Vedio – Tundu Lissu amchana Lipumba live, asema ni Kibaraka

Written by  //  31/03/2017  //  Vidio, Habari  //  Maoni 4

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 4 katika "Vedio – Tundu Lissu amchana Lipumba live, asema ni Kibaraka"

 1. mzeekondo 31/03/2017 kwa 3:51 um ·

  Hivi karibuni niliwahi kuandika kidogo “scenario” niliyoiona ambayo kuna uwezekano mkubwa tukafika huko,ikiwa huu unaoitwa mgogoro utafanikiwa kutuletea matokeo tusiyo yatarajia,katika mkanda huu wa leo wa mhashimiwa Tundu Lissu,nae pia amegusia yale yale ambayo niliyanena awali, kuwa wanasubiri kwa hamu mpango huu ufanikiwe, ili iwe neema kwa upinzani,hapa ndipo nina poshindwa kuwaelewa kina Balozi Iddi na wenziwe wanaousuka mpago huu,kwa kutumia gharama kubwa huku wakisaidiana na Lipumba, ili kuimaliza cuf na Maalim Seif kwa mawazo yao.

  Tatizo liko hivi,CUF sio jengo au chama, ni WATU, sasa hata kama ccm tukifanikiwa kukiuwa chama hiki cha wananchi{cuf}kwa hapa Zanzibar,hawa wanachama wao wa miaka yote hii wanao tusumbua kila uchukuzi/uchaguzi ukija, ghafla ndio watakuwa watu wetu, na watakipigia kura chama cha mapinduzi na wagombea wetu wote?

  Jawabu ni hapana,sasa kwa nini tunapoteza nguvu nyingi na muda wote kukifuta chama ambacho hata kikitoweka duniani leo, bado sisi tatizo letu halijakoma?huu ni uwenda wazimu wa kisiasa,tusichanganyikiwe kiasi hiki baada ya kukataliwa kwa kishindo katika uchaguzi halali uliopita wa oktoba 25.2015,mpaka tukadhani “solution” ni kukiuwa chama cha CUF,huku ni kujipalia makaa.

  Turudi nyuma na tuimie historia kidogo,ccm kuna wakati tulimtumia Zitto Kabwe ili akiuwe au akichafue chama cha chadema, na tuliitumia pesa nyingi na mahamaka kumhalalishia ubunge wake baada ya kufukuzwa na chadema,hatimae akaendelea na ubunge na kuamua kuanzisha chama chake binafsi cha siasa ACT {alliance for change and trasparency, yaani umoja wa mabadiliko na uwazi}hivi sasa bado mbunge kwa tiketi ya chama chake na yuko bungeni anawakilisha jimbo lake.

  Mara kadhaa inapobidi yeye binafsi hujiunga na wapinzani katika kuiweka msalabani ccm ndani ya bunge,tatizo lengo letu la kukiuwa au kukichafua chadema tulivyo kusudia haikuwezekana, badala yake ndio tukapata upinzani wa hali ya juu, ambao haukuwahi kutokea katika uchaguzi uliopita, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, mgombea wa urais wa upinzani wa chadema Lowassa, alipata kura millioni zaidi ya sita baada ya kuzipunguza, na yule wa ccm Magufuli alipewa millioni zaidi ya nane huu ndio ukweli”facts”

  Ninachotaka kukisema hapa,ni lazima tukubali hatuna hiari haya tunayofanya sio uungwana wala sio demokrasia,huu ni uhuni wa kisiasa na huu hufanywa pale utawala unapokuwa hauna watu tena wa kuwaunga mkono,hapo ndio hutumika nguvu za dola na mikakati ya ovyo kama hii, ili kujiweka katika uongozi tusiostahiki,hili nalo kuna wasomi watabisha, msibishe ovyo leteni vigezo”data” mdomo mtupu sivyo mlivyosomeshwa na kuhitimu, na kwa wale vichwa viwazi kama mimi utawalaumu vipi? na wao hawana wanachokielewa.

  Maalim Seif kwa nilivyo msoma kwa miaka kadhaa sasa, nina imani anaelewa nini kinaweza kutokea huko usoni kuhusu mgogoro huu wa cuf,na yeye ameshajipanga kwa mabadiko ya aina yoyote kuhusu muelekeo wa kisiasa wake binafsi na umati wake wa cuf unaomuunga mkono,Lipumba hana chama wala watu katika cuf hili linaeleweka, yeye na Zitto Kabwe kama alivyokuwa chadema anaweza kuondoka na kuanzisha chama chake, ambacho kitamhakikishia ruzuku anayo ipenda tu, sio kingine,na kama atafanikiwa kukiuwa cuf kwa msaada anaoupata kutoka kwa Magufuli,msajili wa vyama vya siasa na mahakama, basi atabakia na chama cha cuf kama jina, pamoja na majengo yake, hasa lile la pale buguruni, lakini watu hatowapata,wote watakwenda kule alipo kiongozi wao wanae muamini, yaani Maalim Seif,sasa nani anajua wapi maalim ataelekea? suala ni wapi,nahakika harudi CCM.

  Chadema kina nguvu Tanganyika kama CUF ilivyo hapa Zanzibar,Ukawa imewafunua macho wapinzani hawa wawili na kujua, ili kuiondoa na kukabiliana na CCM, ni lazima wafanye kazi kwa kushirikiana,pamoja na kubadilishana mawazo,hivyo vyama vingine vingi unavyo visikia vya siasa hapa Tanzania, ni wasindikizaji na watafuta ruzuku tu.

  Vyama hivi havitaki kuungana kwa hiari yao, kitu ambacho kingekuwa kizuri kimikakati, kidemokrasia na kuleta ushindani wa vyama tunao utarajia, bahati mbaya wala hawana mpago huu,lakini serekali ya ccm inafanya kila inalo weza, kuwa unganisha kwa nguvu bila kujua, sijui kwa faida ya nani?sidhani kama ni ya ccm,sasa ikiwa kuungana kwao ndio mauti ya ccm, basi msajili wa vyama vya siasa,mahakama,Magufuli au ccm mpeni chama cha cuf Lipumba, halafu muone kama 2020 ikulu zote mbili ya bara na hii yetu hapa Zanzibar, marais watakao hamia humo watakuwa Lipumba na Makufuli.

  Sio kila unachoomba unapata,omba chenye kheri peke yake, na mtangulize Mola kwanza, kila ukijaaaliwa.

  Inshaalah Zanzibar itakomboka.

 2. Jino kwa Jino 31/03/2017 kwa 5:15 um ·

  @Mzee Kondo Baraka Allahu fiyk ww ni jabali la siasa na mwenye kuona mbali au kama kama wanavyosema watanganyika moto wa wa kuetea mbali ,lipumba anijichimbia kaburi lake kwa mikono yake leo amesahau kipigo alichopata kwa ccm kwa ajili ya cuf leo anawatumikia mabwana zake kutaka kukiuwa chama cha cuf lkn mnafik Allah hatasimama nae .

 3. Smart 01/04/2017 kwa 1:49 um ·

  Mahakama Kuu imemuamuru Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutotoa ruzuku kwa Prof. Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi, CUF, na kundi lake.

  Zuio hilo ni mpaka shauri dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

  Uamuzi huo umefikiwa na Jaji Dyansobela baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa kwa hati ya dharura.

  Jopo la Mawakili wa CUF, liliiomba Mahakama Kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali shilingi milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa chama kuhusu fedha hizo ikizingatiwa kwamba, Prof. Lipumba alishavuliwa uanachama.

  Mawakili hao akiwemo Juma Nassor , wamesisitiza kwamba, mazingira yaliyopo ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia serikalini.

  Aidha, wameiomba Mahakama Kuu kwamba amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya msajili kumtambua Prof Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa rufani ya kufanyiwa marejeo mbele ya Mahakama ya Rufani Tanzania.

Trackbacks for this post

 1. Vedio – Tundu Lissu amchana Lipumba live, asema ni Kibaraka | Asali: KIGANJANI KWAKO…

Comments are now closed for this article.