Jambo limezua Jambo!

Written by  //  23/03/2017  //  Habari  //  Maoni 11

Kuhusu Mtunzi

View all posts by

Maoni 11 katika "Jambo limezua Jambo!"

 1. mohamed 23/03/2017 kwa 4:11 um ·

  Namnukuu Mh Tundu Lissu”Safari hii tumepata raisi wa ajabu haijapata kutokea tanganyika”.

  Magufuli pengine kaghushi vyeti pia,baina yake na makonda kuna kitu kati ila itajulikana.

  Insha Allah.

 2. mzeekondo 23/03/2017 kwa 4:33 um ·

  Naona hiki chama safari hii kitatushinda wengi,huyu mwenyekiti wetu wa taifa Magufuli iko haja ya kumfukuza chama kabla hajatumaliza,leo Nape kawa adui na ndie aliyehangaika mikoa yote kuiletea ccm ushindi,mshindi mwenyewe ndie rais wa ccm, sasa Bashite kawa bora zaidi kuliko sheria au Nape?

  Ushauri wa bure ni vema akamfuta kazi Bashite kabla wananchi hawajaamua wao,jee kwa bahati mbaya ikiwa watu watamdhuru Bashite, ni bora iwe hivyo kuliko kumfukuza kazi kwa kuwa hana vyeti,hili ndio swali la JPM kujiuliza?yeye sio mzee wake inawezekana hana uchungu na roho ya huyu kijana,kama hao wazee wake Bashite wako hai basi huu ni wakati wa kuinusuru roho ya kijana wao.

 3. Bin Rajab 23/03/2017 kwa 8:02 um ·

  Wazalendo

  Kuna nini nyuma ya pazia? Kuna nini between Kufuli na Makoonda?

  Ushirikiano wa jinsia moja au utapeli wa vyeti feki au pegine

  utapeli wa kura za 2015. Bashite naona ana siri nzito za makufuli.

  Ndio maana anashindwa kumtubuwa.

  Hapa dhulma tuu

  Wakati wa Ukombozi umefika.

  Asanteeni

 4. zamko 23/03/2017 kwa 8:17 um ·

  @ mzeekondo

  Mara nyingi nakuwa na kubaliana na maoni yako lakini haya ya leo mdogowangu naona umekuja haraka haraka.. Hivo Unafikiri kwa Tanganyika na Zanzibar kuna mtu ataweza kumdhuru BASHITE wa POMBE?

  Hii nikwasababu Yakwamba Hatujiwezi Watanganyika na Wazanzibari na Tunawaogopa Polisi, Jeshi na hata hao Viongozi Waliokaa madarakani kwa Nguvu za Dola Tunawaogopa. Na Woga huu Umetokana nakutokuwa na Uzalendo wa Nchi zetu hizi mbili au kuangalia Athari na matokeo ya Wapi tulikotoka na Wapi tunakopelekwa. Kisha tukafanya tathimini hizo na Nchi za jirani zetu.

  Hichi chama cha CCM kama kitaendelea tena kutawala zaidi ya miaka 5 ujayo, basi nakuhakikishia Matokeo yake ni sisi Wananchi ndio tutakao dhuriwa na hawa wanaojiita Watawala au malaika. Haya yote yameletwa na huo Utii wetu uliogeuka Woga halafu ukazaa kujipendekeza na ukajukuu Unafiki.

  Nakubaliana na maneno ya Babaenu wa Taifa @ Mzeekondo.
  Nyerere aliwahi kusema hivi namnukuu

  “…Nakwambia utii ukizidi, unakuwa uoga na siku zote uoga huzaa unafiki na kujipendekeza- na mwisho ni mauti. Sasa kama nyie watumishi wa Umma kwa wingi wenu, mmeshindwa kupiga kura yakuwaondoa Viongozi dhalimu ni bora mfe tu” Mwisho wakumnukuu Nyerere.

 5. zamko 23/03/2017 kwa 8:21 um ·

  @ Bin Rajab

  mimi naona Magu analoliogopa Nikufukuzwa Bashite kwa Huu Uibaji wa Vyeti Visivyo Vyake na Magufuli inasemekana Hana Elimu anayojidai anayo.. Alifeli na hakupata Cheti. Na unamuona hata usemaji wake unamjuwa kama ni Mtu asiekuwa na Vission ya Elimu ya PHD..

  Hata hivo Huo Ndio Mtindo wa Viongozi wote wa CCM Tanganyika na Zanzibar.

  Magufuli anajuwa akiacha Wananchi kumuondoa Bashite basi na yeye atahojiwa uhalali wa Vyeti vyake. Ndio amaewakata Watu Midomo.

 6. salali 23/03/2017 kwa 10:20 um ·

  Fadhila za Punda mashuzi, kweli pombe kinywaji haram, tumefajirika sana kwa kuiyona ccm inaviongozi vihiyo hata Bara kufika 2020 ni maajabu ya Mlevi kuazini.

 7. Piga nikupige 23/03/2017 kwa 10:27 um ·

  Na mimi niungane na wenzangu. Inawezekana na Magufuli labda akawa ana vyeti vya kurukia rukia.

 8. mzeekondo 23/03/2017 kwa 11:28 um ·

  @zamko

  Ujumbe wa leo mdogo ni wa wazee halali wa Bashite,tahadhari kwa anae mpa jeuri ya kuvunja sheria na wana ccm wenye misimamo ya kale.nimetoa wito kwao wa kufikiria kumfukuza JPM kabla hajawadhuru na wao au sote,kama kuna haraka haraka katika ujumbe huu sio vibaya,harakati za kuanza mikakati ya kumshughulikia ndio ombi langu kwao.sisi wengine tuligundua zamani kuwa huyu sie kiongozi na tulimkataa,mimi binafsi nilikuwa kambi ya Lowassa ndio maana nimetengwa kwa sasa.

  busara siku zote hushinda ubavu.lakini pia haina maana usitumie ubavu ikiwa busara hakuna au haifai hapo ndipo ninapoihofia roho ya Bashite,mimi kama mzazi niko pamoja nao sio kijana wao.

 9. jazba 24/03/2017 kwa 12:51 mu ·

  mi nataka niwapelekee salam hawa wenzetu ccm wa hapa zanzibar na kujipendekeza kwao huko,kwa hali hii inavyokwenda watie maji, tumbili akikosa miti huja mwilini,

  nchi haishi vituko saivi kila siku ,juzi wamepapurana nae majukwaani kuhusu umeme kwa hio wawe na hadhari sana,,,namkumbuka othman masoud na kauli yake juu ya katiba,alisema hapa mambo haya kwenda kwa hisani nakuridhiana itakuja tokea siku aje kiongozi machacha ije iwe balaa, ndio hii ishatokea saivi

 10. sadimba 24/03/2017 kwa 3:42 mu ·

  Mtoto hata alelewe na nyani bado atahesabika kama ni mtu japo atakuwa na vitendo na hulka ya nyani, nikimnukuu Tundu Lisu basi nakuwa sina haja ya kupata muda kumtafakari huyu limbukine wa madaraka mwenye kudhani ukiwa ni rais una akili kuliko unaowaongoza. Mara nyingi mtu huwa na rafiki wanaoshabihiana kwa matendo hivyo naona Bashite na Pombe wanarandana aidha ka upande wa mkondo wa kupata elimu au kwenye mchezo wa tumbo kwa mgongo.

  Othman Masoud alisema harama moja huzaa haramu mia moja ndio tunayaona katiba na sheria ziko mfukoni, ni udikteta mtupu kama alivyosema nyerere namnukuu “udikteta ni serkali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache na wao huwa sheria. Anaepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni Julai 19, 1967” mwisho wa kunukuu. Huyu bwana kwa historia nasikia aliwahi kuugua wazimu hivyo mwendazimu huwa hapoi hupata nafuu tu lakini watanzania sasa ndio tumekuwa wendazimu zaidi ya wagonjwa wa mirembe na kidongo chekundu.

  Nape kama ayasikia maneno aliyoyazungumza katika uwanja wa Samora Iringa basi si wakumuonea huruma ila ni malipo kwa matendo yake, alimsifu Pombe Makufuli kama ni Jembe,Tinga Tinga na kusema ikulu si wodi ya wagonjwa. Kwanza tukiangalia haya maneno matatu jembe kawaida yake ni kutiwa mpini ndio lilime sasa mpini wake ni bashite au wote mchicha mwiba, Tinga tinga ni machine ya kutumia maguvu lakini haina mwendo hivyo sote tumekuwa vinyonga au Maana nyengine ni katuni na la tatu tumuulize Je ikulu imekuwa ni sehmu gani.

  Nikumuangalia huyu Pombe naona Watanzania tushaanza kulewa kwa kukosa muelekeo, uchapa kazi wala elimu ka huyu bwana sio muhimu kwake yeye muhimu ndio mzee, na haya ni madogo tu tusubiri makubwa yanakuja maana sasa polisi badala ya kuwa usalama wa raia imekuwa ni genge la kihuni lenye uhasama na raia.

 11. Smart 24/03/2017 kwa 7:44 mu ·

  Anaandika Dr.Christopher Cyrilo (MD).
  ____________________
  Pongezi kiduchu zimfikie Nape Nnauye kwa kuonesha kuwa kinyume na ufedhuli, lakini pongezi hizo kiduchu na hatua yake ya kuwa kinyume na ufedhuli, havifuti ufedhuli wake. (Nape ni fedhuli anayevuna alichopanda).

  Kwa maneno machache tu;

  1. Nape na vijana wenzake wa CCM ndio waliozunguka nchi nzima kumtukana Lowassa, ambaye wakati huo alikuwa moja kati ya watu muhimu ndani ya Chama chao. Lakini kwa sababu ya kutumikia makambi na makundi ya chama, wakazunguka kutukana na kupakaza uongo kwa manufaa ya kundi fulani.

  2. Nape ndiye aliyetangaza ushindi wa CCM hata kwa goli la mkono, akijua kabisa ni kinyume cha demokrasia.

  3. Nape ndiye aliyewatolea maneno machafu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, waliodai uchaguzi ulikua na mapungufu mengi.

  4. Nape ndiye aliyetangaza kulifungia MILELE gazeti la Mawio, kwa madai ya uchochezi, kwa sababu tu liliandika habari zisizowafurahisha watawala.

  5. Nae mdiye aliyelifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 (miaka mitatu) kwa madai ya kuandika habari zenye kumchafua Naibu waziri wa Ujenzi Edwin Ngonyani.

  6. Nape ndiye aliyefungia Radio Magic Fm na Radio Five Arusha kwa madai ya uchochezi, kisa tu radio hizo zilikua zilitoa nafasi kwa viongozi wa upinzani kuongea na wananchi.

  7. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kufuta bunge Live, na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kufuatilia kazi za viongozi wao bungeni.

  8. Nape ndiye anayedaiwa kuagiza Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi Selemani Mathew afungwe gerezani kwa kufanya mkutano bila kibali, kwa sababu Mathew alimshinda kwenye kura za maoni jimbo la Mtama mwaka 2015 akakatwa, na kwenda Chadema.

  9. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ndiye aliyesema CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa vipande vya karatasi.

  10. Nape ndiye aliyetengeneza propaganda ya kusema Lowassa ni mgonjwa na hafai kuwa Rais. Propaganda hiyo ilitumika na viongozi wa CCM kumchafua Lowassa na kumpunguzia kura.

  11. Nape akiwa mkoani Ruvuma kwenye ksmpeni za uchaguzi, alimuita Magufuli Rais hata kabla ya uchaguzi. Yani alijiona kama Mwenyekiti wa Tume ya ucjaguzi mwenye uwezo wa kupanga matokeo na kuamua nani awe kiongozi.

  12. Nape akiwa Katibu Mwenezi wa NEC na mjumbe wa Kamati Kuu ndiye aliyewasilisha azimio kwenye Kamati ya maadili la kumkata Lowassa katika hatua za awali za mchujo. Azimio hilo liliungwa mkono na wajumbe wengine na Lowassa hakupita hata kwenye 5 bora.

  13. Nape ndiye aliyeshawishi wafuasi wa Lowassa waliobaki CCM watimuliwe akiwemo Mhe.Sophia Simba ambaye amevuliwa uanachama na kupoteza ubunge wake na uenyekiti wa UWT.

  14. Nape ndiye aliyekuwa injinia wa kupitisha muswada wa sheria mbaya kuliko zote ya habari, ambao tofauti na lengo linaloelezwa, ukiisoma sheria ile na kuielewa, utagundua sio tu inaminya uhuru wa kupashana habari lakini pia inapingana na stratejia za kupambana na ufisadi, stratejia ya ‘Whistle blower policy’ inayotajwa kuwa bora kabisa katika kupamabana na ufisadi, inawekewa ukinzani na sheria ya Habari ambayo Nape alihusika moja kwa moja katika kuipitisha.

  15. Nape ndiye aliyepigania sheria ya mitandao ipitishwe akiwa Katibu Mwenezi wa CCM ili kuzuia nguvu ya vijana wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  16. Nape ndiye ameongoza juhudi za waandishi kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa. Hakuna kipindi waandishi wameishi kwenye mateso kama kipindi cha utawala wa Nape.

  17. Nape ndiye aliyewasilisha hoja bungeni ya kutaka vyombo vyote vya habari (Radio na TV) vijiunge na TBC kila siku saa 2 usiku kwa ajili ya taarifa ya habari.

  18. Nape ndiye aliyepitisha muswada wa habari (ambao kwa sasa ni sheria) ya kulazimisha waandishi wote wa habari kuwa na degree moja kabla ya mwaka 2021. Mwandishi ambaye hatakuwa na degree wakati huo HATATAMBULIKA kama mwandishi wa habari.

  Huyo ndiye Nape Moses Nnauye ambaye leo kuna watu wanamuona shujaa, kwa sababu amevuliwa uwaziri. Hivi yeye ni mtu wa kwanza kuvuliwa uwaziri? Mgogoro wake na Makonda haumfanyi kuwa shujaa.

  Kuna watu wanasema ni shujaa eti kwa sababu ya kuunda kamati ya Uchunguzi uvamizi wa Clouds. Lile ni jukumu lale kama Waziri. Na asingefanya hivyo umma ungemiwajibisha. Sasa mnamuonaje shujaa mtu aliyetimiza wajibu wake? Hivi housegirl wako akideki nyumbani utamuona shujaa wakati ametimiza wajibu wake?

  Labda tumpongeze kwa ujasiri wa kujitokeza hadharani na kupinga udikteta wa Rais wake. Udikteta ambao Lissu ameupinga kwa muda mrefu. Wakati akina Lissu wanaongea akina Nape walidhani hawahusiki, kwa hiyo wakakaa kimya. Leo yamewakuta wanataka kufanya ni msiba wa kitaifa.

  Yani wakati Lema anakamatwa na kudhalilishwa akina Nape walikaa kimya. Lissu kukamatwa na kudhalilishwa Nape kimya. Vijana wa upinzani kunyanyaswa, kupigwa (refer Mdude), kufungwa magerezani (refer Mwaifunga) na wengine kupotezwa (refer Ben Saanane) Nape na wenzie walikaa kimya kama vile hayawahusu, leo yamemkuta yeye anaonekana shujaa?

  Ukweli ni kwamba Nape hajawahi kuwa mtu muhimu kwa taifa, bali amekuwa mtu muhimu sana kwa CCM. Ameisaidia CCM, ameipigania CCM alijitoa kwa ajili ya CCM. Alifanya kila aliloweza kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Nape, January na Mwigulu ndio waliomuweka JPM madarakani kwa kutumia mbinu halali na haramu. Bila hawa watu watatu pengine tungekuwa tunsongea mengine kwa sasa.

  Kwahiyo kinachomtokea Nape ni matokeo ya kile walichokitengeneza wenyewe. Anavuna matunda ya ufedhuli wake. Nape kafanya uovu mkubwa sana kwenye nchi hii ili kuisaidia CCM. Ni uovu wenye manufaa kwa CCM, sio kwa Taifa.

  Kwa hivyo, ikiwa Nape anahitaji huruma, basi atahitaji zaidi kuonewa huruma na a wanaCCM wenzake kuliko watanzania aliowanyanyasa, kuwakebehi na kuwadharau kwa muda mrefu.

  Ushauri wa bure: Nape kama mwanasiasa mwingine yeyote ana tamaa ya madaraka makubwa zaidi kuliko aliyowahi kushika. Kwahiyo ni veama akawa mkimya kwa kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile. Akae kimya, arudi kuwatumikia watu wa Mtama. Asome kitabu cha Robert Green; 48 laws of power, aangalie amekosea wapi.

  Zaidi ya hayo, amtafute mzee Lowassa amuombe msamaha na kuomba somo zaidi la siasa. Ajifunze kwa nini Lowassa bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa pengine kuliko aliyemteua na kumtumbua. Alamsiki.!

  ┬ęDr.Chiss Cyrilo, 23/03/2017.

Comments are now closed for this article.