Tathmini yangu, Mwaka mmoja baada ya Uchaguzi wa Zanzibar

Written by  //  05/12/2016  //  Habari  //  Maoni 4

Jecha-19Nov2015

Na Mzanzibari Halisi
Ni mwaka mmoja sasa tangu upite uchaguzi Mkuu, kwa upande wetu Zanzibar hali ni tete, maisha yamekuwa magumu kupita maelezo, hii inatokana na kwamba Serikali ambayo ipo madarakani kwa sasa haikubaliki na wananchi wengi wala haipewi mashirikiano, tunathubutu kuiita Serikali haramu ambayo inatawala kwa mabavu si kwa ridhaa ya wananchi.

Hata tujaalie kwamba ipo madarakani kihalali basi kama itakumbukwa katika kampeni za Rais aliepo madarakani Balahau Shein alisema atavigeuza visiwa vya Zanzibar kuwa kama Dubai ya Afrika Mashariki, mwaka umepita hatujaona harakati zozote za kuipeleka Zanzibar Dubai zaidi ya ugumu wa maisha na unyanyasaji wa Raia, tumeshuhudia wafanyaBiashara wamehamishwa katika Jumba la Treni lililopo Darajani Mjini Unguja, katika kipindi cha Ramadhan Kuelekea Sikukuu, kipindi ambacho kinaaminika ni cha Biashara, lakini SMZ kwa makusudi wameamua kuwahamisha wafanyaBiashara hao kwa sababu ni wapinzani kwa makusudi ili kuwatia adabu, na karibuni pia makontena yaliopo Darajani nayo yamevunjwa, kila wanapokaa wafanyaBiashara kujitaftia riziki wanawaondoa.

Uhasama, Chuki baina ya wananchi ndio yanayoikabili Zanzibar kwa sasa, na katika historia ya Wazanzibari tar 28 Octoba haitosahaulika na kuitwa JECHA DAY kwa kitendo chake cha kinyama alichowafanyia Wazanzibari kwa ajili ya kulinda ya Pishi ya mchele na maslahi yake Binafsi, kama alifanya vile kwa haki kwa nini Kibabu Jecha haonekani mitaani, anaishi kwa kulindwa, hana raha ya kuishi na kuchanganyika na jamii yake, maslahi aliyoyapata kwa kufanya utumbo huu yatamtokea puani hapa duniani na huko mbele ya safari, sisi hatumsamehe kwa alichotufanyia na ataendelea kupata laana za viumbe vyote vilivyohai mpaka mwisho wa dunia.

Napenda kuwasilisha

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 4 katika "Tathmini yangu, Mwaka mmoja baada ya Uchaguzi wa Zanzibar"

 1. Jino kwa Jino 05/12/2016 kwa 7:07 mu ·

  AJITIA UNA HODHA KUSAFIRIA UBAO .

  BARA ZOTE AMEPITA HAJUI IPI ENDAYO.

  ULIMWENGU WATELEZA WAANGAPI WAANGUKAO.

  Kazi kwako Jecha umehaidika kwa pesa mbili tatu nakuona uko vile vile au zaidi ya vile kimekukwama KISIKI CHA ROHOOOO.

 2. moyo 05/12/2016 kwa 9:30 mu ·

  Mchimba kisima hutumbukia mwenyewe.

  Allaah atuokoe na janga hili tulilo nalo.

 3. salali 05/12/2016 kwa 1:39 um ·

  Aendelee tu kukaa maisha ya kificho ficho ole wake tuje kukutana naye ana kwa ana hapo ndipo ataikumbuka siku alochakachuwa matokeyo ya uchanguzi wa Zanzibar ulokuwa huru na haki. Huyo ni wakumkata viungo kimoja kimoja kama kuku.

 4. Z.I.7 06/12/2016 kwa 7:15 um ·

  huyu kaona bora awafuramishe wazanzibari wote kwa tanganyika na yeye mwenyewe sasa hana thamani wala heshima yoyote anaishi kwa mitego na wanazidi kumtengenezea kumzamisha eti baada ya kufanya aliofanya na kuifikisha zanzibar ktk hali ilio.

  wanasema apewe tunzo inaweka wazi kuwa haya hakuyafanya peke yake kwani chaguzi zinafanywa kila baada ya muda na karibu ktk kila nchi duniani haijatokea kuwa mkuu wa tume kupewa tunzo kwasbb kazi yake ni kama kazi nyingine yoyote kwanini huyu wanasema apewe tunzo? its simple walishirikiana ktk kuharibu uchaguzi kwa manufaa ya kundi sio ya wananchi.

  lkn jee! baada ya walioyafanya na jecha wao kuna faida kwao? na jecha nae baada yakuwafurahisha hao wanosema apewe tunzo yeye anaishi vipi? nafkiri ni maisha ya mshumaa

  sasa jecha chukuwa tunzo na itakuwa muhuri ktk paji lako la uso utakuwa maarufu kwa wanaadam na mbele ya MOLA hakutakuwa na tabu ya kutafutwa.

  na wale mloshirikiana nao siku ya siku watakuja kukushangiria kwa uzuri wako wakupewa tunzo cinema ya maisha iko ktk reel za mwisho mwisho kwa hiyo the END haiko mbali

  tunasubiri sherehe ya TUNZO

Comments are now closed for this article.