HUU NI UJUHA WA DHAHIRI

Written by  //  13/11/2014  //  Habari, Kitaifa  //  Maoni 10

Assalaam alaykum warahamullahi wabarakatuh!
Leo wadau napenda kupanda jukwaani kama ifuatavyo:

Sote tunajua kwamba Passport/Pasi ya kusafiria ni kitambulisho cha mtu hata akjuilikana ni raia wa nchi gani.

Tukiangalia nchi nyingi duniani mtu anapozaliwa tu anapewa utaifa wake lakini cha ajabu na cha kusikitisha hapa kwetu Tanzania si kila mtu ana miliki passport/pasi ya kusafiria, na hata ukienda Ofisi za uhamiaji kuomba pasi ya kusafiria basi hakika utakabiliwa na vikwazo hata havingii akilini.

Hivi serikali zetu hazijui kama kuwapa raia wake utaifa wao/uraia wao ni kuweza kuwadhibiti hata wageni kuingia kiholela?? kwa mfano anaweza kuja kutoka Mombasa,Malindi au Lamu kule Kenya anaezungumza Lugha ya Kiswahili vizuri kama wanavyozungumza Wenyeji wa Kiswahili, akadai kuwa yeye ni mtanzania halali na akadai uraia na kupewa.

Leo wazanzibari ndani ya nchi yetu tumepewa Kadi eti za Mzanzibari Mkaazi ina maana sisi ni wahamiaji tunakaa Zanzibar kwa Ikama tu sio kwetu???

Kuwanyima wananchi haki yao ya Kitaifa ya kumiliki pasi ya kusafiria mara tu baada ya kuzaliwa kunaongeza jopo la uhalifu ndani ya nchi yetu.

Hivi Serikali imewahi kuyafikiria haya???

Napenda Kuwasilisha.

Kuhusu Mtunzi

BLOGGER/DEVELOPER/JOURNALIST/BROADCASTER

View all posts by

Maoni 10 katika "HUU NI UJUHA WA DHAHIRI"

 1. Ghalib 13/11/2014 kwa 8:19 mu ·

  Hawa viongozi wameweka huo utaratibu ili watanzania kuwa wakimbizi katika nchi yao, Unajua unapokuwa na passport inakufanya ije hamu ya kusafi ili kuona ulimwengu. Hata kama Huna uwezo lakini utaweka nia tu.

  Na viongozi wetu hawataki wananchi wao wasafiri, kwani kusafiri ni njia moja ya kujifunza au kusoma, unakwenda nchi nyengine unaona maendeleo tofauti na culture tofauti, hii inaweza kukufumbua macho wewe nani na unatabia gani, unatoka wapi,madhingira gani, utajifunza kuona sheria za nchi unakwenda, mengi tu.

  Wakati wa nyerere kumiliki passport ilikuwa shughuli kwani mtu huyu hakutaka watanzania kusafiri ili kuamka usingizi mnonono.

  Cha msingi Zaidi passport ni identity muhimu katika utambulisho, kitaifa na mataifa.

  Hivyo sisi wananchi tupiganie haki hii tupewe bila ya shuruti zozote, tuwaombe wanasheria legal services kufanya kazi hio ili immigration wabadilishe huo mfumo wao,kwani hauna manufaa kwetu.
  Nchi nyengine unapewa passport bila shuruti zozote, hapa Tanzania ukitaka lazima uwoneshe uthibitisho wa safari yako, pili lazima fomu ikasainiwe mahakamani, pamoja na picha. Huu ni mzunguko mkubwa na vikwazo vikubwa inatunyima haki zetu kama wananchi wenye kupewa haki za kiraia.

 2. Wamtambwe 13/11/2014 kwa 9:57 mu ·

  Nataka kupingana na mwandishi kidogo, Passport ni document ya kusafiria na mtu anaweza kuwa nayo na anaweza asiwenayo.
  Identity Card ndiyo mtu anatakiwa awe nayo wakati wote anapokwenda na hiyo ni sheria, polisi anaweza kukusimamisha wakati wowote akakuuliza Kitambulisho chako. Ni kwamba mtu anapozaliwa Data zako zinaingizwa kwenye Computer kule kule Hospital , siku ya pili yake tu unakwenda kunakohusika kuchukua cheti cha kuzaliwa. Unapotimiza umri wa miaka kumi na 18 tu Automatik wewe ni mpiga kura na unaletewa barua nyumbani ukapige kura, unachagua kama utakwenda kituani, au unaweza kusema huna nafasi uletewe nyumbani ili upige kura baadaye utume kwa posta, au kwa internet. Hiyo ni haki yako huna haja ya kumuona shekha au diwani au mwenyekiti wa Jimbo.
  Zanzibar walikuwa wafanye hivyo hivyo watoe hivyo vitambulisho kwa watu wote, angalau kwa wale watakaofikia miaka 18
  Kwa wale waliozaliwa miaka ya 60 watakumbuka wazee wetu wote wakati ule walikuwa na kadi za Uraia na sio passport.

 3. wagombero 13/11/2014 kwa 12:47 um ·

  mmmh.haya amani iwe kwenu .wachangiaji.

 4. Alhabib 13/11/2014 kwa 1:42 um ·

  wamtambwe hiyo unayozungumzia ww ni ulaya sio africa ammi, mtuoa mada anazungumzia hapo kwetu hakuna sharia kitu haki yako basi lazima utoe mlungula maisha gani ayo

 5. NKARAFUU 13/11/2014 kwa 3:16 um ·

  JAMANI MIMI NAULIZA NIKITAKA KUANDIKA MAKALA AU MADA MZALENDO .NET NIFANYEJE AU NITUMIE NJIA GANI MANA NAONA SIONI LINKI AU MAELEKEZO .TAFADHALI NAOMBA MSAADA KWA AJUAE

 6. mas-albimany 13/11/2014 kwa 5:10 um ·

  @wamtambwe ahsante kwa maoni yako mazuri, lakini kama utafumbbua macho kidogo angalia kadi zetu za zanzibar zimeandikwa kitambulisho cha mzanzibari mkaazi ina maana sisi ni wakaazi tu tunaokaa zanzibar kwa ikama/kwa viza na kama ni hivyo usemavo tulikuwa tupewe kadi za utaifa kama zinavyofanya nchi nyingi, kwa mfano Oman, UAE, KSA na nyenigne za huko ulaya na marekani,
  kwa mfano me kwa sasa nipo haoa Gulf Countries nimepewa kadi ya Iqama yaani naishi hapa kwa viza, na raia pia wanazo zao za uraia.

  knachofanyika kwetu vitu kama hivi vinatolewa kisiasa zaidi

 7. al-akhi 13/11/2014 kwa 6:24 um ·

  Kwa bahati mbaya baadhi ya wachangiaji wanachanga mambo, kila nchi duniani ina utaratibu wake katika kuwatambua raia wake, kwa kuwapa vitambulisho vya taifa na pia utaratibu wa kuwapatia pasi za kusafiria. Baadhi ya hizi taratibu zilizowekwa ni nzuri na ziko ambazo hazikidhi haja. Si lazima utaratibu wa UK, Saudia, Denmark, Oman, Bukina Faso au Afrika Kusini ndio uwe utaratibu wa Tanzania. Kwenye suala la utaifa Zanzibar kwa bahati mbaya, utaifa wetu tuliupiga bei 1964, pale tulipoiunganisha na Tanganyika. Tanzania imeweka utaratibu wa kutoa pasi za kusafiria. Ni kweli masharti yapo, ila kwa mtazamo mtu aliyekuwa na lengo la kusafiri kweli anao uwezo wa kuyatimiza. Kwa bahati wengi wetu vijana tunataka tuwe na hizo pasi mifukoni kwa tamaa ikitokea safari nianze. Ama kuhusu vitambulisho vya uzanzibari, tena mkaazi kama vilivyoandikwa ni imani yangu muandishi wa wengine wengi munaojua siasa za zanzibar munaelewa kwamba vitambulisho hivi vilianzishwa ili kuwanyima baadhi ya watu fursa ya kushiriki uchaguzi wa wawakilishi na Rais wa Zanzibar. Wanzibari wako wengi, tena kila pembe ya dunia lakini hawapewi hivi kwani hawakukusudiwa wao. Pia wapo ambao wapo ndani ya nchi, wamezaliwa hapo, wamezaa na kujukuu hawapewi, sikwambii aliyetoka Micheweni akahamia Tomondo au Bububu akahamia Ndijani. Jambo hili la kuwanyima vitambulisho hata hao wanaostahiki kisheria linazidisha uaadui baina ya wazanzibari wenyewe na pia kwa serikali yao, ni jambo baya, halifai na linapaswa kupingwa na kila mwenye kuipenda Zanzibar na watu wake. Pamoja na kuwa hivi vitambulisho vya wazanzibari wakaazi, kuna haja kuanzishwa vitambulisho kwa wazanzibari wote.

 8. nuramo 13/11/2014 kwa 6:53 um ·

  Kuna mambo mawili lazima tuongelee Kwanza maana ya Passport ni Pass Port yani pasi ya kusafiria kiswahili sahihi wala sio kitambulisho cha uraia ila Kwa tulivozoea kwetu au kwa lugha ya kwetu ni sahihi kabisa kama alivosema muandishi

  Haya ninapoenda kuomba Pasi ina maana nataka kusafiri sio nataka kama kitambulisho Mbona BIBI YANGU HAJAENDA KUOMBA? kwa sababu hahitaji kusafiri

  Pasi ni kitu cha mwanzo hata kama huna safari karibuni lakini safari yoyote itahitaji ni kitu cha mwanzo kukikusanya na ni haki yako kama msafiri

  Lakini hawa mabwana zetu pale uhamiaji wanafanya kama utapata vile utafanikiwa ukiwa na pasi watu wenyewe 100 wanoomba kwa kila miezi 6

  Sasa hivi kwa taarifa yenu pasi hazitoki kutokana huyo anotia saini namhifadhi jina amesafiri YUPO ITALY sasa na ofisini kwake haingii mtu hadi arudi haya ndio mazingira yetu

  Ushenzi huu haupo ZNZ tu hata kwa mabalozi wetu

 9. nuramo 13/11/2014 kwa 6:57 um ·

  kuhusu ZAN ID hata mi naomba kuuliza ina maana kama huna hii ZAN ID huwezi kupewa kazi au kupewa huduma yoyote ZNZ?

  NA JE MASHARTI YAKE KUIPATA NI YAPI?

  Ni sahihi kutoa hizi ID lakini ziwe za aina mbili kama vile ulaya

  ID ZA WAZAWA NA WAKUJA

  SASA KUWE NA UTARATIBU WA MKAAZI NA SIO MKAAZI HILO HATA NCHI ZA ULAYA IPO KWA MFANO UNAWEZA KUWA RAIA WA ULAYA LAKINI HUJAKAA ULAYA KWA KIPINDI CHA MIAKA 3 BASI UKAKOSA ZILE HAKI AMBAZO ALIEKAA ULAYA AMEZIPATA

  KITU KINACHOJUULISHA HILO NI BILL ZAKO KAMA ZA UMEME HIZO AU VOTE REGISTRATION sasa huwezi kuongopa

 10. star 14/11/2014 kwa 8:38 um ·

  @al-akhi, ni kweli kitambulisho kile ni kwa ajili moja tu ya kupigia kura na ndio njia ambayo ccm wanaitumia kwa sasa kuiba kura kwa mazingira hayo lakini haihusiani na identity card na la pili , kuhusu iyo passport yenyewe pia haitolewi kisheria na imekuwa ndio njia moja kubwa ya mlo kwa hao wanaofanya kazi uhamiaji kwanza kihaki za binaadam haikubaliki kwa mtu anayetaka passport kuulizwa unataka kwenda wapi na ulete ticket au viza , hii ni dhahir kua tanzania hakuna democracy wala haki za binaadam ni udictator na ubadhirifu mtupu lakini haya yote mwisho mwakani mungu akituweka lakini kwa maisha haya basi bora mtu afe

Comments are now closed for this article.