Tumsaidie Mwenzetu yuhali mbaya

Written by  //  18/05/2016  //  Matangazo, Habari, Misaada  //  Maoni 2

Bi Asha Khamis, anaeonekana pichani ni mkaazi wa Pemba, ambae pia ni mama wa watoto wanne, ambao watatu katika hao ni walemavu wa akili, mabubu na hawawezi kutembea na wala hawana hisia za mahitaji ya kuenda haja kubwa au ndogo, bila ya uangalizi wa mama yao, anakabiliwa na mtihani wa kupoteza miguu yake miwili kutokana na majeraha makubwa yaliyosababishwa na ugonjwa wa kisukari.

Tayari mama huyo ameshakatwa vidole vitatu katika mguu wake mmoja na kama hatopatiwa matibabu ya haraka basi anaweza kupoteza miguu yote miwili kwa vile mguu wa pili nao unaonyesha dalili ya kuharibika. Hivi sasa mama huyo anatembea kwa kugaragara kutokana na kuathirika kwa nyayo za miguu yote miwili.

Kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya zaidi, wahisani na familia yake wamempeleka Dar kwa matibabu. Kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa, wamelazimika kumuuguzia nyumbani kwao Kawe, ambako humpeleka na kurejesha hospitali kutokana na kukosa fedha za matibabu na gharama nyengine zikiwemo za kumlaza katika wodi maalum kwa uangalizi zaidi.

Huyu mama ni maskini na hana uwezo wa kugharamia matibabu yake. Kwa watakaoweza kuchangia chochote, namba zifuatazo zitumike kuwasilisha michango yao kwa kupitia NGO yetu ya ZAVCO ambayo inatoa huduma kwa jamii katika masuala ya Afya ya jamii na Elimu.

Wawakilishi wetu katika Diaspora ni hawa wafuatao: Ndugu Haji Jingo, kwa walioko Marekani, Bibi Sophie Msomali kwa walioko Uingereza, Bwana Hilal Hilmi kwa walioko Oman, Bwana Mohammed Ghassani kwa walioko Ujerumani, na Bibi Layla Salum (Mamaaisha) kwa walioko Sweden.

Tunatafuta wawakilishi kutoka Dubai, Canada, Belgium na Norway, ambao watasimamia michango ili kuwezesha huduma za dharura kama hizi na yenginezo katika masuala ya afya na elimu kwa kupitia taasisi yetu hii.

Kwa waliopo Tanzania, munaweza kutumia contacts hizi hapa kwa michango yenu: +255 714 870 004 Jina ni Dhamir Yakout na +255 713 187 733 Jina ni Maryam Marshed. Kwa ambao watapenda kwenda kumuona Bi Asha, wawasiliane na watu hawa: +255 776 041 420. Anaitwa bwana Khatib, huyu ndio anaemshuhulikia Bi Asha huko Kawe Dar es salaam. Mwengine ni Bi Hadia mwenye nambari +255 777 877 920. Tafadhali sambaza ujumbe huu.
Ahsanteni

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 2 katika "Tumsaidie Mwenzetu yuhali mbaya"

 1. matata 19/05/2016 kwa 12:45 mu ·

  Jamani wakati tunachangishana ili kujaribu kuokoa miguu ya mama, dada, ndugu yetu ni vizuri tuelewe Kisukari si maradhi na tiba yake ni nyepesi. Tuelimishane kuhusu kisukari.

  Wakati athari alizozipata mama yetu huyo ni mbaya kama wanaomshughulikia wakifata ushauri wa mlo katika kitabu hichi ambacho rafiki yangu alinitanabahisha

  kiungo hiki http://biswaroop.com/wp-content/uploads/2015/01/book-How-to-cure-diabetes-type-I-II-within-72-hrs-ebook.pdf aliye karibu naye na awezaye kukitafsiri afanye hivyo ili wengi wanufaike na elimu ya kisukari.

  Au video hizi

  https://www.youtube.com/watch?v=4edofibXOiM

  https://www.youtube.com/watch?v=2pjkC71exKU

  Kukinga ni bora kuliko kutibu.

  Huyo mama apatiwe majani 10 ya mrehani mabichi na tangawizi mbichi kama gr. 10-20 ale pamoja kila asubuhi kabla ya kula chochote na baadae asubiri dakika 30 ndio ale mlo wake.
  Ama aina ya mlo inashauriwa katika kitabu na video.

  Huu natumai utakuwa ni mchango mkubwa ili kujiepusha na kisukari.

  Andiko hili halikusudii kuondoa umuhimu na kasi ya kumchangia mwenzetu. Tumchangie kwa hima.

 2. Abdul Zakinthos 19/05/2016 kwa 9:21 mu ·

  Subhana Allah
  Mungu atampa nafuu nasisi kutuepusha na majanga haya
  Jengine tuwahi hospitali tusikae ndani tukitokewa na matatizo sio dk ya mwisho

  Na uzuri wasimamizi wa michango pia watu wakichangia warudi kutueleza kiasi gani kimepatikana

Comments are now closed for this article.