Maafa yakuepukika ikiwa tutazingatia usalama wa bahari na anga kama ni kipaumbele

Written by  //  18/07/2012  //  Habari  //  Maoni 9

Nianze kwa kutoa mkono wa pole kwa wazanzibari na watanzania kwa jumla kwa janga lililotukuta kwa mara ya pili la ajali ya kuzama kwa meli. Mungu awarehemu ndugu zetu waliopoteza maisha, na kutupa moyo wa subra kwa janga hili lililotufika.

Kwa sasa ni muhimu kwa serikali kuzingatia mambo yafuatayo:-

1. kuundwa kwa kikosi maalum kinachowajibika moja kwa moja kutoka kwa baraza la usalama wa usafiri nchini likiongozwa na rais mwenyewe.

2. Kuweka bajeti ya kitengo hichi maalum kama “priority” kama ilivyo kwa sekta muhimu za nchi kwani ndio muhimili wa kuwepo kwa taifa la Zanzibar.

3. Kitengo kiwe na majukumu yote kuanzia ukaguzi wa meli husika, abiria na mizigo kabla na baada ya upakizi pamoja shughuli zote za usafiri wa abiria hususana bandarini.

4. Kuhakikisha kunawekwa vituo maalum katika coast ya nchi ili kurahisisha shughuli za uokozi na dharura zozote katika masuala ya usafiri hususan wa bahari.

5. Kuwepo na team maalum inayoweka classification ya meli za abiria zikiendana hasa na uwezo wake wa safari katikamachafuko ya bahari, vile vile kuweko na taarifa za hali ya bahari ilivyo na meli gani zinaweza kuruhusiwa kutoa huduma za usafiri. Serikali iwe na uwezo wa kufunga bandari zake kwa vyombo vidogo kuendana hali ya bahari hususan katika vipindi vya upepo mkali.

6. Kuzifutia leseni vyombo vyote vya usafiri vyenye rekodi mbaya ya usalama wa wasafiri na kuanzishwa upya usajili kwa kutumia independent audit kwa gharama za makampuni husika chini ya uangalizi wa kikosi maalum chenye mamlaka ya usalama wa bahari na anga.

7. Kurejesha matumizi ya pasi za kusafiria kwa kila mwananchi na wageni zikiwa zinaendana na tiketi za wasafiri, ili kuweza kucontrol wasafiri na watendaji wa kampuni zinazopakia abiria kwa misingi iliyokinyume na sheria za usafiri.

8. Kuwepo na ukaguzi wa abiria wote waingia nchini kwa kupitia kikosi maalum cha usalama wa abiria, pamoja na kuwa na sheria kali kwa wamiliki na abiria wasio na tiketi halali za usafiri na pasi zao. Ipo haja kwa sasa serikali kuliangalia hili kama ndio njia moja wapo ya kulikabili suala la overloading ya abiria na mizigo katika meli husika.

Hayo machache yatasaidia kurejesha imani ya wananchi kwa serikali, nna kuirejeshea heshima nchi kutokana na fedheha kubwa inayotupata juu ya maafa yanayowachwa kutokea huku tukiwa na uwezo ya kuweka vizuizi mapema vya kulinda maisha ya wanchi wetu hususan wanyonge wanaotumia vyombo vya bei ya chini kwa usafiri ambapo kwa sasa vinaonekana kuwa chini ya standard zinazotakiwa.

Kuhusu Mtunzi

Muungano wa heshima haki na usawa.

View all posts by

Maoni yamefungwa.