La Uamsho na ukimya wetu
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 15/12/2012 // Habari // 11 Comments
Mohammed Khelef,
Hadi sasa jeshi la polisi na serikali za Zanzibar na Tanzania zinataka iaminike kwamba viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wanaowashikilia kwa zaidi ya mwezi sasa, ni washukiwa wa uhalifu. Uhalifu upi? Fujo, vurugu, kuharibu mali na matusi, angalau kwa kutaja machache. Wanataka sana hilo ndilo limezeshwe kwenye akili zetu. Kila mtu aimbe wimbo huo na mwisho wa siku, sote tuingie kwenye kapu moja la uzembe na uvivu wa kufikiri.
Lakini shukurani kwa mifumo ya sasa ya kimawasiliano, serikali na vyombo vyake wametukuta wengi wetu tukiwa hatudanganyiki tena na ulaghai wake. Hata kama tunaweza tusiwe na nguvu za kimabavu ilizonazo serikali, maana sisi hatuna polisi, jela wala mahakama, lakini tuna nguvu ya dhamira zetu. Nayo ni nguvu kubwa, kwa hakika.
Kwa nguvu hiyo, ya kuwa na akili huru, ndipo tunakataa kuumeza uongo wa serikali wa “kuwahalifisha” viongozi wa Uamsho na wafuasi wao. Tunajua – kama inavyojua hiyo serikali na vyombo vyake – kwamba viongozi wa Uamsho wanaadhibiwa kwa sababu ya msimamo wao wa kisiasa. Msimamo wa kuitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, nje ya Muungano.
Ikiwa kuna kosa lolote ambalo leo hii limemfanya Sheikh Msellem Ally ajikute akishindwa kumuuguza na hatimaye kumzika mwanawe mzazi, ni hilo la kwamba ni kiongozi aliyewaongoza Wazanzibari kuidai haki yao ya kuwa huru, heshima yao ya kujiamulia na dhamira yao ya kusonga mbele kama taifa.
Kwa kufanyiwa wanayofanyiwa viongozi wa Uamsho, serikali na vyombo vyake wanajidanganya kwamba wanalizima vuguvugu lililokwishapamba moto la Wazanzibari kudai mamlaka kamili ya nchi yao.
Na hili la upande wa serikali na mawakala wake linaweza kuelezeka ingawa halikubaliki. Lakini ambalo haliwezi kuelezeka, kukubalika, wala kuvumilika ni hili la kimya chetu sisi wengine, ambao tunaguswa na dhamira wanayoisimamia akina Sheikh Msellem.
Kwa sababu ya kutotaka kuitwa Uamsho, mimi na wenzangu wengi, tumeshindwa hata kuandika mistari miwili mitatu ya kusimama na viongozi hawa. Tunawaachia waadhibiwe, wateswe, wadhalilishwe kimwili na kisaikolojia. Kama nilivyosema hapo kabla, inawezkena hatuna nguvu za kuwanusuru na mkono dhalimu wenye nguvu wa dola, lakini tunao uwezo wa kuwahuisha mbele ya makini za watu: kuwasafishia majina na kuzitukuza thamani zao, kwa kutokubali “kuununua” uzushi dhidi yao.
Hawa si magaidi, si mahaini, si majambazi, na kwa hakika hata si wahalifu. Hawapo walipo sasa kwa sababu wameiba, wameua au wamemdhulumu mtu. Wapo walipo kwa kuwa wanapigania nchi yao – heshima ya taifa lao. Hawa ni wa kutukuzwa si wa kupewa mgongo! Si wa kupigwa pande!
chanzo:zdaima





11 Comments on "La Uamsho na ukimya wetu"
Pengo awaonya wanasiasa
• Asema wananchi waachwe watoe maoni yao
na Shehe Semtawa
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo, amewaonya baadhi ya wanasiasa na taasisi mbalimbali kuacha kuwashinikiza wananchi kutoa maoni kwenye tume ya kukusanya maoni hayo.
Kardinali Pengo alitoa onyo hilo jana wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuelezea ujumbe uliotolewa na maaskofu wa kanisa hilo kwenye mkutano wao uliofanyika Oktoba 7-28 mwaka huu mjini Rome nchini Italia.
Alisema kuwa kwa vile suala la Katiba linagusa maslahi ya nchi ni vyema kila mwananchi akatumia fursa yake ya kuwasilisha maoni yake mwenyewe.
Msimamo wa Kardinali Pengo unakuja zikiwa ni siku chache tangu kuzuka vurugu kubwa visiwani Zanzibar katika mkutano wa kutoa maoni, ambapo baadhi ya wananchi walijeruhiwa kwa mawe na visu.
“Watu waruhusiwe kutoa maoni yao lakini lazima tukubaliane kuwa kila mtu ana maoni yake na maoni yote hayewezi kuingizwa katika Katiba hiyo,” alisema.
Aliongeza kuwa kuna mfumo ambao baadhi ya nchi zimetumia kwa kuandaa Katiba mbili kisha kutafutwa watu maalumu wakakabidhiwa Katiba hizo kisha wakaandaa moja mpya.
Katika hatua nyingine Kardinali Pengo aliwataka viongozi wenye dhamana kuacha kushabikia udini katika kusimamia haki za jamii ya Watanzania.
Alisema wapo watu makini wenye uwezo wa kusimamia mchakato huo ikiwemo tume iliyoteuliwa kusimamia mchakato huo mzima wa ukusanyaji maoni.
Kuhusu vurugu za kidini Kardinali Pengo alibainisha kuwa nchi imegawanyika katika dini mbalimbali, na kwamba inapotokea dini moja kuitukana dini nyingine na kuharibu mali zake, serikali haipaswi kukaa kimya bali inatakiwa kusimamia haki za makundi yote.
Alisema kuwa endapo serikali itaamua kulishughulikia suala hilo kwa upande mmoja na kuacha maswali kwa wengine basi itakuwa imekwenda kombo.
Alibainisha kuwa malalamiko yanapotolewa na mtu kama yeye huwa hayana nguvu sana katika jamii kuliko yanapotolewa na Rais wa nchi na kwamba Rais ana nguvu hivyo kila analolisema huwa linapokelewa kwa uangalifu mkubwa.
Pengo alimsifu Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, na kumtolea mfano kuwa licha ya kuwa Mkatoliki bado hakutumia mwanya huo kuwabagua wananchi wa madhehebu mengine.
“Ni lazima viongozi wajiepushe na ubaguzi wa kidini kwa mfano Rais Benjamin Mkapa hakuwahi kusema Wakatoliki wenzangu na wenye mapenzi mema kwa lengo la kutekeleza majukumu ya maendeleo,” alisema.
Alifafanua kuwa Rais si lazima awe Mkatoliki wala Muislam, bali anapochaguliwa anakuwa kiongozi wa nchi ili kuwatumikia watu wote kwa kulinda, kusimamia mali za madhehebu yote na si vinginevyo.
Akizungumzia kuhusu ujumbe wa Noeli na mwaka mpya, Kardinali Pengo alisema maskofu wa Sinod, wamewapongeza waumini wao kwa kudumisha imani.
Alitanabaisha kuwa licha ya mazingira magumu ikiwemo uchumi duni, njaa maradhi na imani potofu za kidini, bado wameweza kustahimili na kuwafanya kubaki kitu kimoja.
Alibainisha kuwa familia ya Mungu haibaki katika dhehebu fulani, bali neno hilo linasaidia kuwa watu wote wenye mapenzi mema kuwa wa familia moja.
“Kutofautiana katika jamii ni jambo la kawaida na kisha watu hurudi na kubaki familia moja,” alisema
Mihadhara ya dini
Kuhusu mihadhara ya dini Kardinali Pengo alisema hakuna mtu mwenye haki ya kumtukana mtu kutokana na imani yake.
Alisema kama serikali inashindwa kuwakemea wanaotukana wengine, anaogopa kuwa hali ikiachwa iendelee hivyo inaweza kuvuruga amani na mshikamano na nchi kuingia kwenye mgogoro.
Kardinali Pengo aliongeza kuwa haoni tatizo kama mtu atasema Yesu si mwana wa Mungu katika nia ya mtazamo wake na kwamba hapo kutakuwa na tatizo kwa kuwa hata yeye anaweza kusema Mohamed si Mtume tena kwa ushahidi kutokana wa vitabu vya dini alivyosoma.
Elimu
Kardinali Pengo alisema watu wote wenye nia njema na mapenzi ya nchi hii wanapaswa kutoa kipaumbele ili kila Mtanzania apate elimu iliyo bora.
Alisema hapendezwi na mpango wa elimu inayotolewa nchini kwani mfumo wa baadhi ya shule nyingi zimekuwa kitega uchumi hivyo kuwa kikwazo kwa watu wenye kipato cha chini.
Hali hiyo ikiachiwa iendelee inaweza kuwafanya wale waliokosa elimu kuvuruga amani kwa kudai haki zao za kioungozi na maslahi mengine.
Chanzo Tanzania Daima
Wanaotaka tuendelee na Muungano huu,wasubiri tusulubiwe na kanisa Katoliki.
Kwa upande wa Tanganyika waislamu hawana nguvu zidi ya Kanisa na wamefunikwa na kuzibitiwa na kusalitiwa na Baraza la Kislamu BAKWATA.
Indio maana ukawaona Wakristo wametowa takumu fake ya kusema wao ndio wengi kwa hio nilazima serekali na sensa ijuwe hivyo ili kupangiwa bajet maalumu.
Kwa Upande wa Zanzibar tunakwenda huko huko kuzidiwa nguvu na ichara nyingi zipo za viongozi wetu wa smz kupiga makoti kwa kanisa na kuwazibiti waislamu kila ucheo.
Wasemao kuwa kanisa halina nguvu zanzibar wanajidanganya, angalia sala za Jumapili watu huanza safari tokea Jumamosi kuja kutia wingi Zanzibar ,Baali ya mmiminiko uloko zanzibar bila kujulikana ni wangapi.
Hizi zote ni agenda kabambe za zamani kwa mategemeo ya baadae chini ya wanafiki wetu Smz na hivi sasa kuna kampeni za chini kwa chini , kwanza kila katika watoto 30 wazaliwao Zanzibar katika hospitali ya mwembe ladu Basi Wazanzibar ni 6 tu.
Jengine ni Kanisa kusaidia miradi midodo midogo kwa watu wenye asili ya Tanganyika hata kama sio Mumini wao, hii ni kuangalia kuwa focus yao ni kuwa Watanganyika wa zanzibar wote chama ni ccm na lengo ni kulinda Muungano na kufanya chuhuli zao bila kero kwa mgongo wa chama kuwalinda.
Hivi sasa wengi wao wamechafanikiwa kuwa Wazanzibar ID na kukabidhiwa haki zote na fursa zote na hata ukiangalia watendaji wakuu wa Serekali ulimwenguni sio Rais na mawaziri , niwakurugenzi na wahasibu.
Sasa angalia wahasibu,Wakurugenzi na Majaji Zanzibar utajuwa ni watu wenye asili gani?
kamateni wakiristo na kuwatia moto wa matako na kurudi makwao mikoani.
mie sijaona waznz kwenda bara kupe;eka uislam
ila mikiristo kuja zanz kuifanya znz kisiwa cha makiristo. hili ni jukumun la waznz wenyewe munafikiria smz itafanya nini?
itatuuza, na tutakuwa hatuna nguvu tena, na makafiri hawa watupanda na kutupandia wake zetu mpka watoto wetu, na mtaliona hili kwani lishaanza.
Suala la Serikali zetu kuwadhalilisha Mashekhe na waislamu halikuanza leo lakini cha kufurahisha Waislamu wanaendelea kudai haki zao pamoja kuwa hawana nguvu kama zilivyo hizo dola husika, na kamwe Muislamu anaejua thamani ya dini yake hawezi kusalimu amri kwa watu wanaoichukia dini ya Mwenyezi Muungu.
Wazanzibari walio wengi wanajua kuwa Mashekhe wamewekwa ndani kwa sababu ya msimamo wao wa kukataa Muungano wa dhulma na si vyenginevo, na kwa hilo tutasimama pamoja nao mpaka mwisho wa safari yetu.
Kwa wale waliofuatilia mihadhara mbali mbali ya UAMSHO watakumbuka kwamba Mashujaa hawa tayari waliuelezea umma kwamba wanafahamu kwamba jambo la kuelezea ubaya wa Muungano ni hatari lakini wamejitolea nafsi zao kwa lolote lile lakini ukweli wa haki na ubaya wa dhulma lazima wauseme wazi wazi. Hili linatupa faraja kwamba wao ni mashujaa na hawatishwi na kuwekwa ndani, ikibidi hata kama watauliwa ilimradi tu wamesema ukweli kwa ALLAH watakuwa na malipo na ujira usio na mfano.
Kwa upande mmoja ALLAH kaleta rehma zake kwamba katika kipindi hichi ambapo tume ya warioba ipo mjini magharibi na hizi kashkashi ambazo zimetokea si ajabu ingekuwa hawa mashekhe wako nje wahafidhina wangepanga hujuma zaidi za kutaka kuwatia makosani.
Tuendelee kusimama kidete kutetea nchi yetu, na INHA-ALLAH TUTASHINDA.
Mwanafunzi hakuacha kitu lakini kwa kuongezea ni kuwa mbali na kuwa Masheikh wako ndani na serikali ingeleta hujuma zaidi ktk mchakato wa mjini , Lkn pia ni kuwa wamemfanya Maalim azungumze kwa zote na hawakutarajia sasa yalobakia hawajui wazibe wapi manake Masheikh wako ndani lkn uku nje watu wamezidi hasira khs mchakato feki wa kuwafanya Wazanzibari wapumbavu . Kwa kweli mda huo umepita bali walobaki ni wanafiq tu ambao kila pahali always wapo kwa hivyo si jambo la ajabu ila tumekusudia kupambana nao mpaka kieleweke na tupumuwe . Hamna hili wala lile.
Balaa letu lote sei Zanzibar nihili JINI LINALO ITWA CCM ( Chama cha makanisa) . Ni lazima lipungewe litoke kwenye vichwa vya wa Islamu walo sibiwa na jini hili.
Pengo asema nayeye aweza kusema kutokana vitabu alivyo soma Kuwa Muhammad (S.A.W) si mtume . Astaghfur Allah! Ni Allah (S.W.T) katika quraan yake takatifu ana sema wazi : Isa ( A.S) ni MTUME SI MWANA WA MUNGU. NI MWANA ADAMU . AKILA CHAKULA KAMA MWANA ADAMU YEYOTE. KWA ZALIWA KWA MIUJIZA KWA AMRI ALLAH (S.T) . Kwani yeye akitaka kitu kiwe huwa. Yeye ndie Muumbaji.
Hicho katabu cha wakirito ( Bible) ambacho Pengo pia anakiamini hakikuandikwa kuwa Mutume Muhammad ( S.A.W) si mtume. Wala hakikutaja kuwa Nabii Isa (A.S) kuwa mtume wa mwisho.
Pengo huto weza kwazuia Wa islamu wastangaze misjngi ya imani yao kwa mujib wa Quraan. Hivyo vikao vya vatikan hitofua dafu . Isipo kuwa fitna. Na kupoteza mapesa mengi.
Hata hiyo chrismas sasa kanisa katoliki wana kubali tarehe ya kuzaliwa nibii Isa ( A.S) hakuwa winter na wala sio kwenye mabanda ya farasi. Bali KAZALIWA SINAI
Kwenye miezi ya joto. Ukweli huwo haukupata publicity kubwa. Bali ime waudhi wengi . Maslahi ya kibiashara na mengineo.
WALE AMBAO NI WAISLAMU NA WAMO KWENYE CCM.MUNA BEBA JUKUMU KBWA LA UWOVU WAKUSHRIKINA NA MAADUWI WA UISLAMU.
PEVUKENI KIAKILI. TUIYOKOWE ZANZIBAR NA NJAMA ZA MAKANISA.
ZANZIBAR KWANZA!
@ Mohammed Khelef
Brother Mohammed ama umetueleza ukweli mtupu na maneno mazito ambayo kila mzanzibari mwenye akili inafaa kuyazingati.
Your statement is short but very effective and very touching, kwa sisi tulio mbali imekua siku ya huzuni kubwa leo kupata habari kua maskin shekh wetu Msellem imefikia hadi mtoto wake kuumwa mpaka kufa yeye rumande na kutopata fursa kujumuika na family yake katika kipindi hichi kigumu.
Mimi naskitika sana brother kwani kama tunavojua na wewe leo kukumbushia hawa ndugu zetu kina Ustadh Farid na wenziwe wametupwa na kusahauliwa huko rumande kwa sababu ya kuitetea nchi yetu, kutetea utu wetu na thamani yetu. In other words kujinasua kwenye muungano huu haramu na Tanganyika, na sio sababu nyengine yoyote, leo wameekwa ndani na kupachikiwa kila aina ya uhalifu inatupasa sisi kama wazanzibari na waislamu tusiburuzwe na hizi fitna zinavopikwa na SMZ & STZ na kuwasaliti mashekh wetu ambao wamejitolea kwa hali na mali kuiokoa nchi yetu kwenye deep storm iliyozama almost 50 years sasa.
Tusiwavunje moyo viongozi wetu lets get up and raise our voices, lets do whatever it takes kuhakikisha kwamba lengo letu la kujikomboa linafanikiwa plus tuhakikishe kwamba mashekhe wetu wanatoka huko rumande walikoekwa kidhulma as soon as possible kwani ni tough situation walionayo huko jela, tujaribu kuipicture situation walioekwa kama ni mimi au wewe tungejiskiaje?
Mimi naamini wazanzibari tukiwa serious na kusimama pamoja basi Biidhnillah mkoloni Tanganyika tutamuondosha kwani wazanzibari tumeenea dunia nzima na ni watu wenye vipaji kila aina sasa ikiwa soote tutaeka dhamira hio basi kwa uwezo wa Allah sioni sababu ya kushindwa kujinasua kutoka muungano huu haramu.
Mifano ipo mingi ambapo wananchi waki-decide they no longer need such and such leaders in their country or mfano wa hayo basi naam wananchi hupata wakitakacho na sio akitakacho kiongozi wa nchi hiyo wala Warioba au mjinga yoyote mfano wake.
Jamani tunaishi katika zama za uwazi na ukweli besides ni zama za wananchi kuamua mudtaqbal wa nchi zao sio a buch of puppets kuburuza watu kama ilivo Zanzibar right now.
MUUNGANO HATUUTAKI HATUUTAKI HATUUTAKI THAT’S IT FULL STOP, HILI SHENZI WARIOBA NA HAO WALOMTUMA PLUS WAHFIDHUNA TUSIWAPE CHANCE WAKATUPOTEZA MALENGO.
REPUBLIC OF ZANZIBAR ITARUDI BIIDHNILLAH….
Ndugu zangu waislamu tuwe na upendo na wakristo na watanganyika ni ndugu zetu
Aslaam Aleykum Wanaukumbi. Wallah Ghassany umekuja vizuri. Inasikitisha kama vile tumewasahau, kama vile tumeamua kwa makusudi kuwakandamiza, kama vile tumeona hakuna haja ya kuwatajataja kila wakati, kama vile wamejitakia. Sivyo. Tujue tunavyonyamaza hatuwatendei haki wanayostahili, na tukinyamaza tunaifurahisha serikali dhalimu na chama chao CCM. Hawa na wahafidhina wao wanafurahi na kuchekelea kwamba “umeona hakuna anayewaunga mkono.” Hali hii inawafanya wajikunje huko gerezani waliko.
LAKINI
Mimi naona vinginevyo. Masheikh inaweza kuwa tumenyamaza kwa kuandika tu mistari miwili mitatu kama asemavo Ghassany. Hatuandiki kusema la haki. Lakini ukifikiria ile kampeni nzito waliyoifanya ya kuitakia Zanzibar irudishiwe mamlaka yake kama dola huru, Wazanzibari wema kwa nchi yao adhimu Zanzibar, wanawaunga mkono sana Masheikh zetu. Kuimarika na kushuhudishwa kwa SAUTI YA NGUVU ya TUNATAKA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI chini ya mfumo wa MUUNGANO WA MKATABA, wamewaunga mkono sana Masheikh zetu hawa.
Kile walichokuwa wanakililia kifikiwe, walichokuwa wakitaka viongozi wakiamini kuwa ndio matakwa na utashi wa Wazanzibari walio wengi, ndicho walichokisema kwa sauti kubwa wananchi wengi ktk mikutano ya kutoa maoni ya katiba mpya inayotafutwa.
Masheikh wanaungwa mkono kwa sababu kila wanapopata nafasi ya kusikia, kwa njia yoyote ile, matokeo ya utoaji wa maoni mbele ya Tume ya Warioba, basi watatambua namna kampeni yao ilivotiiwa na wananchi wa Unguja na Pemba.
Kila wakisikia, kwa njia yoyote ile, kwamba wahafidhina wa CCM wamejitahidi kuvuruga sauti za mabadiliko zisikike lakini bado wananchi wamejitokeza na kila walipoipata nafasi wameeleza bayana mahitaji ya Serikali ya Mkataba, watatambua kuwa hawakufanya kazi ya bure, bali imeleta msukumo mkubwa na imeibua mchango muhimu wa kutia nguvu hoja ya mabadiliko.
Mwenyezi Mungu anawapenda sana Masheikh hawa maana anajua fika kwa kile walichokuwa wakikipigania, walikuwa wakifanya vile kwa ajili moja tu: Ya kutetea haki za wananchi ambao ndio waumini wanaotakia ucha mungu.
Tunawaombea sana ALLAH awatie nguvu kila nukta ya dakika na awaongezee uvumilivu na awape wepesi wa kufanya ibada wakiwa hukohuko kifungoni. Amin.
Wakatabahu.
kwa nini wananchi wanaotetea maslahi ya nchi yao watiwe tkt hatia bandia?
sijengine ila ni kua kanisa limechukizwa hebu tembeleeni blog hii muone hawa wenzetu malengo yao kwa znz na matokeo ya propaganda zao zilivyomalizikia kwa viongozi watetezi wa znz http://zanzibar4jesus.blogspot.com/
wana mikakati kabambe ya kuwabatiza waunguja na wapemba wanaona zanzibar ikiwa huru itakua ni tatizo hivyo wamezua propaganda ili kutiwa hatiani viongozi wa uamsho,
na si nchi hii inaongozwa na mfumo kristo la pengo ndio linalitiiwa na vyombo vya dola.