TAARIFA KWA VYOMBA VYA HABARI

Written by  //  14/06/2013  //  Habari  //  Maoni 28

Bimani

Imekuwa ni mazowea kila inapojiri kwa Wazanzibari kushikamana katika mwamko wa maslahi ya Nchi, kuwajengea mazingira ya hofu, vitisho, uchokozi, hujuma na kuwaparaganya, kupitia visingizio mbali mbali vya propaganda, vipigo, ubabaifu, na unyang’anyi.

La kusikitisha ni kuona kwamba vitendo hivyo vinahamasishwa na kutekelezwa na hata sehemu ya Mamlaka za Serikali, wakiwamo baadhi ya watendaji wa vikosi vya ulinzi na usalama.

Lengo ni kuondosha utengamano, na kuhamisha fikra juu ya mstari wa maslahi na kuwapeleka watu, ndani na nje ya Nchi, katika ajenda za kisiasa za kistratejia.

Hakuna mwenye busara na mpenda haki, na zaidi aliyeshuhudia, ambaye hataamini kuwa kilichotendeka maeneo ya Darajani Mjini Unguja, Siku ya Jumatano tarehe 12 Juni 2013, majira ya Saa 6.30 mchana, kama si uchokozi wa makusudi wa wahuni na wanavikosi, dhidi ya Wananchi watulivu, wapitanjia, na waliokuwepo katika harakati za kawaida za kujitafutia pato na riziki za halali kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Si maadili ya askari, mlinzi, au mwanausalama yeyote aliyefundishwa kutangulia kufyatua risasi, zaidi ya nane, katika mazingira tulivu na mikusanyiko ya kawaida ya binaadamu, bila ya hata hali tete au mzozo wa kiasi kidogo kabisa, pasi na kuwa na ajenda ya siri; na hivyo ndivyo ilivyojiri katika maeneo hayo muhimu ya uchumi na haiba ya Nchi yetu.

Ni lipi, kama lengo siyo kuchokoza, kupora, kufitinisha ili kuharibu, haiba na shaksia tulivu, tena machoni mwa hata wageni wanaotembelea Visiwa vya Unguja na Pemba, ambao sasa wanashuhudia hadhiri na dhahiri yake.

Chama cha Wananchi, CUF, kinaiomba Serikali ichunguze kwa kina mwenendo na wahusika wakuu wa vitendo hivyo, watu wachache, ambao bila shaka wamekosa hikma, uchungu wa maendeleo na wasiojali maslahi ya Nchi ya Zanzibar.
Ni vyema ikazingatiwa kwamba siku zote busara ndiyo njia bora maishani, kulikoni matumizi ya mabavu na mtutu wa bunduki, hasa pale ambapo Mamlaka za Dola na Wananchi, kila upande unamuhitaji mwenzake ili kuleta maendeleo.

Chama cha CUF, kinawaomba wananchi wote kuwa watulivu, wasichokozeke, wakielewa thamani ya sasa ya subira yao, ndiyo malipo ya maslahi mema ya baadae au hivi karibuni, ya Nchi, wakati huu ambao Taifa linaelekea katika mabadiliko makubwa ya kihistoria.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imesainiwa na:
Mheshimiwa Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Haki za binadamu, habari, uenezi na Mahusiano ya Umma

Kuhusu Mtunzi

Mwalimu wa Sekondari na Mwanaharakati wa Mamlaka kamili ya Zanzibar

View all posts by

Maoni 28 katika "TAARIFA KWA VYOMBA VYA HABARI"

 1. Multiways 14/06/2013 kwa 4:45 um ·

  dah,,napatwa na huzuni sana,,kuona,,watu wa nyumbani hapa znz wanapigwa na kuporwa mali zao,,ni ukweli wa dhahiri,,yoyote alieona,,yale yanayotendeka pale darajan..atakua na hisia za huzuni sana sana,,bila ya kuzingatia uchama na kuona wale ni wananchi wanaojitaftia rizk halali,,serikali haion,,ndio inazid kuwapa mazingira magumu ya kuish,,!!,,kama serikali yenye kuwapenda,,na kuwajal wananchi wake,,inafikia kufanya hivyo,,haioni wananchi wanazid kutokwa na imani na uendeshaj huu,,yasiishie tu,,,serikali hii inaish kwa mujibu wa sheria na kanuni,,,wakat uhalisia hasa,,unakua tofauti,,dah,,inauma sana,,mungu atawapa hifadh watu hawa,,amin

 2. Multiways 14/06/2013 kwa 4:45 um ·

  dah,,napatwa na huzuni sana,,kuona,,watu wa nyumbani hapa znz wanapigwa na kuporwa mali zao,,ni ukweli wa dhahiri,,yoyote alieona,,yale yanayotendeka pale darajan..atakua na hisia za huzuni sana sana,,bila ya kuzingatia uchama na kuona wale ni wananchi wanaojitaftia rizk halali,,serikali haion,,ndio inazid kuwapa mazingira magumu ya kuish,,!!,,kama serikali yenye kuwapenda,,na kuwajal wananchi wake,,inafikia kufanya hivyo,,haioni wananchi wanazid kutokwa na imani na uendeshaj huu,,yasiishie tu,,,serikali hii inaish kwa mujibu wa sheria na kanuni,,,wakat uhalisia hasa,,unakua tofauti,,dah,,inauma sana,,mungu atawapa hifadh watu hawa,,amin

 3. serelly 14/06/2013 kwa 7:42 um ·

  Na leo wakati ninaelekea kazini kwangu majira ya saa moja asubuhi niliona harakati za kufunga maturubali katika eneo la Darajani, katika sehemu ambalo huegesha gari za Makunduchi, Michamvi na Fumba. Je kulikuwa na harakati gani? Maana maturubali yalikuwa rangi ya kijani na viti vya plastiki rangi ya kijani na vimepakwa umanjano kwa nyuma sehemu ya kuegemea, au ulikuwa mkutano wa CCM?.

  Kama ni mkutano wa CCM kwanini wafanye pale Darajani ndani kituo cha magari ya Abiria?

  Jamani anaelijua ilikuwa nini atuambie tujue maana hii nchi yetu sote na tuna haki na wajibu wa kuilinda na kujilinda. Na wala CCM hawana hati miliki ya Zanzibar.

  Nawasilisha.
  SERELLY.

 4. makame silima 14/06/2013 kwa 8:35 um ·

  Kifo cha Mende ndio ccm itavyo kufa Zanzibar, Hawajuwi kuwa Enzi za Serekali kuendeshwa kiubabe zimepitwa na wakati, Kumbukeni ccm kuwa Hossen Mubaraka (Mjukuu wa Firauna Misry) alikuwa na Jeshi kubwa na Sauti na nguvu yenye kutisha na Kuwatisha watu wa Misry?.

  Leo Jeshi lake lile na nguvu alokuwa nayo iko wapi? imeyayuka kama Pande la Barafu lililopigwa na Juwa. Na hivi sasa ana makesi Kapu tele, na yuko Gerezani anasubiri hukumu ya kunyongwa.

  Yale majumba na marasili mali yote alio jilimbikizia yamemtumbukia nyongo Mwisho wa Ubaya ni Aibu na Fezeha.

  Kwa hio washe viongozi wa ccm wenye misimamo mikali , hatuko mbali kula nao sahani moja, kikiwaka tu , basi tutakula nao sahani moja hatuto wacha hivi hivi tu ,mpaka kieleweke.

  • xkalasinga 15/06/2013 kwa 12:51 mu ·

   Unajifurahisha nafsi yako mzee wa tumbatu … Mubaraka na ccm wapi na wapi? sometime u talk nonsense mjomba, unanifanya nikujumlishe kwenye kundi lile la micuf inayodanganta watu Kuwa ati wazalendo .GTFO

 5. Bosco 14/06/2013 kwa 9:31 um ·

  @makame silima humuogopi rais docta shein ambao yeye hamuogopi mtu? Shauri yako ngoja akusikie.

 6. bin nassor 15/06/2013 kwa 5:47 mu ·

  1. wadau nimesoma na nimepitia kwa kina ila ninachotaka nielezwe kwa makini hivi kwa nini habari ikisemwa na c.u.f inakua ya wazanzibar na inayosemwa na c.c.m inakuwa si ya wa znz,wakati c.c.m imekuja miaka 15kabla ya c.u.f je kama habari itasemwa na wafuasi wa chadema wambao ni waznz haitokua kauli ya waznz?

  2. la pili naomba nieleweshwe wapi zanzibar wapi Unguja wapi Pemba,kwa sababu ukisoma ramani hakuna kiti kilichoandikwa unguja labda ramani inayoonesha visiwa hivi viwili lakini ramani ya ulimwengu inaonesha zanzibar na pemba,ramani ya Africa inaonesha Zanzibar na Pemba,ramani ya Tanzania Bara inaonesha zanzibar na Pemba ila ramani ya visiwa viwili inaonesha Unguja na Pemba hata hiyo Unguja itaandikwa zanzibar.

  3. Hata ukipanda ndege kutokea popote pale Abroad,Arabic,Asian,hata Tanganyika kama unaenda Unguja itaandikwa unaenda zanzibar,lakini ukenda Pemba itaandikwa Pemba,hata vyama vya siasa vya kabla ya mapinduzi vilikua vinaitwa ZPPP and ZNP maana yake (ZPPP) Zanzibar and Pemba People Party na (ZNP) Zanzibar Natuonal Party sasa hii kuita wazanzibar kila kitu wakati wenyewe wa zanzibar hawako hivo si vizuri…bora iandikwe tu c.u.f au c.c.m wamesema hivi wamesema hivi bt msitumie majina ya wazanzibar wakati historia inaonyesha wazanzibar wenyewe ni watu wa Unguja sio Wapemba

 7. fey 15/06/2013 kwa 6:27 mu ·

  @Bin Nassor: kwa maana hiyo muungano ni wa Tanganyika na watu wa unguja wa Pemba hawamo? Kwa nini wasiwe na nchi yao na mammlaka yao?

 8. bin nassor 15/06/2013 kwa 6:42 mu ·

  @ Fey,sina maana hiyo nnachotaka kujua ni wapi zanzibar na wapi Pemba,kwa sababu kutumia neno zanzibar katika maslahi ya mtu mmoja mmoja au chama si vizuri bora mtu asema C.U.F au C.CM au NCCR wamefanya hivi na hivi au kiongozi wa chama fulani amefanya hivi kwa sababu maalim seif au Bimani au Vuai wa c.c.m au hata shein akukaa kwenye jukwaa la chama hawawakilishi wa zanzibar wananwakilisha vyama vyao ,lakini seif Mweusi au seif madevu,au shein wakizungumza ki serikali wanaiwakilisha zanzibar.

  @Fey,halafu lazima tujue wapi zanzibar na wapi Pemba sio kitu kinatokea pemba mtu aseme kimetokea zanzibar,au kitu kinatokea Tanganyika mtu aseme kimetokea tanzania hapana kuna Tanganyika na Zanzibar na Pemba,neno unguja historia yake limetokana na unguja ukuu sehemu ya watu wa mwanzo kufikia hapo zanzibar,lakini kisiwa kinaitwa zanzibar so Pemba ni Pemba na znz ni Zanzibar hata birth certificate ukizaliwa Pemba inaandikwa Pemba bt ukizaliwa unguja inaandikwa Zanzibar

 9. xkalasinga 15/06/2013 kwa 8:11 mu ·

  Umeona eh @bin nassor ! afadhali umewashtukizia hawa jamaa hatari sana.MOFO

 10. rasmi 15/06/2013 kwa 9:48 mu ·

  @bin nassor

  Kwa waliozaliwa jana na wakakataa kuisoma historia mutawababaisha ni nini Zanzibar, lakini kwa wanaotaka – hata hao wahafidhina basi ni tusi kuja kuwaambia maneno ya aina hio.

  Ukitaka ushahidi angalia nembo ya SMZ utajua ni namna gani maneno yenu hayatoingia akilini mwao. Ile nembo imeandikwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na ina visiwa mle ndani vya _______

  Ni wazi ni kujipotezea wakati kujaribu kujibu masuala yalio wazi, lakini kwa faida ya munaotaka kuwababaisha Zanzibar si Unguja tu – ni eneo ambalo leo tu limebakishwa hio Unguja na Pemba, soma historia. Hivyo Pemba pia ni Zanzibar…

  Shangaa na hili basi, ukienda wewe huko kunakoitwa Bongo, utaitwa Mpemba na si Muunguja mbona huulizi kwa nini!?

 11. bin nassor 15/06/2013 kwa 10:46 mu ·

  @ rasmi,

  mm ni mpemba tena mzaliwa baba na mama kama wakujua jondeni ndo kwetu lakini hili ninalosema ni kweli na ukitaka ushahidi hata hao viongozi wa smz wakitanka kitu kuhusu Unguja hawasemi unguja wasema zanzibar,hili neno unguja tunlikazania sisi wapemba kuwaita wazanzibar ni watu wa Unguja lakini wenyewe wala hawalitamki hilo Unguja kwa sababu halipo,hata enzi za masultani utasikia ntawala wa zanzibar na ntawala wa Pemba usibishe ki ubishi tu,historia haiko hivo tena ndani na nje ya nchi kama unavosema,hata katika miradi ya maendeleo ndani na nje ya Zanzibar inaandikwa Zanzibar na Pemba na hata ukiasoma gazeti lazanzobar leo ukurasa wa nje kuna tangazo la meli ya kili 4 imeandikwa ratiba ya kutoka anz to Dar,na tangazo la Sea bus 3 limeandikwa ratiba ya meli kutoka Znz-Pemba-Dar

  mimi mnareudi pale pale kama kitu kimefanywa na C.U.F au C.C.M au CHADEMA itamkwe kimefanywa na chama husika mkisitamkwe wazanzibar,kama kitu kimetamkwa na kiongozi wa serikali kwa idhini ya serikali basi kiandikwe wazanzibar hata iwe katanka seif au shein…kwa hiyo sio kila linalosemwa na CUF liwe la waqzanzibar wote au linasomwa na CCM liwe na CCM peke yao huo ni ubabaishaji,

  I am the CUF supporters and i have Fan card,lkn kwa hili twakosea hakuna kitu Unguja na wenyewe watu wqa zanzibar wana haki ya kukataa kuitwa Unguja na wala hakuna wa kupinga na historia ndivyo ilivo,kama unajua kusoma google ulimwengu nzima utaona,mpaka vitabu kikiandikwa utaona kineandikwa Zanzibar na kineandikwa Pemba,hata mawizara ya serikali yanaandikwa WIZARA YA JJJJJ -PEMBA lakini pale Unguja twasemapo yaandikwa WIZARA YA JJJ -ZANZIBAR

  na kuhusu bara Waznz wanaitwa wapemba kwa sababu wapemba ni watu wa mwanzo kuchakarikia biashara kuliko waznz na pahala popote alipo mpemba lazma atajiexpose kama yy ni mpemba,bt pahala ambapo wapo waznz (waUnguja ) hawapendi kujiexpose wajulikane ndo mana sisi wapemba kila pahala mpaka msumbiji twajulikana.

  huo ndo ukweli na utabaki kuwa ukweli mpaka waunguja watufukuze kwao

 12. MAWENI 15/06/2013 kwa 2:00 um ·

  Hayo ni matekeo ya kikao cha NEC. YA CCM. Katika mkutano wao kutoa msimamo wao kuhusu rasimu ya katiba inayo pendekeza sirikali tatu.
  Linalo wa shughulisha wao ni kuwa Zanzibar itapata mwanya wa kuelekea mamlaka kamili. Ndio maana vitisho vyote hivyo, ili kuwatoa watu kwenye njia ilo nyooka kudai nchi yao. Nina wasiwasi mengi ya mesha pangwa. Lakini wazanzibar wasimame kidete wasi chokezeke au kubabaishwa.

  ZANZIBAR KWANZA YENYE MAMLAKA YAKE KAMILI NJE NA NDANI!

 13. makame silima 15/06/2013 kwa 2:33 um ·

  Akina Warioba kibaruani tena Waandishi Wetu Toleo la 298 12 Jun 2013 Zanzibar wahoji katoa wapi maoni serikali tatu? WAJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Tanzania Bara, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, ndiyo wanaotarajiwa kuandika Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara), vyanzo kadhaa vya habari vya Raia Mwema vinaeleza. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ya habari, tayari maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yamefikia hatua ya kuridhisha na wakati wowote, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema atawasilisha bungeni muswada huo. Ingawa vyanzo hivyo vya habari vinathibitisha kuwapo kwa maandalizi hayo, lakini AG Werema hakuweza kupatikana hadi tunakwenda mitamboni, simu yake ikiita bila kujibiwa. Tayari Jaji Warioba ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akihojiwa kupitia kipindi cha televisheni cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, amesema hakuna haja ya kukusanya upya maoni ya wananchi wa Tanzania Bara kwa kuwa yamekwishakusanywa na Tume yake na kwamba watakaopewa jukumu la kuandika Katiba ya Tanzania Bara, wanaweza kutumia maoni yaliyokwishakusanywa. Lakini wakati hayo yakiendelea, taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC-CCM) zinabainisha kwamba kikao hicho kilichoitishwa Jumatatu wiki hii mjini Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, kimesikiliza hoja nzito zikiwamo za kuhoji ni wapi Tume ya Warioba imepata maoni ya kuwapo kwa serikali tatu. Mjumbe mmoja wa kikao hicho kutoka Zanzibar anaelezea kuchachamaa kwa wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, wakisema maoni ya Katiba kuhusu Muungano kutoka visiwani humo yalikuwa ya aina mbili tu na si tatu. “Zanzibar tulitoa maoni ya aina mbili. Kwanza ni maoni kuhusu muundo wa Muungano uwe wa serikali mbili kama ilivyo sasa, lakini wengi walitoa maoni ya kuwapo kwa Muungano wa mkataba. Haya ndiyo maoni yaliyopo kule hadi sasa. Kwa hiyo, Warioba na wenzake wamepata wapi haya mawazo ya serikali tatu?” kinaeleza chanzo chetu hicho kutoka Zanzibar, kwa sharti la kutotajwa gazetini jina lake. Katika hatua nyingine, viongozi na watu wengine mbalimbali nchini wameendelea kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela ambaye akiwa katika wadhifa huo, mjadala wa kuundwa upya kwa Serikali ya Tanganyika ulichukua nafasi kubwa kiasi cha Bunge kuridhia Serikali tatu na kisha Mwalimu Julius Nyerere kufanya kampeni iliyofanikiwa kuzima jaribio hilo, alisema ni vizuri zaidi kwa viongozi wakuu kuacha maoni ya wananchi yasikike badala ya kuharakisha kutoa maoni yao. “Mimi kwa kweli nadhani ni vizuri kuacha kwanza maoni ya wananchi yasikike, tukizungumza sisi viongozi, kama mimi, kuna hatari watu wakaacha kujadili kilichomo kwenye rasimu na badala yake wakajadili maoni yangu. Si vizuri maoni ya viongozi yatawale wakati wote maoni ya wananchi, kiongozi unapoharakisha kutoa maoni yako ina maana unawagawa watu kimtazamo na uwezekano wa kutumia nguvu kubwa kujadili maoni yako ni mkubwa,” anasema Malecela ambaye alipata kuwania ateuliwe mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, mwaka 1995 na baadaye mwaka 2005. Naye Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mazungumzo yake na mwandishi wetu alizungumzia hofu ya uwapo wa serikali tatu kuhatarisha uhai wa Muungano. “Kwanza serikali tatu si suluhisho la matatizo ya Muungano. Hili suala la ama kuvunja au kutovunjwa kwa Muungano kwa sababu ya serikali tatu kwa kweli kwa sehemu kubwa inategemea na dhamira ya viongozi wanaochaguliwa kuongoza nchi. “Na kwa sababu ni dhamira ya viongozi ndiyo inayoweza kuvunja Muungano, basi ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi wenye dhamira safi na Muungano, mamlaka ya wananchi sasa ifanye kazi kwa uangalifu sana.” Hata hivyo, alipoulizwa ni kwa namna gani wananchi wataweza kuwa na utabiri wa mgombea gani mwenye dhamira ya kulinda Muungano kwa kuzingatia ukweli kwamba dhamira si jambo la kudumu kwa anayepewa madaraka, Baregu alisema kwa kuwa viongozi wanatokana na jamii ya Watanzania, wanajulikana wasifu na dhamira zao. Lakini, Dk. Honest Ngowi, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, mkoani Morogoro anazungumzia rasimu ya Katiba Mpya katika muktadha wa kiuchumi hasa kuhusu deni ya taifa. “Ni lazima Katiba Mpya iweke ukomo kwenye Deni la Taifa. Ukomo utokane na asilimia ya Pato la Taifa. Kusipokuwa na ukomo, taifa litakuwa na matatizo makubwa ya kiuchumi,” “Baadhi ya nchi za Ulaya kama vile Ugiriki hivi sasa zina matatizo ya kufilisika kwa sababu kwenye kukopa hawakuwa na ukomo. Katiba ya Marekani imeweka ukomo huu na ndiyo umeisaidia kuvuka kutoka kwenye mdororo wa uchumi,” anasema Dk. Ngowi. Kuhusu rasimu ya Katiba kuweka idadi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri kuwa 75, Dk. Ngowi anasema ni muhimu kwa wabunge hao 75 kupata mafunzo ya hali ya juu kuhusu masuala ya Deni la Taifa, ili washauri vizuri na kuibana serikali kwenye masuala ni muhimu, wapewe ufahamu wa kutosha kuhusu maana na athari za deni la taifa. – See more at: http://www.raiamwema.co.tz/akina-warioba-kibaruani-tena#sthash.0MzFTtWA.dpuf

 14. Ghalib 15/06/2013 kwa 3:16 um ·

  @Bin Nassor

  Hujakosea kabisa,mimi leo hii nilikuwa najaribu kumfahamisha mtu wapi natoka, mana nilimwambia natoka zanzibar ikawa tabu kumfahamisha ,ikabidi nimwambia Tanzania, na nikamuonesha ramani ya zanzibar, kilicho nishangaza Unguja imewekwa jina la zanzibar na kisiwa cha pemba imeandikwa pemba.

  Miaka ya nyuma ilikuwa unaona majina Unguja na Pemba ikisha unaona neno zanzibar. Huu ni mpango wa mkoloni kutugawa wazanzibari, wao ndio wanao fanya juhudi hizi kutugawa, hili halikubaliki, tunatakiwa tupiganie, badala ya kuandika UNGUJA NA PEMBA then Ikafuata zanzibar wao Wameliondoa jina la unguja kabisaa.

 15. kemit 15/06/2013 kwa 3:39 um ·

  AA,
  @Bin Nassor.
  Ami wa Jondeni.
  La kwanza, sio kila kinachoandikwa katika google ni sahihi.
  La pili, umetoa kiufupi unguja inatokana na unguja ukuu! Je “Zanzibar” umejaribu kujiuliza inatokea wapi! Kama unaelewa basi tufahamishe na usiwe unapinga kila unalofahamishwa na akina @Rasmi kwa kupoint number za gari na tickets za maboti.

 16. rasmi 15/06/2013 kwa 4:19 um ·

  @Ghalib,

  Sikufikiria kama unaweza kunasa katika mitego ya kitoto kiurahisi hivyo, tokea lini kila kilichoandikwa kikawa sahihi! Bin Nassor kakupa kila aina ya mifano ili uingie mtegoni na wewe umeingia kichwa kichwa.

  Wewe ulipoitizama hio ramani ulipomuambia huyo jamaa unatoka Tanzania, je uliweza kumuonesha hio Tanzania ama ulimwonyesha Tanganyika – maana hata Zanzibar sasa hivi ni Tanzania pia ama sivyo! Kama hukuweza kuona kisiwa cha Unguja kimeandikwa Unguja bali Zanzibar, wewe tokea ulipoanza kuulizwa unatokea wapi na ukasema Zanzibar ulitegemea hilo jina katika ramani liekwe wapi, kati kati ya bahari baina ya kisiwa cha Unguja na Pemba!

  Unachokiona katika ramani ni Capital city ya kisiwa, ambayo huekwa katika kisiwa kilicho kikubwa, angalia Comoro mji mkuu wao wa Moroni uko katika kisiwa gani.

  Pia unachokiona ni eneo dogo ambalo kabla ya huo usanii wa kikoloni lilikua likiitwa Zanzibar, kumbuka miaka hiyo ya zamani mtu wa Mombasa pia angelikuambia ni raia wa Zanzibar – anaetoka katika eneo/mji unaoitwa Mombasa.

  La mwisho unaposema wewe ni Mzanzibari unakusudia nini kama si Utaifa! Kilichopo hapo kwenye ramani ni jina la taifa na hao wakoloni shukuru hawakuliondoa hilo jina hapo lilipo, Watanganyika wanatafuta namna sasa ya kulirudisha lao – Unguja na Pemba ni visiwa ambavyo mji wake mkuu ni huo Zanzibar. Muulize mtu yoyete ambaye kazaliwa Unguja atakuambia kazaliwa Unguja; halikadhalika aliezaliwa Pemba atakuambia kazaliwa Pemba. Muulize uraia wake atakuambia ni Mzanzibari, hatokuambia Muunguja ama Mpemba.

  Raisi anaitwa wa Zanzibar ama anaitwa wa Unguja! Je ikiwa hivyo ndivyo ulivyofahamu kwamba Zanzibar ni Unguja huyu raisi tulienaye ni wa wapi!

  Usibabaishwe na hoja za kitoto, watu wana hasira tokea walipoambiwa warejeshe Tanganyika yao wanakuja na hoja za kukuondoa kwenye ajenda. Ungeliuliza pia kwa nini huioni Tanganyika katika ramani ikiwa kila unachokiona ndio ukweli ulivyo!

  Zanzibar Kwanza

  • Ghalib 15/06/2013 kwa 4:27 um ·

   @ Rasmi

   Kama ni mtego basi tumeganda wote wazanzibari, mimi nimekubaliana na hoja ya bin Nassor moja tu, Ramani ya dunia kwa muonekano wa zanzibar, haiko sahihi, ukweli nda google map, hivyo ndo inavyosomeka zanzibar, jiulize nani ambaye anapeleka hio map huko kwa wana mitambo ?

   Neno Unguja linajisapia taratibu na badala yake kuna Zanzibar and Pemba, ni aina flani kisaikologisti kugaiwa wazanzibari, vizazi vya leo tutawachanganya,mimi leo nilitaka niweke habari hii hapa mzalendo, na leo hii hii ndio niemgundua hilo, Bin Nassor aliniwahi.

  • zinjibar.asli 16/06/2013 kwa 3:09 mu ·

   rasmi

   Maneno yako mazima ndugu rasmi… since Tanganyika wameambiwa wairudishe Tanganyika yao basi wanatafuta kila njia kutuondosha katika focus ambayo kwa sasa ipo very clear ”WAZANZIBARI TUNATAKA NCHI YETU”.

   Jamaa wamerithishwa kila kitu na baba yao wa taifa Nyerere LAANATULLAH yaani mpaka his way of thinking wamebatizwa nayo duh ama yule mzee alikua na sumu kali.

   I hate him to bits just like the way alovoichukia nchi yetu na watu wake kwani mshenzi yule ndo aloifikisha nchi yetu hapa ilipo leo kwa chuki zake lakini BIIDHNILLAH tutaikomboa Zanzibar yetu soon inshaAllah ameen,

   ZANZIBAR KWANZA

 17. kemit 15/06/2013 kwa 5:16 um ·

  AA
  @Rasmi- mimi sikubaliani na hii kauli ya kua Zanzibar ni mji mkuu wa visiwa hivi viwili ila nakubaliana na maelezo yako ya awal kua Zanzibar ni nchi iliyojumuisha unguja na Pemba na nyenginezo zinazotambulika kihistoria. Asili ya jina la ZANZIBAR @Rasmi anaifahamu vizuri na labda tumuombe atupe vitu kidogo.

  @Ghalib and @Bin Nassor
  Msichukulie vigezo vya google, narejea tena is not a reliable source of information. Leo hii ukioneshwa ramani ya Afrika ya karne zilizopita utakuta Afrika ilikua na nchi nne tu moja wapo ni ZANZIBAR.

 18. Bosco 15/06/2013 kwa 6:33 um ·

  Kwanza huyo mtu anaejiita bin nassor nafikiri si mpemba kama anavojidai sema anajifanya tu. Na kama ni mpemba kweli na anipe namba yake ya simu mm nitamfata huko kwao nikaonane naye.

  Mambo mengine naona rasmi ameshatoa darsa ya kutosha kwa anaetaka kuelewa ama kwa asietaka ni shauri yake mana waweza ukamchukua punda hadi mtoni lkn huwezi kumlazimisha kunywa maji.

 19. mzaliwa 15/06/2013 kwa 10:10 um ·

  Mie naona vituko baada ya kujadili upatikanaji wa nchi watu tunaanza mipasho wenyewe kwa wenyewe,UN mwanzo kwenye kiti cha Zanzibar ndio kaulizeni mtapaja jibu,hapajaekwa pemba wala unguja,
  Izo ramani munazoziona google ndio hao Watanganyika wamekuekeni,kwana ata raisi twaekewa sasa ndio maana tutapota Zanzibar yetu kwenye ramani itaekwa na majina na kila ushuzi maana tutaitangaza wenyewe tunayoijua,
  Wazanzibari tunajuana ndio maana ukisifari ukikutana na mzanzibari mwenzio utamuliza atokea unguja au pemba na ukiona kashikilia anatoka zanzibar ujue sio uyooooo.
  Tuache mipasho tuongee la maana.

 20. nuramo 15/06/2013 kwa 10:16 um ·

  Upuuzi mtupu imesemwa hapa Zanzibar ni Tanzania je ulishawahi kuona Tanzania imeandikwa kwenye hiyo ramani yako katika kisiwa cha Zanzibar au inaandikwa kwenye Tanganyika?jibu zuri la pili wewe mwenyewe unajuaje au hadi atoke Mzungu kukuambia ?
  Zanzibar limeletwa na washirazi wa iran kitafsiri ila jina halisi visiwa hivi katika karne ya 1 ni Menuthias na raphta Mazoea na uhalisi ni tofauti,hukusoma nursery wewe au hukuimba Mungu ametubarikia Unguja na Pemba yote sote tunashangiriia,au Unguja na pemba we mwakawetu ndio huu,twendeni pemba we tukachume karafuu

 21. Multiways 16/06/2013 kwa 5:31 mu ·

  nakualiana na wachangiaji wote,,lkn kwa tulipofika,,tuangaze hili tulilojitwika, hili la chini tuliwache uporo,baada ya kupata zanzibar yenye mamlaka kamili,,sasa kama waznz,,tutarud kwa hili lipatiwe ufumbuzi ambao co mkubwa saana,,just cmple issue,,unguja na pemba,,mana hata ktk ukweli haliwez kutumika znz kama unguja,,look,,wakuu wa wilaya na mikoa,,wanatajwa vp,,makamanda wa polisi pia??,,zanzibar huru ndio la mwanzo

 22. bin nassor 16/06/2013 kwa 2:36 um ·

  @ Ghalib
  @ Kemit
  @Nuramo
  @Bosco

  mimi sio kama napinga nnachokieleza hapa ni ukweli mtupu na tusiwasingizie wakoloni hakuna neno au kisiwa cha unguja kila pahala unguja inaitwa zanzibar,sasa kama mnabisha ukweli bisheni kwa hio isiwe kitu kimesemwa na C.U.F au C.C.M kwenye mikutano ya siasa kikasemwa cha wazanzibar wamesema isemwe C.UF au C.C.M ndo walosema coz kuna waznz wengine chadema,nccr,wengine hata vyama hawana ili kitu kisemwe cha wazanzibar ni kile kitu ambacho kimesemwa na viongozi wa nchi.

  hata wananchi wakisemwa itasemwa wananachi wa zanzibar wamesema…

  @ Bosco,kwa taarifa yako mm ni nzaliwa wa Pemba hospitali ya mkoani mwaka 1988,mama yangu mwenyeji wa wesha baba yangu kwao macho mane kwenye nyumba za gorofa,ila sa hivi waishi jondeni karibu na kwa maalim sheha km kweli unapajua,so usihukumu watu kwa mawazo yao…na mm naishi zanzibar na biashara zangu ni kusafiri nje na ndani ya nchi kama unataka namba yangu ya cm nipe yako kwanza ila mm si mpuuzi wa kufata mkumbo naangalia maslahi kama anavofanya maalim Seif.

 23. kifupi nyundo 19/06/2013 kwa 10:58 mu ·

  Kuna mambo mengi ambayo Salim Bimani nadhani ingekua vyema akayaongelea sio haya ya darajani….. Kwa nini asisungumze suala la viongozi wakuu watatu wote kurundikana Zanzibar? Kwa nini Maalim Seif makamo wa pili wa Rais yeye ofisi yake isiwe Pemba akarahisisha kuleta maendeleo kule? chanzo kikubwa cha mrundikano wa watu pale darajani ni vijana kutoka Pemba ambao wamekuja kutafuta maisha Zanzibar, kuna haja ya bomani kulieleza hili kwa lengo la kuzuia uhamiaji huu na kuifanya Pemba kuwa sehem nzuri ya kuishi na sio kukimbiwa na wenyeji wake. Ni lazma tuwe na darajani yetu kule Pemba ili kuchangamsha biashara na kuepusha sehemu moja kuwa ndio kila kitu… Salim Bimani kuwa mchambuzi wa mambo sio msemaji pekee

 24. Vizuke 20/06/2013 kwa 12:05 um ·

  Rasilimali za Pemba zimetumika kuijenga Unguja bila kufikiria mtazamo wa mbali wa hatma ya maendeleo ya Pemba. Kwa hivyo Wapemba wana haki zote za kuja Unguja kufaidi matunda ya rasilimali zao.
  Vyenginevyo badilisheni hali hii kwa kuhakikisha kuwa asilimia 95 ya rasimali za Pemba zinatumika kuijenga Pemba.

  Bimani hakukosea hata kidogo.

  Zanzibar kwanza.

 25. kifupi nyundo 21/06/2013 kwa 5:19 mu ·

  @Vizuke
  Huwezi kuwa na mtazamo finyu kiasi hicho cha kushangaza! Pemba ni lazima iwekezwe na isimamiwe, na maalim Seif ndio mtu sahihi wa kukaa huko kwani anakubalika sana na itakuwa wepesi kwake yeye kuwahamasisha watu kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Comments are now closed for this article.