Mgogoro wa kukata umeme ni hoja ya kitaifa, Wazanzibar tuungane

Written by  //  11/03/2017  //  Habari  //  Maoni 16

Kutofautiana kimitazamo au kuwa na maoni tofauti ni kawaida ya binaadamu. Faida yake kuu ni kuongeza ushindani baina ya pande zinazotofautiana muhimu zaidi pale yanapofikiwa makubaliano.

Kwanza ni mpongeze Dr Shein kwa msimamo wake juu ya mgogoro wa kutaka kukatiwa umeme Zanzibar. Dr Shein katika taarifa yake ni nyepesi sana kuifahamu. Ukianzia lugha aliyotumia hadi body language ili kamilika, nampongeza kwa hili.

Magufuli angekuwa kiongozi makini na kama alivyosema Tanesco sio taasisi ya kisiasa alikuwa aiwacha Tanesco nje ya uwanja wa siasa. Sasa hivi tayari ameishaitumbukiza kwenye siasa.

Wazanzibar tunahitaji kujenga hoja za pamoja kwenye mgogoro huu. Hili ni suala la kitaifa. Tuanze kubainisha baada ya hoja za kivyama na hoja za kinchi

Mgogoro wa ulipaji umeme ni suala la miaka mingi sana. Hii ilitokana na dhana zilezile za Kikoloni walizo nazo mabwana zetu.

Zanzibar kwa decades ilikuwa ikizalisha umeme kwa generator zake wenyewe. Hadi ilipofika miaka ya 80 kuongezeka mahitaji ya utumiaji nishati hii ndio wazo la kununua umeme kutoka Tanganyika likazaliwa. Wakati suala la nishati halikuwa katika orodha ya mambo ya muungano.

Bila ya shaka kwa vile ni suala la kibiashara baina ya nchi mbili, Zanzibar na Tanganyika kulikuwa na mikataba ya kibiashara. Hapo sitokwenda mbele zaidi

Kwa umri wangu, makubaliano haya ya kibiashara yamekuwa yakivunja na kila upande. Zanzibar kwamba imekuwa hailipi vile inavyotakiwa. Tanganyika nayo inashindwa kutoa good service na value for money. Wakati huohuo wamekuwa wakiiadhibu Zanzibar kwa kuiuzia bei ya juu.

Hoja hizi mara kadhaa zimepigiwa kelele. Nakumbuka hata kwenye majukwaa ya Chama cha Wananchi CUF ikizungunzwa kwamba Tanganyika inaiuzia umeme Zanzibar kwa malipo ya dola.

Mwanzo Tanganyika ikizalisha umeme kwa kutumia maji (hydropower), sasa hivi wanazilisha umeme kwa kutumia gas, ambayo ni ya Muungano, vipi hapo?

Hivyo basi mgogoro huu umechochewa na dhana ya wakamue uwatawale. Ni wakati Wazanzibar kuwa kitu kimoja, kujenga hoja za pamoja kudai haki zetu. Na pale tunapodaiwa tubebe deni hilo kwa pamoja.

Tuje na hoja katika kipindi hichi kifupi zenye muelekeo wa muda mfupi pia zenye muelekeo wa muda mrefu.

Tukubali ZECO imekuwa ikiwapatia umeme Wazanzibar kwa bei rahisi ikilinganishwa na Tanganyika kwenyewe unakotoka.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 16 katika "Mgogoro wa kukata umeme ni hoja ya kitaifa, Wazanzibar tuungane"

 1. Wamtambwe 11/03/2017 kwa 9:03 mu ·

  @Ashakh
  Mimi napingana na wewe kwa hili kuwa tuwe kitu kimoja na Serikali hii Haramu. Kama wanataka kutuweka kitu kimoja kwanza waiondowe hii Batili ya October 25. Kwanza nikueleze yote haya yanayotoke ni Matokeo ya Batili hii. Nakumbuka kuna Sheikh kule Pemba alisema bayana, huwezi kukoroga kinyesi halafu ukangojea kunukia harufu ya Waridi au Asmini.
  Kama ni kuwagawa wananchi wao ndio waliowagawa . Tangu hio Serikali ilipojiweka madarakani Sijawahi kusikia wamekahadharani kuhutubia wananchi kama Raisi wa Wanzanzibari wote, kubwa wanalolifanya ni kuwapiga vijembe na kuwakejeli halafu kupeleka Mazombi wakiwapiga na kuwadhulumu mali Zao. Jee unatuambia tuwaunge mkono madhalimu hawa?
  Kama ni deni la Umeme wanachi wa kawaida haliwahusu. Kila Mzanzibari anyetumia umeme analipia Kila unit anayotuimia. Halafu isitoshe gharama zote za kuvuta Umeme pamoja na Mita zinamuangia mwananchi huyo huyo wa kawaida ingawa akishazilipia ina kuwa ni mali ya Shirika.
  Mbona walipotaka kufanya uchaguzi wao haramu pesa walizipata?
  Imefika wakati wananchi tujuwe haki zetu sio tudhulumiwe Kila Pembe.
  Zanzibar ni Kijinchi kidogo ambacho unaweza kuitosheleza kwa Umeme. jua au Upepo
  Nawakate tutatafuta Investor atakayewekeza Zanzibar tutazalisha Umeme zanzibar na Utakaozidi tutawauzia Bara

 2. Ashakh (Kiongozi) 11/03/2017 kwa 9:37 mu ·

  Basi jitayarishe Mkoloni hapo apiga kofi kwa mdomo.

 3. Ghalib 11/03/2017 kwa 10:04 mu ·

  Ahsante kwa nakala yako, ila mimi sitakuwa tayari kubeba jukumu la deni la umeme kwa sababu nalipa kila mwezi na ikafika wakati kuwekewa luku, sasa kwa nini zecco hawalipi? Kama mutafuatilia wafanyakazi wa zecco wana mali nyingi sana kwa kuhujumu shirika.

  Sijiandai kuwasha kibatari Najiandaa kufunga solar, tena unalipa nusu kwanza, halafu kila mwezi unalipa pesa zao walio kufungia, kwa mwezi umeme nalipa 120,000, kwa nini nisinunue solar kwa muda wa miaka18-20 sina mgao?

 4. Ashakh (Kiongozi) 11/03/2017 kwa 10:15 mu ·

  ZECO sio kuwa hawalipi, wanalipa sehemu au ile kima wanachotaka wao.

  Kinachodaiwa nikuwa ZECO hailipi ile bei wanayotaka mabwana wakubwa, ambayo bei hiyo itaufanya umeme uwe ghali mara mbili zaidi

  Kuwa na vyanzo mbadala wa umeme hiyo ndio njia moja ya kuachana nao. Lakini kuna factor kibao kwa vile hili halikuja kwa bahati mbaya. Mfano kulipa kodi,

 5. sadimba 11/03/2017 kwa 10:56 mu ·

  @Ashakh
  Mimi naweza kulitia katika mizani wazo lako tu kama Babu Ali na wenzake watakiri wamedhulumu na hawana uwezo wa kuwatetea wazanzibar hivyo watubie na kurudisha haki ya watu, Najua maguu fool ni mto wa kufoka foka ili wavimba macho wapate kupiga makofi. Binafsi najua huu ni muendelezo wa kuidhalilisha zanzibar lakini sidhani kama watakata umeme maana waliomfingaiguzoni ni mbuzi wao wenyewe. Hii ni kuwanyamaizsha wazanzibar wajione wanapendwa na ndugu zetu wa damu kumbe wanatupa bakuli la maharage baada ya kutueka na njaa.

  Mimi naamini wenzetu wazanzibar wote ni wabaya ila wale tu wanaofuata amri na matkwa wao, ndio maana wakaleta mpaka jeshi kuhakikisha wanaweka msukule wanaemtaka ndio maana ata akihojiwa anafanya ukomedy tu. Muheshimiwa anasema hizi sio taasisi za kisiasa pesaa kufanya uchafuzi wa machi zimetoka wapi kama si Zecco, halafu tuangalie wafanyakazi wote wa juu kama sio watoto au jamaa wa vigogo wa kigozi. Halafu wanatwambia chama kinashika hatamu vipi utasema sio taasisi za kisiasa.

  Huu ni muendelezo wa kuiua zanzibar tu ndio mana wafanayakazi wa Zanzibar wanalipwa mishahara midogo ili waone bora muungano, kodi kubwa. Tanganyika iligharimika kuleta majeshi na magari kwa kuwanyima sauti wazanzibar. Sasa musilalame bebeni mzigo wenu wa kulazimisha maamuzi lakini iko siku kila kitu kitakaa sawa na atajulikana mzungu na albono.

 6. Mrfroasty (Ufundi) 11/03/2017 kwa 11:44 mu ·

  Mie nashauri hayo mawazo ya 1980 ya kununua umeme Tanganyika yageuzwe au kufutwa kabisa.Hiki ni kitu cha kuboreshwa kila mwaka, ni miaka zaidi ya 30 tokea tuje na wazo hilo (wazo ni kongwe na haliendani na mahitaji ya sasa).Nina wasiwasi yalikuwa ni mawazo ya kisiasa zaidi kuliko kiuchumi.

  Ufahamu wangu mdogo naamini kuna wawekezaji wengi wanaitaka deal waliyopewa Tanesco.Tena nataka niamini kuwa huduma itaboreka zaidi kwa kuzingatia transportation ya umeme ambayo ni moja ya gharama zinachangia bei yake kupanda itaondoka na kupunguza mzigo kwa wazanzibari.

  Zeco ni mteja, mdundo tunaopelekwa na Tanesco pamoja na Magufuli unaonesha dharau ya juu.Si mwenendo kabisa wa kibiashara, umekalia zaidi kama kasi ya mfadhili au mtu anaetufanyia hisani.Ni dharau ilioje.

  Nashauri Dr.Shein akatoa tenda kwa makampuni kuleta quotation na mpango wa kujitegemea ndani ya visiwa kwenye suala la nishati ya umeme.Vibatari iwe ni mpango wa muda mfupi, sioni kama uchumi wa visiwa unaweza kuendeshwa kwa vibatari.

  Wasalaam,

 7. Ashakh (Kiongozi) 11/03/2017 kwa 1:04 um ·

  Mrfroasty

  Ndio nikaja na hoja ya kitaifa. Tuangalie short term halafu tuje long term.

  By experiance, Tanganyika imefanya utafiti, kuchimba na kuibinafsissha gas kwa kipindi cha miaka 5 tu.

  Kwa vile Bab Ali keshatia sign kitabu, na sie Zanzibar kipindi cha miaka 5 gas tayari, umeme tunazalisha, Tanesco mwisho.

  Tukiangalia short term ndio hapo (mzaha wa Bab Ali turudi kwenye vibatali) tutafute umeme wa uhakika. Hata Kenya tunaweza tukachukuwa ikiwa bei inakhalis

 8. Papax 11/03/2017 kwa 2:32 um ·

  Acheni porojo hawawezi kukata umeme hata maramoja kwa hio wao wana blabala kama nyie cuf, maneno mengi hakuna kitu

 9. mzeekondo 11/03/2017 kwa 3:02 um ·

  Ya awal nianze kwa kukuunga mkono ndugu yangu mtoa mada @ Ashakh{kiongozi} kwani katika maoni na uchambuzi wako katika hili mimi na wewe tuko ukurasa mmoja,ulivyo yasoma maungo ya mwili wa daktari Sheni yaani “body language” ndivyo nilivyo yanukuu na mimi,huyu muungwana kama utapenda kumuita hivyo,alikuwa anajizuwia tu, lakini aliyokuwa anataka kuyatoa hasa moyoni hakuyatowa yote.

  Ni wazi kabisa hata akafika kumwambia Magufuli kuwa sisi tutawasha vibatari vyetu ni kumwambia kuwa kuwa wewe fanya unavyotaka yaani kata umeme,pia aliponukuu kuwa hili lipo miaka nenda miaka rudi tangu yeye alipokuwa makamo wa rais wa Tanganyika alikuwa anamfahamisha kuwa hili suala sio dogo na linahusu “siasa” sio biashara ya kuuziana umeme sokoni,na hatari zake ni za kisiasa ikiwa hutokuwa na akili ya kulitafutia suluhu kiCCM, basi awe tayari kwa mmon’gonyoko wa muungano na hilo sio saizi yake juu ya ubabe wake wa kuropoka ovyo majukwaaani bila kujua athari zake kwa taifa.

  Nakubaliana na wewe kuwa Wazanzibari hatuna hiari kwa lolote, ikiwa tunataka kujitawala ni lazima sote tuwe msimamo au kitu kimoja katika kuidai au kuvidai visiwa hivi,hapa nina maana wapinzani na wale walioko serekalini au ndani ya chama cha ccm, pamoja na wale wote wasio jihusisha kabisa na kinachoendelea visiwani humu,basi ni wajibu wetu kuungana,ccm kwa upande wa zanzibar peke yao hawawezi kumuondoa mkoloni bila ushirikiano na wapinzani,na wapinzani wanawahitaji ccm katika kukamilisha mapinduzi haya,sisi tunategemeana ndio maana hata serekali ya umoja wa kitaifa ‘SUK IMEPIGWA VITA’ na kuondolewa, unafikiri mkoloni ana wazimu aiachie iwepo sisi tuje kumgeuka?

  Kuwepo kwa serekali ile ilikuwa ni dalili mbaya kwa anae tutawala,alijua kuwa Karume alipoiweka hakuwa na wazimu,alikuwa ameileta makusudi ili kumuondoa Mtanganyika,sasa kama ccm peke yao wanaweza kumuondoa, kulikuwa na haja gani ya Maalim kukutana na Karume watu wawili tu, na waliweza kufanikiwa kiasi kile,waliviweka vyama vyao pembeni kwanza katika kutafuta uhai wa Zanzibar,baadae ndio tukaletwa au kuitwa sisi wazanzibari katika kura ya maoni, ili tuhalalishe umoja wetu,hivi ndivyo nchi inavyo patikana, sio kwa kutupiana madongo{matusi} kutengana,au kubaguana hayo ndiyo yanayoleta na kuzidisha ubaguzi,chuki na matabaka baina yetu, kiasi cha kumrahisishia mkoloni ili aweze kutugawa vizuri na kutuweka mafungu kama nazi”devide and rule/conquer”

  Nishati ya umeme kwa visiwa vyetu ni suala dogo sana kutatuliwa nje ya muungano, bara wanajua na daktari Sheni anajua ndio maana anaomba waukate, kwa sababu hana mpango wa kutumia kibatari, ana mpango wa kutafuta umeme wake wa uhakika sehemu nyingine, sio TANESCO, na anahamu Tanganyika waingie katika mtego huu, ili apate sababu ya kuwakimbia na umeme wao.

  Daktari Sheni mimi muungwana nakuomba kwa hisani yako, hata kama hawato ukata huu umeme wao safari hii, hii ni “wake up call” amka baba,usingoje tukawekwa gizani ndio mkurupuke kutafuta umeme kwingine, wakati ndio huu dalili za mvua sio ukosefu wa mchele ni mawingu.

  Mtawala mpya wa Tanganyika hana wala haujui utu wala ustaarabu,mila na desturi alizo kulia nazo hazimruhusu kuwa na udhaifu wa aina yetu au viongozi wenziwe waliomtagulia, ukiwemo na wewe daktari, ndio maana ana tawala kama Mkoloni anavyotakiwa, hapo hafanyi kosa, anatekeleza wajibu wake,makosa tunafanya sisi tunao tawaliwa, tunategemea rehmma kwa kiumbe sie.

  Tuungane ndugu zangu,kwa manufaa yetu sote na vizazi vyetu.

 10. shawnjr24 11/03/2017 kwa 6:43 um ·

  Mimi nitakubaliana (nitawaunga mkono) zecco(SMZ) kama watasema wakati umefika wa kuzalisha umeme wa Zanzibar, na kuwacha kununua kutoka tanganyika. Kwasababu huu umeme ni kama mkate wa mkoloni siku tukisema tunataka mchuzi wetu na wao watasema mkate wetu basi. Kipindi sisi tukijipanga kuwa na umeme wetu. Atatokea msaliti atakaeleta mapinduzi wakati tukiwa gizani. Katika kitu kimoja tanganyika wanajivunia kwenye utawala wao ni jeshi na umeme wao. Hakuna zaidi ya mawili hayo ndio maana wasaliti hutumika kuhofia jeshi na kukatwa umeme, na kupinduliwa wakiwa gizani.

 11. Piga nikupige 11/03/2017 kwa 7:22 um ·

  Ndondocha wa Tanganyika akiwemo Papax na CCM wenzake wa Zanzibar, wana hofu kubwa ya kukatwa umeme, kwani watapatwa na aibu kubwa na kutahayari hivyo wako tayari hata watowe miili yao pasi na kujalikuwa wana jinsia gani, ilimradi tu umeme usikatwe.

  Kwa hili la kukatwa umeme ni wazi CCM zanzibar wanalia kwa mabwana zao na kuwaeleza kuwa huu si umeme ndio Muungano wenyewe, mkiukata tumekufa watu hawato tuelewa.
  Na mimi nahisi kwa sasa umeme ndio Muungano ulio iunganisha Zanzibar na Tanganyika kwa waya, wacha waukate sitegemei kuwa kutakuwa na Muungano tena. Na hili CCM Zanzibar wanaliogopa kuliko uchaguzi mkuu.

 12. Ashakh (Kiongozi) 11/03/2017 kwa 8:43 um ·

  Mie niulize swali moja:

  Tatizo ni Tanganyika au tatizo na vibaraka wao? Na lipi muhimu zaidi la kuondolewa?

  Ninavyofahamu vibaraka wapo kwa nguvu ya Tanganyika. Kuondoka kwa Tanganyika na vibaraka wao hawakai.

 13. salali 11/03/2017 kwa 11:33 um ·

  Samwell sita alisema kama wa Zanzibar hawataki muungano watakatiwa umeme mimi naona haki yetu iloporwa ipo karibu na kuipata ndio sababu mkononi anaanza kuweka nguvu ili Maalim Seif Sharif Hamad atakapo kabidhiwa nchi iwe giza, hilo sisi halitubabaishi tulianza kutumia taa za umeme na kutazama tv kabla ya wawo, watupe nchi yetu tutaanza na (0)Daud bashite.

 14. abuu7 12/03/2017 kwa 5:26 mu ·

  Ufike wakati sasa kujibu kwa mdomo iwe basi. Kwa maisha haya ya kuteswa kila kukicha.

  Kuanziya sasa hamna mtu kwenda kununuwa umeme.bora kununuwa generates mafuta tutachimba japo kwa jembe.

 15. Abdul Zakinthos 13/03/2017 kwa 2:52 mu ·

  Malengo ya CCM Bara kuimaliza Zanzibar ndio yanaendelea..CCM Zanzibar hawasomi kama wanaendeshwa dodoma

  HAYA MNAKATIWA UMEME HATA MKIJA KUVUNJA MUUNGANO ZANZIBAR HAINA CHOCHOTE,KWA SABABU FURSA ZOTE ZIPO CHINI YA MUUNGANO.

  HATUNA NDEGE WALA MELI WALA POSTA WALA BANDARI NA SASA UMEME

  NDIO TUNAMALIZWA KISHA TUACHIWE WENYEWE

 16. sadimba 13/03/2017 kwa 6:16 mu ·

  @Ashakh

  Tatizo ni Tangayika hawa vibaraka ni sawa na kupe tu ng’ombe akifa na wao watakufa maana hawatopata damu. Na wanafiki haweshi kwani walikuwepo toka enzi za mitume, wao wako tayari usiku kuuita mchana na mgomba kuuita mnazi ilimradi wanapata tonge haijalishi kama nchi inamomonyoka kidogo kidogo kwenda kwa mkoloni.

  Na hapa tunapata kuona tofauti baina ya waungwana na walioshuhudia harusi za wazee wao.

Comments are now closed for this article.