Nani wa kutatua mzozo wa CUF

Written by  //  06/04/2017  //  Habari  //  Maoni 7

Baadhi ya wananchi wametowa Wito wa kufanya sulhu juu ya mgogoro ndani ya Chama Cha Wananchi CUF.

Nami niungane na wale wote wanaona wakati umefika kwa pande mbili zinazovutana kukaa pamoja na kufanya sulhu itakayozika sintofahamu iliyopo.

Nani wa kusimamia sulhu hii? Nitajaribu kuangalia baadhi ya wadau wakubwa wa kutuo mchango wao.

Msajili wa Vyama: anaamini kuwa kupevuka kwa mgogoro ndani ya CUF kilitokana na maamuzi ya Msajili wa Vyama vya siasa kutengua maamuzi na kuthibitisha kuwa bado Prof Lipumba ni Mwenyekiti halali wa CUF. Hivyo basi Msajili ndio mdau mkuu wa kusimamia sulhu hii.

Baraza la vyama vya Siasa: Ingawa majukumu hasa ya chombo hichi sijafahamu, Kwavile linashirikisha vyama vyote ni vyema kusimamia sulhu baina ya pande mbili.

Prof Lipumba: tukubaliane kuwa licha ya kuwa prof Lipumba ndio mchochezi wa mgogoro huu na juhudi zake za kutaka kutatua kwa njia za mazungumzo bado anatakiwa kufanya zaidi kwamba yuko tayari wala sio kufanya usanii au usaliti.

Maalim Seif: kwa upande wake naye amewekwa katikati kwa vile mzozo ulipoanza chama hakikuwa na Makamo Mwenyekiti. Anatakiwa asome alama za nyakati na kuangalia mustakbali mpana kwa chama, nafasi yake,na wananchi.

Taasisi nyengine: niwakati kwa taasisi nyengine za kupigania haki,demokrasia, au sheria kujitokeza kuupatia sulhu mzozo huu.

Mafanikio ya demokrasia yatapatikana tutakapokuwa na ustawi wa chama imara ambacho kimenawiri pande zote za muungano

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 7 katika "Nani wa kutatua mzozo wa CUF"

 1. Smart 06/04/2017 kwa 8:18 mu ·

  Mgogoro wa CUF Ulivyoibua Mvurugano Katika Uchaguzi wa Wabunge ELA…..

  IWakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wakipatikana juzi usiku, suala la wawakilishi wa upinzani limetawaliwa na hali ya kutoeleweka, huku ikibainika rasmi kuwepo kwa CUF “A” na CUF “B”.

  Kikao cha juzi kilichotawaliwa na mjadala wa kikanuni kuhusu wawakilishi wa Chadema na CUF, kiliweka rekodi ya kuchukua muda mrefu baada ya kumalizika saa 7:00 usiku kikikipiku kikao kilichojadili sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.

  Bunge lilichagua wanachama sita wa CCM kuingia Bunge la Afrika Mashariki, pamoja na mmoja kutoka CUF, ambaye amezua mjadala baada ya jina lake kukubaliwa na msimamizi wa uchaguzi licha ya kusainiwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho badala ya katibu mkuu ambaye aliwasilisha jina jingine.

  Waliopitishwa ni Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe na Alhaj Adam Kimbisa kutoka CCM, wakati Habib Mnyaa, aliyekuwa amevuliwa uanachama na CUF, alichaguliwa pia kuingia kwenye chombo hicho.

  Hata hivyo, wanachama wawili walioteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Eala, Ezekiah Wenje, aliyepata kura 124 za ndiyo na 174 za hapana, na Lawrence Masha, aliyepata kura 124 za ndiyo na 198 za hapana, hawajaingia kwenye chombo hicho, kitu ambacho kimeifanya Chadema kuamua kwenda mahakamani.

  Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema jana kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni batili kutokana na taratibu kutofuatwa.

  Pia, hoja ya kuwepo kwa CUF A na B iliyozungumziwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo imeibua mvurugano kwa chama hicho ambacho kimekuwa na mgogoro na mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba tangu alipojiuzulu mwaka juzi na kujirejesha mwaka jana.

  CUF na pande mbili
  Katika uchaguzi huo uliofanyika bungeni mjini Dodoma, CUF ilipeleka wagombea wanne baada ya upande wa Profesa Lipumba kutuma majina matatu huku upande wa Maalim Seif ukipeleka jina moja.

  Majina yaliyopelekwa na upande wa Profesa Lipumba ni Mnyaa, Thomas Malima na Sonia Magogo huku upande wa Maalim Seif ukipeleka jina la Twaha Taslima.

  Kitendo cha Dk Kashililah kutangaza kukubali majina ya pande zote mbili, kilifanya wabunge waanze kuhoji sababu za ofisi ya Bunge kukubali kupokea majina ambayo hayajasainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

  Akihoji suala hilo, Lissu alisoma barua ambayo ofisi ya Bunge ilimwandikia Maalim Seif kuthibitisha kupokea jina la Taslima na kuandika kasoro ambazo zilionekana katika fomu, akisema huo ni uthibitisho kuwa Maalim Seif ndiye katibu wa chama hicho.

  Alihoji sababu za kupokea fomu za upande mwingine wakati Maalim Seif yupo. Spika John Ndugai alisema hana taarifa za mawasiliano hayo na hivyo kumtaka katibu atoe maelezo.

  “Nafikiri anachokisoma (Lissu) ni sahihi na tuliandika. Msingi wa andiko letu ulitokana na barua ya tarehe 28 Machi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema Dk Kashililah wakati akitoa maelezo.

  “Hatukuviandikia vyama kuviomba, tulitoa GN 376, vyama viliandika vikaomba. Mimi sikuvitambua, aliyevitambua vyama ni mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ninayo orodha ya CUF “A” wamewasilisha kupitia kwa naibu katibu mkuu, na CUF “B” kupitia kwa katibu mkuu.

  “Mheshimiwa Spika ni vizuri tuelewane. Katika barua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndipo viongozi wawili wa CUF wanapokutana na wala si ofisi ya msimamizi wa uchaguzi.

  “Mimi nieleze wazi. Kwani aliyepeleka jina la Mnyaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni nani? Na aliyepeleka jina la Taslima ni nani? Sasa mbona wote wameleta?”

  Hivi karibuni Profesa Lipumba alitangaza kumteua Sakaya kukaimu nafasi hiyo, akisema Maalim Seif hatii maagizo. Kwa mujibu wa katiba ya CUF, katibu mkuu huchaguliwa na mkutano mkuu wa chama.

  Akieleza utaratibu wa kuwathibitisha wagombea wa Eala, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Ramadhani Kailima alisema walipokea majina ya wagombea kutoka vyama vya siasa na kwa suala la CUF hawajui kuhusu mgogoro unaoendelea.

  “Sisi hatupitishi majina ya wag- ombea. Soma taarifa ya Spika kwenye GN (Gazeti la Serikali). Kazi yetu ni kuthibitisha wagombea. Mimi sijui kama kuna mgogoro CUF. Tena andika kwa wino mweusi kabisa,” alisema Kailima.

  “Sifa ya mtu kugombea ubunge ni lazima atokane na chama cha siasa na ni lazima awe raia wa Tanzania. Sasa kama amedhaminiwa na Maalim Seif au Lipumba, sisi hatujui kama kuna mgogoro.

  “Mwenye jukumu la kusajili chama ni Msajili wa Vyama vya Siasa na akishasajili anawasiliana na taasisi nyingine. Kwa hiyo sisi tunaangalia uongozi alioutambua. Nec inaangalia sifa ya mtu kuwa mbunge, vyama vya siasa kama CCM, CUF Chadema ndiyo wanatuletea majina,” alisema Kailima.

  Alipoulizwa kuhusu katibu aliyetakiwa kutia saini za wagombea wa CUF, Kailima alisema Nec haifungwi na mgogoro uliopo.

  “Tume haifungwi, tunawasiliana na mwenyekiti au katibu. Mwenyekiti wa chama anawasiliana na mwenyekiti wa Tume na katibu mkuu anawasiliana na mkurugenzi wa uchaguzi,” alisema.

  “Ninyi si mliandika kuwa Magdalena Sakaya ameteuliwa kuwa kaimu katibu mkuu wa CUF na msajili akaridhia? Sisi tunawasiliana na huyo huyo pia.

  “Lipumba anawasiliana na mwenyekiti wa Tume na Maalim Seif anawasiliana na mimi mkurugenzi.”

  Akizungumzia kuhusu wagombea watatu wa CUF, Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua, alisema alitia saini fomu zao kama kaimu katibu mkuu.

  “Majina yalipelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuthibitishwa kisha yakapelekwa Idara ya Uhamiaji kuthibitisha uraia ndipo yakapelekwa kwa katibu wa Bunge,” alisema Sakaya.

  “Fomu zao nilitia saini mimi kama kaimu katibu mkuu kwa sababu katiba yetu inasema kama katibu mkuu hayupo, nafasi yake inakaimiwa na naibu katibu mkuu.”

 2. Smart 06/04/2017 kwa 8:20 mu ·

  Mbunge ataka Zanzibar ipewe fedha na Tanzania Bara ili ilipe Deni la umeme

  Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Jaku Hashimu Ayoub ametaka makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali za Serikali yapelekwe Zanzibar ili kulipia deni la umeme.

  Jaku alisema hayo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, ambapo alisema kuna kodi zinazolipwa Tanzania Bara, lakini hazipelekwi Zanzibar kwa ajili ya kusaidia maendeleo ikiwamo kulipia deni hilo.

  Mbunge aliyedai kuwa na ushahidi juu ya kauli yake hiyo na kwamba yupo tayari kuutoa, alisema fedha hizo ni muhimu zikapelekwa ili zisaidie ulipaji wa malimbikizo ya deni la umeme.

  Machi 9, mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilitangaza kuikatia umeme Zanzibar kutokana na limbikizo la deni la zaidi ya Sh275.38 bilioni.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema wameipa siku 14 kuhakikisha kuwa inalipa deni hilo. Hata hivyo, siku chache baadaye Tanesco ilitangaza kulipwa Sh10 bilioni kama malipo ya awali ili isikate umeme visiwani humo.

  Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Magomeni (CCM), Jamal Kassim Ali alitaka kujua iwapo Serikali haioni haja ya kodi ya mishahara (paye) kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) isikusanywe visiwani humo kwa ajili ya kusukuma maendeleo.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mapato sura ya 66, kifungu cha 4(a) na (b), kodi za kampuni ni za Muungano na zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Pia, alisema hata kampuni ambazo zimesajiliwa Tanzania Bara lakini zinafanya kazi Zanzibar, kodi zake zinakusanywa Bara.

  Naibu waziri alisema iwapo kampuni itakuwa imesajiliwa Zanzibar na ikawa na matawi Tanzania Bara inatakiwa kulipa kodi yake Zanzibar.

 3. Papax 06/04/2017 kwa 1:46 um ·

  Hapa hapahitaji suluhu, kwakua uzembe ulifanya na kambi ya maalim kwa makusudi, ilionekana wazi pr, kajiuzuli , chama kilikuwa kikae na kumjibu, lakini walizarau, kama kawaida yao kujifanya wajuaji, sasa wache waisome namba na tunajua wazi maalim, hamuwezi pr,lipumba, lipumba ni mshindi daima, , sasa mungu amekuonsheni kuwa ndani ya cuf, kulikuwa na kundi kubwa la wanafiki ndio maana mungu haja kupeni madaraka kwa miongomiwili tangu urudi mfumo wa vyama vingi

 4. Ashakh (Kiongozi) 06/04/2017 kwa 3:13 um ·

  Pia nayo hiyo ni miongoni mwa sulhu. Ikiwa kilikuwa na Wanafiki ndio kutumia platform hii kusafiana nia na kuendelea umoja wao.

  Lengo la sulhu ni kufuta mabaya yote na kupiga mstari wa kwenda mbele

 5. Abdul Zakinthos 06/04/2017 kwa 9:47 um ·

  suluhu ni Mahakama msiwe na kiherehere

  Maalim alisema Kesi ipo mahakamani- asa kitakachoamuliwa mahakamani watakiangalia kisa wa kukata rufaa atakata kisha ndio kutambulika

  UNAFIK WA TUME NI HAPO
  wakatti wa uchaguzi huangalia wagombea wote wakaweka pingamizi lakkini inapokuja kuuwa chama hukubali kinyume cha sheria

  Upumbavu huu ndio maana tukakata vyama vya siasa kuchaguliwa Bara

 6. Ashakh (Kiongozi) 07/04/2017 kwa 7:12 mu ·

  Abdul
  Soma alama za nyakati.

  Kesi zaidi ya miezi 6 ndio kwanza inatajwa ikipangiwa date. Fikiria muda gani itachukuwa?

  Kumbuka mwakani ni wakati wa uchaguzi mkuu wa chama.

 7. MAWENI 08/04/2017 kwa 10:33 mu ·

  Lupumba aliendewa na kila aina ya watu wanao itakiya wame kafu na mustakbali wa harakati za upinzani. Lakini aligoma katu , kubadilisha msimano wake wa kuji uzulu. Matokeo ya uchaguzi mkuu yalionesha kuwa wananchi wa imani na upinzani ; kwa lengo la kuingowa ccm madarakani.
  La msingi kwa chama ni kufuata kanuni za uwendeshaji wake kwa kila kitu. Suluhu ni kheir ; lakini, lakini katiba iyangaliwe. Ila itakuwa ndio mtindo. CCM uhai wake na huwo ukoloni wao ulioko Zanzibar utakoma ikiwa ccm itashidwa Zanzibar. Hivyo mbinu za hali ya juu wana tumia kuwagawa wapinzani kwa kuwatumia baadhi ya wanachama walio dhaifu . Wadogo kwa wakubwa.
  Tuseme suluhu ime patikana sidhani kuwa umma wa cuf , hasa ZNZ , Watakuwa na imani na proffessor kama hapo mwanzo. kucheleweshwa kusikiliza kesi ni moja ya mikakati ya kudumisha mgogoro.
  Lupumba ikiwa ana hamu bado ya kuongoza chama cha kisiasa; aunde chaka asajili. Hapo atajipima vizuri.
  HUYU LIPUMBA NI QUISLING ( coloborator).
  Watautumia ugomvi huu (wa kutengenezwa) ; ili , Jambo la msingi ambalo ni knyimwa wa Zanzibari haki yao 20/10/2015 , lisi suluhishwe. Watajidai ( wakoloni wetu) kuwa hatuna wakuzungumza nae. Na kuwa ili mtu aongoze sirikali ni lazima awe mwanacha alie teuliwa na chama chake.

Comments are now closed for this article.