Malkia wa Nyumbani

Written by  //  28/01/2017  //  Vidio, Habari  //  Maoni 6

Habu sasa tujikumbushekipindi kile ndio kwanza nahamia Unguja. Wakati huo taarabu ilikuwa katika “maximum peak”. Licha ya udogo wangu wakati ule nilikuwa na upenzi mkubwa wa taarabu kiasi kwamba nilikuwa nafuatilia na nazijuwa baadhi ya nyimbo.

Mwaka 1987 nakumbuka nyimbo ya “Nimesalitika” iliyoimbwa na Sihaba Juma, “Pendo linaloelea”, nk. Mwaka 1988 ndio pale Abdalla Issa alipokuja na “Mthamini wa Pendo”, Maulid Mohamed “Chorichori”.

Najuwa wapo magwiji wanaojuwa zaidi, sasa nampasia Sh Rashid Seif atupe zaidi.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 6 katika "Malkia wa Nyumbani"

 1. rasmi 28/01/2017 kwa 7:00 um ·

  Ahsante mzee kwa kutupeleka kwetu, ‘ntu n’kwao’. Love Zanzibar -Bin Seif.

 2. jazz 28/01/2017 kwa 7:45 um ·

  Maashallah…1988 nawaona warembo,wachuchu na wamevaa mabaibui ya asilia,wanawake wako huru bado mambo ya kulazimishwa lazima wavae hijabu hajaletwa Unguja…

 3. shawnjr24 28/01/2017 kwa 9:10 um ·

  @Ashakh (kiongozi) au mtu yeyote humu.
  Kuna wimbo huu kama unamjua muimbaji au kama unao au unayo link yake naiomba. Inaimbwa hivi:-
  Ewe swahiba mwandani nisikize ninayo sema. Huyu muimbaji anatokea Dubai au Muscat sina uhakika.

 4. brenda 29/01/2017 kwa 7:12 um ·

  Inna lilahi wainna ilayhi rajjiuuun, keshatangulia mwenzetu na wengine wengi Allah awasamehe makosa yao Yarrabil alameen

 5. brenda 29/01/2017 kwa 7:55 um ·

  @ Jazz

  Assalaam aleykum

  Mdogo wangu, rudia tena messege yako hapo juu,

  kwa karne tulonayo sasa, ni khatari sana kusema kua, wakati huo wananawake walikua wako huru na bado mambo ya kulazimishwa lazima wavae hijabu haijaletwa Unguja.

  Mimi….. kama ni mwanamke wa kiislam nimehuzunika sasa kusikia kauli hii, sijatarajia kusikia kauli kama hii kusemwa na mtoto wa kiislam wa kizanzibari,
  Kwani hijjab ni Vazi la mwanamke wa Kiislam tokea enzi ya Bwana wetu Muhammad rehma na amani zimshukie miaka 1438 iliyopita, na tokea wakati huo wanawake ni warembo mpaka hapa tulipofika bado ni warembo pamoja na hijab zetu, sijui kwa upande wako unamtazamaje mwanamke asiekua au asievaa hijjab, kwangu mimi nakhisi na najua kua ni Kharaaam

  kuna sura nzima katika kur aan…. Suratu An Nisaa(The Women) angalia vipi Allah alivotutukuza na alivotupangia sheria na mipango mizuri mizuri, tokea kivazi, kurithi, kuoa na kuolewa na mpaka namna ya kuongea nao kwa upole.
  Sentesi kama hizi hukumbana nazo watoto wetu katika skuli za kikafiri

  wabillahi Tawfik

  Allah atuongoze maana yake ni kua sote ni wakosaji na atujaaalie ni wenye kukumbushana mema na kukatazana mabaya

  samahani sana kama kuna mtu nitamkera…..sio matarajio yangu

 6. sadimba 30/01/2017 kwa 11:31 mu ·

  @brenda

  Kwanza naomba uniwieradhi huna uhakika kama huyu jamaa ni muislamu pengine ni kundi la kina doctor Abdallah na maana kwa mtu mwenye hulka ya kiislamu huwezi kuzungumza kama hivi. Naomba muachie mwenyezi mungu usiingie kwenye dhana ya kufikiria ni mtu wa hulka na na kufuata tabia ya mtume muhammad kumbe ni kinyume.

  Lakini kwa mtazamo ni katika wale waliopofuka kwa chuki na nyoyo zao zina maradhi na husda dhidi ya wazanzibar mwenyezi mungu anatosha kumuonesha ukweli.

Comments are now closed for this article.