LENGO LETU LIWE ZANZIBAR HURU SIO MFUMO WA SERIKALI NGAPI WA MUUNGANO???

Written by  //  13/07/2012  //  Habari  //  Maoni 19

(Naomba tumia japo dakika chache soma habari hii..tafadhali)
Ikiwa tunaendelea na utoaji maoni katika mkoa wa kusini, ni vyema wazanzibari tutanabahishane kuwa maslah…i ya vyama yatatuponza na hayatazaa matunda halisi ya mchakato huu wa katiba Mpya. Hem mzanzibari jaribu kutafakari haya kabla ya kwenda kutoa maoni ili iwe dira ya muelekeo wako:-
1. Serikali huwa na Jeshi la ulinzi na usalama???? Kwanini watu wasiadai kurejeshwa kwa jeshi la Zanzibar.
2. Serikali huwa na sarafu yake, tumenyang’anywa uwezo huo tangu 1965 na rasilimali fedha zetu Pauni milioni 800 kuchukuliwa.
3. Serikali huwa taifa pale wananchi wake wanapokuwa  na uraia; imedhihiri kuwa sisi ni wakaazi tu na sio raia tena wa Zanzibar mana hata vitambulisho vya mkaanzi vina muda maalumu.
4. Serikali huwa na polisi na ms-ala ya uhamiaji (citizenship). Zanzibar hatuna vyote.
5. Serikali huwa na uhusiano na nchi za Nje (MABALOZI). Zanzibar hatuna hilo- kumbula wakati wa rais Salmin tulijiunga na OIC nini kilisibu ni kujiengua kwakua hatuna mamlaka hayo.
6. Serikali humiliki Benki kuu. Sisi hatuna. (kumbuka ukiwa huna Benki kuu huwezi kuendesha uchumi wa nchi yako)
7. Serikali huwa na madaraka ya kupitisha sheria za ushuru na kodi kwa faida ya maendeleo ya nchi. Sisi tunapangiwa na baadae kugawiwa fungu chache lisilo tosheleza.
8. Serikali humiliki eneo la anga lake na eneo lake la bahari pamoja na maswala ya posta na simu. Vyote hivyo havipo kwa Zanzibar maana hata leseni ya kutumia bahari yetu wenyewe ni lazima wende ukaombe Dar-es-salam.
9. Serikali humiliki rasilimali zake kuu na mali asili zake,  leo MAFUTA NI MALI YA MUUNGANO, ila DHAHABU , TANZANITE, MBUGA, GESI, MADINI, MAKAA YA MAWE NA KADHALIKA SIO MALI YA MUUNGANO.
10. Serikali huongoza sekta za elimu ya juu wenyewe, leo matunda yake wanafunzi zaidi ya 3000 wamefutiwa mitihani wapo nyumbani wanabanja kokoto.
11. Serikali huwa na mamlaka ya kutangaza hatari, kutangaza vita; leo serikali yetu haina mamlaka hayo.
12. Serikali huwa na uwezo wa kukopa na biashara za nchi za Nje, leo SMZ hadi waziri kutoka Bara atoe idhini ya mambo ya mikopo.
 13. Serikali huwa na uwezo wa kuanzisha na kutoa leseni za viwanda. Leo Zanzibar nzima haina viwanda vitu vyote tuagizie.
14. Serikali humiliki vyama vya siasa. Maajabu ya dunia tuna serikali lakini vyama vimemilikiwa nchi jirani na ukifurukuta unafutiwa chama, ndio maana hakuna chama kinachothubutu kuongea kama wanavyoongea UAMSHO hivyo ni wazi Zanzibar hatuna uhuru kamili wa vyama vya siasa.
 15. Serikali huwa na kiti Umoja wa Mataifa. Zanzibar tumefutwa katika ramani ya dunia kwakua hutuna uwakilishi wa UN.
Mimi binafsi niseme, Ikiwa tutayadai mambo yote ya juu hapo, na tukayapata itakuwa tumepiga hatua kuliko kudai mfumo wa serikali ngapi na ngapi haitosaidia……………..maskitiko makubwa kuna watu wanadai tubaki katika mfumo huu huu, nikuulizeni kulikua na haja gani ya kuletwa katiba mpya??? Ikiwa mfumo uliopo unafaa???????? Jamani tuwe wamoja kudai mamlaka kamili ya Zanzibar yetu, tuache kutumiwa na vyama vya siasa.
Nikutakieni Ijumaa Njema.
AHSANTENI SANA. BY SAID SALUM, BUBUBU ZANZIBAR.

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni yamefungwa.