SIRI YAFICHUKA:MEMBE& MWAKYEMBE,Wamuondoa H MASOUD

Written by  //  25/07/2012  //  Habari  //  Maoni 17

Asalamu alaikhum ndugu Wazanzibari wa ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu.Natumai kila mtu atakua amekasirishwa na matokeo yanayotendeka huko nyumbani hasa kuzama kwa Skagit. Lakini kuna wale waliopata afueni kwakuondoka madarakani kwa H.Masoud (Waziri Wa Usafiri). Wengi wetu tumeona hatua aliofanya HM ni hatua nzuri hasa kwavile yeye alikua Waziri na alikua na uwezo wakuondoa uoza wa ubadhirifu lakini hakufanya hivyo. Sio hivyo tu, ila wengi wetu tunaamini wabadhiru ndio waliobakia madarakani na H.Masoudi amekua muhanga wa SMZ vs Tanganyika.

Hii nikutokana na Msimamo wa H.Masoudi juu ya ufufuaji na uboreshaji wa Bandari na Airport katika Nchi yetu ulikua umeshaonekana ni tishio kwa Bandari ya Tanga-Tanganyika na Airport ya Mrimani.

Msimamo wa H.Masoudi juu ya kuifanya Zanzibar kua bandari huru na usajili wa Meli (wanazosema ni za ki Iran) kuliwakosesha usingizi Benard Membe, na Mwakyembe kule Tanganyika. Kwani walijua uombaji wao wa Misaada kutoka USA na Nchi za EU umo hatarini.Hivyo njama za kwanza za kumuondoa H.Masoud zilianza kupangwa wakati wa MV Spice Islander. Lakini hizi zilipangwa na Wahafidhuna-Seif Ali Iddi na Aboudi ili kutekeleza matakwa ya S.Tanganyika – Kwamba Bandari ya Zanzibar isitengenezwa kama wanavotaka CUF (Sobotarge).

Wito wa Ni liazima CCM watumie Sera zao katika uongozi wa SUK ulitoka kutoka Tanganyika/ Muungano na waliambiwa (wahafidhuna) wasiachie Sera za CUF ku- “SHINE THROUGH” kwani Wazanzibari waliokua na imani na CCM watapoteza Imani zao.

Hivo Sobortage ya kwanza yakumuondoa H.Masoudi ilishindikana na ikapangwa ya pili ambayo ndio iliomg┬┤oa Hamadi Masoudi.Wazanzibari tukumbuke kwamba Boti zote mbili zilizozama ziliondokea Dar (Tanganyika) na zilikua zimeshajaza.

Ikiwa tutangalia Katiba ya Tanganyika/Muungano inasema kwamba Usalama wa Nchi na Ulinzi ni katika Mambo ya Muungano. Hapa Usafiri Usalama wa Baharini na angani ni Mambo ya Muungano ambayo Wizara ya VIP2 na Ile ya Tanganyika walikua wanatakiwa Washirikiane kuhusu upakiaji na upakuaji wa mizigo. Au uondokaji na Uingiaji wa Boti. Lakini Spice Islander iliachiwa kupakia kule Tanganyika na ilipofika Unguja hakukua na Onyo wala taarifa kwamba meli iangaliwe kwani imeshapakia sana. Na matokeo hayo yalijirudia hivyo hivyo katika Boti ya “SKARGIT”.

Hivo sababu zakumgoa H:M zilipikwa kwakushirikiana na Viongozi wa CCM-Tanganyika na wale waliopo VIP2 pamoja na Wahafidhuna wengine wa ZMA na bandari akina (GAVU). Lakini hili alionywa H.Masoudi zamani na yeye aliwakumbatia Wahafidhuna nakusahau kwamba (Wahafidhuna) wakisaidiwa na S-Tanganyika wataweza kuivuruga Amani na Umoja wa wazanzibari.

Tukitaka kujikumbusha yaliopita natuangalie tunavokumbuka kabla ya H.Masoudi au (CUF) kuingia katika Uozo wa SMZ. Airport ilikua haijulikani wapi mtu anaingia na wapi mtu atatokea. Mparaganyiko na ubadhirifu wa Uwanja wa ndege, rushwa, jeuri ktk Airport vilikithiri. Licha yakwamba kuna Watalii na Ndege za kila aina zinazoshuka Zanzibar kila siku. Lakini pesa za Airport fees au Tax duty ilikua ikiishia Mikononi mwa Viongozi (Wahafidhuna) na watoto wa Mapinduzi.

Uwanja wa Pemba ulikua ni Shamba la Migomba na Mihogo na watu walifanya njia.Baada ya CUF kuingia ndani ya SUK na H.Masoudi kua Waziri wa mawasiliano wananchi waliofanya mashamba ktk Maeneo ya Uwanja wa Pemba walilipwa compasation nakupewa mwaka ili wamalize kuvuna vipando vyao. H.Masoudi waliweza kuweka Uzio wa Uwanja huo kwa Upanuzi na alianza mbio zake yeye na Waziri wa Fedha Mh. Omar Yusuf. Hili ni jambo jengine ambalo liliwakera sana CCM-Wahafidhuna (hata Abdul Hamid na Kificho) pamoja na Tanganyika. Kwanini uwanja wa Pemba ujengwe wakati ni kaji-Kata kadogo tu. Masuala haya yalikua midomoni mwa Watanganyika na Wahafidhuna walihakikisha hili halita tendeka.

Ndani ya SMZ kabla ya SUK au (CUF) – Zanzibar ilikua mwananchi wa Chini hathaminiwi, Mawizara ya SMZ yaliacha kuajiri Wazanzibari wenye hakki yakuijenga na kuitumikia Nchi yao. Na kujaza Watanganyika, Wakenya, Waburundi na hata Wakongo kama wakitaka kazi wangefanikiwa. Uoza wa wafanyakazi hewa wasiokua na sifa za kufanya kazi ulikithiri. SMZ iligeuka Kinyanganyiro cha Wanamapinduzi na Wahafidhuna kila Mmoja anataka yeye.Wakati wa Abedi Karume ulirudi kwamba Wasomi Wazanzibari walionekana Maadui wa Nchi na kuanza kutafuta kazi Tanganyika.Hii ndio Ajenda ya Kuimaliza Zanzibar waliokua nayo Serikali ya Tanganyika.Ilimradi ilikua paraganya ndani ya SMZ.

Tumeona wenyewe kwamba hata kama kuna makosa mengi ndani ya SUK lakini wananchi sasa wameshikana (Alhamdulillah) Na wengi wetu tunajivunia kua Wazanzibari. Hata kua H.Masodi amefanya Uzembe lakini tunajua Serikali ya Tanganyika ikisaidiwa na Wahafidhuna Wamemuondoa Hamadi Masoudi kwa msimamo wake juu yakusimamia Maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari.

Kupepea kwa bendera ya Tanganyika/Muungano ndani ya meli (wanasoma za Iran) kumeifanya Tanganyika kutafuta njama zakuwaondoa viongozi wa CUF katika madaraka na kuanzisha mizozo ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Zanzibar. Hivyo Siri hii ilisikilikana ikizungumzwa na mmoja wa CCM kindaki ndaki ambaye anatumiliwa na S-Tanganyika. Kusema wamefanikiwa na sasa wanataka kuhakikisha usajili wa Meli za Iran unafutwa.

Samahanini kwakuandika makala ndefu lakini niliposikia haya jana nilisema niwataarifu.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni yamefungwa.