Msaada unahitajika

Written by  //  12/10/2016  //  Matangazo, Habari  //  Maoni 28

Uamsho korti

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu na wenzao zaidi ya 50 wapo gereza ni Segerea Dar es salaam kwa zaidi ya miaka mitatu sasa lakini familia zao wake zao watoto wao wapo majumbani mwao hapa Unguja wa nahitaji msaada wangu mimi na wewe ndugu yangu.

Tunapaswa kama waislamu kuzisaidia hizo familia kwa hali na mali ingawa kiasi chochote cha fedha tutakachotoa hakiwezi kupunguza wala kuondosha maumivu walionayo kwa familia hizi kuwa kosa waume zao na baba zao muda wote lakini angalau tu wasaidie kwa kile kilicho kwenye uwezo wetu na yale ambayo hatuna uwezo nayo basi tumuombe Allah a wafanye wepesi. Shame ndugu zetu tuzisaidie hizi familia unapotoa fedha yako hata kama ni elfu moja kumbuka hiyo ni sadaka yako kwani baadhi ya hao Masheikh wanalea watoto mayatima majumbani mwao na kwa sasa wanahitaji msaada wangu mimi na wewe. Tafadhali tuma fedha zako kupitia mzalendo.net kupitia paypal na ref ya mchango wako andika uamsho.

Kwa wale ambao watapenda kutuma michango yao kwa TIGO PESA nambari ya simu ni 0656668457.

Ahsanteni.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 28 katika "Msaada unahitajika"

 1. AHLAN AIRAB 12/10/2016 kwa 5:20 mu ·

  Mwenyezi Mungu IN SHAA ALLAH atuteletee heri yasije yakatufika ya Somali na Mashehe

 2. MichipukoSiodil 12/10/2016 kwa 5:52 mu ·

  Allwah Ataleta Rehema zake tuamini Mungu kwanza mengine baadae kwani ukimtegeema baba atakufa mama atakufa na mwengine yoyote atakufa Bali Mungu Yuhai Daima

 3. Wamtambwe 12/10/2016 kwa 7:03 mu ·

  Tuwekee Nr ya Tigo ya kuchangia hizo pesa

 4. popote 12/10/2016 kwa 8:15 mu ·

  Hakika Dhulma Haidumu Na In Sha Allah….Allah Atatuongoa Na Rehma Yake Itatufikia Kwa Kila Anochukiwa Na Kitendo Cha Kuzalilishwa Kwa Mashekhe na Waislam kwa Ujumla.

 5. Joti 12/10/2016 kwa 9:24 mu ·

  Wewe @michipuko wacha uccm wako huo, kama hujui dini wala tawhiyd nyamaza kimya kwani ulisikia watu kuwategemea wazazi wao ndio yamaanisha hawamtegemei Allaah!

  Umesikia wapi Allaah akaja na mchele na kitoweo nyumbani? Kila kitu kina sababu yake na sababu ya maisha ya familia ni wazazi. Hebu nawe usifanye kazi mtegemee Allaah akuruzuku bila ya kazi uone mambo yatakuaje.

  Wewe kama hutaki kuchangia kwa kuwa hao mashekh wamewekwa ndani na ccm na hilo limekufurahisha kwa kuwa limefanywa na uwapendao basi usichangie, wala usipotoshe watu kwa itikadi yako mbovu.

  Admini tuwekee wazi jinsi ya kufikisha misaada yetu tafadhali.

 6. SAFUWAN MOHD SAFWAN. 12/10/2016 kwa 9:55 mu ·

  @nd yangu Joti huyo mwangalie tu inaoneshea laana za hawo wazazi wake zinamsulubu .huyo michipuko.anafurahia huyo hana kheri anayowatakia wenziwe ni fitna na ubaguzi ndio jadi yake .ila mm namuombea hwenda mungu akamuongoa akaona njia ya kheir inshaallah .ila namwambia ikiwa kweli ni muislam asome hadithi za mtume.zinazosema kuhusu muislam juu ya muislam mwenzie .

 7. Fuad 12/10/2016 kwa 10:19 mu ·

  Wewe MichipukoSiodil hujaambiwa utoe hutaki kutoa nyamaza kimya kwakuwa wewe humjui Mungu ndio maana ukasema hivyo sote tutakufa sijui umekusudia nini mtu wewe

 8. MichipukoSiodil 12/10/2016 kwa 10:58 mu ·

  Sasa Ndg Zanguni kwa nini mnausemea moyo wangu ? Nilihokisema ndo ambacho ninakiamini sasa habar ya kuchangia na kutokuchangia hiyo ni mimi hiyari yangu nacww pia naamini kuwa unahiyari yako

 9. huzurungi 12/10/2016 kwa 11:24 mu ·

  Assalamu alaykum kiufupiii waislamu tujitahidin kuchangiaa waislamu wenzetuu Allah atatulipaaa kheri NA Alla anasema ktk suratul Zilzalah”aya7had8atakae Fanya kher atalipwa hatakama kias chacjembe ya mchanga nauovu vilevile atalipwaaa.NA tunaambiwa waislamu tusaidiane kwa mambo mazur Siokusaidiana et ndobesti wake rafki yake Ati anampa chumba au gari au vespaa akapakie au amtie mwanamke kwa ZINAAA ah haya yote madhambi makubwaa hebu tutumien nafasi tusaidien waislamu wenzetuuu. Hatujui link tutaondokaa au nan anajua kesho ataamkaa asemeee!

 10. Wamtambwe 12/10/2016 kwa 11:30 mu ·

  @Adnministrator
  Weka Nr ya simu Tigo wengine tuko nje ya Nchi tuchangie

 11. Salim nassor 12/10/2016 kwa 11:32 mu ·

  Type njia ya kutuma

 12. Joti 12/10/2016 kwa 11:32 mu ·

  Admini naomba hili suala la mchango lisiwe mara moja tu bali liwe la kila mwenzi, kwani mahitaji ya familia ni ya kila siku.

  Twamuomba Allaah ajaalie watoke haraka.

 13. MichipukoSiodil 12/10/2016 kwa 12:25 um ·

  Ila pia usijekuwa Mradi wa kujinufaisha wewe huu pesa zifike kwa walengwa

 14. Fuad 12/10/2016 kwa 12:27 um ·

  Ulichoongea @ Michipuko kina maana kumbe kuna wakati unaakili Icho Admni cha msingi lazima tujuwe mapato na matumizi na wahusika walopokea tutajiwe

 15. Joti 12/10/2016 kwa 12:33 um ·

  Sahihi kabisa @MichipukoSiodili kwani wengi hutumia njia kama hizi kudhulumu wachangiaji na kujinufaisha matumbo yao kwa kutumia kivuli cha Uwamsho na majanga mengine yanayotokea

 16. ukwelippt 12/10/2016 kwa 1:32 um ·

  INSHAAA ALLAH TUKO TAYARI KWA HALI NA MALI KUWACHANGIA MASHEKHE WETU
  kwani ALLAH ANAWASIFU WENYE KUCHANGIA KWA KUSEMA.

  وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا

  “Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.”

  na hakuna dhambi mtoto kumtegemea Baba ake( kuwa ni sababu ya rizki zake) mpaka ajiweze madam sio kama kule kumtegemea kwa Ibada( kumuabudu)

  Na yeyote asiye kuwa Imani akidhani pesa yake italiwa basi atulie( ila pesa ni dhamana kwa anaechangisha)

  ALLAH AWATOE MASHEIKH WETU KIFUNGONI, KWANI HAKUNA JAMBO AMBALO LIMEWAKERA ZAIDI WANZANZIBAR KULIKO KUVUNJIWA HESHMA MASHEKHE WAO.

  LAKINI ONE DAY KITANUKA INSHAA ALLAH.

 17. Joti 12/10/2016 kwa 1:57 um ·

  Naona sasa mzalendo net hamko sawa kiufundi tayari jina langu la uchangiaji (JOTI) limeweza kutumiwa na mwengine bila ya idhni yangu.

  Hii inaonesha kuna matatizo ya kiufundi system kuweza kukubali jina moja kutumiwa na watu tofauti. Kuweni makini kwa hilo la sio hivyo litaleta mashaka humu.

  Comment ilokuja kwa jina la JOTI kabla ya hii sikuandika mimi wala siwezi kumuunga mkono mtu mwenye mawazo finyu kama @michipuko.

  Hili lifuatilieni kwa haraka.

 18. Joti 12/10/2016 kwa 2:27 um ·

  Hata ukitazama comment hio utaona tofauti ya maneno yaliokuwemo humo na comments zangu zilizotangulia.

  Iweje mimi nihimize kudumishwa michango na wala yasiwe ya mpito halafu nianze kuwakatisha watu tamaa ya kuwatia wasiwasi ya michango yao kutokufika mahala palipokusudiwa!

  Hata makala hii tuichangiayo hivi sasa natarajia imezalika kutokana na comment yangu katika mada iliokuwa na kichwa kisemacho:
  Must read : Viongozi na dhamana walizopewa – kisa cha Sayyidna Omar Bin Khattab
  Written by Mrfroasty (Ufundi) // 09/10/2016 // Makala/Tahariri //

  Nilicomment kwa kusema:

  Joti 10/10/2016 kwa 7:19 mu · Jibu
  Maneno matupu hayawasaidii kitu mashekhe zetu wala familia zao kama sisi ni wakweli kwa tunayoyasema basi tuweke namna ya kuchangia familia za mashekh sio porojo lisilo maana.
  MKONO MTUPU HAURAMBWI. Mwisho wa nukuu.

  Yaonesha comment hio imeandikwa na @michipuko na lengo lake ni kuwarudisha wachangiaji wasichangie na hio ni furaha kwake mashekh wateseke wao na familia zao.

  HASBUNALLAAHU WA NIEMALWAKIYL

 19. Fuad 12/10/2016 kwa 2:45 um ·

  michipuko ikiwa hutaki kusaidia usisaidie na ikiwa unataka kusaidia wapelekee mwenyeo au mpe mtu wako apeleke sio unawakashifu watu kuwa wananufaisha matumbo yao usimfikirie mtu kabla hujamuona huyo muhusika anaepokea wewe michipuko huna nia nzuri ndio maana unatoa maneno yasiokuwa na maana Mungu akuhidi na atuhidi na sisi na vizazi vyetu.

 20. ahmed 12/10/2016 kwa 4:37 um ·

  Kuzisaidia familia za wenzetu wanaoteseka kwa miaka bila ya kuhukumiwa ni wajib wetu sisi wazanzibari na kwa ujumla waislamu wote, ndani na nje ya Tanzania.Lakini isiwe msaada wa vitu tuu bali kwa kupaza sauti kila panapo kuwa na mkusanyiko wetu ili sauti zetu zisikike kwa wahusika na walionje.Ukimya ndio unawaponza hawa wazee na ndugu zetu.

 21. SAFUWAN MOHD SAFWAN. 12/10/2016 kwa 6:33 um ·

  Mm nimesema na nilitoa koment moja kumuelezea huyu mtu anaeitwa michepuko .huyu jamaa kwakweli ni mmoja ktk watu fitna sana .na ktk dini kuna aya isemayo fitna ashaaduminalkatil. Huyu nathubutu kusema ni sawa na balozi mkaazii.hawapendi maulamaa hata kidogo .nimesoma koment zake nyingi huyu mtu .kwanza ni m’baguzi hatari na anachuki binafsi na maalim na masheikh .hasa wa muamsho .yuko na mwenzake mmoja .nadhani munamjua wanaukumbi .hawa ni bora ukutane na simba hwenda ukanisurika kuliko watu hawa .ila wakae wakijua inshaallah karibu yataisha haya.

 22. Bin Rajab 12/10/2016 kwa 9:42 um ·

  Kama inazekana mchango huu uwe na meter ya kuhisabu pesa zilizo ingia.
  On the front page below mchango wa mtandao wa Mzalendo.

  MIMI NAUGA MKONO Mchango mfululizo tutowe kila mwezi kwa uwezo wako.

  Dhulma ina mwisho.

  Shukran

 23. MKOMBE 13/10/2016 kwa 10:04 mu ·

  Uzoefu unaonyesha kuwa hata wale waliokuwa wanawatembelea kuwapa faraj. chakula, nguo, wote walijumuishwa nao katika mkumbo wa pili na mpaka leo wko gerezani.Tutahakikisha vipi usalama wetu na kujumuika ” kunyia ndooni/”?

  Ukweli umma wa kiislamu unaonekana wazi umewasahau na hakuna mtu anaejali zaidi ya unafiki. Mamufti, makadhi sote tumetoka jamii moja leo tumewasahauMaimamu zetu na kuwasalimisha kwa mikono ya makafir nje ya Zanzibar wapate adabu stahiki ya ” kikatoliki”

  Zanzibar hakuna Imam wala maamuma ni makafir watupu ndani ya nafsi zao. Sheikh anapopanda kwenye kizimba bila ya kukemewa na kuhubiri utetezi wa Masheikh kufungwa na kusema Rais ana uwezo wa hata yakuua watu arobaini bila kuulizwa itakuwa hawa magaidi?Sheikh anafananisha Quran na Katiba ya CCM na umma wa kiislamu unaitikia kwa kishindo Allah Akbar badala ya ASTGHFIRU’LLAH

 24. Ghalib (Kiongozi) 13/10/2016 kwa 12:12 um ·

  Mchango unaweza ukapita mzalendo.net, angalia hapo upande Wa kulia juu, donate, weka reference uwamsho. fedha hio itafikishwa kwa wahusika,

 25. mrisho Haji 13/10/2016 kwa 1:10 um ·

  In shaa Allah tupatie namba ya Account au hata ya tigo, Air tel, Zantel ila Account ya Benki muhimu kwani wengine tupo mbali na Zanzibar.
  In shaa Allah, Mungu azidi kutupa subra kwani ni subra ni ushindi tosha.
  Awajaalie mashehe wetu watoke ndani ya mikono ya wasiopenda haki.

 26. mamaqadaff 13/10/2016 kwa 10:30 um ·

  INSHALLAKH TUTAJITAHID KADRI TUWEZAVYO HATA KUWAPELEKEA WENYEWE WALENGWA YATOSHA

 27. Stonetown (Kiongozi) 14/10/2016 kwa 12:58 um ·

  Kwa wale waliokuwa na uwezo na moyo wa kutoa, sio mbaya kama unahisi unaweza kufikisha kwa walengwa wenyewe, lengo ni kuwasaidia na hii itapelekea kujiona waathirika sio peke yao ni sisi sote.

  Ukihisi utafikisha moja kwa moja, ukihisi kuwa utawatumia kwa njia ya Bank transfer au kutumia paypal ya mzalendo ama kutuma kwa Tigopesa, basi timiza wajibu wako.

 28. Mona 16/10/2016 kwa 10:13 um ·

  Tuzidishe kusoma Halalbadri kwa hawa vibaka wa demokrasi Zanzibar na Tanganyika inshallah yawakute zaid ya yaliyomkuta balozi wa Tanganyika sharobaro wa kitope.

Comments are now closed for this article.