Maoni ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya Silima
Written by Stonetown (Kiongozi) // 07/12/2012 // Habari // 21 Comments
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya Silima, leo katoa maoni yake katika Uwanja wa Alabama, Shehia ya Miembeni. Katika maoni yake kasema anataka Serikali Mbili, ya Muungano na ya Zanzibar, lakini kila Serikali iwe na mamlaka yake kamili. Akasema pia anataka waendelee kuwepo Marais wawili, wa Muungano na wa Zanzibar, lakini wote wawili wawe na hadhi sawa na wawe na mamlaka kamili. Akamalizia kwa kusema anahimiza umoja na mshikamano. La kufurahisha ni kuwa pamoja na kukwepa neno Muungano wa Mkataba lakini sasa viongozi wahafidhina wa CCM nao wanaungana na Wazanzibari kutaka mamlaka kamili. Sisi tunawaambia wasiwe na wasiwasi, tuko pamoja katika kutetea haki za nchi yetu tukufu ya Zanzibar. Pamoja Daima




21 Comments on "Maoni ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya Silima"
Big up Bora Afya wewe siyo Samaki, Zanzibar kwanza siasa baadae
Chewa kauvaa wavu mbona anaanza kuitingisa Wakojani mvuteni juu tayari huyo….
alikuwa kalewa huyo
anapika gongo mwenyewe
Ndio kwanza anavisikia vigoma vya waamsha daku, naye kaamka kula daku .
Huyu jamaa ni samaki kweli nafikiri hata darasa ka pili hakumaliza. Hata hivyo shule sio hoja wako wengi wasio soma lakini wana akiili zao nikaja. Itakuwaje kuwe na serikali ya zanzibar na ya muungano na zote ziwe na manlaka kamili? Labda amekusudia ya zanzibar na ya tanganyika. Kwa maana hio yeye ndie anaetaka kuvunja muungano.
Haywezaekani kabisa kuwepo muungano waina hiyo baina ya Tanganyika na Zanzibar bila makubaliano maalum . Kwa jina lengine ni MKATABA. NDIO UTAO RATIBU MAHUSIANO BAINA DOLA HIZO MBILI ZILO HURU NA ZENYE MAMLAKA YAKE KAMILI. KWA WALE WANAO JITIA ATI AWAFAHAMU , AU HAWAJUWI NPMUUNGANO WA MKATABA.
ZANZIBAR KWANZA!
hawa wanalijuwa wanalolifanya lakini au watumia mikono yao kujisikia sikia maana kwauhakika nini wanataka haweki wazi wanbania bania na wala msimpe sifa hana la maana hapo alilolisema ni nuksitu na mtaona siku sio kibao hasid
BORAFYA haina haja ya kutafuna maneno! we sema tu ZANZIBAR mamlaka kamili na WANYIKA mamlaka kamili! ukifuatia mkataba wa kuziana vitunguu na nyanya! muda wa kutafuna maneno ushapitwa na wakati.
Kaona walo wengi ndio wa kufuatwa kwa iyo tena ndio mmoja baada ya mmoja msimuache Mansour tu peke yake basi pingine na Shein nae atasema kwa vile ishakua aibu tena yaani kila mtu hataki muungano!
Mimi ufahamu wangu mfinyu juu ya maoni ya huyu Mh.Borafya imenifanya ni mfananishe na mtu aliyepata ugonjwa wa ghafla!! Akapelekwa hospital kuonana na Doctor!! lakini akawa na khofu kubwa sana; pale alipomuona Doctor!! akwa anababaika hajuwi amuelezee nini kimemtokea au tuseme nini kimemsibu, akaanza kuboboja boboja kamavile yuko usingizini anaota ndoto; lakini ya mchana!! lakini kwa vile Doctor ameshabobeya na matokeo kama haya? huwa hapati taabu wala hafanyi ajzi kumtambuwa mgonjwa huyu nini cha mno kilichomsibu na ni itakuwa utibabu wake.
Kwa hivo huyu Mh.Borafya maoni yake ni mfano wa mtu kuzungumka DUWARA, badala ya kutumia njia fupi ya mkato na akatamka bila ya kigugumizi au kutafuna maneno, kuwa na yeye vile vile anataka Muungano wa MKATABA kama vile wanavodai waZanzibari wenzake.
Lakini bila shaka tumefahamu makusudio ya maoni yake. Hainahaja kumlaumu sana!! kwani KIGOMA cha daku kilipopita nyumbani pake? saa hizo alikuwa amelevywa na usingizi, lakini alijimudu kujikokota kokota na akawahi kuila daku yake kwa wakati munasaba.
UJANJA WA WAVUVI:-
Wavuvi walionaujuzi wakuvuwa; wanapomkamata SAMAKI ALIYEMKUBWA ((ALIYEPEA)) kwa kutumia NDOWANA? hawamvuti kwa kishindo; humuachia akatembea tembea mpaka mshipi ukamaliza urefu wake!! huanza kujivuta vuta mwenyewe ijapokuwa ndio anajizidisha maumivu ya ile dowana!! na hatimae humalizikiwa na nguvu na akangojea mvuvi muhusika ili amvute na kumpandisha kwenye NGARAWA au tuseme ((SAFINA))
Kwa hivo tusiwe na pupa wala wahka, hao makada ((WAHAFIDHINA)) waliobakia karibu sana na wao wataingia kwenye URIMBO kwa hiyari yaooooooo!!!!
NAWAKILISHA
MCHONGOMA
UAMSHO WAKO NDANI LAKINI ALLAHA ANAONESHA UWEZO WAKE “INNA-LLAHA ALAA KULLI SHAYY-IN QADIIR”
HUU NI USHAHIDI TOSHA KWAMBA YALE MATUSI WANAYOWATUKANA WAZANZIBARI WENZAO HUWA WANATAKA WAPATE ULAJI KUTOKA KWA WATANGANYIKA LAKINI NDANI YA NYOYO ZAO WANAJUWA KABISA KWAMBA UAMSHO WAKO SAHIHI.
VIONGOZI WOTE WA CCM WAKITOA MAONI WANALALAMIKA KAMA WANANYOSEMA UAMSHO LAKINI HAWAWEZI KUSEMA “TUACHIWEEE TUPUMUEEE!!!!!!!!!” MAANA WATAKOSA ULAJI,
HUU NDIO UNAFIKI WAO NA MAJIBU YA ZILE DUA WAISLAMU WALIZOOMBA, MWENYEZI MUUNGU ANAWAFICHUA MMOJA MMOJA.
SASA TUMUULIZE MOHAMED ABOUD, KAMA MAWAZIRI WANALALAMIKIA , WAKEREKETWA WANALALAMIKA( BORAFYA NA WENZAKE) JUU YA MFUMO WA MUUNGANO NA HAIKUWA NONGWA MBONA MASHEKHE WAKISEMA (UAMSHO) MNAWATIA NDANI? NYINYI SI MNATAFUTA LAANA ZA ALLAH KWA MAKUSUDI???
INSHAALAAH KWA BARAKA ZA ALLAH ZANZIBAR HURU IKO NJIANI, TUENDELEE NA UZI HUO HUO WA KUDAI HAKI POPOTE BILA YA KUTAFUNA MANENO.
WABILLAHI TAWFIK.
kuwepo au kutokuwepo mamlaka kamili ikiwa kuna serikali mbili ya tanzania na ya zanzibar bado hatuja fanya kitu isipoku iwe serikali mbili tanganyika na zanzibar la sihivo zanzibar haitokuja juu kama ZANZIBAR itakuwa ipo chini ya tanzania tu.
mi nasema mara nyingi viongozi wote wa Zanzibar hata hawa viongozi wa SAMAKI wanayajua madhila ya muungano huu dhalinu tatizo lao ni kuogopa kusema ukweli hadharani sababu wamepata huo uongozi kwa njia aidha dhulma kama sheni urais wa kuibiwa,,ama amepewa kupitia tangayika hivyo akitamka kinyume na maoni ya waliomueka atakosa nafasi manake hana hadhi ya kuepo pale.
isipokuwa wale viongozi wa samaki ambao wao ni watanganyika baba- mama hawa husema moja kwa moja manake wanajua Zanzibar sio kwao hivyo hawana la kukosa ikipotea kabisa, mi naamini borafia alitia ndio kura ya serikali ya umoja na naamini pia yakija mawazo kuwepo serikali moja tu atatia hapana manake anajua madhara hata hiyo GONGO yake itabidi akaikatie kibali tanganyika.
Ni tu kwa sababu Borafia ni mwanasiasa na saa nyengine hata asiyeonesha kumwogopa Muumba wake na hatujaona dalili za kutubia inatupa mashaka kumwamini 100% hata ikiwa wengine tunataka kufanya hivyo.
Hal mwenzetu keshaona kuwa Zanzibar Huru iko njiani na ulwa bado atauhitaji? Au ni kutapatapa tu? Au ni MUUMINI wa kweli ambaye anaumwa na nchi yake kutawaliwa?
Time will tell…laakin ala ala mti na macho!
Tuombe kheir
Hii habari nina mashaka nayo. Borafia itakuwa alikunywa kibuku kabla hajaenda kutoa maoni.
Kwakiasi kichache tu ninachomjua huyu mzee,ni kwamba hata maka kaongea maneno yote hayo au zaidi yake,binafsi nasema kazungumza kutoka mdomoni na sio ndani ya nafsi yake japo kua binaadam anabadilia muda wowote hapa kwa borafya ngumu sana.
Simuamini.
ITAFAHAMIKA TU INSHALLAH
hakuna serikali ya mkataba ila kuna mkataba wacha na ziwe hizo serikali mbili na Tanganyika iwe inaitwa Muungano lakini yetu iwepo pale pale inayoitWA ZANZIBAR-Safari hii raha tupu hata kura 2015 naona watu wataandika mkkatabaaa badala kuchagua wagombea.
Wallahi ukimuona huyu Baradhuli Afya vile vidole anavyotowa akianza kutukana utafikiri anagombana na mke mweziwe. Kidole jichoni. Si wakumtia maanani huyu si rizki hafai pesa moja.
Assalaamu Alaykum.
Inachekesha. LAKINI JAMANI:-
Kweli huyu ni BORAFYA na sio AFYA BORA haaminiki lakini, tusimvunje moyo.
Kwani kutetea maslahi ya Zanzibar ndio lengo letu na ndio shida yetu kwa mtu yoyote, sasa kama kaamua kuwaacha mkono Wanakisonge wenziwe na kuungana na Wazanzibari wenziwe ndio kosa au ndio sahihi kama watakavyo waliowengi?.
MUUNGANO HUU HATUUTAKI.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.
“When peacea fails apply force’
Nawasilisha.
Serelly.
Ni sawa na kujamba majini borafia, unajaribu kuficha ushuzi lakini mabofu yanakuja juu,pale ni wewe na warioba tu wazanzibari wako pembeni wanakutizama ukijikanjaga na kujitafuna vidole,
wariaba sijui alikuwa wapu akakuuliza utowe ufafanuzi,ila mimi sasa ndio nitakuwa warioba
swali———- .je unataka serekali mbili ya muungano na yazazibar kwani serekali zipi zilizoung ana na kupatikana muungano hata leo ukasimame na kuutaja muungano kama ni serekali mmwenza na zanzibar.mimi nilisubiri ile mechi ya tanganyika na zanzibar tatavaa jazi gani tanzania ua muungano wakati sisi tumevaa zanzibar .hawakufanya makosa wabongo ila wahafithina wakizanzibari ndio wanachezehwa vibwebwe.
Sema nataka serekali mbili huru tanganyika na zanzibar zenye mamalaka kamili, utafahamika unataka nini ikiwa hutaki mkataba.
Heri Borafya kajitutumua kutaka raisi wake na serikali yake iwe na MAMLAKA KAMILI.Maana Shamsi Vuai Nahoda yeye kataka mambo yabaki kama yalivyo ila mambo ya muungano yapunguzwe na ushirikiano wa kimataifa zanzibar waachiwe ,lakini mafuta yabaki kuwa ya muungano,na ulinzi kwa sababu yeye ndiye waziri wake hivi sasa .Maslahi tumbo yayana wasumbuuwa wazanzibari