Magufuli acha maneno, fanya vitendo: naona huwezi kukata umeme Zanzibar

Written by  //  06/03/2017  //  Habari  //  Maoni 11

Taarifa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuitaka Tanesco kuikatia umeme Zanzibar zimeenea katika vyombo kadhaa vya habari. Magazeti, mitandao ya kijamii vimemkariri Magufuli akitoa amri hiyo mbele ya hadhara.

Wengi wa wananchi wanaona kwamba Magufuli hana maskhara katika kauli zake. Naweza kuwa peke yangu mwenye mawazo tofauti wa hayo.

Nilichokiaona nikuwa Magufuli hawezi na huthubutu kuikatia umeme Zanzibar kwa madai ya kudaiwa. Labda alikuwa akistarehesha barza au kutaka watu wacheke.

Licha ya kufanya baadhi ya kutumbua majipu, bado Magufuli hana ubavu wala mamlaka ya kuinyima umeme.

Kwanza ununuzi wa umeme ni mkataba wa kibiashara baina ya nchi mbili, Zanzibar (mnunuzi) na Tanganyika (mchuuzi). Hivyo lazima kuwe na heshma kwenye makubaliano baina yao.

Pili Zanzibar, imeanza kuwa na umeme kabla ya Tanganyika. Hivyo njia walizopitia hadi kumiliki zinajuilikana kiasi kwamba kwa kitisho cha kukatiwa hakiwezi kufuadafu.

Licha ya unyonge wake, Zanzibar inaouwezo na mbinu za kujitoshelesha kupata nishati mbadala.

Magufuli kama kweli asemalo ndio afanyalo tusubiri kesho tuone umeme umekatwa. Vyenginevyo wananchi wataamini na nitazidi kuamini kuwa ni yayo kwa yayo, maji ya futi na nyayo.

Langu jicho, Ngosha nasubiri ushahidi kamili

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 11 katika "Magufuli acha maneno, fanya vitendo: naona huwezi kukata umeme Zanzibar"

 1. maalim 06/03/2017 kwa 4:27 um ·

  Hahahahahahahahahaaaaaa
  NI RAISI WA AJJJAABUU.

  Naona usaniii wake unazidi kuendelea kila kukicha.
  Awamu hii tutaona na kusikia mengi.
  Kutumbua majjipu, kutumbua mapele, kukata umeme, na mengine yatakuja.

 2. sadimba 06/03/2017 kwa 4:35 um ·

  @Ashakh
  Mawazo yako ni sawa na yangu kwanza viongozi wa nchi hii ni wasanii wanapenda wazungumze kufurahisha wenzangu mie warubuniwaji wa vitenge na fulana wa kicheka na kupiga makofi tayari wameshatekeleza sera zenye matumaini. Hata watangulizi wake walikuja kwa gia nzito baadae tukajiuliza kulikoni kumbe ni nguvu za soda tu.

  Aliingia kwa style ya unesi wa kutumbua majipu, lakini jipu la Makonda limemshinda kwani itatuchukua karne moja kumpata kiongozi wa ccm muadilifu. Suala la Zanzibar yeye ndio ameliwekea ubeleko na alimtuma babulii akichokozwa tu aseme sasa leo anataka kutwambia mwanawe keshamuachisha. Hebu mvinyo bin makomeo kama ni mtendaji kweli fanya vyenginevyo tutajua ni yeye kwa yeye na kuamini hujui unalotenda ila kubwabwaja na kufanya ucomedy.

 3. Piga nikupige 06/03/2017 kwa 6:40 um ·

  Magufuli au tukuite Magufuru, wew ni mshamba na mpenda sifa za kijinga tu. Wafanyie mijisifa yako hao Ngosha wenzasko na huko Unyikani kwenu.

  Magufuli kwa suala la kuikatia umeme Zanzibar tunasema kwa kinywa kipana Huthubutu huthubutu huthibutu, na sio wewe tu hata angekuwepo Nyerere asimgethubutu wala asinge kuacha burebure lazima angekukaripia, kwani Watanganyika wamebeba ajenda mbaya mno dhidi ya Zanzibar.

  Huo umeme wenu ni miongoni mwa chambo kinacho tumika katika kuwapa wanamapinduzi utulivu fulani ili mpate kuendeleea kuangamiza Zanzibar.
  Namalizia kwa kusema Magufuli kama unajiamini kweli na kwa unavyo jigamba kwamba huogopi mtu.
  Sisi tunakwambia ubabe wako si kwa suala la umeme, kwa hili hutubutu huthubutu huthubutu, hata muunganishwe Watanganyika wote katu hamtothubutu kuikatia umeme Zanzibar.

  Ulikuwa unajifurahisha tu Suala la Umeme Zanzibar ni zaidi ya Uraisi wako huna ubavu huo kama huna la kusema kaa kimya.

 4. Abdul Zakinthos 06/03/2017 kwa 7:32 um ·

  Mashuzi ya Bata

  Ni chuki zake tu binafsi kwa matajiri ,ndio zinamuendesha nyege zake..

  mwache ajifurahishe

 5. Reyhana 06/03/2017 kwa 10:09 um ·

  Kumradhini humu ndani, Tena nyege si za kitoto za utuuzimani. Kata uone Kelbu wahed wewe. hapo ndio tutakujua wewe mwanamme au ukifika chumbani mama Jesica ndio anavaa suruali wewe unafunga kanga ya kiuno. Mjinga sana huyu kichwa cha korosho ee. Eti kateni umeme Zanzibar.

 6. salali 06/03/2017 kwa 10:48 um ·

  Akikata umeme na kumuweka kiza kummadoo wa udongo basi na muungano Wanaukata. Kwaheri (CCM) – Tanesco karibu – (ASP).

 7. abuu7 07/03/2017 kwa 5:54 mu ·

  Kuna kitu wanataka kufanya hawa. Iko namna hapa .pengine wanataka kufanya mapinduzi madogo wazime umeme wapate kumuuwa Rais wetu MALIM SEIF
  Hata hivo jaribu kukata umeme kama wewe mwanaume kweli. Wee si useme tu vunja muungano ya nini yote hayo kukata umeme .

 8. zamko 07/03/2017 kwa 2:42 um ·

  @ Asheikh

  Ahsante kwa Makala yako Yenye Ukweli Mtupu kabisa lakini Sababu zetu Zitaweza kutofautiana na sio hizo za Mteja na Mchuuzaji. Lakini kubwa nilaloliona kwenye Statement yake ni kwamba Huyu Mzee Wa Pembe anahaiba ya COMMEDY na hapo alikuwa katika kuwafurahisha Washika Veli. MAGU hawezi Kuikatia Umeme ZANZIBAR hasubutu Hasubutu Hasubutu.

  Kwanini Magufuli hawezi Kuukata Umeme?

  1. Kwasababu Kwanza hawezi kumkera Muuza Nguru akakosa Mchuzi. Kwa Tanganyika Zanzibar Ni Koloni Lao Hivo Wanahiari WAIPIGE CHUCHULI Huku Kina Babu ALI na Mazombi Wenzake Wakijiachia Hadi Mikono na Denda Likiwatoka. Lakini Mkoloni Hata kama Kachoka Kubeba hata Utuwa Mzigo Wa Zanzibar mpaka Ahakikishe Visiwa Vimebaki Na WAKURYA na Beach Zote Zimeenezwa Vilabu Vya POMBE.

  2. Sababu ya Pili, CCM na Uongozi wa Tanganyika Kuendelea Kwake Kunategemea Zanzibar Kuwa na Machafuko. Hapo Uongozi Wa Tanganyika na Viongozi Wake Watakuwa na Afya nakuendeleza Nchi yao. Suali la Kuukata Umeme Zanzibar kwasababu Ya kutolipa Inaweza Kuja kuiweka Tanganyika Pabaya. Kwani Hao Waliobebwa Watatumia Majenereta lakini Wenzangu mimi ambao ni Wfanya Biashara na Vibaraka wengine Wa CCM wanaweza Kukihama Chama na Kuungana na Wazanzibari Waliowengi Kudai HAKI yao. Hapo hilo Linaweza Kuwa Kosa kwa Tanganyika

  Kama nilivosema Awali Tanganyika Haitaki Wazanzibari Washikane na Suala lakuukata Umeme Linaweza kuwaweka Wazanzibari pamoja.

  @ Sadimba
  Kama alivosema Sadimba Nchi Hii ina maajabu kuliko ya Firauni Tunayaona Mengi na Mengine yanakuja. Maana yule Kibaraka Wao Lipumba ( Ati) Kamfukuza Maalim Nafasi ya Ukatibu.. Who are YOU Lipumba?…

  Zaidi Tuwaache CCM Wakiendelea Kujitekenya Huku Wakicheka, na Kuipeleka Nchi katika Giza. Naamini Kuna siku 1 tu Wananchi Watafika pahali Watasema Enough Is Enough. Na siku hio Haiko Mbali Inshallah.

 9. Asili haipotei 07/03/2017 kwa 5:55 um ·

  u are not serious Magu and now i know u are really comedian na sio comedian wakawaida tu yule mpenda sifa ila kata tu itakua umetusaidia pakubwa sana kwa wale wachache waliobakia ktk ile agenda yenu yaukoloni mweusi kuitawala zanzibar watakua wamefunguka vichwa kdg na pia utakua umempatia muangaza mzuri raic wetu ajae wazanzibar kipenzi cha wazanzibar kulifanya hili suala la umeme kuwa kipaumbele chake kutupatia umeme wetu zanzibar pumbavuuu

 10. Abdul Zakinthos 07/03/2017 kwa 8:42 um ·

  Subirini Umeme utakavopandishwa na pia Sio Tanesco watakao kata umeme ni ZECO
  mtaona hata ukidaiwa elfu 10 basi utapigwa mkasi

  halafu nauliza tena

  Kuna maana gani ya kuwepo shirika la umeme Zanzibar? kazi yake ni kitu gani?

 11. mzeekondo 09/03/2017 kwa 4:48 um ·

  Umeme,umeme kata umeme kwani unamtisha nani Magufuli?asili ya Chato kwenu iliyopo mkoa wa Geita,ambayo zamani ilikuwa wilaya ndani ya mkoa wa Mwanza, hakukuwepo na nishati hii,Chato ilikuwa ni kijiji tu, kwa asili hiyo Magufuli ulisomo shule na kuishi katika giza,kibatari,jua,kandili,karabai,mshumaa ndio nishati zilizokupa wewe kiburi au jeuri ya kusimama leo jukwaani huko Mtwara, na kutoa amri ya kuikatia umeme Zanzibar, kwa kuwa hatuna fadhila na hatutaki kulipa deni kwa mkoloni TANESCO.

  Mimi nakuomba na nakuangukia miguuni, na hii sio desturi yangu kufanya hivyo, shughuli hii huifanya kwa Mola wangu tu, sio watu au binaadamu wenzangu ambao hudhani vyeo vyao au sura zao ndio vigezo sawa na utukufu, nakuangukia ili “UUKATE” umeme haraka hapa Zanzibar, ili hawa vibaraka ulio waweka hapa kutunyanyasa kwa niaba yako, waelewe kuwa wewe huwathamini na hutowathamini,unawaona kama wanavyostahiki kuonekana kuwa wao ni watu tu, ulio amua kuwatumia kuwatesa ndugu zao{Wazanzibari}

  Deni gani unaloidai Zanzibar?Zanzibar wanaidai Tanganyika fedha kiasi gani? tangu mlipoamua kuviibia visiwa hivi pamoja na rasilimani zake zote, ikiwemo fedha taslimu za kigeni mlizozichukua kutoka mfuko ule wa sarafu za nchi za Afrika mashariki ulipovunjika,Tanganyika mkachukua sehemu au hisa yenu, pamoja na ile ya Zanzibar pia mkaiweka katika jina tukufu la Tanzania,nyinyi ndio hamna utamaduni wa kulipa madeni mnayo daiwa na Zanzibar sio kinyume chake.

  Mlikubaliana kutupa asilimia 4 na kitu ya misaada yote inayokuja nchini kwa jina letu tukufu,kwa miaka zaidi ya hamsini sasa hamjawahi kutufa hata asilimia 2,sasa nani mwizi hapa? fanya hesabu ya mapato yote mnayotuibia sasa na mliyotuibia tangu tuungane kwa nguvu, kwa sababu hakuulizwa mwananchi au raia hata mmoja wa upande wowote,ukipata jumla yake,chukueni hizo BiIllioni 121 mnazo tudai za huo unene,zilizobaki Billioni zisizohesabika, tafadhali tuwekee katika akaunti yetu kwenye banki ya watu wastaarabu wa Zanzibar haraka,kama huwezi kufanya hivyo basi kinywa chako unaweza kukifunga kuzuwia harufu na matamshi yasio na mashiko.

  Wananchama wa chama chako unachokiongoza,wewe ukiwa kama mwenyekiti wa ccm hapa visiwani wanahesabika,sasa kama na wao huna haja nao waweke katika giza uone kama hukuja mwenyewe kupiga kura laki tatu huku ukisaidiwa na CDF Mabeyo msukuma mwenzio, uliemchagua aliongoze jeshi, akulinde wewe pamoja na koloni lako la Zanzibar.

  Sisis hatuna hajana umeme Zanzibar ina uwezo wa kujipatia nishati hii na ikajitosheleza boila kukutegemea wewe Magufuli au Tanesco,tatizo ni hawa wenzetu unao watumia hapa hawana maamuzi magumu,tamaa ndio udhaifu wao,mimi hujiuliza seychelles,Mauritius na visiwa vyengine vilivyopo ukanda huu wao wanapata pia umeme wa Tanesco toka Tangayika? kama hawapati sasa wanajiendesha vipi? kumbe upo uwezekano wa kutumia nishati ya jua kuzalisha umeme pamoja na bahari, sasa hawa Tanesco wana mringia nani hapa?ni viongozi wetu wabovu ndio mnao tuzidishia matusi ya kila siku kutoka kwa Sultani mweusi.

  Kabla huu umeme wako mtukufu haujawasha majiko yetu huku sisi tuikuwa tukitumia kuni za mkarafuu nk kupika pilau na kusongea halua kwa raha zetu,hatukuwa na dhiki wala misiba ya ovyo,umasikini tuliuzowea kwa kuwa ujamaa ndio siasa ya nchi hii miaka yote hii,sasa hata ukiukata umeme sasa hivi hizi video,maluninga na computer tutazitumia tu hata kwa kutumia mafuta ya taa au karafuu,bora shida iwe hiyo kuliko kusengenywa na mkoloni kila siku kwa kuwa yeye umeme kaujua ukubwani.

  CCM zanzibar tangu utoe amri ya kukata umeme,hakuna anae lala akapata usingizi,tunaogopa mengi lakini sio popo bawa,tunahofia mpaka hawa viongozi wa SMZ huenda na wao wakaanza kuurudia uke mtindo wao wa zamani, wa kuwa na kadi mbili mbili,yaani asubuhi wakiwa majukwaaani na kweupeni wao ccm, lakini ikiingia magharibi na giza, hugeuka wapinzani wetu,sasa mzee wa amri na matusi ya reja reja, unanifanya nimeanza kuamini kuwa CCM itakufia mikononi mwako,na ukiiuwa ccm, ndio umeinyonga Tanzania, na ukiinyonga Tanzania, ndio umeifufua Zanzibar,na ukiifufua Zanzibar ndio umeuuwa Muungano, na ukiuuwa muungano, NDIO umetusuuza au kutuweka hoi sote Wanzanibari, sasa na tuache maneno….

  “KATA UMEME.” msukuma.

Comments are now closed for this article.