Kufanywe uchunguzi wa kuharibika kwa barabara Pemba

Written by  //  17/05/2017  //  Habari  //  Maoni 1

Waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji Balozi Ali Karume amewataka wafanyakazi na wahandisi wa wizara hiyo kushirikiana katika kufanya uchambuzi na utafiti wa kina ili kuangalia mapungufu yaliyojitokeza katika miundo mbinu ya barabara kisiwani Pemba kwa lengo la kuepusha uharibifu kwenye miundombinu hiyo.

Amesema wizara ipo kwa kufanya kazi kwa vitendo hiyo waendelee na nguvu waliyonayo katika kuihudumia jamii kwa kurejesha mawasiliano ya barabara pale yanapoharibika
Balozi Karume ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha wahandisi wa wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji cha kutathmini utendaji wa wizara katika kurejesha huduma ya miundo mbinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kisiwani Pemba .

Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa wizara ya ujenzi Mawasiliano na miundo mbinu Mustafa Aboud Jumbe amewapongeza wahandisi hao kwa kuirudisha huduma ya mawasiliano kwa muda mfupi na wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za kawaida .

Hata hivyo amelaumu ni kwa nini barabara zilizojengwa zimeharibika kabla ya miaka mitano na kuwapa muda wahandisi hao hadi Ijumaa kuelezea kwa kitaalamu kitu cha kufanya cha kurudisha mawasiliano kutoka katika sehemu zilizoharibika.

Naye Afisa Mdhamini wa wizara ujenzi Mawasiliano na usafirishaji Pemba Hamad Ahmed Baucha na muhandisi wa wizara hiyo wameahidi kuyafanyiakazi maagizo hayo kwa kuhakikisha wanayasimamia na kazi inaendelea kama ilivyopangwa.

Pemba News

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni Moja katika "Kufanywe uchunguzi wa kuharibika kwa barabara Pemba"

 1. zamko 17/05/2017 kwa 5:20 um ·

  Hahaha.
  Serikali ya Ma Abunuasi ( Samaki)

  Hivo Hawajuwi ni Nini kilichozifanya Barabara za Pemba Zivurigike?

  Hata Mimi Niliekuwa Sio Balozi, Wala Mtoto wa Mwana Mapinduzi au Mtaalamu Kama Hawa Jumbe Na Karume.

  Najuwa kwamba Barabara zote Ziliojengwa na Watanganyika Visiwani. Zilijengwa na Fusi tuu na Sio JIWE. Na fedha Nyingi sana zililiwa na Wao Wenyewe Akina Sefu Ali Iddi.

  Na sababu hiyo ndio imefanya Barabara hizo Zivunjike kwasababu hazina Kiwango hata chakuitwa ni Bara bara.

  Mfano wa Viwango vya Barabara Bora Basi tutizame Ile Barabara ya Kinazini na BUBUBU mpaka Mtono. Barabara ya Bububu ilijengwa na Wataalamu Kutoka COJIFA kutoka Finland. Na hata kuje Mvua gani barabara ile iko Imara.

  Nyengine ni Zile Barabara Tulizojengewa na Mkoloni Mweupe, mfano Barabara ya Chambani, Imejengwa wakati Mama angu Hata hajazaliwa na Sasa ana miaka 80. Na barabara jiwe lilikuwa bichi pamoja na Pechi za Lami ya Mkoloni Mweupe.

  Leo Tunatawaliwa Na WATWANA Wakisaidia na Hawa Watoto Wa Wana Mapinduzi, Barabara Zote za PEMBa walizitia VUMBI na UTOSI wa LAMI. Maana sio Lami Safi. Kweli barabara hio itahimili Maji?

Toa maoni

You must be logged in to post a comment.