Precision Air yazuiwa kutua Zanzibar

Written by  //  31/12/2012  //  Habari  //  17 Comments

Kuna taarifa za kuaminika kuwa ndege za Precision Air zimezuwiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kitendo hicho kimetokea kutokana na sababu kwamba tokea shirika hilo lilipoanzishwa na kuanza safari zake Zanzibar hakuna hata shilingi moja iliyolipwa.

Uamuzi huu ulichukuliwa na Zanzibar Reveniew Board (ZRB) ambao ndio waliochukuwa hatua ya kuisimamisha kutua kwa ndege za shirika hili, kwa kushindwa kulipa ushuru kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza. Hakuna pesa hata moja walizozilipa kama sehemu ya ushuru licha ya kutumia rasilimali za Zanzibar kama vile ardhi, runaway, umeme, na mambo mengine.

Kuna fununu kwamba SMZ Ikulu imeingilia kati hatua hiyo na kutaka Precision iachiwe iendelee kutumia uwanja wa Zanzibar, lakini ufumbuzi kamili bado haujapatikana.

Sasa hivi kampuni hii imekuwa, kwa siku moja, ikileta zaidi ya ndege 15 – zinatuwa na kuruka katika uwanja wa ndege wa Zanzibar zikiunganisha safari kutoka miji mbalimbali kama vile Nairobi, Mombasa, Daressalam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, na kwengineko.

Vilevile ikumbukwe kwamba Pricision Air imeungana na Kenya Airways, hivyo kuchukuwa jukumu la safari zote kutoka Nairobi kuja Zanzibar

About the Author

View all posts by

17 Comments on "Precision Air yazuiwa kutua Zanzibar"

  1. pambanua 31/12/2012 at 5:31 mu ·

    hawa ZRB ni wapuuzi tu, wanawafanya Precision Air ni wajinga wawalipishe kodi mara mbili kama wanavyowafanyia wafanyabiashara wetu? kodi wameiuza tanganyika sasa wanabaki kujamba jamba tu. Precision wanalipa kodi TRA na ndio kodi ya mapato ZRB ni kodi ya nini? si ni ya kuwadhalilisha wananchi wa kawaida tu.

    na wazifungie waone uwanja utakavyo ota ukungu manake hao ZRB,, futeni TRA nyie akina omar yussuf acheni kuunya unya unaitia nchi katika udhalili wa makusudi.

  2. Ashakh (Kiongozi) 31/12/2012 at 5:50 mu ·

    Mimi nadhani kimoja kinachopendwa na kuvutia mzalendo.net ni maoni yanayotolewa hapa. Sio tu kwa watu wa kawaida bali hata viongozi wa serikali wamekuwa weakifaidika na maoni yetu.

    Hivyo ningeomba utumiaji wa lugha za kistaarabu na busara zilizozidi mizani iwe ndio hulka yetu. Hii itaimarisha hadhi na kunyanyua haiba ya mzalendo.net

    Napenda kusisitiza kwa wazalendo wote tutumie lugha zinazoendana na maadil, silka na mila zetu. Lugha za matusi, dharau, au jazba hazifai, tujiepushe nazo.

    @Pambanua
    Ni miongoni mwa wazalendo munaoshindwa kuzuwia jazba zenu. Mara kadhaa nimejaribu kukuasa juu ya hili bado unashikilia bango lako, hivyo sivyo.

  3. salma 31/12/2012 at 6:18 mu ·

    Asalamu Alaykum. taarifa hizi hata mimi nipo nazo lakini tatizo letu kubwa ni kwamba tunapofuatilia hatufikii mwisho kwa kuwa wahusika wanakupa taarifa lakini wanakataa kukuonesha ushahidi wa barua na vielelezo vyengine lakini taarifa zilizopo ambazo hazijathibitishwa na bila ya shaka haziwezi kuthibitishwa kwa sababu ndio utamaduni wetu wa kukataa kusema nyekundu na tukasema kijani hata kama ni kweli nyenkundu lakini ni kwamba mhusika alipigiwa simu na ofisi ya Ikulu na akaambiwa airuhusu ndege kwa hivyo hili ni tatizo jengine ambalo tunatupa mapato yetu lakini pia tunaingilia mamlaka husika, na hivyo ofisi ya Ikulu inatumika katika kuvunja sheria na hilo linajulikana ingawa halisemwi hadharani mambo mengi ofisi ya Ikulu inaingilia na katika baadhi ya ripoti mbali mbali zilizowasilishwa katika vikao vya baraza la wawakilishi limethibitika hilo kwamba Ikulu inaingilia ama kwa maafisa wake kwa kutumia jina la Rais au wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na baadhi yao tunawajua kwa majina ambao wanaingilia mamlaka nyengine ambazo hawapaswi kuingilia.

    Salma Said

  4. Ashakh (Kiongozi) 31/12/2012 at 6:29 mu ·

    Da Salma

    Hili nakubaliana na wewe ni suala la urasimu wa habari kwa watendaji wetu. Hata hizi taarifa mtu kuzitowa yeye anaona wewe utafaidika.

    Hata hivyo nadhani kwenye mzalendo.net tunayo hiyo sehemu za taarifa kama hizi za wikileaks. Pamoja na kuwa hazijafikia mwisho, unaweza kuzileta hivyohivyo. Najuwa kama nyinyi waandishi by professional linapunguza haiba yenu, kwa upande mwengi litasaidia kuibua na kufichua siri nzito zilizoko kwa hao mabakhili wa taarifa.

  5. mwanafunzi 31/12/2012 at 9:02 mu ·

    Kama sheria za zanzibar zinasema shirika au mtu alipe kodi ni lazima alipe kulingana na sheria za zanzibar kwa kuwa hata sisi raia wa kawaida tunaoishi zanzibar tunalipa kodi mbili (TRA na ZRB) sasa kwa nini mtu mwengine asilipe?

    Hii ikulu ikiwa inatumia majukumu yake vibaya ni vizuri wanaoelewa haya wawaeleze wananchi waelewe na kama kuna taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yao, hakuna hata mmoja alie juu ya sheria.

    Ikiwa raia wa kawaida anapofanya kosa anahukumiwa tunataka hivyo hivyo ifanyike kwa viongozi wanaovunja sheria na huu ndio utawala wa sheria tunaoutaka kwenye zanzibar yenye mamlaka kamili.

  6. sale 31/12/2012 at 10:53 mu ·

    Hii mzalendo yangu Kweli inanifurahisha Saa nyengine huwa na matafrani yangu lakini nikiingia hapa hupata afueni. Saa nyengine hujiuliza hawa wasomaji wa mzalendo.net Sijui wanaishi dunia gani ? Leo hii mnazungumzia Zanzibar,viongozi, nasheria Kkkkkkkk..Zanzibar na Sheria ama Sheria na Zanzibar ?

  7. Hisba 31/12/2012 at 1:33 um ·

    Moja ya miza za utawala dhalim ni kuwabana wanyonge na kuwadhalilisha na hili hata asiye na macho analiona katika Zanzibar yetu. Yanayowahusu wakubwa yanapigwa danadana na hii tumeona katika ajali za meli, hakuna lilochukuliwa hatuwa. Milioni zimetumika za walala hoi eti kufanya uchunguzi na kuandika ripoti, hakuna lilofanywa. Lakini nakuambieni nyie Waheshimiwa kuwa huku ni kujiiongezea maswali mbele ya Allah (SW). Fanyeni mufanyavyo lakini angalieni waliokutangulieni wako wapi leo, jee hamusomi na kutafakari?

  8. kingjokery 31/12/2012 at 2:27 um ·

    hapo la msingi ni lile alilolisema maalim seif mara kadhaa kwamba serikali ya zanzibar itaanzisha shirika lake la ndege linalomilikiwa na SMZ, na hilo likifanyika safari za kwenda katika nchi za jumuiya ya afrika mashariki zitafaikiwa sana, mashirika mengi ya ndege ya zanzibar hayafanyi safai za kwenda nairobi, entebbe ,bujumbura au kigali kutokana na kampuni hizo kumiliki vidge vidogo visivyomudu safari ndefu kwa kuwa avinachukuwa abiria wachache na bila shaka kutokana na kodi za mafuta, viwanja nk videge hivyo havimudu ushindani. fikiri leo zanair au tropical air iende nairobi haya hizo gharama uendeshaji , mafuta na kodi nyenginezo ni kiasi gani? na ili nauli iwe nafuu ya ushindani ndege ni lazima iweze kubeba abiria wangapi? jee kuna kampuni yoyote ya ndege znz yenye uwezo huo?
    sasa kwa maoni yangu ZRB kuchukua hatua hizo ni jambo zuri kwa kutaka kuongeza makusanyo ya serkali na hilo lingewezekana lingesaidia sana kufanikisha mambo mengi, lakini swali ni jee ZRB ishatafuta usafiri mbadala wa kwenda nairobi au entebbe kutoka znz?
    maoni yangu ni kuwa hapo serikali ilione hilo tatizo na itafute suluhisho na hao ZRB wasikurpuke kwa vishindo ni afadhali wakubaliane na wenzao TRA ili kijulikane chetu lakini huduma iendelee.
    hao precision wanalijua hilo ndio maana hawajali wana uhakika kwa siku nyingi zijazo na kwa tawala hizi za zanzibar na SMZ hawatakuwa na ubavu wa kuwazuwiya wasitue znz na hata wananchi wenyewe watapiga kelele.
    SMZ tafuteni suluhisho kwanza na nyie ZRB msikurupuke ulizeni wakubwa wenu kwanza! vyenginevyo mtajidhalilisha siku zote.
    zanzibar ukweli haijawa na ubavu huo kwasasa.
    wakuwahukumu hapa ni wale waliofanya visa hadi kusitishwa kwa upanuzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege , mana ukiwa na uwanja mzuri kama ilivyokusudiwa hapo awali ndge nyingi zingekuja zanzibar na kwa hivyo tungeweza kuwa na ndege zenye destination nyingi zaidi kuanzia national wide, regional na international flight , kwa hivyo tungekuwa na choice na meno za ZRB yangeweza kung’ata vyenginevyo hatujui tulitendalo.
    kamateni waliohujumu ujenzi wa uwanja!!!!

  9. nuramo 31/12/2012 at 4:30 um ·

    Just think,hatuna hata ndege ya moja kwa moja kutoka ulaya yoyote bila kupitia Tanganyika,ukiacha za kitalii,hili linasababisha hata tukituma vijimzigo vinakwama bara na vikitoka utajuta huo ushuru wake,ukishuka bara usumbuliwe us upekuliwe airport kisha na bandarini,no comments

  10. hilal 31/12/2012 at 5:43 um ·

    mimi nadhani ulipaji kodi ni lazima kwa visiwa vya zanzibar ili yapatikane yale ya mahitajio ya lazima kwa raia wa zanzibar sasa hichi ni kitandawili uwanja ni wa zanzibar na kodi inalipwa bara wahusika wajitokeze kuwafahamisha wazanzibari ili wapate elewa.

  11. star 31/12/2012 at 7:32 um ·

    Mie nahisi ayo alozungumza Salma ni miongoni mwa utamaduni wa ccm la ajabu hamna. Na naamini hata yeye bi Salma haoni ajabu ila analizungumzia tu km kawaida lkn hayo ndio miongoni mwa mambo yanayotufanya kutokuendelea na kwa upande wa walokua wanyonge ndio wao hutupwa kabisa kwa unyonge wao. Ivo passport km huna laki huipati that means kuna wanyonge kibao ata passport zinawashinda na kuna wengine hawana haja ya kwenda uhamiaji wanapelekewa nyumbani kwa umaarufu wao hiyo ndio Zanzibar ufisadi mtupu hatuendelei maisha kwa ukiritimba wa wachache lkn is so deep

  12. MAWENI 31/12/2012 at 8:13 um ·

    Tatizo hili na mengi kama hayo hayato toweka mkapa Zanzibar itaporejesha UHURU WAKE NA MAMLAKE YAKE KAMILI YA NJE NA NDANI. HIZO TAASIS ZINAZO ITWA ZA MUUNGANO KUZUGUMZA NAZO, AU KUZIZUIYA ZISIFANYE KAZI ZANZIBAR NA HATA KUZIGOMEA HAITO LETA FAIDA. YOYOTE. HAO TUNAO AMBIWA NDUGU ZETU WA DAMU WANATU DHARAU SANA. LA KUFANYA NI KUREJESHA MAMLAKA YETU YOTE. MAMBO YOTE YATA KUWA SAWA.

    ZANZIBAR KWANZA!

  13. pambanua 01/01/2013 at 6:11 mu ·

    @Ashakh(Kiongozi)

    Haya baba nitajaribu kuzuia hizo zinazoitwa hasira au sito-comments tena kuanzia leo mwaka huu wa 2013

  14. Ali wa Ali 01/01/2013 at 1:04 um ·

    Hivi viongozi wetu wa z’bar kabla kupewa huo uongozi wanapewa nini na ccm mpaka kuwa hivi na kuitelekeza z’bar na kufata kila amri inayotoka tanganyika hata kama haina maslahi na z’bar vipi ndege zinatumia uwanja wa z’bar lakini malipo yanakatwa bara ZRB wameliona hilo wamezuia ndege kutua lakini viongozi wanapigiwa simu kutoka bara wanafyata mkia kwa hali hii tusitegemee z’bar yenye kipato kizuri milele na kuendelea kulipana mishahara ya laki na hamsini kwa mwezi. MUNGU IBARIKI Z’BAR HURU.

  15. abdisalum 01/01/2013 at 2:39 um ·

    Nchi zooooooooote duniani zinaendeshwa na kodi. Zanzibar pekee inasamehe zaidi ya asilimia 80% ya kodi. Itakwenda vipi?

    Si Precision Air pekee ambao wanachuma na kula katika shamba la ‘bamkubwa Shein na wenzake’.

    - Ama ZRB inasamehe mabilioni ya kodi kwa wawekezaji, au ZRB inataka kudai kodi lakini SMZ inakinga kifua, baadaye wawekezaji wanaitwa ili ‘kuelewana na kugawana mgao kwa mlango wa nyuma’.

    - Zanzibar inaweza kujiendesha kama ni nchi ya kutoa huduma tu, lakini wallah kila penny inayoingia inachukuliwa. Airport pekee ya Zanzibar inaingiza kama 50bn na ushei, inaweza kulipa mishahara yoooote ya civil servants wa Zanzibar’ lakini hata ule umeme wanaoutumia wao wenyewe inabidi wapate ruzuku kutoka treasury. Naomba mfanye utafiti wa mapato ya bandari na airport mtaona nini ninasema.

    - Kuna wawekezaji hawalipi hata umeme wala maji, sikwambii kodi ya ZRB. na Ndio maana ukiajiriwa ZRB miezi mitatu utajenga nyumba zaidi ya nne katika posh areas kama vile Mbweni, Chukwani au kule Pemba wanaita ‘mnyonge hajengi’ (pekee hili jina kufru).

    SMZ na ki-GNU chake wamebaki kuwakamua dying cow/or horse — wanawakamua civil servants kwa kila penny wanayoipata, wanawalipisha kodi tena kubwa mno.

    Precision Air ni tip tu katika iceberg.

    Nakumbuka moja ya dream — sweet dream ya Maalim Seif (VP1) ni kuwa Zanzibar iwe ni service centre na itajiendesha kwa mfumo w autoaji wa huduma tu — asalale balahau, walaji umewasahau wapi? Sasa yumo serikalini GNU, na ameufyata, na Maalim Seif anajua A-to-Z haya yote tunayozungumza humu, akiwemo Bablee — [umetoa mada bomba kabisa] umenikosha kuanzia juu ya utosi hadi vidole vya miguu. Wallah PONGEZI NYINGI.

    usijali tunacho kitufe chetu GNU — tunazidi kupoteza direction.

    Wewe ukitaka kuja kufanya ufuska hapa Zanzibar (njoo), kuzindua album za uchafu, ukahba (njoo), kucheza uchi (njoo); juzi kulikuwa na party — beach party ppahala, party hiyo imepewa jina la ‘chupi nje nje’ (samahanini sana kwa kutumia neno hili) lakini ndilo jina la hiyo party.

    Ukitaka kuja kuzindua ubalaa wowote ule njoo — rukhsa.

    Siku moja pale Ngome Kongwe — walicheza jamaa uchi mpaka nje, na huku wanakunywa bia na kuzimwaga. Njoo ujitanafas, SMZ-GNU haina neno. Uamsho tu hauruhusiwi wala kudai HAKI yetu.

    Si mmeona jana new year eve, kila kona ya ukahaba, muzic LIVE, na burudani zote zilifanyika zaidi kuliko hata Dar, or Nairobi, or anywhere — washiriki alitoka kila kona ya dunia kuja hapa kusherehekea mwaka mpya 2013. Basi iwe bora Zanzibar kwa starehe nzuri kuliko Dar.

    Hiyo ndio service industry anayoikusudia Maalim Seif na wenzake.

    SMZ-GNU inakubali kuwakamua wale petty traders Darajani — wazawa kila penny, lakini wameisamehe na kuiachai precision airo inayodaiwa mabilioni. Shamba la kaka Shein — hongera Amiiiiii Mohammed Aboud kwa kufanya ‘deal’. hey super boy!

    Pale Aiport kuna mchezo unachezwa siku nyingi tu, zinakatwa manifesto list, yaani kama ni 300 passengers, inapelekwa kama 100, baadaye jamaa wanakaa chini na kugawa ‘ngawira’ mgao; kuna bint mmoja pale (mke wa xxxxx) yeye kwa siku anachukua kama 1000 dola hapo ndio hakupata, kuna siku anaramba mpaka 5000 dola. Dear wake anafanya kazi xxxx na ni katibu mkuu pahala fulani fulani hivi! na wengine wengi. Mbali madawa ya kulevya yanayopitishwa pale na baadaye mgao mbele kwa mbele.

    Haya TUMETHUBUTU TUMEWEZA, SASA TUNASONGA MBELE.

    Sisi wengine maradhi yetu ni kuwepo kwa UAMSHO tu, hii ndio inatukera. sasa hivi burdaaaaa kabisa. Tunakula na kunywa tunavyotaka. Si mmeona matokeo ya sensa hayo? chakachua— nikuchakue baba. Hesabu fake hizo, lakini ndio amesema bosi JK, hakuna kupinga.

    Farid na wenzake waendelee kubaki ndani ili tupate kuiunganisha Tanganyika-Zanzibar iwe MOJA TU.

    Ohhh…..akina jenerali ulimwengu wakisema wanataka Tanganyika yao, it’s OK, lakini sisi tusiseme tunataka Zanzibar yetu, au ‘N’kataba au sijui nini na nini.

  16. pambanua 01/01/2013 at 5:03 um ·

    @abdisalum

    Hongera baba endelea kuchangia mi sitii neno naambiwa eti natukana hivyo nasoma tu waliyochangia wenzangu.

    Ila hongera abdi

  17. Bosco 01/01/2013 at 8:13 um ·

    Precision air imefanikiwa kuuwa shirika la ndege la tanzania halafu waje washindwe kutua znz bila ya kodi?

    Inshort precision air ni shirika la ndege la viongozi wa serikali ya tanganyika.

Comments are now closed for this article.