Mnazimmoja yakosa umeme kwa masaa 8 Lifti yakwama

Written by  //  18/12/2016  //  Habari  //  Maoni 8

15542069_10154807493902640_4834353674542775237_n

Dhamir Ramz

Kufuatia tukio la kuzimwa umeme mchana wa leo kwa karibu masaa manne, katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, mama mmoja alinasa kwenye lift ya taasisi hiyo muhimu ya afya kwa muda mrefu hali iliyopelekea kupoteza fahamu kwa kukosa hewa (suffocation) hadi muda aliotolewa. Kama angechelewa kutolewa basi angepoteza maisha yake kwa kukosa hewa.

Maswali ambayo najiuliza ni haya:
1. Kwamba hospitali kuu ya Zanzibar inakosaje huduma ya umeme wa dharura (back-up power supply) wakati ni sehemu ya kuokoa maisha ya watu?

2. Kama hiyo huduma ipo, tuseme jenereta la dharura, ni nini kimesibu hadi kukakosekana umeme wa dharura ili kuepusha maafa?

3. Wagonjwa ambao wamelazwa ICU, nini kimewasibu kwa kadhia hii?

Tunakazania kuweka jenerators kwenye majumba yetu, lakini sehemu muhimu kama hospitali huduma hiyo hamna. Muliopewa dhamana ya kuendesha taasisi hii, Mungu anakuoneni. Yaliyompata mama huyu na wengine, iko siku yatawafika walio wenu. Acheni ubinafsi na fanyeni kazi mtimize wajibu wenu. Kama hamuwezi ONDOKENI wapisheni wenye uchungu na uzalendo wa taifa hili. THIS IS TOO MUCH!

Inaendelea: Kadhia ya kuzimwa kwa umeme na kunasa kwa mwanamama katika lift ya hospitali kuu ya Mnazi Mmoja:

Muda mfupi uliopita, nilipokea simu kutoka kwa Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, ambae ni Waziri dhamana wa Wizara ya Afya na nimepewa maelezo yafuatayo kwa ufupi kuhusu tukio la leo:

Kwanza, hakuna jenereta inayotosheleza kupatikana kwa umeme wa dharura kwa hospitali nzima. Iliyopo sasa hivi haitoshelezi, na hutoa umeme wa dharura katika vyumba vya Theatre, Makeniki na Neuro-surgery.

Pili, jenerator iliyopo huwekewa mafundi wa zamu, na muda wote inatakiwa awepo fundi mmoja wa zamu ili kukabiliana na dharura. Wakati umeme unazimwa, fundi aliepangiwa kuwepo hakuonekana katika eneo la kazi, na ilibidi atafutwe fundi mwengine kusaidia zoezi la kurejesha umeme wa dharura. Mfanyakazi huyo atawajibishwa kwa uzembe alioufanya.

Tatu, ni kwamba kwa kawaida shirika la Umeme huwasiliana na Wizara ya Afya kila inapotokea dharura ya kuzimwa kwa umeme, lakini kwa siku ya leo hilo halikufanyika kwa sababu hitilafu imetokea kwenye gridi ya taifa. Hivyo hakukuwa na matayarisho ya kukabiliana na hali hiyo.

Zaidi, ni kwamba Serikali inalifuatilia suala hilo kwa karibu zaidi ikihusisha uongozi wa juu. Hivi karibuni, jenereta ya dharura iliyotolewa kwa hisani ya mfuko wa UNFPA itawasili Zanzibar kwa ajili ya kufungwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Binafsi, nitoe pole kwa walioathirika na tukio la leo, na pia nimshukuru Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwa kulitolea ufafanuzi jambo hilo ambalo linamgusa moja kwa moja akiwa kama ni kiongozi dhamana wa taasisi hiyo nyeti.

Tujifunze kutokana na makosa. Na pia tusiwache kukosoa pale panapostahiki.

Ahsanteni sana
Dhamir Ramz

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Mnazimmoja yakosa umeme kwa masaa 8 Lifti yakwama"

 1. abuu7 18/12/2016 kwa 5:45 um ·

  @ashak. unasema iko siku itawakuta wao. rabda nikukumbushe.hawawenye nchi wakiumwa na kidole tu basi huduma ya kwanza.uwanja wa ndege kukimbiliya india. au pingine popote lakini sio mnazi 1.

  alivokuwa juma duni waziri wa afya.kuna mkereketwa wa kijani wakati wa mchakato wa katiba. nafikiri yule mwanamke alosema kuwa tunafaidika na mbogamboga kutoka bara. alisrmama na kumwambiya anashangazwana waziri wa afya kuwa hospitali hakuna hata mashine ya kuchomeya vifaa vilivokuwa vishatumika au expere dat.

  serekali ya zanzibar muuogopeno mungu. mnaalaniwa na wananchi kila siku kila dakika kila saa.
  mpeni haki yake Maalim kwani mnsogopa nini.

  hebu fuwateni wasiya wangu nyinyi unganeni nyote pamoja halafu vunjeni majina ya vyama venu vote Cuf na Ccm. tafuteni jina jengine jipya.basi yote yatakwisha.kwani shida nini .nyienyote mtakuwamawaziri kama kawaida na wala matumbo yenu hayatarejea chini.mtanawiri tena kuliko sasa ikiwa mtarejea kwa mungu
  lakini kwahivi mnavokwenda mtakula laana kila siku.
  zazibar kwanza dini kwanza haki kwanza.halafu ndio siasa na kidumu na sawasawa badae

 2. rasmi 18/12/2016 kwa 6:49 um ·

  Thanks brother Dhamir kwa taarifa hii, very informative indeed. Katika yanayojitokeza siku za hivi karibuni ni SMT kuanzisha juhudi za kuwanyamazisha wananchi wasitoe taarifa katika mitandao za kufichua maovu, SMZ wajiepushe na mtego huu kwani hauna tija yoyote kwa mustakabali wa Zanzibar.

  SMT imeanza kukamata wamiliki wa mitandao mfano Max Melo wa jamiiforum kwa kutumia sheria ya uzibiti wa mitandao na pia mchoro aliokuja nao William Lukuvi wa kutaka kunyang’anya watu viwanja na majumba yao kwa kisingizio cha watu wasio raia kutoruhusiwa kumiliki ardhi, huu ni mtego pia ambao SMZ umetengezewa kwa choyo cha SMT kuona koloni lao linawaponyoka.

  Kuna miradi tofauti mfano ZSSF Mbweni, ambao ulikusudiwa wazanzibari waishio nje ya nchi waweze kununua nyumba hizo, na katika kongamano la Wazanje walipelekwa hadi kutembelea mradi huo, mtego uliowekwa kwa ZSSF ni washindwe kuuza zile nyumba, kwani ilitegemewa wanunuzi wengi wawe ni wageni kutokana na ukweli kwamba wanaweza kununua, leo wamewekewa mtego waige sheria ya Lukuvi ili wanase na wakwame kuuza.

  Si tu ZSSF, kuna miradi kama ya Bakhresa ya ujenzi wa nyumba, Pennyroyal nk, miradi hii yote inatarajia kuuza nyumba kwa kutegemea zaidi walio na hizo fedha ambao ukweli wengi wao ni walio nje ya nchi, mtego umewekwa SMZ iige sheria ya Lukuvi ili kukwamisha mipango ya kuiendeleza Zanzibar kwa hali yoyote.

  Sheria ya udhibiti wa mitandao si lolote ila mbinu za kutaka kuzuia wimbi la ufichuaji uovu na ufisadi katika SMT, SMZ haina la kuhofia hili upande wa Zanzibar kwani litaisaidia kufichua uovu badala ya kuuficha mvunguni, waache SMT na sheria yao na kwa upande wa Zanzibar SMZ iendelee kuruhusu kukososolewa na kufichuliwa kwa ufisadi ilimradi mitandao hiyo haihatarishi amani na utulivu wa visiwa vyetu.

  Uigaji na uruhusuji wa sheria za SMT kuzifanya sheria za Zanzibar kuwa hazina meno, mfano urusiwaji wa masheikh wa Uamsho kupelekwa SMT haisaidii bali kuipokonya mamlaka yake Zanzibar, hakuna sababu yoyote ya masheikh wale kama wana kosa kwa nini wasishitakiwe Zanzibar ambako hilo kosa linaambiwa lilitendeka,

  Habari iliyopo juu haina chembe ya uchochezi bali ni uamsho kwa wahusika kufanyia kazi changamoto kama hizi na wahusika kuwajibishwa.

  SMZ iwe makini na mitego ya kuimaliza Zanzibar inayotengenezwa na SMT kwa visingizio tofauti ambavyo havina tija kwa Zanzibar, Wazanzibari sio maadui wa kwao bali ni watu walio na hamu ya kuona maendeleo na hali zao zinaimarika kwa kuimarika uchumi wa visiwa vyao.

  Zanzibar Kwanza…

 3. Z.I.7 18/12/2016 kwa 10:53 um ·

  Kuwasana na kushauriana ndivyo waungwana watakiwavyo kufanya lkn hapo anae waswa na kushauriwa ni nani?

  wapi SMZ ni nani aliewachaguwa, hao ni watu wapo kwa nguvu ya bunduki yetu, kama wangekuwa wamechaguliwa wangeitetea zanzibar lkn wao ndio wanaotumika kuangamiza,

  hapo ilipokuwa SMZ kina sita na lukuvi walijiuliza mara mbili na tatu waanzie wapi au labda wafanye ujanja kwa kutumia bunge kanisa lao huwashauri lkn leo hakuna haja wao hujiimbia tu wenyewe hawa wazanzibar wakata viuno ili lukuvi na kanisa lake wafurahi zaidi.

  iko wapi SMZ ya marehem Bavuai na bastola mkononi kwenda kutaka ufafanuzi kwa nyerere!
  iko wapi SMZ ya Mzee Karume ya mwisho chumbe!
  iko wapi SMZ ya kumtoa baluti Amir Jamal kwa kunyatia fedha ya zanzibar
  na kadhalika ktk hayo, sasa mbali ya kuwa madarakani isivyo halali na nakutekeleza mpango wa kuidhofisha na kuifuta zanzibar kupitia ajenda maalum ya kundi maalum la tanganyika bado nyinyi wazanzibari mnaita hiyo ni SMZ?

  au ni yale maneno ya rais mteule wa marekani bado mnahitaji kuendelea kutawaliwa

  tuseme bado hamjaelewa tu kuwa hao mission town hawapo kwa ajili yenu ! kama ni kwa ajili yenu kwa nini wafanye kila vitimbi katika chaguzi na baada kwanini?

  nimesema haya ili ndugu zangu mpunguze msongo wa mawazo kwani ikiwa tayari umeelewa
  kuwa waliopo sio hutopata mfadhaiko kwa wanayoyafanya lkn utafkiria ufanye nini ili alau uskume siku ktk nchi iliobarikiwa lkn wakatokea kundi kwa tamaa zao na vitimbi vyao nchi imelaaniwa haina mbele haina nyuma.

  Ndugu zangu msishangae walisema tutakula dongo sasa ndio tunakoelekea na naamini

  si peke yetu.

 4. Abdul Zakinthos 18/12/2016 kwa 11:01 um ·

  sasa hamna njia nyengine ya kunasua watu kwenye lift? fire wana kazi gani au ndio hawana elimu ,hatuna hata michoro ya mjengo?

  Tuna jua la kutosha mwaka mzima 32 Celsius tunashindwa kuwa na umeme wa jua ambao hata hatulipii?

  Ama kweli ZNZ bado sana wenzetu wanopata JUA mara moja kwa mwaka wanatumia fursa hiyo hiyo kusave mionzi hiyo

 5. Mfalme 20/12/2016 kwa 7:27 mu ·

  @ Rasmi

  Hizo nyumba lengo lao ni kununuliwa na kanisa katoliki . Utakuja kuniambia. Kule bara walikuwa wankwenda mikoani kununua ardhi kwa watu kwa bei juu. Nina rafiki yangu ameendewa mara nyingi kuombwa auze ardhi yake ya urithi na ameongezewa dau kubwa lakini amekataa kabisa kuwauzia.
  Allah atunusuru na hawa maadui

 6. Mfalme 20/12/2016 kwa 7:33 mu ·

  @Abdul Zakinthos

  Ndugu yangu mimi nimejaaliwa kusoma hayo malift na kuya fanyia installation. Kumkwamua mtu aliyekwama kwenye lift , unaweza kulifungua lift bila umeme . unaweza kulipeleka kwenye ghorofa ya karibu kwa kutumia manual method . Kidogo ushibe lakini lift unaweza kuliendesha mpaka unapohitaji na ukalifungua bila tatizo. Hata robo saa haifiki

  NCHI WAIWEKE KWENYE SHERIA TUJE TUWAFUNZE VIJANA HII ELIMU

 7. MAWENI 25/12/2016 kwa 8:59 um ·

  Wakoloni wetu wawaogopa Wazanzibari walipo nje kurudi kwao . Ndio hizo mbinu za kila aina za kuwavunja moyo kushughulikia nchi yao na miundo mbinu yatoweza wao kurudi kuishi Zanzibar.
  Wanjuwa wakirudi wata waamsha wenzao kutoka kwenye usingizi wa Ahli llkahf.

 8. serelly 01/01/2017 kwa 6:54 mu ·

  Kazi ipo. Allah amua’fu huyo mama.

Comments are now closed for this article.