UVCCM YAMUONYA MAALIM SEIF

Written by  //  05/07/2013  //  Habari  //  Maoni 14

Mwandishi wetu (TANZANIA Daima) Pemba.

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) umemuonya Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuacha matamshi ya kichochezi yanayoweza  kuleta  mgawanyiko.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alitoa kauli hiyo jana wakati  akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika huko Micheweni, Pemba  na kusema Maalim Seif anatakiwa kukubali kufanya kazi chini ya Serikali ya Umoja  wa Kitaifa (SUK) au ajiuzulu.

Shaka alisema anachokitafuta Maalim Seif ni kutokea kwa mpasuko katika SUK  kabla ya mwaka 2015 kwa kuamini hata akigombea kwa mara ya tano, hatapata  ushindi.

Alisema Maalim Seif, anaposema anabaguliwa na hashirikishwi katika SUK  Zanzibar, ni dhahiri anakusudia kutokee ghasia, mpasuko na mkorogano, ili  Zanzibar irejee katika mivutano iliyokuwepo mwaka 1995 na kusababisha watu  kupoteza maisha.

Aidha, mtendaji huyo wa UVCCM Zanzibar alimtaka Maalm Seif  kuacha kumsakama  Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd kwa hoja zisizo na msingi katika  majukwaa ya kisiasa.

Alisema kitendo chochote cha Maalim Seif kitakachoashiria kumpaka matope  Balozi Seif, UVCCM hautakaa kimya na kuacha atambe.

Alimtaka Makamu huyo wa Kwanza wa Rais ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF  kukubali kukaa pembeni na kuwapisha vijana.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 14 katika "UVCCM YAMUONYA MAALIM SEIF"

 1. zamko 05/07/2013 kwa 8:16 um ·

  aMA KWELI HAWA mAQGANDWA WANATAKA wATENDE WAO TU NA wAKITENDA wENZIWAO hUPAYUKA NA kUAANZA kUTUKANA..

  Nawauliza hao UVCUF wako wapi_ Au wao hawana midomo yakukaa wakamuonya Seif Mweusi_ Kwasababu Anagimba nini_….
  Hawa jamaa wameona kwamba hawana watu na Sasa wanaanza kubbaika na kupayuka.. Mara wamekwenda kwa Salimini.. Wakatolewa Shuti huko maana Mawazo ya Komandoo hayaendani na Waoo Magwanda .

  Sasa Wanahangaika tu.. Mara hii hata Mapuri Awape kura ngapi za kwiba basi Wazanzibari wenyewe hawawaachii mukaimaliza Nchi hii. Mutaitema tu..

  Nyinyi mulikua munaandika vikaratasi nakutukana Wapemba Ati Wahame kwasababu ya watu Wa Uwamsho kutoa taaluma. Sasa jamii inawakataa Munababaika.

  Hao watu Wa Micheweni kwanini wakawapokea wanadhani ccm wanawapenda.. NINI

 2. MAWENI 05/07/2013 kwa 8:49 um ·

  TIME OUT !

  ZANZIBAR KWANZA !

  ZANZIBAR KWANZA YENYE MAMLAKA KAMILI SHENGESHA BAADAE.

 3. mohamed 05/07/2013 kwa 9:09 um ·

  Nyani haoni kundule,hawa ni wale walopanda viririni na kumtukana jussa,maalim na hata maimamu wa uamsha hususan sheikh farid,au sio hawa au walikua hawatukani nakukashifu watu?ccm mnaongoza kwa kila balaa katika nchi hizi ila nyie mkiambiwa hua mnaumia.

  Sikuhizi wamekuja na mpango wao eti”seif kishakua mtumzima apishe vijana”sasa wewe shaka je motto tuambie na kama mtu mzima basi hata wewe unafaakuachia ngazi.

  Maalim seif mnamuogopa kwasababu anakwambieni ukweli mukubali tu na siku zote ukweli unauuma.

 4. Foum 05/07/2013 kwa 10:36 um ·

  Bado vijana wachanga na dhamana ya kuunda serikali za aina hii za umoja wa kitaifa. Sishangazwi na mchanganyiko wa aina hii kwa vile tulishazowea ile kuali ya zidumu hekima na busara za kiongozi mkuu na ndio maana vijana wamekuwa wakali na kutaharuk.

  Labda tuwape darsa kidogo namna ya mifumo ya aina hii inavyofanya kazi, kwanza nitoe mifano ya aina ya coalition governments duniani hasa kwa vile uchaguzi mkuu haujatoa clear mandate kutoka kwa wananchi kwa namna gani ya uongozi ujao uwe. Kule Nothern Ireland, sinn fein na unionist wameunda coalition gov huku kila mmoja akiwa na agenda ya future aitakayo, na kutofautiana kwa dhahiri pale mmoja anapopendekeza jambo ambalo mwengine halipendelei.

  hapa Uingereza tumeona namna gani waziri mkuu na makamo wake wanavyopigana vijembe na hata kufanya campaign against each other katika issues wasizokubaliana. Leo hii kulikuwa na kura katika house of commons ya kuahidi referendum ya EU out ambayo imependekezwa na kupendelewa zaidi na upande wa waziri mkuu wakati makamo wake na chama chake wamejitoa na kuabstain katika referendum hio. Ni jambo la kawaida katika mfumo wa iana hii wa serikali waundaji kutafautiana hadharani tena wakati mwengine kwa kauli kali na za utata. Democracy si lele mama, na zaidi hamujiulizi kwa nini katika miundo hii ya serikali za coalition inakuwa migumu kwa mkuu wa serikali kubatilisha uteuzi wa makamo wake hasa kwa vile hawapatani kwa lugha moja?

  Labda nitoe mifano ya statement tata baina ya wakuu wa coalition government uingereza katika saga la leverson enquiry: waziri mkuu na makamo wake walipinzana katika statement kiasi kwamba Nick Cleg aliomba muongozo kwa speaker wa kutoa statement yake pekee isiofungamana na statement ya waziri mkuu wake katika serikali wanaoiongoza, sasa tujiulize ikiwa bungeni waziri mkuu na makamo wake wanatafautiana itakuwaje ndani ya vikao vyao?

  Angalia statement ya pili kutoka kwa waziri mkuu wa uingereza juu ya serikali yake “David Cameron says he has “fundamental differences” with deputy PM Nick Clegg over what their coalition deal meant for constitutional reform.” hii ilitokana na part mbili za serikali moja kupingana katika lords reforms.

  Zipo pia tafauti kubwa baina ya wakuu wa northern Ireland wanaounda muungano wa serikali ya unionist na sinn fein, mfano ni tafauti zao katika mfumo wa opposition katika Stormont laini wakiendelea kuongoza pamoja na kuwaacha wananchi zamu yao wakati wa upigaji kura.

  Ujarumani pia kati ya chancellor Merkel na westweller wa FDP waliounda serikali ya coalition pia nao wametafautiana hadharani baada ya kupoteza jimbo katika uchaguzi mdogo kufika hadi kuweka bayana tafauti zao.

  Mifano ipo mingi, katika muundo wa serikali za namna hii huna budi kukubali kutafautiana na mwenzako kwa sababu policies kamwe hazitakuwa moja, na ikumbukwe mwisho wa term ya uongozi kila mmoja anahitaji kura za kumzidi mwenzake ili awe na upper hand ya kuunda serikali. Hii karne si ya chama kimoja kushika hatamu, tafauti ni part ya coalition goverments.

  lakini pia sitoacha kueleza kuhuzunishwa kwangu na wachache humu ukumbini wanaondekeza jazba na kujisahau kwa kuwatusi wengine kutokana na tafauti za rangi zao, si vyema kumtukana Balozi seif kwa sababu ana mtazamo tafauti, hoja hupingwa lakini majina ya kuashiria ubaguzi hayakubali kidini, utamaduni na silka zetu. Tujifunze kuheshimiana.

 5. Makame Ame 05/07/2013 kwa 11:12 um ·

  Ahsanteni uvi wa CCM. shikeni uzi huohuo. Ila, mujuwe tu la kusema kesho mbele ya MwenyeziMngu kwa muyatendyo kinyume na myasemayo.

  Tukikaa tujuwe kuwa pepo ni rahisi kupatikana na pia ni rahisi kukosekana. Darsa la Bwana Foum hapo juu linawatosha.

 6. makame silima 06/07/2013 kwa 1:13 mu ·

  Muelekezea shina mwenzako ncha hukuchoma wewe, ccm wamekwisha hivi sasa wanadishwa na kivuli cha Seif Sheriff bila kumuona Seif Mwenyewe.

  Hawa wanaofu na mabadiliko hii ndio ukweli wenyewe, na wakitaka wasitake mabadiliko hayazuwiliki tena, wao Uvccm wanatishwa na Seif Shariffu lakini Seif Iddi anatishwa na Laana tu llah?.

  Hii ndio kuchanganyikiwa ccm Zanzibar na kuto kujijuwa wakamate wapi maana Zanzibar walikokuwa wakifitini hivi sasa Tanganyika imeibuka na Watanganyika kuto kukubali kutia mashoga katika Serekali yao.

  Kindumbwe tumbwe Dodoma na Serekali ya Shirikisho , maana Wabunge 70 mawaziri 15 jee ccm/Zanzibar watapata wangapi?

  http://www.youtube.com/watch?v=3OSD6U8eZmc

 7. Multiways 06/07/2013 kwa 3:10 mu ·

  inaonesha,,ni wazi sasa ccm,,hawana tena cha kuitetea nchi hii,,kama ni matus hassa,,,bas,,naomba,,,warejee mkutano ulofanyika magogon chini ya vuai ali vuai,,,aliemtukana maalim seif,si hilo tu,,,baada ya mkutano wa ccm kumalizika pale kizota,,ccm hawahawa ndio waliokuja kuchana mabango ya amani karume,,pale kisonge na mombasa huku wakimkashifu sana,,,haya yooote hawaoni kama ni kupandikiza chuki,kugombanisha watu,,ndio mwanzo wa kauli kama hizo?,,ilitakiwa wakae na wasimame hasa,,,kuwambia wananchi,,jamaani tulikosea,,sasa tunarud kwenu kuwajulisha,,tuache kauli za matus na kukashifu watu,,kwa mantiki hii,,mwisho munapotaka kusema lolote lile,,kumbukeni huko mlikotoka,,,maana,,,kwa wanaojua na kufuatilia yale mnayofanya ,,watawaona kama vichekesho pindi mkiendelea kusema mambo yasio na mashiko,kama hayo,hasa kwa kipindi hichi kilichosheheni wajuzi wengi wanaojua nn wanafanya,,
  tanbih:ikiwa ccm kwa ujumla,,itaendelea kusimama majukwaani na kutetea maslah yao,wajue ccm wanaizamisha mwisho watakua hawana tena cha kufanya,,ni imani yangu tunaolekea hawa wahafidhina watakua pamoja na waznz ktk kuitetea kwa pamoja,,ila ikiwa kama hawakutaka pia,,,wajijue kwa wimbi hili halirud hata wafanye nn,,nawasilisha

 8. MuikomeZanzibaryetu 06/07/2013 kwa 10:40 mu ·

  Hellow mzalendoz!
  nnachotaka kusema
  nchi nyingi zimeondokana na tawala za kishenzi, sasa ni zamu ya Tanganyika na Zanzibar

 9. makame silima 06/07/2013 kwa 11:58 mu ·

  Jee kuna ulimwengu gani tulionao hivi sasa wa Kijikundi tu cha wahuni eti UVCCM Kumuonya Makamo wa raisi na Kumkashifu ?.

  Jee ingekuwa kumejitokeza kikundi cha chama chengine au Tasisi fulani mbali na ccm na kumuonya Seif Iddi hali ngekuwaje waungwana?.

  Ukisikia Unafiki na Uzabi zabina ndio huu, ama kweli Nyani haoni Ku-n-lake, Serekali ya Zanzibar chini ya chama cha ccm imengiza misigi ya ubaguzi wa matababa ,kuiendesha nchi hii kibaguzi kwa misingi ya huyu cuf asemalo lolote ni Zambi, na huyu ccm afanyalo na kusema lolote ni sawa na Serekali ya Smz inamlinda au kumfumbia jicho.

  Lakini mwisho wa Ubaya ni Fedheha na aibu, ccm hivi sasa wanazirika na wanajipendekeza kuona kuwa huenda upepo ukageuka sasa wanafanya tecnic ya kujifanya victims haliyakuwa wao ndio criminal (Murder) wakubwa kila kiongozi wa ccm kwa njia hii au nyingine mikono yake ina damu za waZanzibar na roho walizo zulumu ndio hizo hivi sasa zinawatesa.

  Kilichobaki hivi sasa wanatafuta watu wawabebeshe msalaba, lakini wamesahau kuwa wanao waongoza sio Mazombi na binadabu wenye upeo wa kujuwa huyu ndie na huyu mnafiki muongo.

 10. leemick 06/07/2013 kwa 2:26 um ·

  hawa mavuvuzela hawajui hata wanachokiongea pumba tupu

 11. fey 06/07/2013 kwa 2:36 um ·

  Nyinyi UVCCM kwani ndio wasemaji wa CUF ? Kuwa munamwambia Maalim apishe vijana, inawahusu nini? Yenu yanawashinda.

  Nyerere alikaa madarakani mpaka akasema mwenyewe sasa basi nang’atuka (mbona hamkuwahi kumwambia lolote? ) na wala haikuwa basi ndipo akajiita baba wa Taifa, na bado hakukaa pembeni mpaka kafa mbona hamkusema kitu? Au kwa kuwa lenu?

  Ni dhahiri CCM kiboko yao ni Maalim Seif na sisi CUF tusharidhika kumuweka maalim, na nyinyi Kama muna wivu jinyongeni.

 12. jabir 06/07/2013 kwa 6:14 um ·

  Aslaam Aleykum Wanaukumbi.

  Katika yote yaliyochangiwa, nimepata moja tu:

  MAVUVUZELA…………………. kwamba hawa UVCCM ndio mavuvuzela siyo? Haya makubwa. Shauri yao maana kama kutukana, wameshamtukana sana Mwalim wa Mtambwe. Narudia UVCCM shauri kama walilikoroga.

 13. furahini 06/07/2013 kwa 8:59 um ·

  assalaam alykum,

  nipo hai ila ilikua nataga tu hao

  ss bac mm nadefine hao uvccm kuwa ni makunduzela badala ya mavuvuzela maana wao wanaona apo apo walipo la jana wala la kesho hawalioni

  ila wamekusha,
  mfamaji tu hawachi kutapatapa

Comments are now closed for this article.