POLE SANA MAMA FAUZIA KILIO CHAKO TUMEKISIKIA NASI TUNAKUSAIDIA KULIA

Written by  //  05/12/2016  //  Habari  //  Maoni 19

15179024_821029758036871_823839526339617651_n

Part-1

Asslam Aleykum

Jina langu naitwa Fauzia Abdullah Saif Al Bahry. Mimi ni mjane wa Said Iddi BAVUAI, na nimeishi nae si chini ya miaka thalathini. Nimezaa nae nimejukuu nae, na nimemkalia mpaka EDA. Na mpaka leo naendelea kuwa mjane wa mzee BAVUAI. Ambae jana nimeshtushwa kusikia katika vyombo vya habari tunatangaziwa kwa jina la mdogo wangu Fadya. Na sijui kwa nini wasinitangaze mimi mkubwa wakamtangaza Fadya ambae ni mdogo na sisi tuko watatu Fauzia, Fadya na Firdaus lakini wametumia jina la mtu mmoja kuwa sisi wabadhirifu.

Hii lugha mimi ngeni kwangu kwa hakika siijui na hata sijui nini maana ya ubadhirifu nauliza nini maana ya ubadhirifu ? Sijui. Lakini nimefahamishwa kuwa ni wizi, kwaivo nakataa ile habari ilosema jana ambayo rikodi yake ipo na watu wamerikodi. Mimi nakataa si mwizi, siibi, sitoiba na sijamuibia mtu yeyote shamba la Kazole. Ni haki yetu tumerithi kwa wazee wetu, babaangu Abdallah bin Saif amefariki, Nassor bin Saif amefariki, na ami yangu Hemed bin Saif amefariki, na mali hii yetu. Mali tumerithi kwa wazee wetu.

Babaangu na ami zangu wamerithi kwa baba yao ambae amefariki toka 1930 na makaburi yake yapo pale pale kazole Muembe Amari, makaburi yapo ya mababu na ndugu na wazee walio tangulia mbele ya haki. Sijui ubadhirifu huu nimeufanya kwenye kitu gani ? Kazole ni kwetu kazole nimeishi kazole nimekaa kazole naijua kwetu pakiitwa Muembe Amari. Tena mie mtu wa Kazole jirani yangu Kitope, jirani yangu Mahonda, jirani yangu Matetema. Shamba letu limepakana mpaka njia ya Mbaleni.

Hao walozuka leo wakasema lile ni shamba lao au sisi tumefanya ubadhirifu. Mh kama unataka kuchukua shamba chukua na kama unataka kuvunja kuta vunja lakini nakataa mimi na aila (familia) yangu sio wabadhirifu.

Mimi nimeolewa na mwanamme ambae ni kiongozi katika nchi sikumuona kufanya ubadhirifu, wala hajanifundisha ubadhirifu, wala kwetu sikuuona ubadhirifu. Niliona yeye (mume wangu) akifanya haki wizarani, maofisini, watu, makazini sijasikia yeye akifanya ubadhirifu wa aina yoyote. Yeye akisuluhisha na kutengeneza ndio hii siasa nilio ikuta wakati huo kwa hao waume walotuoa.

Huyo alochukua na kutoa amri ni Mh yuko katika ngazi ya juu na kajitangaza rasmi na maredio yote yanajua, TV pia. Hajasema siri. Zanzibar iniskie na Tanzania iniskie viongozi wa zamani wake zao wana nyanyaswa katika nchi hii. Wamesahau kila kitu.

NB: SALAMU KWA BALOZI MKAAZI

Part-2
Salam kwa balozi mkaazi

Assalam alaykum Muheshimiwa. Ndio, wewe ni Muheshimiwa Saif Ali Iddi, na mimi raia Fauzia Abdullah Saif Al Bahry mjane wa Said Iddi BAVUAI. Kweli Muheshimiwa, Muheshimiwa mwenye nguvu, Muheshimiwa hodari, Muheshimiwa jeuri.

Lakini Muheshimiwa nakwambia hivi, nnavojua mimi nilivokuwa nimekaa na hao waasisi na wanamapinduzi wa nchi hii walivonifundisha kuwa likitokea jambo lolote khitilafu kwenye wilaya, mkoa, na mambo yanokhusu serekali huwa inachaguliwa tume na watu huitwa na kisikilizwa pande zote mbili.

Ikiwa unasema Waarabu wamekuja kuchukua na kuvamia shamba la Kazole, hakuna alokuja kuvamia shamba la Kazole. Shamba la Kazole ni langu mimi Fauzia Abdullah Saif Al Bahry. Umefahamu ?

Na tulijisalimisha baada ya hao waasisi kutaka kutuoa na tukakubali ili kuondoke hizi FITNA za ukabila. Kwahio Muheshimiwa unarejesha UKABILA ambao kaufuta Karume 1964. Wewe unarejesha UKABILA.

Kwahio wewe unakwenda dhidi ya siasa ya Uzanzibari. Kwahio nakwambia hiyo ni haki yangu, nimerithi kwa wazee wangu, sijabadili uraia wangu, ni Mzanzibari, na watoto wangu ni Wazanzibari, na wajukuu zangu ni Wazanzibari.

Muheshimiwa chukua, na vunja kuta, na vunja makaburi, na vunja MSIKITI, na vunja kila kilichokuwemo kwenye shamba kwa ujabari wako, na kwa uhodari wako.

Na mimi Niko tayari kwa maneno haya uje kunichukua na kunifunga, unasikia ? Nifunge Niko tayari lakini tulijisalimisha kwa kukataa hizi bughdha zenu. Tulijisalimisha kwa kukataa hizi chokochoko, na bughdha na ubaguzi wenu, na ndio tukakubali kuolewa na watu kama nyinyi.

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 19 katika "POLE SANA MAMA FAUZIA KILIO CHAKO TUMEKISIKIA NASI TUNAKUSAIDIA KULIA"

 1. alwattan 05/12/2016 kwa 5:40 mu ·

  hayya hayya! tena, la kuvunda halina ubani dhulma ni kiza tu, dhulma haidumu na ikidumu inaangamiza! Onyo hili alilokupa Allaha hujazinduka tu? au mpka akubogonyoe na miguu uwe unasotaa? shauri zenu Allah yupo na anawaona kila dhulma mnayodhulumu na msidhani kama ndio kaghafilika na nyionyi

 2. mohamed 05/12/2016 kwa 11:21 mu ·

  Asalam alaykum wanaukumbi,
  Nauliza kwa wanaemjua,
  Je huyu seif idi ni mzanzibar au ?

  • Abdul Zakinthos 05/12/2016 kwa 7:01 um ·

   salam huyu anatoka Msitu wa Nyani CONGO ndugu yake wa damu ni KING ONG
   NASIKIA NA BALOZI KAPEWA CONTRACT YA KU ACT KING KONG II

   • shawnjr24 05/12/2016 kwa 9:15 um ·

    @Abdul Zakinthos
    Haifai kumfananisha binaadamu na mnyama ndugu/kaka yangu kumbuka aliemuumba yeye ndie alietuumba sisi. Katuumba kwa tofauti ili tupate kujuana na sio kudharauliana. Hata kama humpendi tafuta njia nyengine ya kuonesha hasira zako, lakini kwenye kuumba hio kazi ya Mola alietukuka.

 3. Mwinyi Mkuu 05/12/2016 kwa 1:45 um ·

  Ni jambazi fulani linatokea Congo

 4. SHAKUSH 05/12/2016 kwa 2:38 um ·

  Shikamoo Bwana Mzeekondo.
  Unapokuwa msafiri ni budi kuchagua chombo kinachofaa na ambacho ibaki ya Allah lakini kiwezacho kukuvusha hadi ng’ambo ya pili. Vyombo vyenye ufa tayari vinahitaji kalafati. Vyombo hivyo ni lazima vichunguzwe sana na upo uwe pe mbeni kwani huingiza maji muda wote wa safari. Hivyo macho na mikono hupata kazi ya ziada. Lakini ndiyo safari.
  Vyombo vyengine kwa uvivu wa nahodha eti huziba ufa kwa lami au nta jambo ambalo halileti tumaini.
  Vyombo vichakavu ndio hatari vimepoteza umakini na ni rahisi kuzama.
  Suluhisho ni kutumiya kalafati inayolingana na material ya chombo chenyewe. Chombo cha msufi kipate kalafati ya usufi na chombo cha chuma kipate kalafati ya welding hapi tumaini la safari huwa kubwa. Ama kupiga welding jahazi la mbao hubaki kichekesho na kuziba jahazi la chuma kwa udongo ni kujionesha mpenda maonesho.
  Nawanasihi wasafiri wote mtumiye kalafati kulingana na material iloundiwa jahazi lenyewe. Tupunguze makosa ya zamani kutumiya kalafati iliyo mbali na nasabu ya chombo chenyewe.

 5. salali 05/12/2016 kwa 11:08 um ·

  Uvundo unaonekana bado yukonao kwa jinsi anavyoonekana lana zote hizo, cheza na qur’ani wewe unazani ni kitabu alichokiandika samt?…

 6. mzeekondo 06/12/2016 kwa 1:06 mu ·

  @Shakush.

  Nakuitikia mzee mwenzangu na mimi nakuamkua, Wallahi leo umeni”kuna” ndio lugha sahihi, nilitaka kutumia neno umenifurahisha lakini nikagundua kuwa halifai, kwani kiwango cha lugha uliyoitumia leo hapo juu, nakuhakikishia kuna wengi wataisoma kalamu yako lakini wakisha maliza wataanza kutafuta “manyakanga” wawasaidie kuilainisha kilma uliyowaachia kimaandishi.

  lugha ni sanaa na ni lazima uwe na kipaji iwe umejifundisha/umefundishwa/au umeikuta kwenu, yaani umezaliwa nayo, lakini kama kipaji huna utaiongea na kuiandika lugha ya watu huku ukifuta maneno halisi na kubandika ya kwako yasiyo eleweka, huku ukipita ukijilabu kuwa shughuli unaiweza kumbe maji yamekupwa siku nyingi. Mola akuzidishie kipaji kwani lugha hizi tatu kiarabu,kiswahili na kiingereza wewe ni Kiongozi na sasa nakupa cheo cha kwetu “Nyakanga” baniani muuweni lakini haki yake mpeni.

  Salaam zimefika,sasa naomba nitimize wajibu,

  Kuhusu Balozi Iddi na kadhia ya kumnyang’anya shamba mke wa marehemu Said Iddi Bavuai,mimi sikushituka sana na hatua hii, ila nimehuzunika kupita kiasi kwa sababu haya niliyategemea kwa mfumo uliopo hapa kwetu kwa sasa,binafsi namjua vizuri sana Mzee Bavuai katika uhai wake tumewahi kuwa na vikao kadhaa vya kusalimiana tu ila alikuwa rafiki mkubwa wa mjomba wangu mara nyingi alikuwa akija kwetu, akituletea ndizi,nazi na chochote alichojaaliwa kupata huko shambani kwake akitugaia bure kwa sababu ya huruma yake na kwa kuwa hatukuwa na uwezo kama uliopo sasa kidogo, siku hizo ilikuwa za dhiki zaidi, leo ndio imechanganywa na dhulma juu yake.

  Serekali ya mapinduzi ya sasa chini ya ccm hapa Zanzibar imefurutu adabu.Leo inamnyanyasa mke wa marehemu Bavuai kwa kuwa hayupo hakuzimia ila amefariki dunia na harudi tena?hili shamba wakati wa uhai wake bavuai, hakukuwa na kiongozi mwenye nguvu za kumyanganya?kulikuwepo na Karume baba mtu,Jumbe,Mwinyi,Salmini,Wakili,Karume mtoto yaani Amani na sasa Sheni, kumezidi nini hata atokee makamu wa pili wa rais balozi iddi, ndio iwe wakti umefika wa kumdhulumu haki yake mjane aliyorithi kwa wazee wake kwa miaka yote hii au ghafla ndio kageuka Muarabu siku zote alikuwa Mmakonde mpaka ulipokwisha uchaguzi?

  Hili shamba sio la huyu hasimu yetu Muarabu huyu mjane wa mzee Bavuai, hili shamba ni mali ya watoto na wajukuu wa mzee Bavuai, ambae ni mwana mapinduzi na muasisi wa nchi hii aliyekuwa mstari wa mbele katika Mapinduzi mnayo jivunia leo kina balozi bila kuyajua,sasa mnapo fanya unyanganyi wenu, msisingizie kuwa mnayarudisha mikononi mwa Waafrika weusi watupu, mjue pia kuwa mnao wanyanyan’ga nao pia ni watoto na wajukuu Walio zaliwa na viongozi wenzenu walio tangulia, ambao nao mlifanana rangi yaani nyeusi tupu, lakini huwezi kwenda kuowa Mchina halafu ukatajia kizazi utakacho jaaliwa watakuwa Wamakunduchi watupu.naelewa ndio maana tuliwatukana Machotara wakati wa uchaguzi kwa sababu tulijua kuwa Waarabu hakuna tena na baba zao wengi wamesha tangulia katika haki lakini ni lazima niwaambie kweli kuwa kwa tabia hii mnayo kwenda nayo hatopona mtu hapa wala kizazi chake kwa sababu hakuna aliyekuwa hajazaa nje ya rangi yake sasa mtawatukana na kuwatuhumu hawa punda milia wakati makosa mnaendelea kuyatenda kama neno kosa linahusika.

  muda sina leo lakini nitarudi,

  Asante.

 7. SHAKUSH 06/12/2016 kwa 2:40 mu ·

  Bwana Mzeekondo. Sina budi kugeuza kilemb kuwa kofia na kuma mzoweya nae afurahi kuziba sehemuya umbo lake. Kwanza nakushukuru kunipa sifa ambayo sistahiki. Kiarabu nimezaliwa nacho, kingereza ni lugha niitumiayo katika masomo kuanzia class one hadi nilipofika nikitia tamati ngwe hii. Kiswahili ninakisoma tu. Huu ni mwaka wa 14 katika zoezi hilo. Natamani sana nifikiye kiwango chako.
  Ni kweli kuna uwezekano mkubwa Simba kufanya urafiki na Chui na Farasi na punda lakini kwa mandhar ya nje inachusha na kwa moyoni urafiki huo hauna uhakika. Kila mmoja huwa kafuata yake katika urafiki huo. Mwisho wa safari alodhibitiwa atatowa sababu ya kukubali kujiytupa katika mazingira yale.
  Hata unaona siku hizi watu tunatumia Solar kuziwasha barabara. Hili ni suluhisho la muda kwa sehemu ndogo tu. Huwezi ukatumia solar kuziwasha barabara zenye urefu usokisika. Umeme bora utabaki wa mafuta, maji au gas.
  Shukran bwana Mzeekondo. Uliitwa na ukaitika. Karibu tena tutumie zafarani kuandikia lakini wino utabaki kuwa ndio kivutio cha kudumu cha maandishi
  walakum jazil shukr wa ttaqdir.

 8. SHAKUSH 06/12/2016 kwa 2:49 mu ·

  Kilemba kumpa

 9. abuu7 06/12/2016 kwa 5:59 mu ·

  hii amri imetoka au imeaanza kwa lukuvi bara.sasa nawao wanaiga au ni amri kutoka bara.
  mimi nakwambieni hawo wote hapa zenji mnawowawita mawaziri basi tunajidanganya.
  tunasema tunae rais kwa kweli rais yuko bara ni makufuli. tunasema tunae waziri wa arrzi wakati waziri wa arzi yuko bara nae ni Lukuvi. kwa kweli hawa watu hawana nguvu yoyote ya kuendesha nchi. tunapotoshwa kiakili . kuwa tuna viongozi. sasa mwananchi ukiona waziri yoyote hapa zenji .basi kwanza tizama nani kwa upande wa bara ili upate kujuwa waziri hassa.
  Kwa mfano
  hii taifisha taifisha kaanza lukuvi.halafu ndio kunguru mataru ndio wanafatiliya .la ajabu utaona hijabu kubwa kichwani utafikiriya ya kujistiri kumbe kichwani kajaaa machawa

 10. SHAKUSH 06/12/2016 kwa 6:37 mu ·

  Bwana Abuu 7 na Bwana Mzeekondo
  Ni kawaida ya abiriya kumfuata conductor na Conductor kumfata Dereva. Hii ni system ya usafiri uivyo. Conductor hawezi kumaster udereva wote na ndio ukaona hutumiya kibao kama handbreak. Hayo ni maelezo ya dereva kuwa atumiye kibao kuikinga gari isirudi nyuma kwenye mlima. Hawezi conductor kupinga uwamuzi wa dereva na akithubutu hukiona cha moto. Basi kuna abiria wengine wanafahamu kutumiya kibao ni upuuzi kwani gari yaweza kuchupa kibao na ikaanguka. Lakini dereva kasema wacha tutumie kibao kama handbreak, kalafati tofauti na material ya chombo na zafarani kama wino. Safari njema kwa idhin ya Aalah.

 11. SHAKUSH 06/12/2016 kwa 9:34 mu ·

  Allah

 12. MAWENI 06/12/2016 kwa 10:23 um ·

  Hawa viongozi wa ccm huku Zanzibar si cho chote isipo ni chombo killo dhaminiwa na mfumo wa nyuma ya paziya ulioko bara ili kuwakandamiza Wazanzibari na kuwadhulumu haki zao.
  Hawana uchungu na uislamu nchi yao wala wananchi wenzao.

 13. SHAKUSH 07/12/2016 kwa 2:35 mu ·

  Bwana Maweni. Tausi kawekewa mtego na akanasa. Baada ya kunasa alianza kumuimbiya mtegaji na kumsifiya ili mtegaji afunguwe mtego tausi awe huru. Haikusaidiya kwani mtegaaji alizifurahiya nyimbo na sifa hizo. Tausi alibadilisha mbinu akaanz kulia na na kuomboleza. Lakini wapi mtegaji alianza kumtusi huyu tausi, kiumbe cha Mungu ndani ya mtego. Tausi akaamuwa kutuma madege yalosoma ili wawakumbushe tausi wengine hatari ya mtego ili watafute njia. Wapi?. Fikra hii iligonga mwamba na madege yalosoma yalikamatwa yote yakawekwa katika tundu la chuma na wakabaki humo. Tausi akaamuwa. Usiku usiku ikawa anaanza kuutafuna kidogokidogo ule mtego. Ni kibaru kipevu na kilichukuwa muda mrefu na hata mdomo wa tausi ulipata athari na mchubuko. Waarabua husema, Ajitahidiye hufanikiwa na apandae huvuna.” Mwishowe tausi alipata upenyo na kutoka. Tausi huyo alianza mikakati ya kuwasaidiya madege yalowekwa katika tundu la chuma ili alipe ihsani.
  Shikamoo Mzeekondo.

 14. SHAKUSH 07/12/2016 kwa 8:28 mu ·

  Nawaombeya safari njema kwa Allah. Mtumie kalafati inayofaa, mtumiye wino badala ya zafarani na ikibidi kuumega mtego kwa utaratibu.

 15. zamko 07/12/2016 kwa 9:31 um ·

  @Shawnjnr24

  Nikweli sio vizuri kumkejeli mtu au kumfananisha Binadaamu mwenzio na Mnyama. Lakini Hii picha ya Huyu Mzee anajepaka Uzanzibari na Kupita akipora pora Mali za Watu na Kuziuza Kwa Washenzi Wenzanke. Nafikiri Ni kibaya Zaidi kuliko hata hivo Kumfananisha mtu na Myama.

  @ Mohamed
  Suali lako Linaulizwa na Kila Mzanzibari aliezaliwa Zanzibar , kutoka Vijana na Wazee ambao Wanakumbuka Mapinduzi na Wana Mapinduzi. Huyu Sefu Ali iddi ametafutwa Ubini Wake Huko Kitope anakojipakazia kwamba Ndio Kwao. Lakini Bahati Mbaya Kila Mzee aliekulia Kitope au kuzaliwa ambae ana Rika yake au Rika Ya Juu yake Hawamjuwi Mtu Huyu katoka Wapi.

  Mimi Namfananisha Huyu Mzee na Yule JABU Mponda Wa 1900 , ambae alikuwa Ni Mtumwa alieingia kutoka Congo au Sudan Ile Iliojigawa. na Huyu Jabu Mpoda Aliwahi Kutunga Kitabu cha Kiswahili . Kwa Vitendo Vyake vya Kinyama na Kishenzi alivowafanyia Watu. Na alifungwa lakini kila alipotolewa alikuwa akijificha Misituni na kukamata wanawake au wanaume nakuwafanya vitendo viovu na mwisho kuwauwa.

  Kwahivo Huyu Mzee hajulikani asili yake Sio Unguja, Sio Pemba wala Sio Huko Tumbatu Kwa Prince Of Darkness Haji Omari Heri.

  @ Shakushi
  Hongera Kwa lugha ya Msamiati Uliotumia, mimi niliposoma maoni yako Kwanza Nilifikiri ni Legend wetu wa Kiswahili @ MzeeKondo. Lakini naona Amekuwachia Mirimo Wewe @ Shakushy na cc tutaanza kufaidika na Maoni yako Ya Swahili Literature.

  @ Wazalendo

  Huyu Bi Fauzia tayari ameshajibiwa hiyo barua Yako . Na ametukanwa kisawa sawa. Na Barua hio Kiswahili chake Sio Safi. Nafikiri Hawa Akina Ting Tong na Tanga Tang- Wamepeleka Kuchapishwa barua Aliojibiwa Bi Fauzi Huko Kwa Mabwana Zao Wanao Watumikia.

  Lamwisho nataka kusema. Allah SW ameshatuahidi malipo ya Matendo yetu Mazuri na Matendo yetu Mabaya huanza hapa hapa Duniani kabla mtu hajafukiwa kwenye Mwana Ndani.
  Na dalili moja ya Malipoa ya Mtu anaefanya Wema Kwa Jamii, wazee, wananchi wake au hata jirani. Basi hutakatishwa Kipaji chake na kutiwa NURU .. Na hata kama Mtu huyo atakuwa Mbaya wa Sura Vipi, basi Nuru yake ya matendo Mema humngarisha mtu huyo katika kipaji chake.

  Na Mtu anaefanya Mabaya kwa Wananchi wake, Wanawe, Jamii yake, Jirani au familia yake. Basi Mtu huyo hatakuwa ana Uzuri wa Kiasi gani , Basi Allah Hu utowa Nuru Uso wake na Akambadilisha Umbo lake likawa la kutisha.

  Hawa Watwana Wengine Wanaotutawala kwa Nguvu na kutuuzia kila kilichomo Ndani ya Visiwa Hivi. Wengine Wameanza kusinyaa. Na Wamebaki macho Kama TOGONYA. Wengine Ndio hao Tunawaona Katika Picha. Subhanallah, Astaghafirullah, Yarabbi-Tubu.alaina. Sura zao Wanatisha na hii nikutokana na Matendo yao Maovu Allah Anawabadilisha Sura zao na kuwa kama Mashetani.

  Tunachotakiwa nikumuomba Allah atujaalie Atupe Imani, Insaf, Huruma, Na Kinaa ya Nyozo zetu. Inshallah Allah Atatufikisha Katika Safari yetu Hii na Chombo Chetu Kiko katika Ukalafati Tena Wakuweka Nta, Usufi na Kukipaka Rangi pale tutakapomaliza Kukitowa Mbao Mbovu na kuweka Nzima.

  Inshallah Biidhinillah

 16. chatumpevu chatumpevu 08/12/2016 kwa 9:22 mu ·

  Ningewashauri wale wanaokaa kwenye baraza za CUF wasikae mikono mitupu , ukikaa nyoosha panga lako vzr kwenye mgongo na kipande cha nondo kwenye soksi. Kujihami ni lazima na ni haki kwa kila mtu. Kadhalika, mkae kimkakati kwa maana ya kuwa wengine ndani, wengine nje na muwe mnaangalia mtazamo wa ndege( bird eye view) kulia kushoto, mbele nyuma huku ukipiga stori na kahawa. Mazombi ni magaidi na maharamia wanaofadhiliwa na dola ( state sponsored )

 17. mzeekondo 08/12/2016 kwa 8:22 um ·

  Bwana Shakush na wana maskani wote.

  Nakuitikia “ya marhaba seyyid” mzee mwenzangu,na kama nilivyo ahidi kuwa nitarudi tena kikaoni basi Mola ameniruzuku wakti na naomba kuendelea na kadhia yetu, ya un’yan’ganyi anao fayiwa mjane wa al- marhum Mzee Bavuai hapa Zanzibar kwa sasa, na serekali hii tukufu ya mapinduzi iliyoasisiwa na kupindua utawala ulio kuwepo 1964 na kamati ya watu kumi na nne{commitee of 14} na Bavuai akiwa mmoja wao.

  Shakush nafikiri utakubaliana na mimi kuwa sisi binaadamu ni viumbe wa ajabu sana,uwezo wetu tulio tunukiwa na Muumba wa kuweza kuwa na akili,kufikiri,kujisitiri na kuamua tofauti na wanyama wenzetu wote{nasikia kisayansi sisi sote ni kaumu moja} au viumbe wengine hakujatusaidia sana katika kututofautisha na tembo na mjusi hata kidogo,tukejifunza kustaajabu na kushangaa mengi ya kawaida japo kuwa ni ya kutisha au kuhuzunisha lakini hatukupaswa kuwacha midomo wazi, kwa sababu tunafahamu vizuri kuwa, sisi sio viumbe wenye mioyo ya dhati iliyojaa mapenzi”huba” au huruma baina yetu japo siku moja au siku zote,ndio maana juu ya kuijua na kuisoma dini kila kukicha tulichojaaliwa kukijua ni kuzikariri tu aya zote, na hadithi za mitume lakini hakuna moja tunalo fahamu,juu ya kuutafsiri msahafu kwa karibu lugha zote za ulimwengu huu kama kiarabu hakipandi basi bado hakuna kulichoingia mioyoni mwetu seuze vichwani.

  Serekali ya mapinduzi ya Zanzibar SMZ inayopewa miongozo yake na chama cha mapinduzi cha Tanganyika CCM kwa makusudi hivi sasa, imeamua kuwagawa makundi mawili makubwa wananchi wake wa hapa kwetu,kundi la kwanza ni wapinzani,kundi hili ndio maadui wa nchi hii na taifa hili kwa ujumla,humu ndani ya kundi hili mmejazwa Waarabu{kama wapo} wapemba,machotara na yeyote anae shirikiana na kaumu ya watu hao,mtu huyu hata awe mweusi mtupu kama mimi basi nae sie mwenzetu.

  Kundi la pili ni la weusi watupu,hakuna ruhsa ndani ya kundi hili kuchanganya damu na kunguni yoyote yule ambae hajahusu bara hili la Afrika jeusi kwa asili na rangi,kundu hili ni lazima uwe muumini wa dhati wa serekali hii iliyopo kwa mabavu,mapinduzi yaliyofaywa kwa mabavu na muungano uliofanywa kwa mabavu, hakuna ruhsa ndani ya kundi hili, kuhoji uhalali wa chochote kinachofanywa kwa jina lolote, iwe la ccm,smz,st,mapinduzi au muungano,ndio maana hata huu uchafuzi wa marudio uliofanywa, na wizi wake uliotekelezwa baada ya amri za wakubwa, na kauli ya Jecha hakuna nae thubutu kukemea au kusema lile lililo wazi, kuwa HATUKUSHINDA na kwa mara ya tano, tume wanyima haki yao wananchi wa Zanzibar, na sio Maalim Seif Sharrif peke yake yeye amechaguliwa tu, sisi tumejikita katika kumkomoa Maalim siku zote, wakati kosa kubwa tunalo tenda na kulihalalisha ni ku’uathibu umati wa Muhammad unao ishi hapa Zanzibar na sio mtu mmoja.

  Kama utaangalia kwa makini utagundua kuwa tumevunja sehemu nyingi za biashara za watu tunao waita wapinzani,darajani,raha leo nk pia tume wafukuza makazini wengi na tunaajiri kwa kuangalia sura au vyama pamoja na rangi,Pemba tuna tawala kwa bakora au mitutu na kila siku tuna fanya uhamisho wa wale wote wakorofi wenye asili ya kisiwa hicho, waelekee huko au waache kazi,hivi naandika risala hii mtoto wa shangazi yangu kesha pelekwa huko, kosa hatukulijua siku za mwanzo baada ya kuulizana tukafahamu kuwa kwa kujificha kumbe alikuwa mpenzi wa cuf,pia upande wa baba yake ni watu wa mtambile baada ya shangazi yangu kunifahamisha hilo siku taka ushahidi zaidi nikajua kuwa mjomba wangu kesha bora aanze biashara mwisho watamfukuza tu huyu.

  Huu umekuwa msiba, kwani leo tumerudi kule kule tulikotoka, tumefika mahali ukihamishiwa Pemba imekuwa ni adhabu, na kwa nini iwe msiba au adhabu?kwa sababu sio siri kisiwa cha Pemba kiligeuzwa Guantanamo siku nyingi, tangu enzi za Mzee Karume na Aboud Jumbe, kisiwa hiki hakikupata bahati na watu wake, kwa makusudi hakukupelekwa maendeleo makubwa, na wananchi wake walipo amua kuyafuata maendeleo yalipo japo kidogo, sasa imekuwa kosa ni lazima warudi walikotoka, sisi ni nchi ngapi tofauti jamani?kuna Tanzania,Tanganyika,Zanzibar,Pemba,Unguja au Zanzibar peke yake ni lazima CCM mtueleze mnazitambua nchi ngapi kwa vitendo? sio maneno kwa sababu vitendo vyenu vitawasuta.

  Chuki na ubaguzi nimezungumzia sana hapa hatari zake kabla na baada ya uchaguzi,sasa tuna tawala kwa kuwagawa watu na kuwa dhulumu haki na mali zao,kwa visingizio vya SIASA hakuna siasa iliyojaa chuki na ubaguzi wa rangi,sisi tulikuwa mstari wa mbele wakati weusi walipo kuwa wakibaguliwa Afrika Kusini,tulisahau kuwa kubagua ni jadi yetu na unafiki, undumila kuwili ndio asili yetu,tuna yahalalisha vipi haya tunayo wafanyia wenzetu baada ya kuwavisha “lebo” au alama ya UARABU, UPEMBA au UPINZANI bila hofu,woga au kumuogopa MOLA.

  Mimi nilisema na kuamua awali kuwa sitoweza kuwa mwanachama wa chama hiki, ikiwa itanilazimu nikubaliane na mauwaji ya watu wasio na hatia,kuwekwa mahabusu au kufungwa ovyo watu wasio na hatia, kuendelea kuiba kura kila uchaguzi,kuwabagua watu kwa rangi,dini,kabila au waliko zaliwa kwa visingizo vya kulinda Mapinduzi,muungano nk.kuwaibia watu mali zao iwe viwanja,nyumba au mashamba kwa kosa la kutokipigia kura chama cha mapinduzi au kuwa muarabu.

  Visiwa hivi tumejivunia siku zote undugu wetu na ukarimu wetu,tumeowana kwa nguvu na kwa hiari ili tuchanganye damu,na damu hiyo iwe ndio kinga yetu siku za usoni, tusije tukadhuriana kama tulivyofanya wakati tunapindua 1964,kwa sababu tuliwauwa watu ovyo bila hatia, ujinga wetu ulitulazimisha kuwaona Waarabu wote ni maadui, hatukuchagua mtoto,mja mzito,mke au mume,mzima au kilema wote tuliwachinja kama kuku na kuwatia katika matanuri na kuwawasha moto, kama haya ndio tunaita mapinduzi, bora tutafute jina jingine, kwa sababu haya ndio yanayotutesa mpaka leo, tunauwana na kubaguana ovyo kila baada na kabla ya uchaguzi, kwa kuwa hatuja kubali kuwa hapa Tulikosea na kumuomba Mola Atusamehe NA KUWAOMBEA marehemu wote tuliowauwa bure kwa jina la MAPINDUZI.

  Hakuna ubaya katika kujirudi na kukubali ukweli,tusikazane kukataa siku zote hii sasa ni historia haiwezi kuwa ni kioo cha siku za usoni siku zote,tunatakiwa kujifunza kila zuri na kuliendeleza na kulikataa kila baya na kulikiuka,ndio maana nayachambua mapinduzi ubaya wake tuyajue, na kama kuna zuri nisaidieni kuyaanika kwa faida yetu sote,ndani ya chama cha mapinduzi kuna machotara tele, wengine mawaziri lakini hawa wamesafishwa kwa sasa, siku wakisubutu kukihama chama chetu au tukiwatuhumu usaliti basi na wao tutawanyan’ganya kila walichochuma,chotara ina tafsiri nyingi katika chama hiki lakini kwa nini tuwe na vigezo vya kibaguzi?

  Zanzibar ccm kama kutawala, itatawala kwa bunduki mpaka kiama kama tutakuwa hai, haitokuwa kwa ridhaa ya watu wake kwa sababu kila tukizidisha ubaguzi na chuki dhidi ya watu wetu ndio wanavyozidi kuhama na kuichukia ccm sasa nani anadhani hapa kutakuwa na uchaguzi ulio huru na haki siku za usoni?ni lazima tujuwe pia hakuna utawala wa milele zaidi ya ule wa Mola wetu tunajidanganya bure kudhani bunduki peke yake inatosha kutuweka madarakani siku zote kama ingelikuwa tunaamini hivyo sasa tunafanya uchaguzi wa nini?si tutoke tu na bunduki,vifaru,panga nk kila baada ya miaka mitano tuwaonyeshe watu wetu kuwa bado zana zipo na wao watatulia,tunawahangaishia nini kupiga kura?

  Tunapo anza kumuadhiri mke wa marehemu Bavuai kwa haki na mali yake,tuwe tayari pia kwenda kumuadhiri na mke wa Marehemu Mzee Karume na Waheshimiwa wote walio tangulia katika haki,kwa sababu kila mmoja wao aliowa Muarabu iwe kwa hiari au nguvu, hakuna alie kosa,wengine waliowa wawili wawili pamoja na wahindi muradii awe mweupe maana kuna wahindi weusi hao sio, Marehemu mzee Thabit Kombo na Said Washoto “to name the few” wao waliongeza upande huo, sasa vizazi vyao vipo na wote wana mashamba na mali,Balozi Seif Iddi umekuja juzi Waarabu wamekwisha na hawapo tena,walio salia wengi machotara ndio maana umeongeza mke wa pili mweupe {maji ya kunde}, lakini sio Muarabu yeye mruguru,alikuwa mke wa marehemu meja Mahmoud tunamjua vizuri muhimu mweupe au sio?

  Sasa chuki za Waarabu na machotara umeziweka kooni kwa kuwa wewe hukupata? hii itakuwa hadithi ya zabibu chungu/mbovu kwa kuwa wewe huna? tafadhali huu ubaguzi wako ulio uchopeka katika chama na serekali sema nao utatumaliza sote na wewe ukiwemo,nchi kama watu serekali hawaitaki sio dhambi duniani ndio maana ya kufanya uchaguzi sikutarajii uyajue haya kwa kuwa hata wewe Mahonda wamekukataa lakini leo ni makamo wa rais wa pili na muwakilishi wao,only in Zanzibar all you do is possible, for the time being no matter how stupid or crazy it sounds.

  Onyo langu la leo kwetu, ni lazima tuyakatae haya mchana,leo mke wa Bavuai tunacheka,kesho mjane wa Muheshimiwa mwingine na mwingine na kesho kutwa nikja kukaa mimi kwenye kiti cha umakamo basi NITASUBIRI balozi kesha tangulia kwenye HAKI kama ataanza yeye safari, basi na mimi namnyan’ganya shamba mkewe kwa jina la mapinduzi,nani alidhani balozi atathubu kumuita mke wa hayati Bavuai DHALIMU?sisi imekuwa tunajivunia mapinduzi lakini hatuwataki waliopindua na familia zao?hivi sasa rais mstaafu Karume anaonekana mpinzani,kisa hapendi ubaguzi wala chuki ndio maana kaowa Muarabu kumaliza mzizi wa fitina, lakini hapo hapo tumemkumbatia MDOGO WAKE na kumpa uwaziri,nae pia mkewe Muarabu tena wa Oman, baniani wabaya viatu vyao murua.

  Acheni hizi mtawadan’ganya hao hao mliosoma nao chini ya miembe,kizazi cha leo wanapendana na hawataki fitina wala chuki zenu za kale,ikiwezekana kufeni nazo, msiwarithise watoto wenu,mtawapa shida huko waendeko duniani hizi karne mpya.

  Naomba radhi kwa makosa ya uchapaji tu, sikupata muda wa kusahihisha ,mengine yote niliyo andika ni maoni yangu na nasimama nayo mpaka siku ya mwisho.

  Asanteni.

Comments are now closed for this article.