SABABU KUU KUMI AMBAZO ZINAASHIRIA MAALIM SEIF KUTOKUTANGAZWA KUA RAIS

Written by  //  23/02/2017  //  Habari  //  Maoni 16

Na Tanzaup

SABABU KUU KUMI AMBAZO ZINAASHIRIA MAALIM SEIF KUTOKUTANGAZWA KUA RAIS WA ZANZIBAR KAMA ANAVYODANGANYA

Ktk jambo muhimu zaidi kwa sasa kwa upande wa CUF kuhusu kudhulumiwa kuiyongoza Zanzibar silaha kubwa nikusema ukweli na sio uwongo usio tija zaidi ya kuwaaminisha wananchi tuliopoteza muda wetu kuwachagua kuliongoza taifa la Zanzibar kwa sasa wazanzibari wanahitaji kuenziwa kwa vitendo na ukweli sio uwongo na propaganda uchwara…

Zufuatazo ni sababu kwa nn maalim SEIF hatatangazwa kua Rais wa Zanzibar kama anavyowaamisha wazanzibari walio na kiu ya mabadiliko

1. Kauli za maalim SEIF alizokua akizitoa wakati akiendelea na vikao na viongozi wakuu wa CCM pamoja na Marais wastaafu mara tu baada ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu

Sote tunakumbuka maalim SEIF aliwaaminisha wazanzibari kua wanaendelea na mazungumzo mazuri na Dr.Shein na marais wastaafu na wamefikia hatua mzuri na atatangazwa kua Rais kwa hio vijana msiwe na hofu mwisho wa siku maalim alienda Serena tena alifanya Tanganyika sio Zanzibar na kufanya mkutano na waandishi na kuonyesha kua kipindi chote cha mazungumzo hayo hawakuwahi kufikia makubaliano ya aina yoyote yale kuhusu maalim SEIF kutangazwa kua Rais Zanzibar bali maalim alikua akitoa propaganda ili kuaminiwa zaid na wazanzibari ktk mazungumzo yale

2. Mazungumzo ya maaalim SEIF na Pombe ikulu

Sote tunakumbuka kua kiongozi wa kwanza wa upinzani kuonana na Magufuli ikulu alikua ni maalim SEIF ukiacha yule profesa uchwara, maalim aliongea na Magufuli na mama Samia na wakapiga picha pale ikulu akiwa na sura ya tabasamu maalim alisema kwa kujiamini kua ameongea na Magufuli mambo ni mazuri na ameambiwa arudi Zanzibar akafanye kazi na maalim SEIF akasisitiza kwa kuimba kauli mbiu ya Pombe hapa KAZI TU, hapa pia aliwaaminisha wananchi na kuanza kumuamini Pombe na mpaka viongozi wakuu wachadema wakathubutu kutoka hadharani na kusema kua Pombe anatumia ilani ya UKAWA

3. Safari za maalim seif nchini CANADA, USA na UK

Sote tunakumbuka kua maalim akifuatana na Jussa walitembelea matifa hayo baada ya uchaguzi haraumu wa march,20.2016 kumtangaza na baadae kuapishwa kwa Dr. Shein ndipo safari hii iliyokua na malengo ya kufungua kesi ICC na kushtaki UN ikaandaliwa, nikweli maalim alienda UN na akutana na taasisi nyingi za haki za binadamu na kidemokrasia ila haikua kwa Zanzibar kupata haki yake ikiyoporwa october . 25.2015. Laiti kama mpango huu ungekua madhubuti ulipaswa kuratibiwa mapema Mara baada ya kufeli kwa mazungumzo na CCM na kabla ya uchaguzi wa marejeo ambapo CUF ingalipata hoja kuu ya kuiyomba jumuiya ya kimataifa kuitaka Zanzibar isiitishe uchaguzi huo maana uchaguzi halali ulishafanyika na mshindi kupatikana, kitendo hiki cha kusubiri mpaka ZEC kuitisha uchaguzi mwengine mpaka Shein kula kiapo ni wazi kua CUF wanafanya propaganda za kisiasa na hakuna ukweli kua jumuiya za kimataifa kua zitasimamia hili

4. Maneno ya maalim SEIF yaliyokosa weledi na mpangilio madhubuti

Ni jambo la ajabu kwa mtu makini na gwiji wa siasa kama maalim SEIF ambaye amekua akikaaa majukwaani na kuongea lugha nyepesi zisizokua na maono kama vile amekua akisikika mara kwa mara kua CCM wamezika Ng’ombe mzima, Mara wamemwaga damu za wato wachanga kama hoja za kuwaeleza wananchi ambao wanahitaji haki yao waliyoporwa kurudi mezani, maneno haya yanaonyesha kua hakuna taarifa makini iliyokamilika ktk suala zima la upatikanaji kwa haki ya Zanzibar na badala yake zimebakia porojo zilizokosa weledi wa kuziwasilisha na kuzisema, kwa mantiki hii huwezi kuona na kusema kwa kioja hiki maalim atatangazwa kua Rais wa Zanzibar

5. Maalim SEIF kukosa confidence (kujiamini ) anaposemea kutangazwa kua Rais wa Zanzibar

Hii sababu nyengine inanyoonyesha kupitia maalim SEIF mwenyewe kutotangazwa kua Rais, tumeona ktk mahojianao ya maalim SEIF na SALIM Kikeke pale BBC na mahojiano ya maalim SEIF na Tido pale AZAM TV wenye kujua kusoma picha na muonekano wa mtu inaonyesha wazi kua maalim hakuonyesha wigo madhubuti unaoshiria ujio wa jambo jipya kutokea bali amekua akilalamika pekee, na kuonyeshwa kua bado wanapinga serikali batili ya shein ila ktk mahojiano yake hakuwahi hata mara moja kuelezea kwa hisia ambazo zinaweza kumshawishi MTU mdadisi kuona kuna jambo jipya

6. Maalim SEIF kunukuu maneno ya Balozi seifu ALI Idii ( Faru John)

Ktk hali yengine ya kutokuamini maneno ya maalim SEIF kua atatangazwa kua rais wa Zanzibar ni ktk hutuba zake akimnukuu SEIF ALI IDDI kua amesema nchi ipo ktk hali mbaya ni lazima tumpe maalim, huku naweza kukuita kuchanganyikiwa kisiasa wanaweza kutoka CCM wote wakasema maneno hayo ila sio Babuali (Faru John) hapa ndio utagundua hizi ni propaganda uchwara ama idea zilizokufa na mwenye maono hawezi kuchukua kioja hiki kua sababu kuu ya maaalim kutangazwa kua Rais wa Zanzibar

7. Naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar ndugu MAZURUI kuandaa mkakati wa kutaka uwepo wa Tume huru ya uchaguzi

Kama ni kweli maalim SEIF atatangazwa kua Rais basi CUF wasingehangaika na mpango huu maana Rais ndio mwenye mamlaka kikatiba kuunda tume ya uchaguzi hivyo basi kwa sasa CUF wangalikua wanajipanga kuandaa mfumo na muundo wa serikali yao hivyo basi kupitia CUF wenyewe unaweza kuthibitisha kua maalim SEIF hatatangazwa kua Rais wa Zanzibar

8. Wajumbe wawili wa CUF wanaounda tume ya uchaguzi Zanzibar kubakia ktk tume hio ya JECHA mpaka leo

Niwazi kua hakuna dalili yoyote ya kutangazwa SEIF kama Rais wa zanzibar maana wajumbe hawa wengejiuzulu hadharani ili kuongeza wigo na uwaminifu kwa wazanzibari ili kuamini na kujipanga kua tayari Rais kipenzi wa Zanzibar atatangazwa

9. Mabadiliko ya uwendeshwaji wa serikali ya Muungano ungeonekana kua kuna mabadiliko ya kimfumo

Bado serikali ya Pombe inaendeshwa kwa mizuka na mihemko laiti kama taarifa za kutangazwa maalim SEIF kua Rais wa Zanzibar nizaukweli basi nilazima kungeonekana mabadiliko ktk uwendeshaji wa serikali kuu ambayo inatambulika kimataifa na wanaamini kua Pombe kashinda kihalali japo kua mm siamini hivyo. Ninavyomjua Ngosha alivyomaridadi kwa kuropokwa angalikua asharopokwa kitambo

10. CUF kuhangaika na mgogoro wa profesa uchwara

Laiti kama maalim SEIF atatangazwa kua Rais wa Zanzibar kama anavyodai basi CUF wasingehangaika na Lipumbavu maana wanajua soon watakua CHAMA dola na wataweka mfumo wa kidemokrasia ambao utambwaga Profesa Lipumbavu

NB…

TUKIWA WAKWELI WAZANZIBARI WATATUAMINI NA KUTUCHAGUA TENA 2020, CCM HAWANA UWEZO WA KUWABADILI WAZANZIBARI WAWAPIGIE KURA, ILA TUKIENDELEZA PROPAGANDA TUSUBIRIE KUSIKILIZIA HARAFU YA DAMU…..KAMA NINAYOISIKIA MM

Fb

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 16 katika "SABABU KUU KUMI AMBAZO ZINAASHIRIA MAALIM SEIF KUTOKUTANGAZWA KUA RAIS"

 1. Jino kwa Jino 23/02/2017 kwa 7:56 mu ·

  Ndugu Muandishi ww ulikuwa wapi siku zote kama ni kisu basi umempa mtu kisu na ala yake na kama ni mtungi basi na katayee. Naam Maneno ni Msumari wa bati usiohitaji kuchunguzwa kwa wale wenye akili watajua kama huo ndio ukweli wa mambo ama wale bunge ya ngoma basi wataendelea kupiga vigelele na madufu ya kumpokea Rasi hewa anaedanganywa na akawadanganya wenzake nakushukuru muandishi kwa kuona mbali kwa kuwa na vision huu ndio ucgunguzi wa kisayansi sio wa kuburuzwa tu anamwambia mtu kitu kama vile alaphabetic abcde & so on au unamtajia mtu number 12345 & so on Hii ndio formula zake huwezi kubadilisha. Kwa kweli nimefarijika na makala haya .Najua kuna watu wanatuona ss wabaya sana kwa kumkosoa maalim lkn maskini roho zao bado wamelala usingizi fofoo hawajui kama ulimwengu huu ni wa DOT COM.
  HATUIPATI NCHI YETU MPAKA SISI WENYEWE TUBADILIKEEEEEEEEEEEE. Hii ya kusubiri fulani atangazwee ni UPUUUZI MTUPUUUUU.

 2. salali 23/02/2017 kwa 9:26 mu ·

  Hata mtume wetu Muhammad (SAW)walikuwepo (banizrail) watoto wa guruwe walikuwa wakimpinga.

 3. Zdaima 23/02/2017 kwa 10:22 mu ·

  Nami nitakujibu kama ifuatavyo.

  Kwanza tuseme kwa ujumla wetu hali inayoendelea Zanzibar inatuumiza wote. Pili nije kwenye hoja zako 10 ingawa nimesikitishwa na lugha ya kusema “anadanganya”

  MAJIBU.
  1. Vikao na viongozi wastaafu.

  Mwandishi umemlisha maneno maalim seif , hakuwahi kusema kuwa atatangazwa baada ya vikao vilivyoendelea, alichokuwa akisema ni subira na ahadi ya kupigania hurejeshwa haki yao. Hadi hii leo mapam,bano ya kupigania kurejeshwa haki anayaendeleza na ndio maana umesifia alifika USA, UN , UK na canada katika kufuatilia haki. Ni uongo kumzushia maalim kuwa alisema atatatangazwa kupitia vikao vile.

  2. Mazungumzo ya Maalim na Pombe ikulu.

  Hapa hakuna hoja. Umetaja maalim kuonana na kuzungumza na pome ikulu. Kwa wanaofuatilia mambo tunajuwa maalim alisema alikwenda ikulu na kuonana na rais magufuli juu ya kadhia ya Zanzibar na kusema aliahidi atalishughulikia suala la Zanzibar. Maalim hakusema kuwa atatangazwa kupitia kikao na POMBE. sasa ikiwa rais Magufuli hakutekeleza alichoahidi (kulishughulikia tatizo) hilo asibebeshwe maalim kuwa kadanganya. Kwani nani hajuwi kuwa hata rais magufuli alionesha nia pale mwanzo lakini baadae akabadilika.?

  3. Safari za Maalim Seif , UK, US, UN na Canada.

  Umejenga hoja kuwa jitihada zilifanyika kwa kuwa Shein alishaapishwa na uchaguzi wa marejeo ulishafanywa kwa hivyo kinachoendelea ni propaganda.

  Unaweza ukaamini hivyo kwa kukata tamaa. Kudai haki ni kitu chengine haijalishi umejiimarisha kiasi ngani katika dhulma. Ni mara ngapi watu hurejeshewa haki baada ya kuporwa hata kama miaka imepita .Hii hoja ni ya kitoto. Cha msingi ilikuwa ni kutaka kujuwa nini kimefikiwa na nini kinaendelea katika kudai haki. Kinachoendelea hukijuwi na hutakijuwana ndio maana unakuja na hoja mfu.

  4. Maneno ya Maalim Seif yaliyokosa weledi na mpangilio.
  Hakuna hoja hapa . Eti maalim kutaja kuwa CCM wanazika ngombe na mbuzi. Mwandishi inaonesha hujuwi siasa ni nini. Hii si hoja ya Maalim ya kuwa eti kufanya hivyo ndio CCM watamtangaza . Hujui delaying tecnics za kusubiri jambo lililofichwa kuja juu baada ya muda kufika. Huo ndio mkakati (nyamaza wewe) muda ulisubiriwa na sasa umefika subiri nini kitatokea.

  5. Maalim seif kukosa Confidence anaposemea kutangazwa kuwa rais wa Zanzibar.

  Masikini. Hii Hoja nayo? Hao waandishi wanafanya kazi zao kiweledi kuchokoza yaliyojificha. Nikwambie tu kama unafuatilia siasa hizi kwa m,ara ya mwisho tilimsikia Baloizi wa AU kusema kuwa wanafanya mazungumzo na JPM na wao wanataka serikali ya Kitaifa zanzibar, na walisema ni imani yao muda mfupi ujao litapatiwa ufumbuzi, Upande wa CCM kuna ukimya hasa kwa JPM aliyewahi kusema kusiletwe fyoko fyoko, na kwa hapa Zanzibar tulisikia pale mwanzo Akijinadi Dr Shein kuwa yeye ndio rais na kwa Upande wa CUF maalim alisisitiza subira na kuahidi haki ya wazanzibari kupiganiwa na kurejeshwa.Kwa ufupi Maalim hawezi kuvujisha kilichokuwa kinaendelea kwa wakati huo ili kulinda (ethics). Wewe ulitaka aropoke na muda haujafika ? Tulia.

  6. Maalim Seif kunukuu maneno ya baloziSeif Ali Iddi

  Hii sio hoja . Ni udhaifu wa mwandishi kuifanya hoja ya Maalim seif. Kwanza atuthibitishie ni wapiu Maalim Seif alinukuu hayo maneno eti Balozi akisema kuwa kwa hali ilivyo lazima nchi tumpe maalim Seif ni wapi na lini ? Hizo ni drip za watu wa mtaani.

  7. Naibu Katibu Mkuu kuandaa mkakati wa kuwepo Tume Huru ya Uchaguzi.
  Kwanza twambie kuna ukweli wowote wa Naibu kuandaa mkakati huu? na kama upo hakuondowi uhalali au jitihada za kutangazwa Maalim ikiwa tu hio hatua ya kutangazwa inaendelea. Una uhakika gani kuwa inawezekana Naibu hakuagizwa kufanya hivyo na katibu wake kwa lengo mahsusi? kwa nini ulijengee hoja kuwa itakuwa hakuna kitu chochote cha Kutangazwa ? huwezi kujuwa nini kinaendelea. Kwa ufupi ni hoja nyepesi.

  8. Wajumbe wawili wa CUf kubaki katika Tume ya JECHA.

  Hii si hoja, Ulitaka watoke ili iweje. Kumbuka kuwepo kwa wale wajumbe wapo kiusheria. Usisahau kuwepo pale CUF ina maslahi yake kuliko wangeondoka.

  Kutoondoka hakupunguzi uaminifu wowote wa Maalim kutangazwa ilimradi tu kuwe na hatua kabambe za kuhakikisha Maalim anatangazwa ambazo wewe mwandishi huzijuwi.

  9. Mabadiliko ya uendeshaji wa serikali ya muungano hayaonekani.

  Umejenga hoja kuwa hakuna dalili za mabadiliko ya uendeshaji yanayoashiria mabadiliko ya mfumo wa uongozi Zanzibar.

  Angalau hapa kuna hoja. niseme chakula hakijapikwa utakila vipi? Kama kuna mabadiliko yopyote kuna taratibu zake. Lazima kwanza negociation ifikiwe una uhakika nini kinaendelea kweli ? Hii hoja itajibiwa na wakati tu. Nadhani mwandishi ungeendelea kuvuta ile Subira anayosema Maalim Seif na wala hapa bado hoja hii si pahala pake. (tulia).

  10. CUF kuhangaika na mgogoro wa Profesa Uchwara.

  Nani anayehangaika CCM au CUF? nijuavyo mimi CUF inalinda hujuma za kupangwa na sio kuhangaika. Waliomtuma Profesa wamefeli hawajuwi tena pa kutokea, walijuwa pa kuanzia tu. Ilikusudiwa CUF iwe haipo sasa na iwe imeparaganyika ili kulipotewza suala la madai ya Zanzibar wewe hujuwi ?. Kesi iko mahakamani jaji kihiyo nkagoma kujitoa licha ya mdai kutokuwa na imani naye. Hili ni suala la kisheria liko mahakamani linafuata mkondo wa kisheria kwa sababu shauri lilishafunguliwa. Halihusiani na kupigania haki ya Wazanzibari na wala halipunguzi madai yaliyopo na hatua iliyokwisha kufikiwa.

  MAELEZO YANGU.

  Mwandishi inaonesha ama umekata tamaa au unachokoza kutaka kujuwa kilichopo. Tutamsuta maalim ikiwa itafika 2020 bila ya kutokea chochote. Aliomba Wazanzibar wasubirie, makaribuni alisema muda mfupi ujao atatangazwa kuwa rais wa Zanzibar, sasa anamshauri Dr Shein kulinda heshima aliyopewa kabla dunia haijafanya maamuzi na kusema ikiwa hawatachukuwa hatua dunia itachukuwa hizi ndozo habari mpya za sasa za MAALIM SEIF.

  Kwa nini kasema hayo ? tusubiri muda ili tuje tumsute vizuri Maalim Seif.

  Stay tuned, Maalim anaendelea na ziara Pemba, atamaliza tusubiri nini kitatokea hapo baadae halafu ndio tuje tumsute.

  Nawasilisha.

  kishada.

  CC

  Jino kwa jino

 4. sadimba 23/02/2017 kwa 12:31 um ·

  Napenda na mimi kutoa mawazo yangu kidogo kwa vile kila mtu ana ufahamu wake na ndio mano hata Allah akasema wenye akili na wenye kufikiri maana hata mnyama anazo akili ila upeo wake wa kufikiri ni tofauti na binadamu, ndio mana havai nguo na wanaweza kuwaparamia hata mama zao ndio upeo wao.

  Mara nyingo hupenda kuongea bila ya kumlenga mtu ila naomba nisamehewe ikitokea kukanyaga paka mkia, inawezekana maalim kachanganyikiwa maana yeye ni biandamu kama binadamu wengine ila kuna uwezekano wengine wamechanganyikiwa zaidi, na ikifikia stage hii inabidi atizamwe yule aliezidiwa apate angalau huduma ya kwanza.

  Katika uzeofu wangu watu wengi ambao kwa sababu zao binafsi au kutokana na maradhi ya chuki, walioambukizwa kupata uhao kwao lazima wamtukane mtu maalum. Ikiwa kwa kujifurahisha nafsi au kujikomba komba kwa watawala, kama mtu ana shughuli za kufanya kwanini ashughulike na mtu aliyechanganyikiwa wakati yeye yuko kwenye upunguani wake, wewe ni busara ukaaendelea na maisha yako. Hii inanikumbusha yule mtu aliyelala barazani kwake na akalawitiwa na kijana mmoja kwa fadhaa ya kusukumwa mnara wa njugu akamnadia mwizi na watu wakamfukuza na wakamkamata yule kijana alipoulizwa yule mzee kakuibia nini hawezi kusema akabakia huyu mpumbavu sana, Naomba kama kuna kitu kinachomnyima usingizi aseme tujue asinadi.

  Kwanza naona serikali zote mbili kazi kubwa za maendeleo ni kuwaashughulikia wapinzani, japo mtu anaweza kuja na hoja mkorogo ati mgogoro ndani ya vyama ambao kwa mwenye akili timamu wanajua kama yote yanaratibiwa na siseme, panya panya hawezi kumuamini panya hata awe na utasbihi wa madagaa shingoni. Lipumba na kupewa ulinzi na polisi hapa ipo namna lakini wanaodhulumu wanampiga vita mdhulumiwa. Dhalimu hutumia wapiga debe na chapuo kuungwa mkono afanikiwe na tabia yake ya kunyonya mali za na haki watu na kuwatumia wapiga debe ila tu ningeomba wakatofautisha baina ya mzungu na zeruzeru.

  Kila binadamu anayohaki kufikiri na kusema anachokitaka lakini asiwalazimishe watu kufiki kama yeye maana huyo bwana aliyechanganyikiwa hajampelekea gari mtu ili akamsikilize ila watu huenda kwa ridhaa yao wenyewe ila kama watu wengi wana muunga mkono basi na kuacha wale wanaowapeleleka magari na kuwapa posho ili ele wende mikutanoni kwao basi ni maamuzi ya mtu binafsi. Mimi naweza kuamini maalimu kachanganyikiwa na jinsi nchi yake ilvyofikishwa.

  Mzulumati na mzulumaji nani kachanganyikiwa zaidi ni chaguo lako.

  Napita.

 5. sadimba 23/02/2017 kwa 12:35 um ·

  sahihisho
  panya hamuamini paka hata avae utasbihi wa madagaa shingoni

 6. Papax 23/02/2017 kwa 1:45 um ·

  sasammeanza kuufahamu mchezo wa kitoto aliokuwa anatuchezesha maalim, kiukweli mungu atamuumbua kwa uongo na hadaa zake za kiole

 7. Abdul Zakinthos 23/02/2017 kwa 2:34 um ·

  Akah! mwandishi unaponda au unawaonesha watu ukweli

  Na wewe PAPAX imekuaje si ulikuwa msemaji mkubwa sasa leo unasema ulikuwa hufahamu kwa maana ulikuwa unaropokwa tu

 8. zamko 23/02/2017 kwa 2:49 um ·

  Asalamu alaikhum Nduguzangu Wazanzibari muliochangia makala hii. Ama na mimi Makala Imenichoma Ndipo kiac ya kwamba nita tawakkal, nitoe maoni yangu jinsi ninavofikiria suala zima la Maalim na Muandishi. katika hoja zango nitakuwa nafanya analysis ya muandishi na kuchangia maoni yangu humo humo ili niepukane kuandika makala nyengine ndani ya makala.

  Kwanza naanza na Muandishi anaejiita @ TANZAUP, mimi kwa uoni wangu nahisi kwanza muandishi amemvunjia Maalim SEIF heshima yake sana hasa pale anapokua baadhi ya maelezo yake muandishi amezidisha chumvi na hakutamka haswa yale maalim SEIF anayo yatamka au aliyo yatamka. Kama Yeye nimuandishi hasa na anataka kumnukuu maalim SEIF kwa kila mkutano anao usema basi angefanya kunukuu neno kwa neno na sio kuzidisha na kupunguza maneno ya maalim. Au ku generalise kama watu wengine wanavotumia neno hilo.

  Hata hivo sikuja hapa kumuhukumu muandishi, hukumu au kama ni muandishi kujisuta mwenyewe au Wazanzibari kuja kumsuta maalim SEIF. Jambo hilo naamini litakuja baadae pale maneno ya Maalim yatakapokuwa sio kweli. Lakini kwa mtu mwenye maarifa na anaezijuwa Siasa za Ki-Africa au Tanzania bac hatakuwa na mdomo wakumsuta Maalim kwani tayari sote tunajuwa ameshafanya kazi yake yakupigania haki yake kama Raisi halali wa Visiwa vya Zanzibar; lakini hakufanikiwa, kuipata haki hiyo kwakutumia njia ya Amani ambayo mimi na ndugu yangu @ JINO KWA JINO tunaona nikupoteza muda – Japokuwa hiyo Njia ya Mkato ambayo sio ya Amani tutakuwa tunaiogopa kuitumia.

  2.Nahisi Muandishi amepatwa na fadhaa ya (Ama) kuamini (AU) kutomini yale yote yaendeleayo hivi sasa katika Mitandao ya kijamii na mikutano au vikao vya maalim Seif alivovifanya na wana habari mbali mbali. Hivo muandishi ameamuwa aje na makala yake hapa ili apate ufafanuzi zaidi wa haya yanayo endelea kuenea katika Mitandao au Maneno alioyatamka maalim katika mahojiano yake na waandishi wa habari, mikutano yake aliofanya Unguja na Pemba n.k.

  Kwakumsaidia tuu Muandishi mimi naamini Maalim SEIF hawezi kutamka kitu ambacho hakipo, hata kuwa Wana siasa wote Wana Propagander zao- Au maalim anawadanganya Wazanzibari. Lakini naamini Maalim Sefu hawezi kuwadanganya Wazanzibari akawaambia Uongo, ila kuna kitu kinakuja. Lakini kama nilivosema serikali zetu za Kiafrica ni Dhalimu na Wauwaji, inawezekana maalim Akaapishwa. Na humo Ndani yake CCM wakaanza SUBORTAGE ya Serikali halali ya Maalim na Wananchi Wanyonge Wasioweza hata Kunyanyua Mkono wao Kujitetea.

  Nikija kwa hizi Fadhaa za muandishi, hata mimi nimezipata lakini zangu haziji kwakumuita Maalim Muongo. Zinakuja kwakuamini kwamba Viongozi wa CCM ni kama WanyamaPori na wanaweza kufanya lolote lakumdhuru maalim au kuidhuru Nchi yetu tuipendayo. Kwa mfano hivi sasa kuna picha nyingi zina rushwa katika Whats Up kwamba Mh Amani Karume kaja na International Organisation analindwa. Mara Sheni Ameitisha BLW jumapili. Mara UN na EEU wamekuja na wako Kwa POMBE na picha tunarushiwa.

  Lakini mimi haya yote naona kama ni njama za CCm kutaka kutupumbaza ili Wampitishe yule Lipumbavu Wao aje atuharibie Visiwa Vyetu. Kwahivo naweza kumuweka Muandishi katika jamvi la hili langu kwa nilio yasikia na naona Muandishi baada yakujiuliza kama mimi “KULIKONI”??? Ametumia njia ya Falsafa na kuingia zaidi kwenye Negative Generalisation ili apate jibu la msingi.

  @ Zdaima
  ahsante sana kwa ufafanuzi wako mzuri sana na wenye undani.
  Kwakukusaidia Tuu nikwamba maalim aliwahi kusema Katika mikutano yake ile ya Awali ile kabla ya Uchaguzi wao haramu wa Mazombi na kabla Kuingia katika meza ya Mazungumzo. Maalim aliwahi kufanya Mkutano Mazizini au Kimbesamaki. Na akasema Watanitangazaa, Nyie Ngojeni Watanitangaza kwasababu mimi ndie Nilieshinda na Ushahidi Upo na data zipo. Kuna siku mm na mdogo wangu tukasema mbona huyu maalim Anasema Maneno haya kama vile CCM hawajuwi vilee tabia zao?… Tukamuona kama yuko Naiv.

  Lakini Ukweli nikwamba CCM walikaa kikao cha Siri na Waaandishi wa TBC Video ilikuweko na Katibu Mkuu wa CCM akaungama mwenyewe kama Wanamtambua Maalim na Watawaambia CCm washerehekee Ushindi. Hivo hata siku zile maalim Hakuwa Naive, bali alikuwa ana uhakika wa aliokuwa akiyasema. Kumbe SEIF Iddi hapa ndie alieingilia Kati na aliitwa Tanganyika na Akaambiwa Serikali wamepewa na Wasiitowe na wao Watalindwa sasa lilobakia Wamuache Maalim aropokwe tuu kisha atanyamaza kwani ndio kawaida ya MA-CUF. CCM Wakageuka U.TURN. Na Wengi wa Wazanzibari Wasiokuwa na Subira au Waliochoka Kusubiri kama mie Huja na hoja zakumuangusha maalim.

  Jamani Wazanzibari tujiulizeni saa nyengine , Hawa CCM hufanya mambo yao ya Siri kwakuitana Wao kwa Wao wanao aminiana kwamba ni Damu Damu. Lakini Siri zao zote huwa nje the same day they have make it. Kwasababu Walipo CCM 10 Bac kutakuwa na watu 2 wanaoitakia mema Zanzibar na hawa ndio Wanaovujisha habari zote za Siri za CCM.

  Hivo maalim Sefu hata akisema kitu kinakuwa tayari kashapewa uhakika na hao hao CCM au watakuwa wameshakitamka..

  @ PAPAX

  Kukaa Unguja Miaka Yote hiyo Kwaajili yakuibeba CCM bado hujuwi kwao SEIF ?

  Masikini Roho yako.

 9. maalim 23/02/2017 kwa 3:20 um ·

  Binafsi nilikuwa nikizitafuta hizo sababu 10 zilotajwa lakini sikuziona. Nilichokiona ni maelezo au ni jitahada alizokuwa akifanya Maalim kupigania haki yake, Si chengine kilichoongewa.
  Siwezi kumwita Maalim muongo au anadanganya watu mpaka pale jitihada zake zitakapogonga ukuta.
  Hivi sasa tunampa muda tuone ahadi anazotupa za muda mchache ujao, ambao anasema si mbali ingawaje hazina mpaka. tutamsubiri kwa uchache wa mwezi tuone ukweli na uongo uko wapi

  Mwandishi hukuweza kutuonesha sababu za kimsingi ambazo zitamzuia Maalim kuwa Rais.
  Halafu umesema kuwa Maalim hakuwa na confidence alipozungumza na BBC na Azam TV. Hii si kweli. Maalim kaongea kwa kujiamini kabisa kama vile anavyoongea wakati wa ziara yake huko .Pemba.
  Ukimya wa CCM ndio ulionifanya kudhani kuwa kuna jambo linaendelea ndani kwa ndani, kimya kingi kina mshindo,

 10. zamko 23/02/2017 kwa 4:30 um ·

  @ Muandishi

  Kwakuendelea na Maoni yangu ambayo hayakufikia Tamati wakati ule nitaka kuchambua Makala yako ktk kifungu cha 9 na 10 : Umesema nakunukuu hapo chini.

  “…9. Mabadiliko ya uwendeshwaji wa serikali ya Muungano ungeonekana kua kuna mabadiliko ya kimfumo..”….. Mwisho wakunukuu

  @ Muandishi hii statement yako haina uzito wowote ule na ni point ya Kitoto. Kwasababu siku hizi hata mtoto mdogo anajuwa kwamba Katika Serikali ya Tanganyika ( Mimi siwezi Kuiita Serikali Kuu, kwasababu Ukuu wake sijauona). Nikirusia kwenye point yangu nikwamba katika Serikali ya Tanganyika Mabadiliko yako Makubwa sana . Na mabadiliko hayo yamesababishwa na Hali ya Hewa ya Kisiasa ya Zanzibar ambayo CCM Tanganyika Wameisababisha. Walifanya hivo sio kwa bahati mbaya bali Wakijuwa Kwamba, wale walio Waweka ( SMZ Mazombi) Watawageuza kama mkate wa maji ulioko kwenye Chuma.

  Lakini bahati mbaya haikuwa hivo, na hii nikutokana nakwamba Walioko katika Serekali harmu ya CCM sio wote Wana haramu wa madaraka ya 20.March 2016. Bali Kuna Wawakilishi Halali walioshinda Uchaguzi halali wa 25.oct.2015. Na baadhi ya hao wana Vission ya Kuiona Zanzibar inapiga hatuwa na inapata haki zake. Hivo Watawala Walishindwa kuwageuza kama Mkate wa maji.

  Sasa mabadiliko ya Serikali ya Tanganyika ndio yale yaliomfanya Pombe afanye Ziara zake Kule Unguja ili Aje Awa- PROVOCK Wananchi wa Unguja na Pemba Kuhusu Jecha. Ile Ilikuwa ni Kuwachochea Watu Waandamane au Wafanye Fujo Kisha wapate Sababu yakupiga na kuuwa halafu waseme Zanzibar ni Fanatik au Islamisim.. Walishindwa kuwaripuwa Wazanzibari kwa Ukimwa na Uungwana Wao.

  Badiliko Jengine ni la Lipumba kumchukuwa na Kumrudisha CUF kuwa Mwenyekiti wa Lazima na Kujifungia Ofisi ya CUF. Lile ni Badiliko Jengine la Uendeshaji wa Serikali ya Tanganyika kutaka kukivuruga chama cha CUF ili waonyeshe Mataifa Kwamba Chama chenyewe hakiko STABLE kuongoza Visiwa hasa kwa Vile Visiwani Kuna Waislamu na iko karibu na Somali. Hivo ndio maana wao waliona haikuwa na haja CUF kuongoza. Hio sababu kwa Mataifa inaweza ikawa na Mantiki kubwa hasa siku hizi kulivotokea Anti-terorisim. @ Muandishi hapa CCM wamefanya calculation na kutumia CUF kuigawa CUF. Lakini Wao wako Nyuma ya pazia kumpa Ulinzi Lipumba na Vibaraka wake.

  Badiliko jengine ni Lile lakuhamisha Fedha zote za Ruzuku kutoka Account ya CUF na Kuingia katika Account Ya Mlala hoi na Lipumba yuko Kimya. Au Msajili wa Vyama yuko Nje hizo Ni Njama za CCM kutaka kuiuwa CUF na lkengo lao sio chama ila Kuwatoa Wazanzibari na Maalim katika madai Yao.

  Sasa Muandishi kama hayo huoni ni Mabadiliko basi badiliko jengine ni Kuwadhibiti Wapinzani hasa Vyama vikuu katika Mbiu yao ya Mgambo ya Madawa ya Kulevya. Kwasababu CHADEMA ni mpizani Mkuu wa CCM kama CUF sasa Kiongozi Wake anatiwa Dosari na Wazanzibari wanatakiwa wawe Focus na Mbowe huku Lipumba Alipenyezwa Pole Pole ktk Kisiwa cha Unguja ili aje Avamie Ofisi ya CUF na asababishe fujo.

  Mabadiliko mengine ya Dhahiri ni Bunge kukosa Meno, Kukosa Fedha katika Serikali ya Muungano na mengi mengine. @ Muandishi kama wewe ulikusudia Uone Pombe Analia , Au Amebadilishwa au Kinana Kaingia Shimoni.. CCM Wanajikaza Kisabuni Tuu Lakini Wamekamatwa Pabaya.

 11. mzeekondo 23/02/2017 kwa 5:40 um ·

  Sioni sababu hata moja ya ya msingi kumtupia lawama Maalim Seif, kuhusu upatikanaji au kuvikomboa visiwa hivi mpaka leo, kuwa lazima iwe kasoro au makosa yote ni jukumu lake,ni kweli yeye ndie kiongozi mkuu wa upinzani kwa hapa kwetu,lakini cha kushangaza sisi wananchi wenyewe tunaoitaka hii nchi yetu atuletee kwenye kisahani cha chai, tumekwenda likizo bara?

  Huu uhayawani wa kumlaumu Maalim haukuanza leo,ccm wanamlaumu yeye kwa kuwanyima usingizi na misaada toka nje,sasa na cuf nao pia wanamlaumu yeye kwa kuwakosesha urais na safari yao ya Singapore,lakini nchi haikombolewi na mtu mmoja hata awe na nguvu kama Jabu Mponda au kinywa kama Boraafya.

  Mara nyingi nimesikia kuwa vijana wana subiri maalim atoe amri, ili waingie barabarani kudai nchi,na maalim bado hataki kutoa amri hiyo,mimi nitawaambia, kabla uchaguzi maalim alisema hivi na nitanukuu , ” yeye atakuwepo mtendeni ofisi kuu ya cuf, anawasubiri vijana waende kumchukua ili wampeleke ikulu” mwisho wa kunukuu.

  Sasa vijana mnataka kauli gani au ipi tena zaidi ya hii,hapa alikuwa ameshajua Maalim kuwa nchi atapewa Sheni kwa wizi,sasa anawataka muingie barabarani mkamchukue kwa maandamano nchi nzima,lawama ni yetu sote sio ya maalim hata kidogo,yeye kwa upande wake hivi sasa, ana zeekea katika hatakati hizi za ukombozi,sisi tumejifungia vyumbani, tunarusha maneno matupu kwa wino mweusi, si afadhali ya yeye alie mstari wa mbele, na kila siku anaikurubia jela kwa kuvipigania visiwa hivi.

  Hapana waungwana, wakulaumiwa tuko wengi lakini sio maalim, ni lazima tuwe na shukurani hata kwa wale wengine, ambao wana sababu binafsi za kumchukia Maalim, ila kwa sasa wameegemea kwenye siasa kuhalalisha chuki zao.

  Mimi niliwahi kunena huko nyuma kuwa, Maalim hakuwa kipenzi changu, kwa sababu CCM walihakikisha nimefaulu mtihani wa kumchukia muungwana huyu, kwa kuwa mimi bado mwanachama wao,lakini Mola wangu amenionyesha njia/ ukweli bado ni mwanachama wa ccm, lakini maalim sio wa kulaumiwa,na sie adui yangu wala wa Zanzibar.

  Adui ni Tanganyika kwa sasa,hapo zamani na siku zijazo,ikiwa hato iachia Zanzibar.

  Masikini mteseni, lakini haki yake mpeni,baniani{Tanganyika} mna hiari yenu.

  Nawashukuru.

 12. mohamed 23/02/2017 kwa 5:52 um ·

  Mimi naona Yale yalee!!!!.
  IIa naona bado kabisaaa hatujawa tayari ,isipokua hadithi nyingi za mapenzi na kula fagi baasi!!

  Hawa jamaa patumike nguvu ndio wataondoka.
  Mkiamua nambieni

 13. rasmi 23/02/2017 kwa 6:39 um ·

  Mwandishi bado ni mchanga katika ulimwengu wa siasa za ndani ya nchi (internal politics) na siasa za nje ya nchi (external politics).

  Mtu mzima huwa haambiwi muongo na katika suala hili alilolitolea ufafanuzi wake, wakati utatoa jawabu ni Maalim ama mwandishi ndie aliye akisema ukweli.

  Ushauri tu kwa mwandishi; mwerevu ni yule anayeweka akiba ya maneno hata kama anajua uhakika wa kitu fulani, kwani ukweli mtupu ama uongo mtupu unaweza kukueka katika sehemu usioitarajia…

 14. zamko 23/02/2017 kwa 7:05 um ·

  @ Mohamed
  Hapa Kuna Mambo 2 ya maalimu Kutotangazwa kwa sababu hizo 10 alizozitoa Muandishi. Na CCM kuto towa Nchi ni sababu Nyengine.

  Wachangiaji wengi hapa Hatukubaliani na hili neno lakuwa maalimu Anawadanganya Wazanzibari. Ila issue kubwa nikwamba hakuna Anae amini kama CCM hawatoi Serikali bila yakutumia Nguvu ( Imwagike Damu nyengine). Na Mara Hii Damu Wanayotaika Kuinywa CCM Wakoloni na Wahafidhuna ni ya Machotara na Wapemba.

  kwani ile Damu ya 1964 ili Nywewa na Babu zao Kina Sadifa na Shalka na kina Vuai Ali Vuai walipata kupora Vitu tu katika maduka ya Wahindi, Washihiri na waarabu lakini sasa wana Kiu ya Damu za Wapemba na Machotara. ile waliomwaga 2000 ilikuwa kidogo sana haikuweza hata kupata kijiko cha chai.

  Sasa kama tunakuja na issue alioitaja @ Muandishi ile ya Uongo na Udanganyifu kwa Wana CUF na Wazanzibari kwa Ujumla hii ndio issue ambayo mimi nakataa kama sio kweli kama maalimu anatudanganya. Na huu sio ushabiki hii ni reality kabisa. Isipokuwa Uzito na Ugumu wa yeye maalimu kutangazwa unatoka kwa Hawa Madhalimu wa Haki za wanyonge CCM SMZ na Mabwana zao Tanganyika.

  Issue yakuwa maalim Sefu kakosa Confidance naona pia haikuwa na ukweli wala uhakika. Maalim anazungumza kwa Confidance kama Haki ya Wazanzibari itasimama INSHAALLAH.. Na Anasema kinywa kipana hata kusema yeye ndie alieshinda uchaguzi na ukitizama ni kweli.

  Kwasababu kama CCM walishinda na Majimbo ya Pemba Walioyaogopa yalikuwa na Matatizo mbona umepita mwaka 1½ sasa wala hawajaja na hizo Data zao zakuonyesha kama Walishinda?.

  Jengine Nikwamba, Serikali ya Muungano kupitia Kamanda Wao Wa Polisi alisema hadharani kwamba maalim Sefu akirudi tu ile Safari yake ya Ulaya Watamkamata kwani ana ushahidi wakutosha wakumkamata maalim. Lakujiuliza ni Kwanini Maalimu hakukamatwa?

  Hivo Tuseme CCM wanampenda sana maalimu SEIF hata Wasimkamate Au Kwakuwa Kuna kitu Behind Kinawafanya Wasichokoze Nyuki?

  CCM Sio Wapumbavu Bhanaaa?

  Hawa Watu Ni Washenzi Wa Mwisho wao wanachojali ni Matumbo Yao Kutoka Mbele, M…du Yao Kutoka Mavi, Na Midomo Yao Kunya Kebehi na Kibri. Kutangaza na kutomtangaza Maalim Sio Lazima Atangazwe na Tume Maalum ya Uchaguzi. Na Kwa Allah Hakuna kubwa. Hasa Ukiangalia Zaidi kwamba aliedhulumiwa Amedhulumiwa kwa miaka mingi na ushahidi anao.

  Na Sio Yeye Tuu Ndani ya Dhulma hizo muna Raiya wasiokuwa na hatia, Mayatima, Wagonjwa, Wazee, Wajane, Vipofu, Vilema, Vichaa. Jamani Dhulma nadumu Maisha? sijawahi kusikia kama Dhulma inadumu Maisha.

  Kwa Upande Wakuwa Process yakudai haki ya Wazanzibari ni Ndefu, Ndio tatizo letu wengi hapa ( hata mimi) Subira imeanza kupotea, na subira ikipotea mtu anakosa HOPE, Na mtu akikosa hope anaweza kukufuru au kumlaumu yule aliemuachia kazi kufanya. Na Muandishi au watu kama mimi na wewe na yule, ndio tuko hivo. Lakini Huyo Kiongozi Tuliempa kazi hio haja lala wala kupumzika. Na huu sio Upendo lakini ni ukweli na hilo linajulikana, hivo tuseme Nchi na haki ni Sisi tu Ndio Inayotuuma kuliko yule anae beba Mimba miaka 20 sasa na kufika miezi tisa akazaa mtoto mzima lakini baadae Akazikwa mzima mzima.

  Hapa ni nani mwenye Uchungu zaidi? narudia Usemi wa nduyangu @ SADIMBA pale aliposema kwenye maoni yake paragraph ya mwisho kwamba…. namnukuu ..”Mimi naweza kuamini maalimu kachanganyikiwa na jinsi nchi yake ilvyofikishwa….”

  Hivo tukiona kama maalim kachanganyikiwa bac tujuwe kachanganyikiwa kwa kuiona Zanzibar na Wazanzibari wanako pelekwa katika umwagaji wa Damu.. Kwani Subira Ina mwisho.. Lakini Hili Kwa Uwezo Wa Allah na Duwa zetu halitofika na likifika huko Watazimwaga zao kwanza. Inshallah Biidhinillah.

  allah Ibariki zanzibar na Wazanzibari.
  Allah Mpe Umri Mrefu, Afya na Umlinde na Shari kiongozi yoyote yule anaeitakia Mema Zanzibar na wazanzibari . Amiin

 15. jazba 23/02/2017 kwa 8:57 um ·

  na mimi nitoe mchango wangu
  tunawaheshimu sana viongozi wetu wa cuf na cuf ndio chama pekee cha wazanzibari,wanaojitambua na wasiojitambua ukiwa mzanzibari halisi wewe ni cuf,

  ila ningeomba tu kwa viongozi wetu waache kututia moyo kwenye mambo yasiyokuwa na muelekeo badala yake tutie nguvu zaidi kueleza jamii ya wazanzibari hali halisi ilivyo na mambo yanayoendelea hatua zilizofikiwa,isije kuwa ni kutiana moyo kisiasa ili kujenga upinzani imara ilhali haki haiwezi kupatikana hii ni kutia maji pakachani

  upinzani wa wazanzibari hauna haja ya kujengwa,sisi wazanzibari ni wapinzani wa asili wa hali halisi inayotukabili ambayo ni ukweli kabisa tangu tulipo khulukiwa sisi tumo katika mifumo ya dhulma na ukandamizaji wa haki,hatujui uhuru wa kweli ni nini au ingekuwa vipi kama tungekuwa huru kujiamulia tunavyotaka wenyewe bila ya kumilikiwa na watu wasio wazanizbari,kwa ufupi sisi ni wapinzani tangu asili na kila mmoja ana wakati wake wa kuamka na kufahamu na muda wa kila mmoja wetu utafika.

  cha muhimu hapa tulipo kwa mtazamo wangu ni kuhubiri ukweli na sio kutia watu moyo,na hayo yanayosemwa kuwa yanakuja kuleta haki ya wazanzibari kama yana ukweli inshallah tuyasubiri, lakini kama ni danganya toto mie naomba bora tuache mara moja kucheza na akili za watu wazima wa zanzibari,ukweli pekee ndio utakao tuweka huru

  mie nakumbuka tangu asili ya kunyimwa haki hapa zanzibar enzi za 1995 tulianza kutiwa moyo huko nakumbuka maneno ya mitaani “mambo yatengezwa chuma kiulaya” na mpaka leo tupo pale pale na tunawapa nguvu zaidi wanaotunyima haki wakijua nini kitatokea baada ya kutudhulumu,kinachotokea kila baada ya dhulma ni kwamba viongozi wa cuf wanavaa mashati na kofia za cuf kubembeleza na kuwatia moyo wazanzibari ili walale huku wanaodhulumu wakifaidi dhulma walizofanya,

  michezo hii tuiwache jamani maisha ya watu ni ya kweli,muda wa watu unapita kweli,watu wamedhulumiwa kweli,watu wanateswa kweli,haki ya wazanzibari imechukuliwa kweli kwa hio kufanya mzaha na maisha na haki za watu si busara hata kidogo bali ni kuwapa nguvu wanaodhulumu

 16. shawnjr24 23/02/2017 kwa 9:36 um ·

  Muandishi wa hii makala kwanini hujaja na sababu kumi Maalim Seif azifanye ili afanikiwe kuipata haki yake. Na umekuja kinyume na matarajio na shutuma telee. Mimi binafsi siamini kwa leo na kesho haki yake itakuja lakini nahakika ataipata haki yake na Inshallah M / mungu atajaalia. Hakika hata mgonjwa mahtuti anahitaji maneno ya kumtia moyo, ama kwa akhera au kumpa moyo kupata uzima na sio kusimanga. Hata kama maalim hatoipata haki yake lakini kafanya kazi kubwa sana kwetu sisi Wazanzibari, na anahitaji pongezi na kupata support yetu kwa njia zote. Kuipigania zanzibar kupata hadhi yake kama ilivyokuwa, kwanini tusijiulize mimi na wewe tupo kwenye keyboard na kutoa shutuma baada ya kuwa mstari wa mbele? Maalim Seif anaipigania haki yetu wewe ulieleta hoja hapa hebu twambie ukweli wako basi unapigania kwa njia gani? Hata Makureshi walisema mtume hatorudi tena makka na mwisho waliuona. 2009 sisi ndio tulifika kumzomea maalim pale kibanda maiti tukisema muongo, kahongwa na msaliti lakini mwisho tumeiona faida yake na kuja na S.U.K. Na hapa anahitaji muda mpeni muda wake hata kama hatipata mbona Morsi nae kanyanganywa na yupo ndani sasa hakuna hata wa kutoa. @ jino kwa jino ndugu yangu punguza jazba subira huvuta kheri.

Comments are now closed for this article.