Majibu ya kiprofesa mwenye(Phd)

Written by  //  04/05/2017  //  Habari  //  Maoni 8

1. Lipumba: Sikushiriki kumkaribisha Lowasa
Mtangazaji: Mbona ulionekana kwenye mkutano wa
kumkaribisha Lowasa?

2. Mtangazaji: Kwanini ulivamia ofisi ya CUF
Lipumba: Sikuvamia
Mtangazaji: Nani alikukabidhi ofisi ambayo hukuwepo
mwaka mzima.

3. Mtangazaji: Kama unasema mkutano ulivurugika, ni nani
aliekubali barua yako ya utenguzi na wewe kurejea
kwenye uenyekiti?
Lipumba: 😖😣😣😣😣

4. Mtangazaji: CUF ina wabunge wangapi?
Lipumba: (anajikanyaga)
Mtangazaji: Kwanini kati ya wabunge wote hao
wanaokuunga mkono ni wawili tu?
Lipumba: Maalim Seif ni mbabe sana

mengine naogopa kumvua nguo kwa ambao hawakuangalia 360

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 8 katika "Majibu ya kiprofesa mwenye(Phd)"

 1. kwaomtu 04/05/2017 kwa 3:47 um ·

  Kwa maelezo ya Lipumba kama kweli MIKAFU mulikubali Mazrui atengue barua yake ya kujiuzulu na ikiwa pia uchaguzi wa Baraka Kuu haukufanyika basi mumekwisha. Siasa ya vyama mbaya na haina ila njaa na dhambi. Bora muingie kwenye siasa ya dini inayoendelezwa na UAMSHO itakomboa Waislamu na kuikomboa Zanzibar.

 2. MAWENI 04/05/2017 kwa 7:40 um ·

  Kwa mara ya kwanza tokeya sisa ya vyama vingi kuanza ” Tanzania” , uchaguzi wa 2015 ulikuwa zilzala kwa CCM. Sababu ni umoja wa upinzani. Na kupata baadhi ya vigo vya ccm kingia upizani na wengine kukaa upande. Shina la ccm lime tikisika . Ukiimarika upinzani zaidi ccm itanngoka tu.
  Hatari hiyo wameiyona ccm . Kwa hivyo moja katika mikakati ya ccm wakishirikiana na Usalama Wa Taifa wanamtumia huyu Lupumba kuvuga upinzani. Cuf ndio chama madubuti chenye malengo yalo wazi.( Ambayo hayo tobadilika kwa wazanzibari kutokuwa na chama kilo sajiliwa kwa msharti ya ccm)
  Lupumba ukibaraka wako na utimbakwiri ; hauto wazuiya wazanzibari kupiganiya nchi yao ILO HURU NA MAMLAKA YAKE KAMILI.
  Hata kwenye nyazifa za kawaida ukijiuzulu au kuhama na kwenda kwengine , ukitaka kurudi, utaambiwa upeleke ombi lako upya . Ni juu ya hao wanao kuajiri kukubali au kukukataa . Ati tunaambiwa huyo ni proffessor. Awafanya watu wote majahil.

 3. Elbattawi 04/05/2017 kwa 10:38 um ·

  ‘Mwisho wa maji ni tope’. Labda fumbo hili ndilo linalomfaa Lipumba. Kusema kweli ndani ya CUF, pande zote mbili (Bara na Zanzibar), Lipumba alipata heshima na kuheshika kwa kiwango cha juu.

  Lipumba mwenyewe hakuitaka heshima aliyopewa na CUF, (viongozi na wananchama) na ameamua kujivua nguo hadharani au nisema amejivunjia heshima yake mwenyewe. Kwa hivyo, yanayomkuta sasa ni chaguo lake kayataka wacha yamfike.

  Kuna ule msemo: ‘Mkataa pema pabaya panamwita’. Lipumba, ajitutumue kama mvumo au ajikuze kama ‘Mlima Kilimanjaro’ hashima yake ya Uenyekiti wa CUF (kabla ya August 5, 2015) ataondoka duniani hataipata tena.

  Kadhalika, hata heshima yake ya usomi wa kiwango cha uprofesa (PhD holder), ameipoteza na si dhani kama ndani na nje ya Tanzania, ataonekana kuwa ni mtu wa kuaminika. Amejitoa maana kitaifa na kimaifa.

  Lipumba, kachagua mwenyewe mlango wa kujidhalilisha na kujivunjia heshima. Kwa mtu kama Lipumba, alitakiwa kuwa na uwezo kuangalia kwa miaka 50 faida/hasara za kutumiliwa kabla ya matukio anayo yatenda sasa. Lipumba ana hali mbaya, isipokuwa anajikaza kisabuni tu.

  Nina wasiwasi sana na Lipumba kwamba, huko mbele ya safari anaweza kuwa mgomjwa wa akili. Haonekani machoni kuwa yuko timamu ki-akili.

  Hawezi mtu kuwa msomi kwa ngazi ya u-profesa, akawa tayari kutumiwili na watu aliyowazidi kwa elimu. Bila shaka, huyo atakuwa na tatizo la akili.

  Nimesikiliza majibu ya maswali aliyoulizwa, nimemuona jinsi anavyo hangaika na kupaparika kujibu. Kwa ufupi, anaonekana wazi wazi kwamba ni mtu aliyechanganyikiwa, mawazo na akili.

  Ni mnafiki asiye na doa, ni mnafiki aliyekamilika aliye tayari kusababisha maafa kwa binadamu wengine, au atakuwa hajui analofanya na analosema. Mwenyezi Mungu, amuhidi..

 4. mzeekondo 05/05/2017 kwa 12:15 mu ·

  Elimu bila pesa huwa shida kubaki na misimamo hasa ukiwa masikini,nakumbuka zamani wazee wetu wakitusisitiza “someni wangu mpate elimu, muwe na maisha mazuri kuliko haya tuliyonayo sasa” Tanzania usomi peke yake haukuwa wala haitokuwa dawa ya kuuepuka umasikin,tujiulize kwa nini wasomi wote wenye vyeti na madigirrii na udaktari au uprofessa karibu wote ukifika wakati wa kugombea ubunge,uwakilishi nk utawakuta huko na hawazitaki tena taaluma zao?

  Siasa ndio taaluma kwa nchi hii,na huo msemo wa ‘someni mpate elimu ili muwe na maisha mazuri’ ilikuwa usiishie hapo tu,”katika siasa”walisahau wazee wetu kuliona hili.kama elimu ni dawa ya kuondoa ujinga, basi hapa dawa hiyo imekosekana, huyu kasoma kujineemesha kwa namna yoyote ile, ndio maana ametengua uamuzi wake wa kujiuzulu, kama vile alijiteuwa mwenyewe.vyama vina katiba,kanuni na miongozo yake hata mimi siku soma siwezi kuyafanya haya ya bwana huyu bila kuangalia katiba husika,tuchukulie alilosema kuwa ni kweli, kuwa Mazurui aliwahi kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu,sasa kama Mazurui kafanya hivyo, basi na wewe Professa umemuiga? jee ikiwa mazurui hana elimu au kichwa kitupu, basi na wewe huna hata za kuvalia nguo?

  Huu mfano dhaifuu umeutumia Professa, mtu mwenye kiwango cha elimu uliyonayo, ilikuwa ujue kuwa hii ni sababu au EXCUSE ya kitoto,kwa nini umempiga mwenzio? amenianza yeye huyo, na mimi nimemrudishia… you got the idea.

  PUMZIKA ‘PRO-PESA’ SIASA IMEKUSHINDA.

 5. Jino kwa Jino 05/05/2017 kwa 6:48 um ·

  Huko mahakamani lipumbavu litashinda na kafu haitafanya chochote na huenda chama kikafungwa sisem wachawajaribu kafu vya kutosha hawana tishio lolote jecha mmoja tu kawashinda anadunda mitaani sasa sisem wamempa lipumbavu mpira ili na yy ashinde wao mwisho ni kugoma tu usipoweza kupigana nae basi join nae hamuna mikakati yyote kazi yenu ni kutanganya watu toka 1995 hamna harakati yyote mmechuuzwa eti musiingie uchaguzi mara ya 2 mmefanya makosa makubwaa sisem wanapeta vizuri BW kwa raha zao .Hamupewi serikali kwenye kisahani abadan .Sisem wameeleza wazi wazi bila ya kutafuna maneno na kuapa munataka pindueniiiiiiii

 6. Mrfroasty (Ufundi) 05/05/2017 kwa 7:59 um ·

  Siamini kama huyu mtu ana elimu ya uprofesa, kakwepa maswali ya msingi kabisa.Niseme tokea zamani sikuwa na imani nae.Sasa hivi ndo naona kama instincts zangu zilikuwa sahihi kabisa.Ni msaliiti huyo kaalikwa ikulu na Magufuli, toka lini paka na ……

 7. Tengoni 06/05/2017 kwa 12:12 um ·

  CUF wajuwe kuwa siasa ni mchezo mchafu, ukitaka ufanikiwe kwenye siasa basi lazima uchafuke, unuke.Tumuangalie Mwalim Nyerere, licha ya sifa shadow sifiwa lakini bado aliucheza mchezo mchafu. Nyerere alikuwa bega kwa bega na Hanga kuandaa mamluki, waliokuja saidia mapinduzi, lakini wapi, kwa maslahi mapana ya Tanganyika, alimnyonga Hanga. Karume nae alishibana na Nyerere, akafikia kumhonga Nchi, Karume alipoonyesha dalili za usaliti kwa mtazamo wa Nyerere, Nyerere ha, kumpeleka Karume mahakamani, Nyerere alifumbia jicho mpango mchafu, na Karume akenda na maji. Nyerere alimvaaJumbe, Jumbe akasabilia mengi, mashallah, kwa kutegemea Urais wa TZ, 1980, Kumbe kadanganyika, aliposaliti kwa mujibu wa Nyerere, Nyerere hakumpeleka Jumbe mahakamani, ponea yake alimfunga gerezani nyumbani, bila simu , gazeti, wala asitembelewe na mtu, yote hayo machafu, Nyerere aliyafanya kwmaslahi mapana ya Tanganyika, na kabla hajafa kamuusia Mkapa na wenziwe kule St Mary London kuendeleza mchezo mchafu ikibidi ili Zanzibar idhiibitiwe na Tanganyika milele. Sasa kama viongozi wa CUF hawataki mchezo mchafu, ambayo ndio siasa yenyewe,basi watasota sana mahakamani na kuchezewa na kina Lipumba na Jecha. Lipumba wakuekwa eda kama ile aliyowekwaJumbe, kama alipofikishwa Hanga na Karume haiwezekani, ndio mchezo wenyewe.

 8. Jino kwa Jino 07/05/2017 kwa 3:56 mu ·

  @ Tengoni Umezungumza lugha ya Kamaria lugha ya mwezini ambayo cku zote maneno hayo yapo kwenye ulimi wangu nashindwa kuyapanga na kuyaelezea Hekoooo Tengonii. Nimekusoma na nimekuelewa ni kweli kabisa CUF hawawezi kufoce mambo na huo ndio udhaifu wao na watabakia hivyo hata kama ni wingi wa aina gani wao na UKAWA wao juzi ktk cloud eti anajisifiya kwamba yy ndio anaoifanya hali kuwa salama ebooo maneno gani ya kitoto haya unazungumza Mchuzi wa kondoo unywe ukiwa moto ukipoa haunywekii ,hata hao wazungu wanaokusaidia watakuona mwehu nchi ipo salama haina harakati ya aina yyote maisha tu magumi watamwambia subiri 2020 .Maadam wao wanaingia asubuhi najioni hakuna khofu yyote Balahau umeokokona msooo>miaka ya 40 yote uliopigania siasa Umewafakisha wapi wazanzibari bado wamekuwa madhalili na wamezidi kuwa chini ya udhalili wameuliwa bila ya kujitetea wamepigwa na kuendelea kupigwa wananajisiwa kila aina ya uchafu .Nakupa mfano wa Ukweli URITREA miaka 30 tu leo wamekuwa huru weye miaka 40 hamna lolote Nenda ukasome URITREA watakupa siri ya 30 yrs.Unataka kula tu hutaki kulima ,lima kwanza ili upate kulaa.

Comments are now closed for this article.