Huyu sio Mwakilishi wa moja katika Majimbo ya Zanzibar?

Written by  //  25/06/2013  //  Habari  //  Maoni 59

Mwakilishi

Huyu ndie ama?

Kuhusu Mtunzi

I am particularly interested in combining photography with graphic design to communicate the message of the peace to a specific audience.

View all posts by

Maoni 59 katika "Huyu sio Mwakilishi wa moja katika Majimbo ya Zanzibar?"

 1. Alhabaad 25/06/2013 kwa 7:33 um ·

  DUHHHHHH!!!!

 2. Ghalib 25/06/2013 kwa 7:57 um ·

  Dah

 3. hamed mazrui 25/06/2013 kwa 7:59 um ·

  AIBU HIII

 4. Alhabib 25/06/2013 kwa 8:09 um ·

  mbona cjaona ndani hii ishu , cjafaham chochote wenye kujua watuelimishe jamani

 5. mzaliwa 25/06/2013 kwa 8:36 um ·

  Hapa nahisi huyu ni raiya wa kikenya sema anagombea uwongozi zanzibar,kama vile kina Raza kusema kwao mwera,mie najua Mwera kunawarabu sio wahindi,
  Wapo wengi zanzibar kama hao wechimba ndani ya ccm wengi wao ni wakuja tu Zanzibar sio wazaliwa halisi ndio maana hawatoki ccm inawalinda.

 6. Feisal Amour 25/06/2013 kwa 9:31 um ·

  Sioni la kushituwa. Mtu unaweza kuwa na vitambulisho nchi kumi lakini unajijua wewe ni mzanzibari. Kwani si mpango wa maisha tu. Watu wangapi waliondoka katika zanzibar kwa hilaki na wapo nchi jirani kibao. kitambulisho ni karatasi inaandikwa na kufutika. acheni fitina hizooooooo.

  • serelly 26/06/2013 kwa 4:05 mu ·

   @feisal Amour.

   Unauhakika gani kuwa huyu ni Mzanzibari? Kama ni Mzanzibari sawa. Lakini kama siye vipi?
   Unajua kaja na agenda gani?
   Je! Baadae akigombea Uraisi na akapewa na Watanganyika atatupeleka wapi? Huoni kuwa huyu hawezi kuwa na uchungu na nchi wala jamii yenyewe.
   Wewe Feisal Amour sikiliza bwana: “hitimisho la haraka haraka ni uvivu wa kufikiri”
   Ungekuwa karibu yangu ningekupiga mbonge la kono.

 7. Fatal 25/06/2013 kwa 9:33 um ·

  Duuh noma munataka kuniambia huyu ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jazira………………..Uhuru Kenyatta atamueleza nini):

 8. Ghalib 25/06/2013 kwa 9:39 um ·

  Aliomba ukimbizi kenya au huyu alikuja kuomba ukimbizi zanzibar ?

 9. serelly 26/06/2013 kwa 3:32 mu ·

  Mashaka haya! Inauma sana.

 10. ssba 26/06/2013 kwa 3:35 mu ·

  Mijitu mingine eti fitina !!!!!
  Hiyo id kama ni kweli lazima jazira awajibishwe na afunguliwe mashtaka kwani makosa kama haya yakiwachiwa watakuja wengi naamini na yeye anawajuwa wenziwe.JUSSA HEBU LIFANYIE KAZI JIMBO TUNALITAKA HILO

 11. serelly 26/06/2013 kwa 3:41 mu ·

  Sasa jamani huyu Kibwengo ni Mkenya? Huyu ni Mzanzibari kaghushi Kenya? Au vipi? Stonetown (Kiongozi) hebu tupe tujue, hii ni issue ya kufuatiliwa kwa kina bwana, inanikereketa sasa.

 12. serelly 26/06/2013 kwa 3:52 mu ·

  Jamani MUUNGANO hasa ni mbaya! Jamani MUUNGANO gani wenye matatizo kama haya Jamani?. Mimi pia napata mashaka kuwa kweli maafisa wa uhamiaji wanaweza kuwajisha huyu jamaa? Maana ndio yumo ndani ya system {CCM-ZANZIBAR}.
  Mimi naona kama itathibitika anahatia hii mbaya kabisa na wakiamua kumlinda basi Wazanzibari tumuwajibisheni mitaani (Chochoroni), tusikubali USHENZI huu.

 13. serelly 26/06/2013 kwa 4:01 mu ·

  Unauhakika gani kuwa huyu ni Mzanzibari? Kama ni Mzanzibari sawa. Lakini kama siye vipi?
  Unajua kaja na agenda gani?
  Je! Baadae akigombea Uraisi na akapewa na Watanganyika atatupeleka wapi? Huoni kuwa huyu hawezi kuwa na uchungu na nchi wala jamii yenyewe.
  Wewe Feisal Amour sikiliza bwana: “hitimisho la haraka haraka ni uvivu wa kufikiri”
  Ungekuwa karibu yangu ningekupiga mbonge la kono.

 14. serelly 26/06/2013 kwa 4:04 mu ·

  Unauhakika gani kuwa huyu ni Mzanzibari? Kama ni Mzanzibari sawa. Lakini kama siye vipi?
  Unajua kaja na agenda gani?
  Je! Baadae akigombea Uraisi na akapewa na Watanganyika atatupeleka wapi? Huoni kuwa huyu hawezi kuwa na uchungu na nchi wala jamii yenyewe.
  Wewe Feisal Amour sikiliza bwana: “hitimisho la haraka haraka ni uvivu wa kufikiri”
  Ungekuwa karibu yangu ningekupiga mbonge la kono

 15. rayun 26/06/2013 kwa 4:43 mu ·

  in whatver case hii ni utata na unapaswa kutolewa maelezo ya kina ili kila kitu kiwe juu ya sheria, ata awe alzaliwa zanzibar akakimbilia kenya bdo tunataka maelezo ya kutosha, yeye ni raia wa wapi kenya au tanzania?, ni harufu ya ufisadi wa kutisha si khasha kuna watu wamo kwenye taasisi nyeti za zanzibar ambao hawastahiki kuwepo.
  dah mumetufikisha pabaya, mumeigeuza zanzibar yetu jamvi la wageni, shamba la bibi, punching bag, …………………..nk sooo bad inanisikitisha
  there is a need to screen other leader in zanzibar.
  asbh njema wakuu

 16. rayun 26/06/2013 kwa 4:54 mu ·

  oh! shit !!! wht kind of guy you are, is it minor issue?, acha kufkiria kw mak….lio, tumia akili, si kwa kua ametokea mombasa ukaona sio issue kua ni mwenzetu, still ni jambo zito linahtaji maelezo ya kutosha, ikiwezekana na uwajbkaji wa baadh ya watumishi wanaohisika,
  kwa nini awe raia wa kenya na saiv awe mwakilishi wa r.leo?, uraia wa tanzania ameupataje?, tangu afike zanzibar alifikisha miaka mingapi? sheria za uchaguzi za zanzibar znasemaje kuhusu wageni kugombea uwakilishi na harakati za kisiasa?, alitimiza vgezo vya kisheria mpk kufikia kuupata uwakilishi na uraia?
  ukiwa unafkiria kw kutumia ubongo unapaswa kufikiria mambo ayo, sio kuja na blaa blaa zako kua sio issue, sijui fitna
  hapa ni facts, huwezi nenda facebook.

 17. Feisal Amour 26/06/2013 kwa 4:55 mu ·

  siku hizi mzalendo imekuwa sehemu ya kuwala watu nyama. hivi mumekaa munajadili mtu nyinyi. Hivo inakubalika kuitia picha ya mtu pasi kuwa na uhakika wa maneno na kumharibia jina au maisha yake?. Tumuogopeni Mwenyezi Mungu. Aliyeileta hii picha ajitahidi sana kuomba radhi.
  wassalaamu aleikum.

 18. Makengeza 26/06/2013 kwa 5:01 mu ·

  Huyu naona hafanani na mwakilishi wa Rahaleo. Lakini kama ndie basi Mheshimiwa Jazira ni mzaliwa wa Zanzibar. Kazaliwa Kengeja. Aliwahi kuishi Mombasa. Aliporudi Zanzibar alimuoa mtoto wa Pandu Kificho ambae ni mkewe mpaka leo. Hana uCCM wa hivyo. Ukereketwa wake ni kutokana na ndoa yake na mtoto wa Kificho.

 19. bin nassor 26/06/2013 kwa 5:10 mu ·

  MZALENDO SASA TUNAKOELEKEA SIKO,HIZI KASHFA ZA KUGHUSHIWA SI NZURI KWA SABABU ZINAGUSA MAISHA YA WATU NA FAMILIA ZAO MOJA KWA MOJA NA ZINAKIUKA SHERIA ZA HAKI ZA BINAADAM ZA KUDHALILISHANA KWA KUFOJIANA.

  MIMI NINGEKUSHAURI @ STONETOWN KIONGOZI,TUWACHE HUU UPUUZI TUNAOUENDEKEZA KATIKA MZALENDO TUWEKE MAMBO YA MSINGI YA KUJADILI KWA SABABU TUKIANZA KUJADILIANA MMOJA BAADA YA MMOJA TUTAADHIRISHANA HUMU,KWA SABABU KUNA VIONGOZI WAKUU WA NCHI NA WA VYAMA VYA SIASA WANA URAIA WA UARABUNI,WENGINE WANA VITAMBULISHO VYA UK,HATA MEMBER WENGI WA MZALENDO NA WAANZILISHI WANA URAIA WA UK NA TANZANIA TUNAWAJUA HUMU AU WAANZWE KUWEKWA NA WAO KATIKA MITANDAO

  KAMA SISI NI WAUNGWANA WA MZALENDO ,TUJITAHIDINI KUWEKA MAMBO AMBAYO YA MSINGI KAMA HII HAITOSHI BASI TUENDELEENI NA KUWEKA MAMBO HAYA YASO MAANA LAKINI TUTAADHIRISHANA HUMU KWA SABABU TUNA DATA ZA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI WENYE PASSPORT NA ID ZA NJE YA NCHI

  TUMUOGOPENI MUNGU KWA FITNA HASA KAMA ANAEPOST HIZI NI MUISLAM,AJUE KAMA MAISHA YA DUNIA MAFUPI MAISHA YA AKHERA NI KILA KITU UTAULIZWA ULICHOKIFANYA

  • Makengeza 26/06/2013 kwa 7:35 mu ·

   Mie nafikiri Bin Nassor kama una ushahidi kama huo wa passport au vitambulisho vya viongozi wa Zanzibar ambao wana uraia wa nchi nyengine bora uuweke. Hatutaki kujenga Zanzibar ya kinafik au ya watu wa sura mbili.
   Kama huna ushahidi isipokuwa dhana tu basi bora ukae kimya.

 20. alfola 26/06/2013 kwa 6:24 mu ·

  Wazanzibari tunajuwani, HATA kama una passport ya mbinguni kwani haya yote yameletwa na kero ,matatizo na dhulma za kimaisha ndio ilosababisha watu kutawanyika kila pembe ya dunia,
  sababu ni ubaguzi uliokuwepo,kukosa ajira n.k.
  Sasa tuzungumzie Zanzibar mpya inayo mtambua kila Mzanzibari na kuwa na haki sawa kwenye visiwa vyetu.
  Namnukuu MAKENGEZA hapo-(Mheshimiwa Jazira ni mzaliwa wa Zanzibar. Kazaliwa Kengeja. Aliwahi kuishi Mombasa. ).
  Basi wakitokea watu wa kengeja 10 wanomtambuwa tosha,
  Zanzubar moja , Watu wamoja na Taifa moja.

 21. serelly 26/06/2013 kwa 8:52 mu ·

  Namfuatilia huyu jamaa nina watu wa Kengeja wengi Classmates wangu na majirani zangu. I will bring the facts. Mr. JUSSA GET PREPARED TO RECIEVE THE TRUTH HINTS.

  @BIN NASSOR.

  1. My God! Kama watu wenyewe ninaowategemea ndio kama wewe Zanzibar must be perished.

  2.Wewe umeona wapi kuwa viongozi wa juu wakiwa wana makosa walionayo wa chini hukumu yake ni kunyamaza ili kuchunga mapenzi ya kisiasa na aibu ya viongozi?

  3. Au na Wewe ndio katika walee wagonjwa ambao mkitajiwa Dr. Shein au Maalim Seif mnaona katajwa Nabii mmoja ma’asum (protect against mischiefs) asiyekuwa na Kosa wala dhambi? Tutafika?. Zindukeni!!

  Je! Haya ni mapenzi kweli? Na aibu hiyo tunayoikwepa kwa kufunika aina hii ya stara ya mkwe, ni stara kweli?

  Sasa ikiwa mambo unataka yaende kama hivyo, utawala wa Haki na Sheria unamaanisha nini?

  Kweli Bin Nassor umefikia kiwango kama hicho cha muhali na uyakhe? Hivi ni bora Nchi iumie na Jamii kwa ujumla ili angalau mambo ya wakuu yaende tu?

  Ni nchi gani Duniani imeweza kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kufumbia fumbia macho mambo kama haya?

  Bin Nassor, mbona nikifumba macho nahisi kama ninazungumza na NASSOR ALI ISSA Mwakilishi wa Rahaleo? Ndio wewe nini?

  Hatukubali aslan. Patachimbika!

  Nawasilisha.
  SERELLY.

 22. Wamtambwe 26/06/2013 kwa 9:42 mu ·

  Mimi sioni kuwa hiyo ni kashfa. Mombasa kiasili ni Zanzibar na wao wanajitambua hivyo . Siasa tu ndiyo ilofanya Mombasa ikaangukia kenya.
  Kuna watu kwa maelfu ambao wamezaliwa Zanzibar na wakajipatia elimu Zanzibar na hivi sasa wanaishi Uarabuni au kwengineko duniani. Muhimu wanapokuja waseme ukweli tu, sio wajifiche, hio sioni kuwa ni Kashfa. Tumuangalie Schwarz Neger yule ni Swiss lakini anaishi Marekani ameruhusiwa kugombea ugavana na hafichi kuwa yeye ni Mswiss

  • kifukumkunyi 26/06/2013 kwa 9:59 mu ·

   Hili lenu ni bobojo tu Karume ni Mzanzibari? Jumbe ni Mzanzibari? Mwinyi(Mzee Condom) ni Mzanzibari. Hao wote walikuwa maraisi wa Zanzibar. Muungano Oyeee !!!!!!!! Mapinduzi Daimaaaa

 23. mohamed 26/06/2013 kwa 10:10 mu ·

  Babababababababa bbaaaa!!!! tumekwisha

 24. battawi 26/06/2013 kwa 12:51 um ·

  Tukiipata nchi yetu basi huyu atawakilisha jimbo la mambasa,kwani ni sehemu ya znzibar,iliunganishwa kenya si kwa muungano rasmi bali makubaliano ya Amana yangu nishikie .
  Mombasa ni sehemu ya zanzibar. Hao hapo juu wote ni ahali porojo hawajakuelewa
  Ahsante

 25. fey 26/06/2013 kwa 12:57 um ·

  Hata iweje huyu awe kazaliwa kengejaa au kingepungua madhali ana uraia wa nji nyengine tayari si mzanzibar labda awe baada ya kurudi Zanzibar ameomba uraia upya kwani alikwisha uwacha ( na vile Tanzania hairuhusu raia za nchi mbili ) Kama sio hivyo ana haki ya kuishi Kama visitor na sio kuwa MP hata Kama ameoa mtoto wa nani

 26. ssba 26/06/2013 kwa 1:28 um ·

  Hao kina mwinyi .karume nani nani tungelipata ushahidi kama huu nao pia tungewajadili hapa mh.salum ana uraia upi kwa sasa KENYA au TANZANIA ?

 27. Abdul 26/06/2013 kwa 2:28 um ·

  ingelikuwa nchi zilizo endelea basi huyu haramia engeli chunguzwa na kufuatiliwa na kuhojiwa lakini hapa kwetu uamsho tu ndio huhojiwa na kuekwa ndani

 28. bin nassor 26/06/2013 kwa 2:59 um ·

  @serelly
  @ makengeza

  mm sina access ya kupost hapa bt kama ningekua nina access ya kupost ningeweka Passport za nchi za nje za viongozi wetu wakubwa katika nchi hii hasa zanzibar na vitambulisho vyab wazanzibar ambao wanaishi nje wana vitambulisho vya UK na nchi nyengine na vitambulisho vya mzanzibar na kura wanavyo na ushahidi wa hivyo vyote vipo

  Foolish usiropoke tu kwa mapenzi yako haya mambvo yapo wakati wa kura wanakuja zanzibar na zanzibar id na vitambulisho vya kura uchaguzi ukimalizika wanarudi Abroad na passport za Abroad .naomba niombee access au nitumie password katika e-mail hii nassorboy@yahoo.co.uk ili niweze kupost uuuone ushahidi ntawaumbua mmoja baada ya mmoja

  TENA USSHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHH kaa kimya usilete mapenzi ya chongo ukasema kengeza,viongozi wetu wanafiki na waovu ukiwemo ww @serelly na @ makengeza

  • serelly 26/06/2013 kwa 4:49 um ·

   Nakuu “kama ningekua nina access ya kupost ningeweka Passport za nchi za nje za viongozi wetu wakubwa katika nchi hii hasa zanzibar na vitambulisho vyab wazanzibar ambao wanaishi nje wana vitambulisho vya UK na nchi nyengine na vitambulisho vya mzanzibar na kura wanavyo na ushahidi wa hivyo vyote vipo”

   Mimi naunga mkono uwaanike wote kama ni kweli ushahidi huo upo na unao.
   Huu mtindo wa kulindana lindana lazima ukomeshwe ni mwanya mkubwa wa dhulma na kuzorotesha maendeleo na ndio unaotutafuna.

   @stonetown and Ashakh
   Tunaomba mumtumie hiyo access bwana mkubwa Bin Nassor atuwekee unuko wa kina………………….
   Tunasubiri, usije ukaingia mitini.

   • Ashakh (Kiongozi) 27/06/2013 kwa 1:14 um ·

    access ya kuomba kupatiwa haki za kkuweko post ni hii:
    admin@mzalendo.net

    Unatakiwa ulete maombi ya kupatiwa haki hiyo.

 29. duduzuri 26/06/2013 kwa 5:08 um ·

  najiuliza kama angekua mwakilishi wa CUF jee stonetown angeweka habari hii hapa. ili kumtendea haki muhusika ingependeza kufanya uchunguzi japo kidogo kujua jamaa kazaliwa wapi nk so ana id ya kenya so what .kuna wazenji kibao mmejiripua kwa kila aina ya utaifa huko nakuchallenge stonetown uweke vitambulisho unavyotumia huko uk tuvione hapa kama na wewe sio msaliti kwa njaa zako.

  • Makengeza 27/06/2013 kwa 4:45 mu ·

   Nahisi kama huna hoja au kama una chuki zako binafsi juu ya stonetown basi usichangie hii hoja. Kwasababu badala ya kutoa hoja unaingia watu mwilini.
   Mambo ya kuzungumza katika sualahili ni 1. jee huyu mwenye kitambulisho hiki ni Nassorr Jazira au laa? Kama sie hakuna haja ya kuendelea. Kama ndie basi 2. Jee alipogombania uwakilishi kwa kuwa yeye ni mkwe wa Pandu Ameir Kificho jee aliukana uraia wa Kenya? Haya ndio mambo ya msingi ya kujadili.
   Kama Stonetown (Kiongozi) atakuja kuwania uwakilishi wa Zanzibar tutamuhoji vilevilekama tutakuwa na ithibati kama si raia.

   • duduzuri 27/06/2013 kwa 6:32 mu ·

    Wewe mwenye hoja mbona huiandiki kwani stone town kaomba msaada wako?sema kama si raia au si mznz umebaku na insinuations za upuuzi tuu, niliuliza mwanzo hapo wangapi wana zan id na sio waznz.I’ve earned the right to comment on mzalendo.

    • Makengeza 27/06/2013 kwa 6:08 um ·

     Mpuuzi ni wewe unaecomment bila ya hoja.Unawaingia watu mwilini. Nafikiri minyenje inakuwasha.Usisumbuke sisomi tena maoni yako kwasababu unaonekane ni mpayukaji.

 30. Stonetown (Kiongozi) 26/06/2013 kwa 5:57 um ·

  Hakuna jina lilosajiliwa kwa anuani hii, vyenginevyo unawaza kutumia hio hio ulikuwa umetolea maoni hapa sheikh Nassor, Access Granted, kwenye masuala ya viongozi kutucheza shere hatuvumilii awe CCM awe CUF. haya sasa vianike hivyo vitu.

 31. Stonetown (Kiongozi) 26/06/2013 kwa 6:07 um ·

  Duduzuri, mimi kwanza nikutosheleze kwa kusema kinywa kipana, I havent claim asylum in UK by deceit ya kusema mimi mtu wa taifa lislo langu, hilo la kwanza lakini pia sijaomba nafasi ya uongozi kwa kuwaomba kura wananchi, kilichofanyika hapo ni kule kudanganya wananchi na pia kuihadaa tume ya uchaguzi, kama angekuwa kweli ana nia safi basi angerejesha tu uraia wa Kenya ama tunaweza kusema kuukana, ili aweze kuwa mwakilishi wa jimbo analolitka na kwa ticket ya chama akipendacho mwenyewe muhimu tu wananchi wamkubali.

  Kuomba hifadhi kwa Wazanzibari hiyo ni juu yao na kama wapo ambao watakuwa wameomba hifadhi kisha wakabahatika wakapewa madhali sheria za uchaguzi hazijabadilika na wao wasemwe.

  • duduzuri 26/06/2013 kwa 6:30 um ·

   this is exactly my point unamtuhumu huyu kwa kitu gani kavunja sheria ipi unajua kama ana uria wa kenya,kitambulisho kinaonyesha nimzawa wa mombasa wakati baadhi humu wamesema amezaliwa znz wangapi wana zan id na si wazanzibari naona zaidi ya hiki kitambulisho huna jengine, this was back in 1996, uraia upi ni native yake upi ameupata baadae, na kuhusu assylum application yako lets just say i know more than you think i do and you are not innocent!!!

   • Stonetown (Kiongozi) 26/06/2013 kwa 10:03 um ·

    Duduzuri, iweje, mwakili, mbunge ama mwengine yoyote kwenye ngazi ya kutunga sheria ama msimaizi wa sheria awe juu ya sheria?! jee hili waliomchaguwa wanalijua? jee tume ya uchaguzi wanalijua? alishawahi kuukana huo uraia mwengine na kama kaukana uthibitisho uwapi?

    Well regarding my back then application weather you know it or you dont it. I dont care, Have i claim otherwise more than who i am.? You wish.

    Kwa kuwa kila mtu ana ID 50 ama Uraia 100 haimfanyi mtu mwengine kama na yeye kafanya iakwa sio kosa. na hiyo ndio point especially lawmaker like him or any.

 32. kifupi nyundo 27/06/2013 kwa 5:54 mu ·

  Wageni hawafai kabisa kupewa uongozi , watatupa tabu kupima uzalendo wao………..Wagenii ni waharibifu ni vyema wakapewa kile wanachostahili-hadhi ya ugeni

 33. serelly 27/06/2013 kwa 6:13 mu ·

  Kama ni mzaliwa wa Zanzibar na hajaukana uraia wa Tanzania na hapo hapo ana uraia wa Kenya basi kosa ni kubwa na uwakilishi wake ni questionable na u-Tanzania wake pia, kwa sababu Tanzania right now hairuhusu uraia wa nchi mbili.

  In whatever case, ufuatiliaji juu yake ni must be done.

  Binafsi nimepiga hatua.

 34. serelly 27/06/2013 kwa 6:24 mu ·

  @Bin Nassor.

  Stonetown I think umemfahamu maelekezo yake juu ya vipi ututumie hayo madudu ya wakuu wetu hapa ukumbini.

 35. Stonetown (Kiongozi) 27/06/2013 kwa 12:09 um ·

  Tatizo mwakilishi sio kama ni mgeni, hapana tatizo ni uraia miwili tu, wakati sheria za Nchi na za uchaguzi haziruhusu.

  • Ghalib 27/06/2013 kwa 6:38 um ·

   @Stone town

   Sio uraia mi naona tatizo lipo hapa, kama unamuuliza nacho kipande cha uzanzibari atakupatia amezaliwa zanzibar, na huku ana kipande cha kenya amezaliwa kenya, jee hapo tumchulie vipi ?

 36. bin nassor 27/06/2013 kwa 2:01 um ·

  @ SERELLY
  sijaelewa boss wangu wa kazi…yaani nimesha scan passport na docs za waznz ambao wanavitambulisho viwili vyab Abroad na znz id na zan vote id niwatumie muone,aibu za wanoyasema ya watu yao wao duuuuuuuu ya wenzao midomo juuuuuuuuuu

  naomba kaka yangu Stonetown nielekeze jinsi ya kuweza kupost….kama ile huipati nitumie hio access katika allyfad@yahoo.com ntaicheck now

 37. makame maarifa 27/06/2013 kwa 3:53 um ·

  hamnakumnyamazia mtu hata awenani weka tuone bina bed

 38. Ghalib 27/06/2013 kwa 6:36 um ·

  Haya vvipi kipande cha uzanzibari pia anacho ? kinasemaje ? Kazaliwa wapi ? Nahofia pia Balozi seif iddi sio mzanzibari wala mtanganyika.Ali vuai Ali vile vile ndo mana wanang’ang’ania muungano.lol

 39. jabir 27/06/2013 kwa 7:22 um ·

  Aslaam Aleykum Wanaukumbi. Msitishwe na wanaojaribu kuvuta kamba mjadala wa mwakilishi huyu usite. Hapana hata kidogo. Endeleeni kujadili hili, huyu ni kiongozi wa wananchi anayelipwa mshahara na maposho kwa fedha za wananchi.

  Sasa ili kukoleza mjadala, kama yupo mtu wa Kengeja humu aulize kule wanaojua aila za mwakilishi watuletee taarifa humu. Naambiwa, ila sijathibitisha, huyu ni mmoja wa Wazanzibari waliokuwa Shimoni baada ya Januari 2001. Alipokuwa kule akapata uraia, sasa ameukana ule wa Tz? Hili ndilo swali muhimu hapa. Kama hakukana ina maana ana dual citizenship, which is unnacceptable in Tanzanian Law. Hapa ndipo penye utata. Tuendeleeni kutafuta ukweli. Mwisho wa khabari tutamuuliza mwenyewe ajieleze.
  Wakatabahu.

 40. xkalasinga 28/06/2013 kwa 10:42 mu ·

  jamaa anajiita kiongozi na hao wafuasi wako sijui hata unakiongoza nini ..mimi nadhani ujiite kikojozi maana kazi yako kuleta harufu mbaya tu hapa na roho mbovo , husda nusksi zilizowajaa. tafuteni kazi za kufanya kama mkikosa nitafuteni mimi nitawapatia za kuparamira.

 41. jazz 29/06/2013 kwa 8:56 mu ·

  Watu wengi humo wanamtetea huyu jamaa kwasababu na asili ya pemba, lakini ukweli wenyewe kama huyu jamaa ana uraia wa kenya basi hafai kuwa kiongozi Zanzibar

 42. serelly 29/06/2013 kwa 9:42 um ·

  NILIAHIDI NATIMIZA BI IDHINILLAH..

  Nimejitahidi kumfuatilia huyu jamaa kwa kina na kwa njia tafauti ikiwemo kuzungumza na watu walioko KENGEJA-PEMBA na kwa bahati nzuri kabisa watu wawili miongoni mwa watu niliozungumza nao ni jamaa zake wa damu kabisa kabisa ambao kwa upande wangu ni marafiki wangu wa pete na kidole. Nilihofia kuwa damu ni nzito kuliko maji. Lakini alhamdulillah jamaa ni Wazalendo kuliko hata mimi mwenyewe maana walikuwa serious kiasi kwamba Mimi mwenyewe nilijiona sijafikia climax kabisa, cha ajabu mmoja wao ni Mwanamama {a woman} na alikuwa so straight foward and to the intended points. Bado ZANZIBAR ina watu hai ingawa sio wote lakini wapo wengi ukilinganisha na mazoba.

  1. Kwanza kabisa Huyu jamaa jina lake halisi ni NASSOR SALUM ALI na sio NASSOR ISSA ALI kama kipande cha Uraia wake wa KENYA kinavyoonesha hapo juu.

  Je! Ni kwa nini Kwenye kadi ya Uraia wa Kenya kajiita NASSOR ISSA ALI? Nitajibu chini huko.

  2. Huyu Ndugu NASSOR SALUM ALI ni mzaliwa wa KENGEJA, amesoma katika skuli ya KENGEJA mpaka FORM III ambapo kama mnavyojua kuwa ilikuwa ndio mwisho wa elimu ya Ordninary Level “O Level”. Kwa mujibu wa wadadisiwa hatukupata data zinazoonesha kuendelea kwake kielimu zaidi ya hapo, kwa hivyo tuko silent.

  3. Baada ya Masomo yake alielekea nchini KENYA (Mombasa) ambako Baba yake mdogo {Ammy} anaishi mpaka hii leo, Baba yake huyu mdogo anaitwa Bw. ISSA ALI. Huko alioa binti wa Kikenya na kupata watoto wawili wa kike, bahati mbaya Mke huyu alimuacha (kamtaliki) na aliporejea nyumbani Zanzibar binti yule alibakia na watoto huko huko kwao nchini KENYA.
  Lakini baadae ndugu yake mmoja ajulikanae kwa jina la Bw. SULEIMAN SALUM ALI alikwenda kuwachukua wale watoto nchini KENYA na kuamua kuwalea katika VISIWA VIZURI VYA ZANZIBAR lakini baadae Mama yao aliamua kuja kuwachukua na Kuwarudisha nchini KENYA ambako hadi hii leo wanaendelea na maisha yao. Allah awape maisha mema na awatunze ili awaridhie. Ameen. Ni wana wetu.

  4. Kuhusu kuoa mtoto wa Mh. PANDU AMEIR KIFICHO, jambo hili limetupa taabu sana ingawa tulijaribu kumtafuta mtoto fulani wa kiume wa Mh. Spika ambaye alhamdulillah ni Muislamu na Mzalendo safi lakini hatukufanikiwa kumpata ili kulitolea maelezo jambo hili.

  Hata hivyo utafiti wetu ulingundua kuwa Bw. NASSOR SALUM ALI anataarifa inayofanana na hiyo, kuwa baada ya kurejea nchini ZANZIBAR, mbali na kumuoa binti mmoja ajulikanae kama AZZA (hatukuipata nasabu yake) ambae baadae aliachana nae kisha alioa katika familia ya Mh. Dr. OMAR ALI JUMA (almarhoum) binti huyu anajulikana kama Bi. ZUHURA MGENI MWALIMU ambae mpaka sasa anaendelea kuishi nae na wamebatika kupata watoto takriban watatu kama sijakosea.
  Hata hivyo Bw. NASSOR SALUM ALI aliwahi kumuoa binti mmoja ajulikanae kama Bi. NURU lakini pia ameshamwacha (treaty breaker), sasa huyu ndio tulitia masha kuwa labda ni katika familia ya Mh. PANDU AMEIR KIFICHO lakini we haven’t managed to collect the data in the field.

  5. TUKIMREJEA YEYE MWENYEWE, Information of our interest ilikuwa ni:
  a) Baba yake ni Bw. SALUM ALI (MZANZIBA- KENGEJA) kashafariki Dunia, Allah amrehemu, amzidishie kheri zake na amsamehe makosa yake. Ameen.
  b) Mama yake ni Bi. MKUBWA WA JUU BINT SULEIMAN (MZANZIBAR-KENGEJA) Yuko hai, Allah ampe maisha marefu na mwisho mwema. Ameen.
  c) Bw. NASSOR SALUM ALI amezaliwa ZANZIBAR katka kijiji cha KENGEJA.
  d) Kweli amewahi kuishi nchini KENYA tena kwa muda mrefu tu.

  6. ENEO TETE KUHUSU Bw. NASSOR SALUM ALI:
  a) Kwa sasa anauraia wa KENYA tu bila ya kuwa na ule wa TANZANIA?
  b) Aliukana Uraia wa TANZANIA ili apate ule wa KENYA na baadae kurejea TANZANIA bila ya kuchukua tena Uraia wa TANZANIA? Na hivyo ni MKENYA ama?
  c) Je! kwa sasa anauraia wa nchi mbili TANZANIA na KENYA? Kama ni hivyo Sheria ya Uraia TANZANIA inasemaje?

  Kuhusu jina lake kuwa ni NASSOR ISSA ALI kwenye kadi ya uraia wake wa KENYA ni kuwa alighushi na kuzidanganya Mamlaka nchini Kenya ili apate haki zote za MKENYA, na ili kulirahisisha hilio aliamua kulitumia jina la Ammi yake ambaye yuko humo nchini KENYA kwa muda mrefu na bila shaka ameshakuwa mwenyeji, na kama lingetokea la kutokea ingekuwa rahisi kumkingia kifua kwa kusema huyu ni mwnangu wa kumzaa. Hawa ndio viongozi wetu tuliowakali vinywa wazi ili watushibishe haki kupitia utawala wa Sheria. Watu wa Raha Leo mpo?

  7. Mwisho nini kifanyike? Na nani akifanye? Nawaachia wanaukumbi.

Comments are now closed for this article.