Kupambana na Uharamia wa CCM.

Ikiwa JECHA na LIPUMBA, MUTUNGI na NDOO wanawashinda, Kweli CUF itakuja kupewa Serikali hio 2020?.

Maoni Yangu ya Haraka haraka:

Ningewaomba Wananchi wa Zanzibar wakae Imara kuyakabili Mavamizi ya Majahili wa CCM yanayoendela Nchini na kwa Upande wa Pemba wananchi wasisahau Mavamizi na mateso, mauwaji tuliokuwa tukifanyiwa na CCM. Njama hizo zote zilikuwa zikipangwa na baadhi ya Viongozi wa CCM ambao sasa wameingia CUF na Nyengine zikipangwa Tanganyika. Hivo Ikiwa Uvamizi kama huu utakuja kufanyika Pemba au Unguja. Ni lazima Wananchi Tujiandae Kuchinja chinja Ziombi lolote la CCM au la Lipumba litakalo letwa Kuvamia au kutuchokoza.

laa kama Mutamsikiliza Sefu Sharifu na Upupu Wake wa Viongozi Wachovu wasio na Mission wala Mikakati kama Yeye. Basi naamini tutapigwa Dane Dane na heshima yetu na Visiwa vyetu Itazidi kupotea.

Wabilahi Tofiq

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Wananchi: Uzembe wa Uongozi wa CUF hauvumiliki tena"

 1. Ghalib 26/04/2017 kwa 3:06 um ·

  Usiwe na wasi wasi, chama kipo imara, na nchi Insha Allah wataitoa, mi sina hofu kabisa, suala la hujuma kwenye chama sio la Lipumba, ni serikali yenyewe chini ya ccm, Lipumba ni kibaraka tu, ccm inatumia pesa za walipa kodi kuhujumu chama, na kamwe hawataweza, wamechukua rudhuku za cuf kwa kushirikiana na msajili wa vyama vya siasa kinyume na sheria. Nikutoe wasiwasi kwamba hivi karibuni kumefanyika mchango wa pesa kila mtu 1000, kwa wingi wa wanachama wa cuf Unguja na Pemba naamini Zimepatikana zaidi ya milioni 300. Na chama kinaendelea kuimarisha

 2. Calif 26/04/2017 kwa 4:14 um ·

  Mwandishi nakuunga mkono 100% na tatizo kuu linaloonekana muda wote ni kumuona maalim seif kama ni “charismatic leader” ambaye kiukwel alipewa jukumu kubwa ambalo niliamin tang kipindi cha “Bismilillah” kuwa nizito kwake hususan udhaifu mkubwa alio nao wa “hewala asante” mpka iliopo sasa hatujui wap matumain yetu tuyapeleke na huo ndio ukwel..siku zote haifa kumpa kiumbe mwenzako matumain makubwa…
  sasa cha msing ni kutafuta njia nyengine lkn ya maalim ni “purely failed mission”

 3. shawnjr24 26/04/2017 kwa 8:46 um ·

  Kule bara walipoona serikali haina ulinzi wa kutosha, basi walianzisha sungu sungu ili kujilinda wenyewe. Na wala hawakuwa na lawama kwa serikali bali vijana wamtaani tu wamejitolea, sasa kwanini vijana kama wewe Zamko na Calif mkajitolea na kutafuta vijana zaidi kuilinda cuf na zanzibar yake??? Kule youtube kuna watu huitwa keyboard gangster ubabe mwingi kwenye keyboard lakini akiwa nje kunguru.

  • Abdul Zakinthos 26/04/2017 kwa 8:50 um ·

   kweli kabisa jibu tosha

 4. chatumpevu chatumpevu 27/04/2017 kwa 4:15 mu ·

  Kwa wote waliochagia, nawaunga mkono. lakn jamani imefika wakti cuf tubadlishe approach ya kukabiliana na hivi visa tunavyofnyiwa na SMZ/ SMT/CCM/ DOLA. Nafikiri Zamko has a valid point aliposema yake ya moyoni kwa ninavyomfahamu aina ya uandishi wake. calif pia namuunga mkono. Kadhia ya Lipumba inaonesha ni mwendelezo ( continuum ) ya dhamira mbaya ya dola kukimaliza chama cha CUF. Wameapa kuwa kwa vile maalim seif alizunguka ulimwenguni kueleza yaliyotokea, wakubwa hawakufurahia ndo wakaamua kula naye sahani moja via Jisinge llipumba na msajili.

  Hizi njama zimerasimishwa kwa kupewa uzito wa kitaasisi ( institutionalized ) kwa kuwa ofisi ya msajili wa vyama ndio anayesimamia na kuratibu uharami huu. Sasa kukabliaba ni vituko vya akina kambaya, lipumba na genge lake lazima tuwe makini na tujipange kwa sbabu hao waharibifu wamepata Baraka za dola na ulinzi imara. Imfika wakti wanapewa bastola. Lakni vyovyote vile inafaa cuf tuwe makini kwa hili na narejea tena kauli za tulieni, tulieni, tulieni kwa sasa haziwezi zikafanya kazi ktk mizania ya siasa za ubabe Tanzania. Kauli kama hizo zimeshapitiwa na wakati. mindset ya wanacuf ni kupata haki yao iliyoibwa oktba mwaka 2015 lakni inaonesha kuwa hakuna uwezekana huo Pamoja na kauli zinazotolewa a viongozi wetu za kutia moyo. Inafika wakti unajiuluza mhh hapa ni changa la kokoto kwenye macho kwa kuambiwa kuwa haki itaptikana karibuni tulieni tulieni, tulieni. Nafikiri viongozi wawaambiye wanachama ukweli bila kuwa na ukakazi wa kauli kwa sababu wanachama wanafakari wanavyoambiwa na uwezekano wa ukweli inakuwa mashakani.

  tujipnge na twende na wanavyotaka wenzetu kwa usataarabu ubabe, uhuni, jino kwa jino alimradi mwosho haki itaptikana lakini sio kwa kauli za tuleini, tulieni, tukieni .Vyenginevyo tuvunje chama.
  .

 5. Jino kwa Jino 27/04/2017 kwa 6:47 mu ·

  Muandishi umenikuna ndipo haya ndio always yapo ndani ya kichwa changu kwa kuangalia dunia inavyokwenda nimetoa mifano mara kadhaa wa kadhaa kwa Mfano wa nchi ya URITREA .VETNAM.SOUTH AFRICA hawa wote walpigana kwa hali na Mali lkn mwisho walifanikiwa naamini 100% vijana wapo wa kuweza kufanya kile kisichowezekena kufanywa lkn Tatizo la CUF Hakuna viongozi wenye kuona mbalii( VISION ) @Zamko Nilitoa mifano hiyo toka zamani ikiwa wameshindwa na Jechaa kweli wataiweza ccm. Wamepandikiziwa mbaya mwengine ndani ya chama chao Lupumbavu huyu ccm walipiga sana mpaka akawa nyanganya lkn hizo ndio fadhila zake za kuwatumikia mabwana zake mnywamwezi wa kwanza asiekuwa na msimamo ,kwa hivyo cuf wanajaribiwa kila upande kila designe na yote cuf Failureeee kwa hivyo ccm washawajua cuf ni wasemaji wazuri majukwaani tu lkn hawana vitendo ni MACAWARD wa mwisho na wakutupwa ndio unaona watu wanavaa masoksi wanawakhanithi kila upande .Ni kweli tumetegemea cuf kupata mageuzi pamoja na nchi yetu lkn hawana mpango wwote na kwa cuf hii na uongozi huu basi ni kukaa kisimani kwa yaleli.Naamini adui wako atakapopata hofu na ikawa halali usingizi hapo munakubaliana lkn adui wako anipiga usingizi vizuri anakuona weye foolish. Wazanzibari Wapemba Waunguja Tuungane tutafuteni njia MBADALA yoyote ile ikiwa nzuri au mbayaa lkn wakati ushafika wa kutumia nafsi zetu na mali zetu na nguvu zetu kwa kujua kwamba sisi hapa duniani tunapita tu ,Tunataka replecment kiongozi mwenye dini hatutaki siasa .

 6. moyo 27/04/2017 kwa 9:30 mu ·

  Maudhui hii niliisoma kabla ya kuwapo maoni yoyote nikasema moyoni mwangu wacha nisubiri wanamzalendo wakereketwa wa cuf na waliokunywa maji ya bendera nione jinsi gani watakavyotupa mabomu huku wakitokwa povu la midomo.

  Lakini mimi nasema rushianeni mabomu mpaka mchoke mimi niko natembea kifua mbele nasubiri masaa tu yakamilike najuwa kuwa mtaimbo umetuganda.

 7. Mkandaa 28/04/2017 kwa 9:33 mu ·

  Ushauri mdogo tu.
  KWANINI WALE WANOPINGA SERA NA MIKAKATI HAWAANZISHI CHAMA KINGINE NA KUANZA MAPAMBANO MAPYA?

  Najua CUF watavuta muda hadi 2019 wakati wa zamu ya kuchagua viongozi lakini mufahamu kuwa Huo mzozo ni hadi 2020, uchaguzi wa chama wa 2019 uko hatarini kutofanyika na kwa mara nyengine wagomea wa CUF watapoteza sifa ya kugombea kwa namna yyte ile.

Comments are now closed for this article.