Risasi na mabomu yarindima Kangagani usiku huu

Written by  //  16/12/2016  //  Habari  //  Maoni 8

Kuna taarifa za kuaminika kuwa milio ya risasi na mabomu imekuwa ikisikika huko Kangagani Pemba. Hali hii imewafanya wakaazi wa Kangagani usiku huu kuyakimbia majumba yao na kukimbilia misituni kupata manusura.

Chanzo cha hali hii ni wananchi kukataa kutajwa jina la Dr Shein kwenye khutba ya Ijumaa.

Tokea mchana wakati wa swala ya Ijumaa hali imekuwa tete kwa wakati wa Kangagani ambapo waliswali Ijumaa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku mkuu wa mkoa wa kaskazini na mkuu ya wete wote wakihudhuria.

Wiki iliyopita vijana 7 wamekamatwa na polisi hadi leo hii bado wako mahabusu.

Bado haijajulikanwa ni watu wangapi wameumia kwenye mashambulizi haya, lakini inasemekana majeruhi ni wengi. Pia haijulikani hadi sasa ni watu wangapi wamekamatwa.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Risasi na mabomu yarindima Kangagani usiku huu"

 1. abuu7 16/12/2016 kwa 8:29 um ·

  sasa maalim kidogo kaaakando. nguvu ya umma ichukuwe mkondo wake. chezeya wazanzibar wa pemba wee.usifanye mchezo. kule .mmulize Tundu lisu..

 2. Piga nikupige 16/12/2016 kwa 8:32 um ·

  Wanapigwa na Mkangagani mwenzao anaitwa Rashidi Hadidi ni mkuu wa wilaya wa DK. Shein, wa wilaya ya ya Wete. Huyu bwana ndio fitna mkubwa, iko haja ya Wana Kangagani kumkabidhi Mwenyezi Mungu huyu Mshenzi.

 3. salali 16/12/2016 kwa 11:32 um ·

  Wasichanganye dini na siasa kama Maalim rais wetu hawataki ahutubiye hata akialikwa mskitini iweje Shein atwaje mskitini kwani yeye nani hapo Zanzibar, sisi wa Zanzibar tunamuona yeye ni haini tu, anaringiya vifaru,kachokonza mzinga ngoja sasa tumuonyeshe makali ya nyuki.

 4. mohamed 17/12/2016 kwa 12:25 mu ·

  Watu wengine hasa mafala,kwani sheni kafa hata atajwe au kuombewa dua?
  Bado hajafa mwache ajiombee mwenyewe dua na kama haitoshi ccm wanamashekhe wengi tu,si wamtaje tu

  • Ghalib 17/12/2016 kwa 12:41 mu ·

   Umesahau na ma padri, mashekh wetu wako rumande, ccm hawana mashekh ispokuwa waganga njaa, kwa dhulma wanazo fanya kama mtu shekh kweli lazima akae nao mbali

 5. Ghalib 17/12/2016 kwa 12:42 mu ·

  Poleni wananchi wa kangagani, kujiokowa muhimu, self defence.

 6. Jino kwa Jino 18/12/2016 kwa 5:50 mu ·

  Hili ndilo ndilo tatatizo moja la watu wa Pemba ni kuwa hawana viongozi wanaona mbali wanaofikiri kwani kuna shida ya kumtaja sheini mwache atajwe baada ya watu kusema amin wakati akiombewa dua waseme laanu Llah sheikh mwenyewe atanyamaza kimya jamani mambo kwa akili dua ikiombwa ya shein watu Laanatu llah sheikh akiomba tena watu laanatu llah Jamani kuweni na akili musicheze na Seriakali( Wapemba wanasema Usicheze na Sirika Lako )Yaani mtu aliokuwa mkubwa wako hamuna nguvu za kupigana hamuna chochote sasa munawatia tabu famila zenu .Tumieni akili zenu zaidi kuliko nguvu zenu .

 7. Z.I.7 18/12/2016 kwa 5:01 um ·

  HILO ni somo lililodhahir na linathibitishwa kuwa hawa mission town hawatakiwi na wananchi lakin wanalazimisha,

  a simple logic hata hapo kabla yakuja hizi znoitwa serikali kuu zinazoambiwa za kisasa zenye wasomi hapo zamani ulikuwepo uongozi kama ni wakikabila au wa kijiji huwepo kwa ridhaa za wote wanao husika kwahiyo haikuwahi kusikika kuwa chifu au mtemi fulani kenda kawashambulia au kuwapiga watu wake kwasbb.>

  chifu alipata madaraka kwa mujibu wa kanuni walizojiwekea kwa maana hiyo wafuasi waliridhia na kfuata mwongozo kwa hiari

  kwahiyo nidham upendo heshima na uadilifu ilijengeka ktk makabila au vijiji ndio maana kukawa na mila tafauti baina ya makabila otherwise usingemjua mnyaturu au mkerewe

  ndio maana viongozi wa wakati huo walikuwa wakiheshimiwa na nidham ya hali ya juu
  na walikuwa tayari kufa kwa ajili ya watu wao kwasbb walikuwa ni viongozi wa watu.

  lkn sijui ni seme cha kuskitisha au chakuchekesha au kioja eti ni kiongozi anatuma watu kwenda kuwapiga na kuwajeruhi hao anasema anawaongoza kwa sbb hakutajwa jina msikitini

  ah utukufu gani huo wakulazimisha! baada ya makosa ya kulazimisha madaraka na kutumia mamlaka na huduma za nchi bila uhalali na wamekuwachia, na wako kimya! kila baada muda mara kuwavunjia mara kuwanyangaya, mara kuwapiga, mara kuwaibiauna haya ni maajabu wewe unajiita kiongozi alafu uwafanyia ushenzi hao unaosema unawaongoza ni utukufu gani huo?

  lkn kumbuka hao unowafanyia hayo ni watu wazima kama wewe ambapo baba zao waliowazaa hawawezi kuwafanyia idhlali kama hiyo sasa kama ni wanamapinduzi

  ni watanzania pekeyenu lkn haikupini uhalali wa kudhalilisha wengine ila mkiona sisi tunao kukumbusheni pia n i kero nynyi endeleeni utkufu utaongezeka. na chama chenu kitapata wafuasi zaidi.

  tuseme hii ndio akhir zaman? au nilaana gani unasema wewe ni kiongozi unatumia askari wakawadhib ndugu zao kwa faida gani na ya nani?

  Bora kuanuwa kabla ya wingu au MBELE KIZA KWENU!

Comments are now closed for this article.