Mchakato utafutaji mafuta kuanza Zanzibar

Written by  //  05/03/2017  //  Habari  //  Maoni 8

zanzibar-tanzania-city

Zanzibar. Hatimaye kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia Visiwani Zanzibar inatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa kwa kutumia ndege maalumu katika maeneo ya nchi kavu na bahari.

Akitoa taarifa ya Serikali jana kuhusu kuanza kwa kazi hiyo, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Zanzibar, Salama Aboud Talib alisema kazi ya awali ya utafutaji itaanza kwa kitalu cha Pemba.

“Taarifa hii inakusudia kuwajulisha wananchi wote wa Unguja na Pemba kuwa hivi karibuni kazi ya awali ya itaanza,” alisema.

Waziri huo alibainisha kuwa utafutaji huo utafanywa na Kampuni ya Bell Geospace Enterprises ya Uingereza ikitumia ndege kukagua miamba iliyoko chini ya ardhi.

Salama alisema hatua ya kwanza ya utafiti itachukua miezi minne na Serikali inawaomba wananchi wasiwe na hofu wakati kazi hiyo ikiwa inaendelea kwa kuwa hakutakuwa na athari zozote.

Kuanza kwa kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kunaanza baada ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kutia saini Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia mwezi Novemba, mwaka jana.


mwananchi

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Mchakato utafutaji mafuta kuanza Zanzibar"

 1. salali 05/03/2017 kwa 10:28 um ·

  Wacheni usanii hayo mafuta tayari yalishaonekana tokea enzi za marehem Asha bakar mwari, Mh Massor Yusuf hamid alilipigilia misumari ya mwisho, chaajabu ni kwamba sababu kuna kada wa ccm alisema kama Zanzibar kungalikuwa na mafuta “hakuna mtu anayependa pesa kama Abeid Aman Karume” huyo aliyesema hayo ni kikada (shamte) eti kama yangalikuwepo Rais mstafu angalikwishayachimba. Mje nyumbani Tundauwa

 2. jazba 05/03/2017 kwa 10:53 um ·

  hamna lolote propaganda na ujiko wa kisiasa tu tangu lini serikali hii ikawataarif wazanzibari kitu chenye neema na manufaa.
  pengine hio kampuni inakuja kukagua kwa ruhusa iliyotolewa tanganyika wao wanaitumia hio kutoa matangazo kwa ajili ya kujisogeza kwenye legitimacy za kisiasa tu

 3. Jino kwa Jino 06/03/2017 kwa 4:10 mu ·

  Huko ni kujifurahisha tu mafuta yapo zamani toka enzi ya mfalme labda kuna Ajenda nyengine sio mafuta ndio kama alivosema @ Jazba kuwa serikali hii ikawataarif wazanzibari kitu chenye neema na manufaa.Huko ni kujihashuwa tu kisiasa waonekane kwamba ccm wanatka kufanya kitu .Mimi naona kuna kitu chengine kabisa .Jamani kweli mafuta yanatafutwa kwa ndege mm naona kama mazishi tu.

 4. abuu7 06/03/2017 kwa 5:52 mu ·

  Baraza la dodoma namba mbili lilioko zanzibar .litaanzisha rasmi kazi ya kutafuta mafuta kwa njia ya anga

  Uharakishaji huo kuwa serekali iliokataliwa na wananchi kufilisika. Na kwa upande wa ofisi yao kuu ilioko dodoma kukataliwa kwenye pesa za meleniam. Kwa vile muungano huu tumeungana kwa mambo 4 tu. Kati ya hayo moja ni tuchimbe mafuta.

  Imekuwa serekali sasa inatafuta pesa kwa njia ya Bingo (LOOTO) maana wanajuwa hawakuchaguliwa kwa rizaa za wananchi.

 5. jazz 06/03/2017 kwa 1:34 um ·

  Wache wachimbeni tu halafu kodi ipelekeni Tanganyika…..

 6. Ashakh (Kiongozi) 06/03/2017 kwa 2:58 um ·

  Hata na mie noana huu usanii. Vipi utumie ndege wakati hakuna kikwazo chochote kufikia eneo husika.

  Hata kama mumetia sain lakini bado katiba ya Muungano haisemi hivyo.

  Jaalia mumekubaliana na Magufuli akifa leo, kesho akija Lukuvi akisema mafuta bado ni ya Muungano. Ni kampuni gani yenye ujinga kama huu wetu itakayokubali

 7. Abdul Zakinthos 06/03/2017 kwa 7:36 um ·

  Ukienda Jaws corner kuna gazeti la serikali la mwaka 70’s Karume akiwa na wataalamu wa British Petroleum (BP) Wakimhakikishia kuwa Zanzibar kuna mafuta.

  Juzi tu mwaka Jana imegundulika kuwa kuna mafuta ya kuteka na kikombe wala hayataki kuchimbwa na ma mblock yashawekwa alama.

  Mwinyihaji Makame,alihudhuria mkutano wa kuchimba mafuta baada ya kutokezea ugomvi na Kenya kutaka eneo la bahari lizidishwe na Sheni alienda Uholanzi kutia mikataba sasa mchakato maana yake nini.

  Wapumbavu nyie

 8. zamko 06/03/2017 kwa 8:28 um ·

  @ Salama Abodu

  @ WAZALENDO ( Naomba Samahani nitatoka kwenye Mada kwanza)

  Jamani Mwenzeni Nimegunduwa Kiti ambacho naamini Nyinyi Wengi wenu hamujakiona hata kidogo. Au Kama mumekiona hamukukitilia maananani kama kinaweza kuleta ATHARI ya Majengo Yetu Ya Mji Mkongwe.

  Angalieni hio picha ya Coast ya Mji Mkongwe, Upande wa kulia kwenye ile Hoteli iliokuwa Jengo la Mambo Msige. Mutaona Huo Mjengo wa Hoteli Hio Ni Shape ya CROSS. ( Msalaba). Kwahuku Juu ya anga. Pengine haina taaswira yoyote ile Kidini. Lakini nahisi imetowa Shape Ya Traditional Culture Yetu hasa kwavile Visiwa Hivi vina asili vya Uislamu na Population Yake ni waislamu kwa 98%

  Kama tunanataka Visiwa vyetu viingie katika utalii na majengo yrtu yawe ya kisasa, Kwanini SMZ hawawi Invigilant kama Vile Mfalme Wa DUBAI.?

  Mfalme Wa Dubai wakija Wawekezaji Wanaotaka Kujenga majengo makubwa au Yakile. Anahakikisha yeye na Serikali yake kwamba Kila Jengo Linakuwa na Traditional au Culture Harritage za kiislamu. Na sio Mijengo ya Makanisa au Ya Cross..

  Nikichangia Mada ya Mafuta alioyaona Bi Mtama.Mungu Amrehemu

  Baniani Mbaya na Kiatu cjhake Dawa, hivo kwanini kila kitu Kitolewe Pemba. Kama kweli munataka kuanza kuchimba Mafuta si Mungeanza na hayo yanayotaka Kuibiwa na MABWANA Zenu Waliowaweka kwenye Madaraka ya Serikali ya Mazombi yalioko Fungu Mbaraka..?

  kwanini Mujipeleke Pemba? Hivo Pemba kwani ni Sehemu ya Muungano wa Unguja? Au kwasababu kuna Mafuta ndio wamekuwa Wema.

Comments are now closed for this article.