Uamsho sasa kuhukumiwa Zanzibar

Written by  //  26/11/2016  //  Vidio, Habari  //  Maoni 10

Uamsho korti

Kwa mujibu wa Salma Said hapo Chini Jana 25/11/2016

Viongozi wa Uamsho wameletwa leo (25/11/2016) Zanzibar kutoka Dar es salaam kwa ajili ya kesi yao ile ya mwaka 2012 ya kufanya maandamano na kuharibu miundombinu ya nchi kesi inaendelea Mahakama ya Vuga.
Natoa pole kwa wake na watoto wao hebu hesabu hiyo miaka ya kukaa mbali na familia zao. Allah ajaalie salama.

Ahsanteni

Kuhusu Mtunzi

Teesside University.

View all posts by

Maoni 10 katika "Uamsho sasa kuhukumiwa Zanzibar"

 1. shawnjr24 26/11/2016 kwa 2:29 um ·

  Hii sehemu mbona imekaa kama kiinua miguu?? Au hio Segerea imefanana nayo.

 2. muwa 26/11/2016 kwa 3:00 um ·

  Wakati mwengine mna ufanya mtandao wetu ushuke Hadhi,kwanza video ya zamabi pili Hapa ni kinwa miguu. Halafu mnasema segerea,Hata hamhakikishi habari.

 3. Abdul Zakinthos 26/11/2016 kwa 4:01 um ·

  ndio tunahitaji data za uhakika kama habari ilivosema, mweye data za uhakika atuletee ,inaonesha alosambaza social media habari hii ametumia video ya zamani kwa mada mpya nasi tumecopy paste tu

 4. rasmi 26/11/2016 kwa 11:38 um ·

  Nakubaliana na maoni ya muwa…

 5. Jino kwa Jino 27/11/2016 kwa 4:01 mu ·

  Namuombna Allah awape subra wao pamoja na sisi lkn ni masikitiko makubwa na hasara kubwa juu yetu ni kuwa tumeshindwa Wazanzibari kufannya chochote .Tusmeshindwa kwa mkono wetu ,tumeshindwa kwa ulimi wetu, na tumeshindwa hta kwa kuchikia leo viongozi hao hao tunacheka nao na kunywa nao kahawa hii ni hasara juu yetu.Lkn nayo hii ni sunna ktk sunna lazima utapigwa vita n aserikali kama alivyofanyiwa( Rasuli llahi sala llahu alayhi wasalam)Naikiri kila umma au kila nchi ina JIHADI na Sisi Wazanzinbari JIHADI yetu ni kudaio nchi Kweli sisi ni Waislamu 100% or 99.9% ni Waislamu tumekuwa woga na dhaifu 200% na hatuko huru tunaogopa kufa.

  • Abdul Zakinthos 27/11/2016 kwa 11:09 mu ·

   Kusema kweli Familia zetu ni maskini sana tena sana, na yametukuta mengi kwa hiyo lazima tuwe na woga, si woga wa kuwekwa ndani bali ni woga wa kujeruhiwa na kusababisha hasara zaidi.

   Nakumbuka mzazi wangu alisingiziwa kesi hii hii, Alhamdulilah tumefanikiwa kumtoa kwa kiwango cha milioni 6 na kuhamishwa nchi.

   Ni kesi ya uongo kabisa kaazimwa CD ya Mkutano wa CUF tena mwanamaskani mwenzao maskani za CUF kisha hapo hapo akakamatwa hapo hapo kuambiwa anasambaza CD za uamsho zimepigwa marufuku..atapelekwa bara.

   Papatu papatu ndio milioni 6 imetoka KILIMANI pale ,tunao ushahidi wote hakuna kesi wala nini -na tukiamua tu basi tunazitoa record zote maana tumewarikodi askari wakiomba hizo pesa wenyewe bila kujijua.

 6. Mrfroasty (Ufundi) 27/11/2016 kwa 8:05 mu ·

  Video imeondoshwa na kutumika picha, nadhani video inatokea kwenye mitandao ya watssup haiwezi kuthibitishika kwa mtu asiezifahamu hizo sehemu….imeondoshwa kwa sasa.

 7. abuu7 27/11/2016 kwa 11:21 mu ·

  yaleo hayo. nyie ma ccm mnaomba razi za wazawa kiujanja.
  hatamfanye nini .hata mfanye nini hamtakiwi

 8. Jino kwa Jino 28/11/2016 kwa 6:08 mu ·

  @ Abdul zakinthos Pole ndungu yangu lkn dhulma inayopita kwetu haisemeki inataka msasa wa hali ya juu ,tatizo letu kubwa hatuko pamoja hawa watu wanatuchezea aikili zetu kwa sababu hatukusoma na hatutaki kusoma .Na kubwa zaidi ya hilo ni kwamba tunaipenda Dunia sana sana tena sana na tumeisahau Akhera hii ndio iliotufanya tuwe madhalili .Allha atufanye mashujaa lkn Dhulma kwetu imezidi sana lazima tuiondosheni kwa mikono yetu.

 9. Mfalme 29/11/2016 kwa 8:53 mu ·

  Pole ndugu Abdul Zakhintos,

  Hayo ya dhulma yanawatokea wengi,

  Nina nugu yangu alikuwa anauza mitungi ya Gesi huko bara. mara kapigiwa simu na mtu anataka apelekewe mitungi ya gesi nyumbani kwake.

  Kijana kachukua bodaboda yake , kuelekea huko alikoelekezwa. Imefika jioni hakurudi. Wazee , vijana , majirani na wasamaria mema wakaanza kumtafuta hakuonekana.

  Polisi wakajifanya kumtafuta , hakuonekana, si yeye wala pikipiki yake.

  Imepita zaidi ya miezi minne kijana hakuonekana.

  Ajabu simu yake inakuwa ina ring lakini haijibiwi.

  Mwisho tukafikiri labda ameuliwa na majambazi na pikipiki yake kuchukuliwa.

  Wazee wakiwa karibu na kutangaza msiba wa kifo , kijana kaingia.

  Kumbuka baada ya zaidi ya miezi 4 .

  Kumbe alikuwa amewekwa ndani korokoroni na hao wanaoitwa usalama wa taifa kwa kuhofiwa ni gaidi.

  Sababu ya kudhaniwa ni gaidi , eti alikwenda kumposa mtoto wa sheikh mmoja mtaani ambaye amewekwa ndani kwa dhana hizo za ugaidi.

  hilo ndilo kosa lake. SUBHANALLAH

  Ndugu zangu hivi vita dhidi yetu waislamu vimefikia level mbaya sana , tujitafakari sana.

  Tumekuwa ni watu tusioaminiwa na watawala wetu.

Comments are now closed for this article.