vunjajungu yakemewa misikitini

Written by  //  05/07/2013  //  Habari  //  Maoni 2

Naaaam, Leo ikiwa ni ijumaa ya mwisho kabla ya kuingia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan. Kama ilivyokawaida khotba zote za swala ya ijumaa zinatakiwa zitolewe kuendana namatokeo.

Misikiti mingi imekemea vunjajungu bila ya kufahamu au kueleza maana yake. Huu umekuwa mtindo wa uchafuzi wa lugha unaoendelea huku wanafalsafa na wasomi wetu bila kujijuwa kufuata upotevu huu

Miongo ya karibuni imehusishwa siku ya vunjajungu na utendaji maasi mkesha wa wiku ya mwanzo ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Hii ni kwenda kinyume na lugha fasaha iliyokusudiwa kwamba unaoposema vunjajungu maana yake ni siku ya mkesha wa ramadhani. Kama vile mkesha wa sikukuu

Nidhani ipo haja kubuni mfumo na mtindo mpya wa vipi kuipokea siku hii badala ya kuinasibisha na mambo machafu, halkadhalika tuepukane na kufuata mkumbo na kuanza kuikataa siku ya vunjajungu.

Vunjajungu sio siku chafu wala siku ya uchafu. Hii ni miongoni mwa sikubora. Hivyo tusiichafue kwa dhana, hoja, maelezo yanayopelekea kuona kama ni siku chafu.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 2 katika "vunjajungu yakemewa misikitini"

 1. nuramo 05/07/2013 kwa 11:28 mu ·

  Samahani Asha matumizi ya Lugha yanakuwa na yanaendelea kukua mfano Watu wengi tunasema naenda Sheli kwa maana ni petrol station wakati hata akienda BP au Castle au hata ZP atasema naenda Sheli

  Sasa kutaka kuibadilisha rejister kwa kipindi hiki utachafua hali yahewa kwa kuwa tayari hiyo lugha ishaeleweka
  Labda kuna kitu kimoja pia kukizungumzia Matumizi ya Lugha inategemea wapi unaitumia lugha mfano
  Kiengereza tutasema She comes au He comes lakini kiswahili tunaposame anakuja tushajua nani tunamkusudia na hiyo Vunja jungu ishakubalika kuwa ni maasi kuuiruhusu leo kuwa vengine naona watu watataftana

 2. Makame Ame 05/07/2013 kwa 10:56 um ·

  Kuna kitu wataalamu wa psychology wanakiita POSITIVE REINFORCEMENT. Bahati ikiwa ni mbaya au nzuri mashekhe zetu wengi (sisemi wote) wanatumia NEGATIVE REINFORCEMENT. Siku zote positive changes huletwa na positive reinforcement, na hivyo ndivyo alivyofanya Bwana Mtume na Khulafaa Rashideen. Negative reinforcements hazileti kitu ila kuongeza negative changes.

  Nchi yetu ina uhuru mkubwa wa watu kuhadhiri dini wanavyotaka mpaka kufikia kutukanana au kuondoleana heshima, uhuni na uchepe. Sababu kubwa ya hili sio uhuru tulionao bali ni kutokuwa na mafundisho ya kidini yaliosawa. Na wengine (akthari yao) hata hayo mafundisho hawana. Hilo limewakumba hata wanasiasa wanaohubiri siasa zao.

  Mimi nipo hapa Unguja na sijaona taasisi yoyote inayofundisha Public Speaking as an art or science. Inachukuliwa tu kuhubiri ni jambo la kila mtu atakaye. Ikiwa Mtume SAW alipata muelekezo wa namna ya kuhubiri sisi ni nani wa kuifanya kazi hii bila ya mafunzo yoyote? Jibu sina.

  Tabia hii tumeijenga sana sisi Wazanzibari ya kufanya jambo au mambo bila ya utaalamu. Mfano mdogo tu mimi mwenyewe nilisomesha skuli bila ya kupata mafunzo ya kitaalamu ya ualimu. Matokeo vijana niliowasomesha walipata mikong’to kwa kuwa nikiamini ndiyo njia pekee ya kufundisha, kwani ndivyo nilivyofundishwa. Nazichukia siku hizo, kwani nilipopata mafunzo ya ualimu niligunduwa kuwa kumpiga mtoto ni kuuuvua utu ukaingia unyama. It is only animals who resort to violence insettling issues. Binaadamu tumepewa akili ili tuitumie kwa hilo.

  Hebu watizame vijana wetu wengi wanaohifadhi Quran, vipi wanafikia hatua hiyo? Kwa kupigwa? La, ni kwa kupata zawadi na kuisfiwa ie positiv reinforcement. Na hao mashekhe wanaokemea vunjajungu watachokipata ni hicho ni vunjajungu lenyewe na kuelekea juu.

  Ikiwa kendesha gari kunahitajia licence na mafunzo maalum, jee kuendesha watu?

Comments are now closed for this article.