TUITAFUTE SKAGIT ILIPO KABLA YA KUWAPELEKA WAHUSIKA MAHAKAMANI

Written by  //  25/07/2012  //  Habari  //  Maoni 1

http://www.interphase-tech.com/chartplotters.htm

http://www.amazon.com/5-Inch-Monitor-Underwater-Camera-Combo/dp/B0043AWU7O
Nimejaribu kukusanya takwimu nyingi tu za kwa vipi meli ya skajit ilizama,ilizamia wapi na kwa hivi sasa itakuwapo wapi.
Moja ya takwimu niliyokusanya ni kwamba meli hiyo ilizama majira ya coodinates hizi.
06’26.23S -039’10.40E
Coodinates hizi ni ngeni kwangu nimejaribu kuzi- convert kwa degmin au degminsec hazikubali sijui amezipataje au ametumia coodinates aina gani lakini pia sio tatizo alietoa coodinates hizi ni madaiva ambao wanategemea meli hiyo ya skagit itakuwa ipo hapo.
Meli ilipozama tutasema (sink) lakini haitakuwapo hapo katika degrees hizo lazima itakuwa imekokotwa na maji na maji aghlabu katika wakati huu wa upepo wa kusi maji yatakuwa yanakwenda kaskazi kwa hivyo meli itakuwa imekokotwa na maji ikiwa bado ipo juu inaelea kabla ya kuzama kabisa na itaweza pia kukokotwa na maji wakati ikiwa imezama kabisa .
Hasa ukizingatia kwamba under sea floor ya pahali hapo ipo tambarare yaani sawa isiyo na tofauti kubwa ya kuweza kuizuia meli isiweze kukokotwa na maji ikiwa katika ardhi ya chini ya bahari.
Katika chart No 665 ya british admiralty chart ambayo ni APPROACHES TO ZANZIBAR position hiyo haimo katika chart hii ya 665 au kwa maneno mengine tunaweza kusema haijaingia position hiyo ya coodinates kwani itakuwa far south na ikiwa far south ni kwamba sio kweli hata kidogo kama meli hii imezama chumbe.
Ripoti iliyopokelewa kuzama kwa meli ya skagit kutoka katika kilimanjaro ilipokelewa ikiwa meli inazamia 6nm kutoka fungu yasin ikiwa ni 6 nm kutoka fungu yasin hii ina maana kwamba meli imezamia katika majira ya dar-es-salaam zaidi kuliko zanzibar ,inawezekana ilikuwa ikichukuliwa na maji kujia zanzibar na pia ikisukumwa na upepo lakini ukweli ni kwamba imezamia majira ya mbweni usawa na rasi ya mbweni ambapo umeme wa kidatu ulipoanzia na sio chumbe kama inavyozungumzwa.
Inazungumzwa chumbe sababu bara wanataka kujivua kwamba ilizamia mbali na wao ili lawama ziwaondoke na hasa kwa vile hawakutoa msaada wa aina yoyote wakati taarifa kamili za kuzama kwa skagit walikuwa nazo.
Sasa nije pale nilipokusudia, gazeti la nipashe limeripoti kwamba madaive hawakuweza kuiona meli ya skagit mpaka wapate chombo kinachoitwa FLASH DIVER FOUNDER na chombo hicho hakipatikani afrika mashariki ambacho kinaweza ku-detect iron na
aluminium.
Sijui kama ni kweli maneno hayokwani hakuna ushahidi wa kuonyesha chombo hicho kama kipo kweli,nimejaribu kusearch lakini tupu hakuna kitu.
Chombo cha kutafutia chombo ambacho kimezama au muinuko kutoka ardhi ya bahari hususan maji kidogo kama yaliyoko sehemu iliyozana skagit ni
chartplotter aina ya interphase.
Hapo ipatikane interphase ambayo inaitwa Navigational chart plotter
ISCAN 180SE
COLOURE TWINSCOPE SE
ISCAN V90 SE
CHART MASTER II
CHARTMASTER I69CS
V6 AND V6i
Moja katika vyombo hivi 6 kinaweza kuditact meli iliyozama kwa mbali kabla ya kuikaribia na ukisha kuikaribia na ukaijua kama ipo hapa chini utatumia under sea tv kabla ya kuteremka mzamiaji yoyote
kila kitu kitajionesha hapo.
chartplotter interphase thamani yake si zaidi ya dollar alfu mbili zipo katika hizo hapo thamani yake ni dolar mia saba tu za kimarekani na unaweza kununua online ukatumiwa popote duaniani kwa chini ya wiki moja tu.
under sea tv inayo camera ditector thamani yake ni chini ya dollar 200 za kimarekani.
Sijui wastakiwa wa meli hiyo kama nahodha na mwenye mali anaweza kustakiwa kupitia kigezo gani kwani ushahidi haujakamilika mpaka meli ipatikane na ijuilikane chanzo lakini kutokana na uzumbukuku wetu ndio tayari wanapelekwa mahakamani.Kupatikana kwa meli hiyo ndio ushahidi kamili utapatikana na kujuilikana chanzo cha matatizo yote.
Meli ndogo kama hiyo bila shaka KMKM wanaouwezo wa kuiibua hapo itakapoonekana kama itaonekana karibuni .

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni yamefungwa.