Sauti:Zanzibar kufanyia mabadiliko katiba

Written by  //  02/10/2016  //  Podcasts  //  Maoni 3

wawakilishi

DW / Swahili

Serikali ya Zanzibar imefanyia mabadiliko katiba ili kutoa uwezo kwa Rais wa Zanzibar kuteua wajumbe wa Tume ya Uchaguzi bila kushauriana na kiongozi wa kambi ya upinzani ndani ya baraza la wawakilishi.

– Ripoti ya Salma Said

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "Sauti:Zanzibar kufanyia mabadiliko katiba"

 1. chatumpevu chatumpevu 03/10/2016 kwa 4:46 um ·

  Nafikiri mabadiliko ya katiba yaliyofanywa hayajaangalia maslahi mapana ya zanzibar. Yamejikita kisiasa zaidi kwa lengo la kuikomoa cuf. Ni hatari iloyoje kwa wajumbe wa baraza kuweka mbele uchama zaidi kuliko mustakabali wa nchi. Time will tell na si muda mrefu tutavuna tulichokipanda cuz usitarajie ulilima mpunga utavuna chooko

 2. salali 03/10/2016 kwa 6:16 um ·

  Hizo zote ni njama za kikabaila ili uchaguzi unaofuata jecha huyo huyo atakaye tunukiwa tunzo aendelee kuwa mwenyekiti wa ZEC bila ya upinzani huku wakijinasibu kwamba ni tume huru.(Endeleyeni kujihashuwae)Lakini mjuwe ya kwamba hakutaka na uchafuzi wowote utakao simamiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi ZEC ikiongozwa na mwenyekiti jecha . Hapo ni lazima tuziombe jumuiya za kimataifa waje kusimamiya na kutangaza mshindi halali.

 3. Mfalme 04/10/2016 kwa 4:14 mu ·

  NYIE ANDIKENI VITABU NCHI ILISHACHUKULIWA NA KANISA KATOLIKI ZAMANI

  Kardinali Pengo anasema Muungano umeletwa na Mungu kwa hivyo ni jukumu la kila Mkristo kuulinda.

  Yaani kwa wao mungu ni Yesu ,

  Suali Jee sisi tusio wakristo ambao hatuamini Yesu ni mungu si ndio uchochezi huo???

  Jumatatu, 2 Mei 2016

  Kardinali Pengo: Muungano si bahati nasibu

  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waamini na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si jambo la bahati nasibu.

  Kardinali Pengo ameyasema hayo ofisini kwake hivi karibuni alipoitisha vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kuzungumzia pamoja na mambo mengine ongezeko la Parokia mpya jimboni kwake pamoja na mabadiliko kwa Maparoko na Maparoko Wasaidizi katika baadhi ya Parokia jimboni humo.

  Asemema suala la Muungano linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee kwa kila Mtanzania hasa waamini Wakatoliki na kwamba kila mwamini anapaswa kutambua kuwa amepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kulinda na kuombea Muungano huo.

  Kardinali Pengo anasema ni jambo la kushangaza jinsi Mungu anavyotenda mambo yake kwa wanadamu kwani alileta Imani Katoliki kupitia Zanzibar na kwamba baada ya Uhuru Mungu aliwapatia neema watu wake wa pande mbili za Zanzibar na Tanganyika kuungana na kuwa kitu kimoja.

  Anasema wakati Kanisa likijiandaa kwa adhimisho la Jubilei ya miaka 150 ya uwepo wa Kanisa Katoliki katika eneo la Afrika Mashariki ifikapo 2018 Zanzibar haiwezi kuwekwa pembeni.

  Kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kardinali Pengo anasema hali inaonesha viongozi wa taifa hili wameanza vizuri na kasi yao inaleta matumaini makubwa.

  Kardinali Pengo anawaomba wananchi wa Imani zote kumuombea Rais Dakta John Pombe Magufuli kwa Mwenyezi Mungu ili alinde uongozi wake na auimarishe uweze kubaki katika malengo yake ya kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

  Anaongeza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuomba kwa Mungu ili ibilisi asije akawabadilisha mioyo wale ambao wanaonekana ni watetezi wa wanyonge wakaanza kutenda kinyume na matarajio ya wananchi walio wengi.

  “Ibilisi ana namna yake ya kufanya vitu mnaweza kushutukia tu mambo yamebadilika wale ambao mnatarajia wawe watetezi wa Watanzania wa chini wanageuka kuwa ndiyo wakandamizaji wakubwa kwa Watanzania wanyonge.” Amesema Kardinali Pengo

Comments are now closed for this article.