Sauti:Mji Mkogwe hatarini kuwekwa kwenye “heritage in danger list”

Written by  //  09/03/2016  //  Podcasts  //  Maoni 3

Salma Said anaripoti zaidi:

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 3 katika "Sauti:Mji Mkogwe hatarini kuwekwa kwenye “heritage in danger list”"

 1. abuu7 10/03/2016 kwa 5:02 mu ·

  Viongozi wa juu asikiye jumba limeanguka. Ndio itaanza visit
  Ngome ya cuf hiyo. Serekali haina habari nayo. Na hata ikifanyiwa ukarabati basi utasikiya kina barakshamte. Unataka kuleta warabu.
  Wacha huu mji mkongwe. Kama mnavosema. Hii serekali wenyewe inataka kuifuta kabisa zanzibar kwenye ramani ya duniya. Tusubirini ipigwe kufuli maana zimebakiya siku chache akabiziwa pombe.

 2. Jino kwa Jino 10/03/2016 kwa 5:46 mu ·

  Wallahi inasikitisha sana kuona mambo haya ya kijahil yanatokea kwetu .Nimeona clip moja ya Qasri ya Sha wa Iran 80% iko vile vile mpaka nguo zake pamoja na picha zake anaetaka nitamfowardia .@Abuu kama unavyosema tuna Wajinga na Majahil kina Baraka shamte na wengineo .Jamani hii ndio Tharwa yetu sote Wazanzibari hususan kwa wakati huu kutokana na Halab ya Syria washaivunja mji mkonkwe wao walikuwa na soko la zamani zaidi ya miaka 14000 elfu lkn washalivunja Daash .Sasa wapuuzi kama kina baraka shamte hawajui thamani ya huo mji mkongwee.Serikali ingeeka mkakati maalum wa kuufanyia matengenezo mji mkongwee.

 3. sadimba 10/03/2016 kwa 12:53 um ·

  Kwaheri Mji mkongwe karibu mji mbovu

  Katika zaznzibar kitu pekee ambacho kimebakia kama ni utambulisho wa zanzibar ni mji mkongwe, mji huu ambao unatoa kielelezo cha utamaduni na historia mbali mbali ya mambo ambayo yanaitambulisha zanzibar katika medani ya kitaifa na kimataifa. Mji huu wa asili ambao shirika la sayansi na utamaduni la Umoja wa mataifa liiutambua na kuingiza katika orodha ya miji ya kihistoria duniani mwaka 2000. Hii inafuatia juhudi kubwa zilizochukuliwa na wataalam mbali mbali, mwaka 1992 ulifanyiwa master plan na mwaka 1994 sheria ya uhifadhi ilipishwa rasmi kwa ajili ya kuulinda na kuuhifadhi mji mkongwa.
  Lakini pamoja na juhudi zote hizo umekuwa ukidorora badala ya kunawiri kwa mambo ambayo nitayataja kwa kifupi tu:

  1) Ukosefu wa uungwaji mkono na wanasiasa “political will”.
  Jambo lolote ili liweze kuendelea linahitaji uungwaji mkono sio tu na wananchi bali pia wanasiasa. Chanzoo kikubwa cha kuzorota kwa mji mkongwe ni wanasiasa kujali maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya taifa, mfano sheria ya ufifadhi wa mji mkongwa inakataza ujenzi mpya wa mahotel ili yale mazingira ya asili yasipotee lakini wapi watendaji kwa maslahi yao binafsi wamezipinda na kuzibena sheria ili yao yawe.
  2) Mji mkongwe sio majengo tu yanayohitaji kuhifadhiwa, maeneo ya wazi pia yanahitaji kuhifadhiwa, ni maeneo mangapi ya wazi yamemezwa na wakubwa, nyuma ya soko la darajani kulikuwa na eneo la wazi muheshimiwa mmoja ambae alikuwambunge wa mkwajuni kalichuwa. Mbele ya duka la vioo darajani kuna bureau de change imejengwa eneo la wazi tena juu ya mtaro wa maji machafu mwenyewe ni muheshiwa mmoja ambae ni muwakilishi. Tuje malindi uwanja wa mpira kuna jengo la ghorofa limejengwa kwenye eneo la wazi na jengo hili ni mtu ambae alikuwa waziri badala ya kufanya juhudi ya kulihda sheria yeye ndio alikuwa mbele kuzivunja.
  3) Mji huu uko chini ya mamlaka ya hifadhi na Uendelezaji mji mkongwe, serikali na uwongozi wa muanzilishi wa kitengo hichi ulisomesha na kuwa na wataalamu wengi tu lakini wamefukuzwa au kuhamishwa kwa ajili ya uongozi uliopo kulinda wadhifa na maslahi yao, leo waliobakishwa asilimia kubwa ni watoto waliomaliza darasa la kumi ndio wanafanya kazi hizo. Tutegemee nini.

  Kwahiyo haitoshangaza mji mkongwa kuwekwa kwenye orodha ya miji iliyomo katika hatari ya kutoweka na hata kutolewa kwa vlie hatujui thamani yake, kama kweli tunataka kuuhifadhi tuchukuwe juhudi za makusudi za kuuhifadhi kuulinda na kuendeleza mji huu wa kihistoria na kuhakikisha sheria ya uhifadhi inaheshimiwa badala ya kuchezewa kama ilivyo sasahivi vyenginevyo ni sawa na kufuga ng’ombe dume tukategemea maziwa.

Comments are now closed for this article.