Bandari zetu Zanzibar na Bara

Written by  //  18/07/2016  //  Kitaifa, DIRA  //  Maoni 3

Bara mizigo imepungua tokea Magufuli aingie madarakani na ziara za kushtukizia,sasa wafanya biashara wameamua kurudi tena Zanzibar kushushia mizigo..Bara wameshtukia hili,wakatoa kwanza sababu ya kupungua mizigo Bara eti uchumi wa China umedorora,ndio maana na mizigo imepungua Bara..

Pili,wakaona mizigo inashushwa Zanzibar kisha inapelekwa Bara,Wakaamua kupitisha bajeti yao juzi kuwa,mizigo yote destination Bara hata kama itashushwa Zanzibar basi ushuru ulipiwe Bara ( imagine kwanza hii ni nchi moja lakini mishuru miwili)

Tatu,Ushuru wa mizigo inotoka Bara kuelekea Zanzibar ilipiwe Zanzibar, mazao yanayozalishwa Tanzania yasamehewe ushuru,na utalii uongezewe kodi ( nimeona mashirika ya watalii wameandika barua kulalamika kodi zimepanda mno kwa nchi za Kenya na Tanzania).. hapa judge mwenyewe.. kitu gani kinachotoka bara kuja Zanzibar saivi? asilimia ngapi itatoka kule kuja ZNZ,na hata ukilipa ZNZ TRA ndio wakusanyaji.

Nne, Juzi Ijumaa ya tarehe 16 nimesikia Rais kazindua kreni mpya ya mizigo kutatua tatizo la makontena msongamano,na Bwana Manji kakubali kuwapa miezi 6 kutumia uwanja wake walomuzia kuweka empty containers walozisababisha wenyewe kwa ucheleweshaji wao.

Tano,Bandari haina hata Ramp ya kushushia magari kwenye container tena ya chini tu,nimeona juzi gari zinashuka kwenye container zimepangiwa mipira chini zinakanyaga,gari moja ikavunjika hapo hapo bumper la nyuma,TRA wanaambiwa wanaharibu, basi wakaanza kuwaka eti hawalipi kosa sio lao, sasa kosa la nani na sheria wao wanasema gari huruhusiwi kuendesha hadi wakutolee nje ya bandari…basic things zinakosekana na watu wanalipa mapesa kibao.

Sita, Baadhi ya kampuni zimegoma kuleta mizigo Zanzibar wanasema destination ni bara kisha ufanye maarifa mwenyewe kupeleka Zanzibar,na nyengine wamesema kuna charge ya ucheleweshaji saivi container kushushwa Zanzibar.

Hivi mambo haya yataisha lini?

Kuhusu Mtunzi

Teesside University.

View all posts by

Maoni 3 katika "Bandari zetu Zanzibar na Bara"

 1. rasmi 18/07/2016 kwa 9:05 mu ·

  labda haya masuala tuwaulize @hamad salum @mpetehalisi na Kessy yule mbunge wao wa ccm aliowashushua Wazanzibari wakiwemo hao wanaojipa uccm kwamba watoke katika bunge Bara wanapozungumza mambo yao.

  Tatizo la Wazanzibari wenzetu walio na ari ya uccm wao zaidi ni kukosa uzalendo, wanakasirika wakiambiwa hivyo ila watuelezee tu ni ipi maana ya hayo yanayotokea?

  Usaliti maana yake ni kuwageuka wale ulioahidi kuwatumikia na badala yake kutumikia ajenda yako binafsi ama mtu mwengine. Je tunakosea tunapowaita ccm Zanzibar ni wasaliti hata wa malengo hata ya ASP yenyewe wanayojidai kuipenda na kulinda madhumuni yake?

  Je leo hali za Wazanzibari zimeneemeka kielimu, kiafya, kimakaazi, kimazingira, kiutamaduni nk ama zimerudi nyuma?

  Shtukeni, munaharibu mustakabali wa vizazi vyenu wenyewe…

 2. Jino kwa Jino 19/07/2016 kwa 4:54 mu ·

  Tatizo la Wazanzibari Waungojaa hawajitambui wao ni Waungojaa au Wazanzibara au ni Watanganyika wao wamo wamo tu .Na vile vile tatizo kubwa zaidi ya hawa jamaa zetu ni kutokuwa MSIMAMO.Sisi Wapemba tunaeleza wazi wazi hata nchi apewe hicho kipenzi cha Umma basi ss tunataka kuwa huru Wapemba.Tunataka kujitawala wenyewe tunataka kuifanya Pemba kama singapore kibiashara au Zaidi ya Singapore ,kwa hivyo twendeni lkn lengo letu ndio hilo tunataka tuwe kama U-A-E au kama U-S-A .Hawa wote wameungana lkn kila nchi na uchimi wake na mambo yake ya ndani na sisi tunataka hivyo hivyo tutakutana kwenye Bunge tu la pamoja kila kisiwa na mfumo wake wa UTAWALA.Na hapo ndipo patakopopatikana thamani ya Mpemba na Muungojaa tutaishi raha mustarehe na amani bila ya kueirena haya mambo yanawezekana na yatafanyika in shaa allah.Na hilo tatizo la bandari sisi tutalimaliza kwa east afrika nzima .Wapemba tuangalieni mfano wa Kurdustan wanavyoendelea baada ya kupata serikali yao ya ndani bila ya kuingiliwa mambo yao ndani ya IRAQ.

 3. Tengoni 19/07/2016 kwa 12:29 um ·

  Kuna muingereza mmoja zamani kidogo alituuliza hii smz inaelewa yanayopitishwa kule bungeni, miaka ile kulikuwa na hotuba za mawaziri wa fedha kama hizi,
  1994/95
  Kiggoma Malima,
  Mr. Speaker
  …. The customs department has been directed to step up its surveillance activities with view to netting illegal imports coming through Zanzibar and curb tax evasion.
  82….. Mr speaker
  As honourable members of this house may recall, the government took measure in April 1994 to plug areas of tax evasion which has been a source of revenue leakage, the affected area are transhipment cargo destined to Zanzibar.

  Waziri kikwete 1995/96

  Mr speaker

  72….. Basically the central bank functions will now also accommodate the revolutionary government of Zanzibar, this in principles means it will also be its bank,
  23…. Plan are underway to move the Zanzibar revolutionary government accounts from pvs to bot.

  43…… The government will also strengthens its stance to curb smuggling through our borders, including strict control on transit goods originating from Zanzibar.

  Waziri Daniel Yona 1997/98

  Mr Speaker

  13….. Moreover the union government and the government of Zanzibar reached an agreement on the harmonization of tax rate for these commodities, sugar, cookingoil, rice, wheat flour aand khanga,

  46 Mr speaker

  ….. In line with harmonised rate with Zanzibar, it is proposed that 30 percent import duty and 20percent sale tax be charged on khanga. All locally manufactured textiles are to be charged 20 percent sales tax.

  Waziri yona 1998/1999

  Mr speaker

  84…. It is proposed that all goods imported through Zanzibar be subjected to pre shipments inspection so as to curb tax evasion,

  Hayo ni mapitio ya mawaziri wa fedha wa Tanganyika kwenye budget zao karibu kila mwaka, ni malengo yao ya kimila kuhakikisha kila budget kuna kifungu cha kuibana kiuchumi Zanzibar. Na kama yule muingereza alivyoshangaa, smz haitambui lolote kuhusu yanayoendelea bungeni, wakitambua hupitia magazetini, sheria ishatiwa saini, yaliyobaki tutazungumza na wenzetu wa smt, hayo ni maneno tu tangu commando, jiti lishazama.

Comments are now closed for this article.